NA ALBERT G.SENGO/MWANZA
TAKUKURU MKOA WA MWANZA YATOA ELIMU Kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba kuelekea kipindi cha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka huu,Takukuru Mkoa wa Mwanza imetoa elimu ya dhana na madhara ya Rushwa kwenye uchaguzi, makatazo dhidi ya rushwa na wajibu wa wananchi kushiriki kuzuia vitendo vya rushwa kabla,wakati na baada ya uchaguzi ikiwemo na kutoa taarifa za vitendo vya rushwa. Takukuru Mkoa wa Mwanza kupitia kazi ya Uchambuzi wa mfumo kuhusu mapato yatokanayo na mauzo ya mifugo katika mnada wa Misasi Wilayani Misungwi imewezesha kuongezeka kwa mapato kutoka wastani wa shilingi milioni 2 laki 5 hadi milioni tatu mpaka kufikia milioni saba hadi milioni nane kwa mnada mmoja ambalo ni ongezeko la zaidi ya asilimia 100Thursday, November 21, 2024
KATIBU MKUU DKT ISLAM AONGOZA MAJUMUISHO BAADA YA ZOEZI LA USIMAMIZI WA PROGRAMU YA KUENDELEZA KILIMO NA UVUVI AFDP
Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Islam Seif Salum, Ameongoza majumuisho (wrap-up meeting), baada ya zoezi la usimamizi wa Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, lililofanywa na Mfuko wa Kimataifa wa Kuendeleza Kilimo (IFAD) na Serikali kukagua maeneo yanayotekeleza Programu ya AFDP.
KATIBU MKUU WA NLD AZINDUA RASMI KAMPENI HANDENI, ATOA WITO KWA VIONGOZI VYAMA VA SIASA KUFANYA SIASA ZA KISTAARABU
Na Oscar Assenga,HANDENI.
KATIBU Mkuu wa Chama cha NLD Doyo Hassan Doyo amezindua rasmi kampeni za wagombea wa chama hicho kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa Kata ya Kwedukwazu wilayani Handeni huku akitoa wito kwa viongozi wa chama hicho hapa nchini wafanye siasa za kistaarabu ambazo haziendi kutweza utu wa mtu.
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu ambapo vyama vya siasa ambazo zimeweka wagombea zitachuana ili kuweza kuwapata washindi ambao wataongoza Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji na wajumbe wa mitaa katika maeneo mbalimbali nchini.
Doyo aliyasema hayo mara baada ya kuzindua rasmi kampeni za chama hicho katika Kijiji cha Kwedikwazu Magharibu Kata ya Kabuku wilayani Handeni mkoani Tanga ambapo katika pamoja na mambo mengine aliwanadi wagombea ambao watachuana na vyama vyengine kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Alisema anatoa wito huo kwa sababu chama cha siasa kina kazi kubwa ya kuwaunganisha watanzania na chama ambacho kitawa sambaratisha wasikipe nafasi katika uchaguzi huo ambao ni muhimu kwa maendeleo.
“Nitoe wito kwa Chama changu cha NLD sehemu tunazokwenda kufanya kampeni tufanye siasa za Kistaarabu ambazo zinakwenda kuwaunganisha watanzania na sio vyengivyo”Alisisitiza Katibu Mkuu huyo wa chama cha NLD.
Aidha pia alitoa wito kwa vyama vyote za siasa ambazo vimesimamisha wagombea katika uchaguzi huo wasifanye kampeni za kukwaza watu bali viheshimu watu na vinadi sera ili watanzania waweze kuamua chama gani kinaweza kuwasaidia katika kipindi cha miaka mitano ngazi ya mtaa na vitongoji.
“Huu ni wito nautoa kwa viongozi wa chama cha NLD nchi mzima wahakikisha wanafanya kampeni za kistaarabu na wasifanye zile ambazo zinakwenda kukwaza watu bali waheshimu watu na tunadi sera ili uchaguzi ukiisha waendelee kuheshimiana”Alisema
Alisema wameamua kuzindua kampeni hizo katika Kijiji hicho kutokana na kwamba kwenye vitongoji 10 NLD imepata wagombea vitongoji vyote wakiwemo wajumbe, Mwenyekiti na wale wa viti maalumu ambao watachukua na vyama vya upinzani katika kinyang’anyiro hicho.
Awali Mwenyekiti wa NLD wilaya ya Handeni Rajabu Zakaria Doyo alimuomba Rais Dkt Samia Suluhu watupie macho kwenye ngazi ya usimamizi wa uchaguzi kwenye wilaya kwa sababu kuna katatizo ambako wenzao wanakileta wakati wa uchaguzi.
Alisema kwa sababu wanapokwenda kusimamia watu kwa bunduki kwani watu hawagombani na wasimamizi ni mawakala ambao wamewateua na wao wanawasainisha na kisheria.
“Chumba cha kura hairuhusiwi mtu kuja na bunduki katika chumba cha kura wala kueleza kwamba wao ni viongozi wakubwa kwa sababu kuna watu wameteuliwa kusimamia uchaguzi huo lakini kubwa tumejipanga kufanya kampeni za kistaarabu”Alisema Mwenyekiti Rajabu..
Wednesday, November 20, 2024
RAIS DKT. SAMIA AKITEMBELEA ENEO LILOTOKEA AJALI YA KARIAKOO JIJINI DAR ES SALAAM.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitembelea eneo lililotokea Ajali ya Kuporomoka Ghorofa kariakoo Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 20 Novemba, 2024.
