ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 26, 2016

RAIS MAGUFULI AAGIZA MAWAZIRI WASIOLEJESHA HATI ZA TAMKO LA MALI NA AHADI YA UADILIFU KUFANYA HIVYO KABLA YA SAA 12 JIONI LEO - LA SIVYO...



RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amesema mawaziri ambao hawajajaza Tamko la Rasilimali na Madeni wawe wamejaza fomu hizo na kuzirejesha katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Dar es Salaam ifikapo leo saa 12.00 jioni (Ijumaa, Februari 26, 2016).

Agizo hilo la Rais limetolewa leo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mbele ya waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika ofisini kwake, Magogoni jijini Dar es Salaam.

“Mheshimiwa Rais ameelekeza mawaziri ambao hawajajaza tamko la rasilmali au hati ya ahadi ya uadilifu wafanye hivyo na kuzirejesha kabla saa 12 jioni na Waziri ambaye atashindwa kutekeleza agizo hili atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye nafasi yake,” amesisitiza Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu amesema wakati akifungua mafunzo ya Mawaziri na Naibu Waziri kuhusu Mwongozo wa Maadili ya Viongozi wa Umma na Utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu yaliyofanyika Ikulu jana (Alhamisi, Februari 25, 2016) alikabidhiwa majina ya Mawaziri na Naibu Mawaziri ambao hawajawasilisha Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Kamishna wa Maadili.

Amewataja mawaziri wanaotakiwa kurejesha fomu za tamko la rasilimali pamoja na hati ya ahadi ya uadilifu kuwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Charles Kitwanga na Waziri wa Nchi (OMR – Muungano na Mazingira), Bw. January Makamba.

 Wengine ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga ambaye anatakiwa kurejesha hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako ambaye anatakiwa kutoa tamko la rasilmali na madeni.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa  Nchi (OMR – Mazingira), Bw. Luhaga Mpina anatakiwa kurejesha fomu za tamko la rasilmali na madeni pamoja na hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma

SERIKALI YAFUFUA KIWANDA CHA KUSINDIKA PAMBA GEITA.

Serikali imeanza kukifufua kiwanda cha pamba katika kijiji cha Mbuye mkoani Geita ili kusaidia kupunguza ukosefu wa ajira na kuinua uchumi wa nchi. 

MITAALA YA LUGHA ZA ALAMA SERIKALI YASHITULIWA..

Serikali imetakiwa kuandaa mitaala ya lugha ya alama kwa wanafunzi wenye matatizo ya kusikia sambamba na kuwa na alama rasmi zinazotambulika nchi nzima.

KAMA UMEKOSA HABARI ZA MAGAZETI YA LEO HII NDIYO NAFASI YAKO.


 Kigogo wa mabasi mwendo kasi mahakamani. Kiwanja cha ndege chageuzwa dampo la kutupia vichanga. Marais wastaafu wapishana ikulu.

Vigogo watatu wanusuru hekalu la Dk.Slaa. Mawaziri wa JPM kikaangoni kwa madili. TMF yajitolea kuilipa TBC irushe bunge live.

Thursday, February 25, 2016

BLOGU YA WANANCHI YATIMIZA MIAKA MITATU SHEREHE KUFANYIKA KESHO HOTELI YA HYATT REGENCY KEMPISKY JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi Mkuu wa Blogu ya Wananchi, William Malecela 'Le Mutuz' , akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Blogu ya Wananchi, William Malecela 'Le Mutuz' , akionesha kompyuta mpakato kwa wanahabari ambayo alianza kuitumia baada ya kuanzisha blogu hiyo miaka mitatu iliyopita.
Mkurugenzi Mkuu wa Blogu ya Wananchi, William Malecela 'Le Mutuz' (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu blogu hiyo kutimiza miaka mitatu na semina itakayowakutanisha wasomi wasio na kazi kuhusu namna ya kujiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa.


Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Blogu ya Wananchi Media kesho itaadhimisha miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake, sherehe itakayofanyi Hyatt Regency Kempisky zamani Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa blogu hiyo, Wiliam Malecela (Le Mutuz), alisema kuwa wameamua kufanya sherehe kutokana na mafanikio waliyopata katika kipindi hicho, bendi ya muziki wa kizazi kipya ya THT itatumbuiza. 

Alisema licha ya kesho kufanya sherehe , leo itakuwa na semina maalumu ya vijana 300, ambao watakuwa pamoja na matajiri 6 vijana na vijana watatu viongozi wa wa kitaifa kwa lengo la  kubadilishana mawazo na matajiri na viongozi hao, ambao wataeleza walivyopigana mpaka kufikia walipo kimaisha. 

Alisema alianzisha blogu hiyo baada ya kuisajili kwa msajili wa makampuni (Brela) 2012, ikianza kwa kutembelewa na watu 200 kwa siku lakini kwa sasa inatembelewa na watu 70,000 mpaka 100,000 kwa siku kitu ambacho anajivunia na kuwashukuru wadau.

Kampuni hiyo ilianza kwa mtaji wa dola ya Marekani 500, ikiwa na usajili wa makampuni wa Brela, na inatoa ajira kwa vijana 4 waliomaliza vyuo vikuu nchini na ina ofisi yake katika jengo la Tancot House Sokoine Drive, Dar es Salaam. 

Alisema katika miaka mitatu blogu imeweza kuwa na domain yake wenyewe ya www.williammalecela.com na kuingia kwenyeFacebook, Twitter, na Instagram ambapo sasa inarushahabari sehemu mbalimbali kwa wakati mmoja na kuweza kuwafikia watu hadi 500,000 kwa siku.

Alisema mipango ya baadaye ni kuwekeza kwenye kampuni mpya ya  African Swahili Media Radio & Television ambayo tayari imeshapata leseni ya kufungua radio na televisheni ambayo inatazamiwa kuwa hewani  Aprili mwaka huu, kituo cha radio kitakuwa Morogoro na  televisheni Dar es Salaam, anatarajia kutoa ajira zaidi angalau kwa vijana 10.


MWANDISHI ALIYEPIGWA NA WASIRA AFUNGUKA KILICHOTOKEA.

Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi aliyepigwa jana na aliyekuwa Mbunge wa Bunda Stephen Wasira leo amehojiwa na kituocha Radio JEMBE FM Mwanza na kufunguka kilichotokea katika mkasa huo ambao ni ishara ya kuonyesha adha wanazokutana nazo waandishi wa habari hapa nchini pindi wanapokuwa kwenye utimizaji wa majukumu yao ya kila siku. BOFYA PLAY KUSIKILIZA.

KILA SIKU MCHANA SAA 7 HADI 10 JEMBE FM WANASIMAMA HAWA HAPA

Mziki mkaliiiii Yaani ki-Nowmer nowmer bila maembe katika 1&2 akisimama @chrissthedj ** HIT ZONE** Kwa hewa kila siku za juma saa 13:00 hadi 16:00 ukiwa na @nattyebrandy  @babajuti wote hawa wa-Bee wakisimama kwenye ma iNFo Radio ni JEMBE FM 93.7 Mwanza.
Tupate popote ulimwenguni kwa kudownload JEMBE FM HD katika Google Play store ya simu yako ya mkononi, kisha utatupata LIVE.
@chrissthedj

LICHA YA CHANGAMOTO MWANZA IMEPANIA KUSHIKILIA REKODI YA JIJI SAFI AFRIKA.

 JIJI la Mwanza limetangaza mpango kabambe na kudumu wa kusafisha jiji, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha kampeni zake kuendelea kushika rekodi ya kuwa jiji safi Afrika Mashariki na hatimaye kuifikia rekodi ya jiji safi Afrika ambapo safari hii licha ya changamoto mbalimbali zilizoweza kujitokeza msimu wa mvua zinazoendelea malengo bado yameendelea kushikiliwa.

Mpango wa usafi shirikishi uko palepale kwa wananchi wa kila kaya, kila mtaa, maeneo ya biashara na huduma kushiriki kusafisha mazingira kwa pamoja kila jumamosi ya mwisho ya mwezi, ambapo tarehe ya mwezi huu February ni 27.

Lengo la mpango huo wa kufanya usafi ni kuhakikisha kuwa jiji la Mwanza, ambalo linakua kwa kasi kwa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara linakuwa safi muda wote hatimaye kuweka rekodi ya kuwa jiji safi Afrika.


Mkoa pamoja na wilaya zake umejipanga vyema kushiriki zoezi hilo ambalo ni sehemu ya muendelezo wa juhudi za kuboresha mazingira zilizo asisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanganyika, na kulitaka zoezi hilo kuwa endelevu. ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA
Mulongo anasema kabla ya mpango huo, jiji lilikuwa na mpango wake madhubuti wa kufanya usafi na kupitia mpango huo ofisi yake imegundua makosa na changamoto kadhaa ambazo zimekuwa zikifanywa na watendaji wasio waaminifu huku akiahidi kuwashughulikia.
“Tunataka kupanda mbegu kwa wananchi wetu ya kupenda usafi na kuchukia usafi kwa kutumia mikutano yetu ya hadhara katika ngazi za mitaa, vyombo vya uhabari na uhamasishaji wa vikundi vya ngoma na matangazo ya kawaida”, anasema Mgoyi.
Kauli ya RC Mkuu wa mkoa, Magesa Mulongo, inawataka wananchi wote kwenye maeneo kushiriki kikamilifu kwenye kazi ya usafi ili kulifanya jiji la Mwanza kuendelea kuwa safi. Katika kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu, anawataka wananchi wote kuweka mazingira yao katika hali ya usafi, ikiwa ni pamoja na kuchemsha maji ya kunywa.
“Tukubaliane na tukiri sote tuna jambo kubwa la kusimamia usafi kwenye maeneo yetu, maeneo ya misongamano ya watu, vivuko vyetu likiwemo eneo la soko la Mwaloni ambalo huingiza wafanyabiashara kutoka nchi za Kongo DRC na Rwanda,” anasema Mulongo.
Hadi kumalizika kwa mwezi Disemba 2015, jumla la watu 613 wameugua ugonjwa wa kipindupindu ambapo 263 ni kutoka Ukerewe, Ilemela kutoka 180 Sengerema 135, Nyamagana wagonjwa 29 na Magu sita kutoka Magu. Watu 19 walifariki dunia ambapo 13 ni kutoka Ukerewe, Sengerema watatu na mmoja kutoka Magu.
Anasema zoezi la kufanya usafi halina itikadi ni zoezi la uzalendo, kwa madai kuwa ugonjwa wa kipindupindu unampata kila mtu bila ya kuangalia dini, kabila au chama chake cha siasa. Anatoa onyo kali kwa watendaji na watumishi watakaotumia zoezi hili katika kuwasumbua wananchi huku wakiwatisha na kuwaomba rushwa.

RIDHIWANI,DIWANI WA VIGWAZA WAGOMEA KUPOKEA MRADI WA MAJI CHALINZE.

NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO
 
MBUNGE wa jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete ameungana na wakazi wa vijiji vitatu vya Kidogozelo,Kitonga na Milo,kata ya Vigwaza ,kukataa kukabidhiwa mradi wa maji uliogharimu kiasi cha sh.Mil 258 fedha kutoka bank ya dunia 
 
Mradi huo umekataliwa kutokana na kutokamilika pamoja na kuonekana mapungufu makubwa ikiwa ni pamoja na mabomba kuwekwa karibu na ardhi,kupasuka kabla ya matumizi na kutandazwa mabomba madogo yasiyokdhi mahitaji.
 
Kutokana na kasoro hizo kubainika Ridhiwani ametoa mwezi mmoja kwa idara ya maji halmashuari ya wilaya ya Bagamoyo kuhakikisha inafanya marekebisho na ukaguzi wa kina .
 
Hayo yamejiri baada ya wataalamu kutoka halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo ambao waliambatana na wahandisi kutoka wizara ya maji kumuita mbunge huyo kwa malengo ya makabidhiano ya mradi katika vijiji hivyo.
 
Ridhiwani amewataka wakandarasi,watalaamu na mhandisi wa idara ya maji katika halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo,Juliana Msagala kuacha masihala kwenye miradi mikubwa inayogharimu kiasi kikubwa cha fedha kutoka serikali na kwa wahisani .

Awali Diwani wa kata ya Vigwaza ,Muhsin Baruhan amesema kutokana na mradi huo kusuasua kunasababisha wakazi wa kijiji hicho kutumia maji ya madimbwi na mtoni hivyo kuhofia milipuko ya magonjwa na kuliwa na mamba.
 
Mhandisi wa idara ya maji katika halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Juliana Msagala amekiri kuwepo kwa mapungufu yaliyoonekana na kumuahidi mbunge wa Chalinze Ridhiwani kuwa maagizo aliyoyatoa watayafanyia kazi .
 
Mradi huo ulianza mwaka 1997 na baadae uliingizwa kwenye mpango wa uboreshaji wa mradi katika program ya maji usafi na mazingira vijijini ambapo halmashauri iliingia mkataba na mkandarasi Sajo Engineering Contractor kwa ghamara ya sh mil.258.

GESI NYINGINE YAGUNDULIKA BONDE LA MTO RUVU INA UKUBWA WA UJAZO FUTI TRILIONI 2.17

Tanzania  imedhihirisha kuwa ni tajiri mkubwa wa rasilimali ya gesi asilia baada ya kugundulika kwa gesi nyingine katika bonde la mto Ruvu yenye ukubwa wa ujazo wa futi trilioni 2.17.

Ugunduzi huo wa gesi asilia umefanywa na Kampuni ya Dodsal Hydrocarbons and Power Tanzania Limited ambayo imekuwa inafanya shughuli za utafutaji wa gesi na mafuta katika Mkoa wa Pwani.

Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Pilavullathil Surendran alisema jana katika mkutano wa wawekezaji wa gesi na mafuta ulioandaliwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuwa, thamani ya gesi iliyoko katika eneo hilo inafikia Dola za Marekani bilioni sita sawa na Sh trilioni 12.

Ugunduzi huo mpya unafanya hadi sasa Tanzania kuwa na amana ya gesi yenye ukubwa wa futi za ujazo trilioni 57.27.

Kwa upande wake, Profesa Muhongo alithibitisha kugundulika kwa gesi hiyo tangu Julai mwaka jana, lakini akaeleza kuwa Serikali imechelewa kutangaza ugunduzi huo kama inavyoagizwa na Sheria ya Mafuta ya Mwaka 2015 kutokana na shughuli za uchaguzi.

“Sheria mpya inatutaka kabla ya waziri mwenye dhamana ya gesi kutangaza ugunduzi mpya wa gesi na mafuta ni lazima athibitishiwe na mamlaka ya udhibiti wa bidhaa za Petroli na Gesi (PURA).

“Wizara yangu itawasiliana na mwanasheria mkuu wa serikali ili kupata ushauri wa kisheria kuhusu jambo hilo na bahati nzuri tayari PURA imeshaanza kushughulikia jambo hilo na naamini kuwa nitatangaza ugunduzi huo mpya hivi karibuni,” alifafanua Profesa Muhongo.

Licha ya ugunduzi huo mpya tayari gesi imegundulika katika maeneo ya kisiwa cha Songo Songo mkoani Lindi na eneo la Mnazi Bay huko Mtwara na katika Wilaya ya Mkuranga, Pwani pia kumegundulika kiasi kikubwa cha gesi.

PRISONS FC YAIBANA MBAVU AZAM FC.

Timu ya Azam FC yalazimishwa sare tasa na timu ya Prisons ya jijini Mbeya katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara uliofanyika hii leo jijini Mbeya.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger akili timu yake kuzidiwa maarifa na wapinzani wao klabu ya Barcelona katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya uliomalizika kwa Arsenal kufungwa goli 2-0

KAMATA SABUNI ASILI ZA KUOGEA NA HAUTOJUTA.

YOUR BEAUTY IS OUR PROGRESS.
HERBAL SOAP UKWAJU:
“Sabuni ya Rutuba kwa kupendezesha ngozi yako kwa muda mfupi sana.
Huondoa mapunye, mba, utangotango, fangasi na kufanya ngozi yako iwe nyororo”
Ingredients: Saponification, Fragnance, Aloe  herbs, Olive oil, Coconut oil.
HERBAL SOAP MANJANO:
“Kuondoa chunusi, madoadoa, mafuta usoni, kuzuia fangasi, utangotango na mapunye”
Ingredients: Saponification, Fragnance, Olive oil, Coconut oil, Tumeric.
HERBAL SOAP UKWAJU:
“Huondoa madoa meusi usoni na kufanya ngozi yako ing’are Zaidi”
Ingredients: Sponification, Fragnance, Olive oil, Coconut oil, Tamarid.
HERBAL SOAP LIWE:
“Huondoa mapunye, mba, utangotango na fangasi na kuifanya ngozi kuwa nyororo”
Ingredients: Sponification, Fragnance, Olive oil, Coconut oil, Sandll wood.
Contact Us:
Ubungo Simu 2000, Near TCRA.

Mobile: +255 714 378 483 | +255 767 378 482 | Email: rebecalebi@yahoo.com

TUME YA MIPANGO YATEMEBELEA SHIRIKA LA MAENDELEO YA VIWANDA VIDOGOVIDOGO

Bw. Omar Jumanne Bakari (wa tatu kulia) Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO) akitoa maelezo kwa timu ya wataalam kutoka Tume ya Mipango ikiongozwa na Bibi. Florence Mwanri Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango kuhusu ufanisi wa mashine ya kutengenezea sabuni katika kiwanda kidogo cha sabuni ambazo soko lake linapatikana jijini Dar es Saalam na mikoa ya jirani.
Bibi. Florence Mwanri, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango (wa tatu kulia) akipata maelezo kutoka kwa Bw. Said Mjuli Mkurugenzi Mtendaji, kuhusu utengenezaji wa batiki katika moja ya viwanda vidogo vinavyofanya kazi chini ya mwamvuli wa SIDO. Wengine pamoja nae ni wataalam kutoka Tume ya Mipango na SIDO.
Bibi. Florence Mwanri, Kaimu Katibu Mtendaji, pamoja na timu ya maofisa kutoka Tume ya Mipango wakipata maelezo kutoka kwa mtaalamu Bw.George Buchafwe kuhusu utengenezaji wa mazulia kwa kutumia malighafi zinazopatikana hapa nchini.
Bibi. Florence Mwanri, Kaimu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Bw. Obedi Sylvester Musiba Mkurugenzi wa kampuni, (wa kwanza kushoto), kuhusu bidhaa wanazotengeneza kutokana na mimea na matunda. Wengine ni Bw. Omar Jumanne Bakari, Mkurugenzi Mkuu SIDO (wa pili kushoto), Bw. Omary Abdallah, Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Mipango na Ufuatiliaji (wa tatu kushoto), pamoja na maofisa kutoka Tume ya Mipango.
Viongozi na maofisa kutoka Tume ya Mipango wakipata maelezo kutoka kwa Bw. Abdallah Kayumbi (wa kwanza kulia) kuhusu uzalishaji wa vifaa vinavyotumika kuzalisha nishati ya umeme kwa kutumia upepo (wind Turbines).
Viongozi na maofisa kutoka Tume ya Mipango na SIDO wakiangalia mashine ya kuzalisha nyuzi kwa ajili ya kutengeneza nguo inavyofanya kazi katika kiwanda cha Fruitful Goshen, Matengenezo Textile
Bibi. Florence Mwanri, Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango, alipata pia fursa ya kutembelea kiwanda cha TEMSO Engineering kinachozalisha vifaa mbalimbali vya ujenzi kama vile mashine za kufyatulia matofali na matoroli (wheelbarrows).
Bw. Omar Jumanne Bakari, Mkurugenzi Mkuu wa SIDO (aliyesimama), akitoa maelezo kwa viongozi na maofisa kutoka Tume ya Mipango (waliokaa kushoto) kuhusu SIDO inavyofanya kazi katika kuwasaidia wazawa ili kukuza uwekezaji katika viwanda vidogo vidogo. Waliokaa kulia ni wamiliki wa viwanda vidogovidogo wanaofanya shughuli zao chini ya SIDO. 

RED CROSS TANZANIA CHATOA MSADDA KWA WAHANGA WA MAFURIKO WILAYANI RUFIJI

NA VICTOR MASANGU,  RUFIJI  PWANI

CHAMA cha Msalaba mwekundu Tanzania  (Red Cross) kimetoa msaada wa mablanketi 300 ya kujifunikia, neti 300 pamoja na ndoo 300 vyenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni 10 kwa wananchi waliokumbwa na  maafa  ya  mafuriko  baada ya mvua kumbwa kunyesha  katika  Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani.

Wahanga hao wa mafuriko wamepatiwa msaada huo kutokana na baadhi yao kwa sasa wanaishi katika mazingira magumu sana kutokana na kutokuwa na makazi maalumu ya kuishi kwani nyumba zao zimezingilwa na maji  pamoja na mazao yao  ambayo walikuwa wanayategemea kwa ajili ya chakula kusombwa na maji.

Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Nurdin Babu katika kijiji cha Utete  Meneja mkuu wa Red Cross Tanzania kutoka kitengo cha kusaidia  maafa   Lenatusi Mkaluka  amesema kwamba wameamua kwenda kutoa msaada   kwa wananchi  hao kutokana na kukumbwa na mafuriko makubwa ambayo yamepelekea  kutokea kwa uharibifu mkubwa wa mali zao pamoja na mazao kusombwa na maji.

Lenatusi alisema  kwamba red cross imeamua kuungana na serikali katika kuwasaidia  msaada huo ambapo kwa upande wao wametoa neti,mablanketi 300 pamoja na ndoo 300 kwa ajili ya kuwasaidia wananchi hao wa wilaya ya rufiji ambao kwa sasa wanaishi katika mazingira magumu.

Kwa upande wake Mkuu wa  Wilaya ya Rufiji Nurdin Babu  mara baada ya kupokea msaada huo amewataka   viongozi na watendaji  kuachana na tabia ya wizi wa  chakula kilichotolewa na serikali pamoja na msaada uliotolewa na  Red Cross  kwa ajili ya wananchi waliokumbwa na maafa ya mafuriko kwa maslahi yao yao binasfi na badala yake wahakikishe msaada huo unawafikia walengwa wenywe bila ya kufanya hujuma ya aina  yoyote ile.

Babu alibainisha kwamba kwa sasa katika Wilaya yake ya Rufiji wananchi  waliokumbwa na mafuriko wanaishi katika wakati mgumu kutokana na kukabiliwa na janga la njaa pamoja na kukosa makazi  licha ya serikai kutoa msaada wa  chakula hivyo viongozi wanapaswa kutokuwa na tamaa wakati wa zoezi zima la ugawaji wa  chakula na sio kupeleka majumbani kwao na kuwaacha wahanga hao kushinda na njaa.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la  Rufiji Mohamed Mchengerwa alisema kwamba katika jimbo lake kata zipatazo 12 kati ya 13 zimekumbwa na maafa ya mafuriko na kuongeza kwamba kwa sasa tayari serikali imeshapeleka tani 100 za mahindi  kwa ajili ya kuwasaidia wahanga hao.

Mchengerwa alibainisha kwamba  licha ya serikali kutoa msaada huo wa chakula lakini bado kunahitajika chakula kingine ii kuweza kukidhi mahitaji ya walengwa kwani kilichopo hakiwezi kutumika kwa mudu mrefu kutokana na mahitaji kuwa ni makubwa na kuongeza kuwa anatoa wito kwa wadau na taasisi nyingine kujitolea katika kusaidia misaada yoyote kwa ajili ya wananchi hao.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kibiti Ally Ungando alitoa pongezi kwa uongozi wa chama cha msalaba mwekundu Tanzania kwa kutoa msaada huo,kwani madhara yaliyojitokeza kwa wananchi wa rufiji ni makubwa kwani mazao waliyoyapanda kwa ajili ya chakula yote yamesombwa na maji pamoja na wengine kukosa makazi ya kuishi hivyo kunahitajika msaada zaidi kwa wahanga hao wa mafuriko.

 Afisa Kilimo wa Wilaya ya Rufiji Bondesi Mwalibalinga alisema kwamba kutokana   na maafa hayo alitoa wito kwa wakulima wote ambao wanalima katika mabonde kuondoka mara moja kwani mvua bado zinaendeea kunyesha na kubainisha kwamba jitihada ambazo tayari wameshazifanya kukufanya tathmini ya watu waliokumbwa na mafuriko hayo ili kuweza kujua ni namna gani ya kuweza kuwasaidia kwa hali na mali.

WAHANGA zaidi ya elfu 60 wa mafuriko katika Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani kwa sasa wanahitaji msaada wa chakula wa tani zaidi ya 1300 ili kuweza kukidhi mahitaji yao,ambao hadi sasa serikali tayari imeshapeleka msaada wa tani 200 za mahindi,ambazo bado hazitoshi hivyo kunahitajika juhudi za makusudi kwa wadau na taasisi nyingine binafsi  kwa ajili ya kuwasaidia wananchi hao.

Wednesday, February 24, 2016

AIRTEL MONEY YAINGIA UBIA NA TOTAL KUWEZESHA WATEJA KUFANYA MALIPO KWA USALAMA ZAIDI

Kushoto ni mkurugenzi wa huduma ya Airtel Money Bw, Aijaz khan wakipongezana na Mkurugenzi wa Biashara wa Total Bw, Romee De Villeneve mara baada ya kuingia ubia na kuzindua Rasmi kadi maalum ya Airtel Money Tap Tap kwaajili ya kufanyia malipo ya bidhaa mbalimbali katika vituo vya TOTAL. anaeshudia kulia ni Meneja wa Biashara Total Bi Maria Lebby. Airtel imezindua kadi hiyo jana ili kupunguza wimbi la wateja na watumiaji wa Airtel Money kutembea na pesa taslim kwaajili ya usalama wao pia kuwawezesha kufanya malipo hata kama simu zimezima.
Kushoto ni mkurugenzi wa huduma ya Airtel Money Bw, Aijaz khan wakionyesha kadi na kifaa cha malipo cha Tap Tap  na Mkurugenzi wa Biashara wa Total Bw, Romee De Villeneve mara baada ya kuingia ubia na kuzindua Rasmi kadi maalum ya Airtel Money Tap Tap kwaajili ya kufanyia malipo ya bidhaa mbalimbali katika vituo vya TOTAL. alieshikilia  kifaa cha malipo cha Airtel Tap tap kulia ni Meneja wa Biashara Total Bi Maria Lebby. Airtel imezindua kadi hiyo jana ili kupunguza wimbi la wateja na watumiaji wa Airtel Money kutembea na pesa taslim kwaajili ya usalama wao pia kuwawezesha kufanya malipo hata kama simu zimezima.
Mmoja wa watangaziji mahiri wa kituo cha EFM redio Gadner G Habash akitumia kadi ya kwanza kutolewa mara baada ya Airtel na Total kuingia ubia na kuzindua Rasmi kadi maalum ya Airtel Money Tap Tap kwaajili ya kufanyia malipo ya bidhaa mbalimbali katika vituo vya TOTAL.anaemuhudumia mtoa huduma wa Total Bi Saumu Othmani (kati) na Meneja wa Airtel Money Bw, Asupya Nalingigwa. Airtel imezindua kadi hiyo jana ili kupunguza wimbi la wateja na watumiaji wa Airtel Money kutembea na pesa taslim kwaajili ya usalama wao pia kuwawezesha kufanya malipo hata kama simu zimezima.

AIRTEL MONEY YAINGIA UBIA NA TOTAL KUWEZESHA WATEJA KUFANYA MALIPO KWA USALAMA ZAIDI

Dar es salaam Jumatatu Februari 23, 2016: Kampuni ya simu za mkononi ya imeingia ubia wa kibiashara na kampuni ya kimataifa nchini ya TOTAL inayojihusisha na kuuza mafuta ya magari pamoja na bidhaa za vilainisha ingini na mitambo, Ushirika huo wa Airtel wa Total ni kupitia huduma ya kifedha ya Airtel Money wenye lengo la kuwawezesha wateja wao kutumia kadi ya kugusisha ijulikanayo kama ‘AIRTEL MONEY TAP TAP’  kufanyia malipo yabidhaa katika vituo vyote vya Total .

Kadi ya Airtel Money ya Tap tap imeunganishwa moja kwa moja na akaunti ya Airtel money ya mteja ili mteja aweze kuitumia mahali popote anaponunua bidhaa yoyote katika vituo vya Total nchini. Kutokana na ushirika huo wateja wote wa Airtel na Total watafurahia kupata huduma zote kwa usalama zaidi bila kulazimika kubeba pesa taslimu.

Huduma hii ya kadi ya malipo kwa kugusisha ya Airtel Money Tap tap  imetokana na ugunduzi wa utafiti wenye dhamira ya kuendelea kutumia teknolojia za kisasa ili kuwezesha wateja kufanya malipo kwa urahisi na usalama zaidi. Mteja atagusisha kadi tu kwenye kifaa maalumu cha kufanyia malipo na kulipa papo hapo baada tu ya kuingiza namba yake ya siri ya Airtel Money,  teknolojia hiyo inajulikana kwa lugha ya kiingereza kama (Near Field Communication)

Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Meneja wa Huduma ya Airtel Money Tap tap hiyo Bw, Stephen Kimea alisema “tunajisikia fahari sana leo kuingia ubia na Total ili kuwaweze wateja wetu kufaidi kutumia huduma ya Airtel Money Tap tap. Hii ni huduma yakwanza kutolewa nchini Tanzania na Airtel ili kuboresha usalama zaidi kwa wateja pale wanapofanya malipo ya huduma na bidhaa mbalimbali. Kila kwenye kituo cha Total wateja wetu wataweza kutumia kadi hii, lengo letu ni kufanya wateja wetu wafurahie huduma zetu zaidi”

Kimea aliendelea kueleza “Airtel tutahakikisha kuwa huduma hii ya kufanya malipo kwa kutumia kadi yaAirtel Tap tap inapatikana kwa wafanyabiashara na watoa huduma wakubwa na wakati zaidi ya elfu 25 nchini, hii nikutaka kutoa suluhisho la usalama wa raia kwa kuondokana na tatizo la kubeba pesa nyingi wanapokwenda kufanya manunuzi na badala yake sasa watatumia kadi hii”  

“sasa kadi hizi zitapatikana katika vituo vyote vya mafuta vya Total na katika baadhi maduka yaliyo na nembo ya Airtel Tap Tap hapa nchini,  tunaamini huu ni mwendelezo wa kuboresha mfumo wa uhakika wa malipo kwa teknolojia inayoendana na sasa” alimaliza kwa kusema Kimea

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Biashara wa Total Nchini, Romee DE VILLENEUVE alisema “Total tunazaidi ya vituo vya mafuta 30 nchini, hivyo basi tunawahakikishia wateja wetu wote kupata huduma ya uhakika kila watakapotembelea vituo vyetu vyote na kununua mafuta au kupata huduma yoyote kwa kutumia kadi hizi za Airtel Money Tap tap. Tumeona umuhimu kuboresha mfumo wetu wa malipo kwaajili ya kuwapa wateja urahisi na usalama zaidi katika vituo vyetu, Tunaishukuru sana Airtel kwa kutuletea teknolojia hii ya kisasa ya mfumo kufanya malipo kwa kadi ya Airtel Money Tap tap”

Huduma ya Airtel Money Tap tap imeanza kutumika kwanza jijini Dar es salaam kwa sasa na baadae itasambazwa nchi nzima katika vituo vyote vya Total

MKALI WA NDONDI THOMAS MASHALI KUTAFUTIWA MBABE PASAKA


 Bondia Salum Nassoro akipasha na kocha wake, Maneno Abdallah katika gym yao iliyopo Mazense Midizini.

 Promota wa mchezo huo, Haruna Musa katika picha ya pamoja na bondia, Salum Nassoro.

Kampuni ya Dippo Boxing Promotion ya jijini Dar inayoongozwa na promota, Haruna Musa imeandaa pambano la Uzito wa Kati ‘Middle Weight’ kati ya bondia Salum Nassoro wa Dar na Benson Mwakyembe wa Ruvuma mchezo utakaopigwa Siku Kuu ya Pasaka, Machi 28 mwaka huu.

Pambano hilo la kukata na shoka litapigwa kwenye uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma ambapo kwa mujibu wa promota huyo alisema kuwa mshindi wa siku hiyo atazichapa na bingwa wa Afrika  ‘WBF, Thomas Mashali.

Mabondia hao ambao kila mmoja alitamba kumchapa mwenzake, waliwataka mashabiki wa ndondi kujitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo ili waone ladha ya ndondi ya asili.

    

ZAKIA MEGHJI AFUNGUA BARAZA LA WAFANYAKAZI MOI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini Taasisi ya Tiba ya Mifupa ,Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI)  Zakia Meghji (wa kwanza kulia) akifungua Baraza la tatu la Wafanyakazi Taasisi hiyo sambamba na utoaji vteti kwa wafanyakazi bora na pesa taslimu kwa kila mfanyakazi, Dar es Salaam leo katika Ukumbi wa NIMR. wa katikati ni  Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi  Dkt, Othman Kiloloma na anayefatia ni Katibu wa Baraza la wafanyakazi hilo Dkt. Clement Mugisha (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)