BASHUNGWA ATINGA UWANJANI KUSHUHUDIA KIVUMBI CHA FAINALI ZA KASEKENYA CUP 2024
NA MWANDISHI WETU
WAZIRI AWESO AMPA SIKU SABA MKANDARASI WA MAJI MUHEZA
Na Oscar Assenga,MUHEZA.
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso ametoa siku saba kwa mkandarasi anayejenga mradi wa Maji wa Miji 28 kwa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga kuanza ujenzi wa tenki katika eneo la Kilulu kutokana na ujenzi wake kutokuanza tofauti na ilivyo kwa wilaya nyengine zinazotekeleza mradi huo.
Aweso alitoa agizo hilo wakati wa muendelezo wa muendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji hasa ile miji 28 inayoendelea mkoani Tanga ambapo akiwa wilayani Muheza kwenye mradi wa Kilulu alieleza na Mkuu wa wilaya hiyo Zainabu Abdallah kwamba mpaka sasa mkandarasi amechimba mashimo na hatuna kinachoendelea.
Kutokana na taarifa hiyo Waziri huyo alilazimika kutoa maelekezo hayo kwa mkandarasi huyo kuhakikisha pia wanafanya kazi Kwa ufanisi ili uweze kukamilika na wananchi waweze kupata huduma ya maji
Awali akizungumza Mkuu wa wilaya ya Muheza Zainabu Abdallah alimuomba Waziri Aweso kumchukulia hatua za mkandarasi huyo kutokana na mpaka sasa kuchimba mashimo tu na hakuna hatua yoyote inayoendelea .
"Mh Waziri tunashuku Kwa ziara hii na tunaamini ujio wako utakuwa faraja Kwa wananchi kwani utawasaidia kuusukuma mradi ufanye kazi kwa haraka na wananchi wapate maji"Alisema
Awali akizungumza kwa upande wake Mwenyekit wa Halmashari ya Muheza Erasto Mhina alisema Baraza la Madiwani walikaa na kujadili suala hilo na mbunge ila hata walipotoa agizo bado hakuna kilichoendelea mpaka sasa hivyo kumuomba waziri achukua hatua ili ujenzi wake uanze.
Naye Kwa upande wake Meneja wa Ruwasa wilaya ya Muheza Cleophace Maharangata wakandarasi hao amekiri kutokuridhishwa na ujenzi wa matenki hayo na hivyo kuhaidia mbele ya Waziri kwamba watahakikisha wanaisimamia ujenzi huo kwa ukaribu zaidi.
Mradi wa Miji 28 wa HTM kwa mkoa wa Tanga unahusisha wilaya ya Handeni,Muheza,Pangani na Korogwe ambapo utagharimu kiasi cha sh Bilioni 170 hadi kukamilika kwake kwa hatua za awali.
BARRICK YATUNUKIWA TUZO YA MDHAMINI MKUU WA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MADINI TANZANIA 2024
Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa akikabidhi cheti cha tuzo ya udhamini mkuu wa mkutano wa kimataifa wa sekta ya madini kwa Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido.
Tuesday, November 19, 2024
HIZI NDIZO SABABU ZA KAMPUNI YA HUDUMA ZA MELI KUBADILI JINA NA KUWA TASHICO
Na ALBERT G.SENGO, MWANZA.
WAZIRI BASHUNGWA AFUNGUKA KUANZIA JANUARI 2025, VIVUKO VITAKUWA VINASUBIRIA ABIRIA,
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa kushirikiana Kampuni ya Azam Marine zinaendelea kuboresha utoaji wa huduma za usafiri wa vivuko katika eneo la Magogoni – Kigamboni jijini Dar es Salaam ambapo kufikia mwezi Januari 2025 vitaongezwa vivuko vidogo (sea tax) kufikia sita (6) ambapo ushirikiano huo utaondoa changamoto kwa wananchi kusubiri vivuko kwa muda mrefu.
MSUVA AIPELEKA TAIFA STARS AFCON 2025
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji wa Al Talaba ya Iraq, Simon Happygod Msuva dakika ya 61 akimalizia pasi nzuri ya kiungo wa Yanga ya nyumbani, Dar es Salaam, Mudathir Yahya Abbas.
Kwa ushindi huo, Taifa Stars inafikisha pointi 10 baada ya mechi zote sita za kundi hilo na kuungana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yenye pointi 12 za mechi tano kufuzu AFCON ya mwakani.
Guinea inabaki na pointi zake tisa baada ya mechi zote sita za kundi katika nafasi ya tatu, mbele ya Ethiopia yenye pointi moja katika mechi tano.
Mechi ya mwisho ya Kundi H DRC wanamenyana na Ethiopia tangu Saa 1:00 usiku Uwanja wa Martyrs de la Pentecôte Jijini Kinshasa.
Hii inakuwa mara ya nne kihistoria Tanzania kufuzu AFCON baada ya mwaka 1980 nchini Nigeria, 2019 Misri na 2023 nchini Ivory Coast na mara ya kwanza kufuzu Fainali mbili mfululizo.
Ikumbukwe kwa tiketi ya uenyeji wakishirikiana na Kenya na Uganda – Tanzania pia watacheza Fainali za AFCON za mwaka 2027.
AWESO ATAKA MRADI WA MAJI MIJI 28 UKAMILIKE KABLA YA WAKATI
Na Oscar Assenga, Pangani
RAIS SAMIA AONGEZA MUDA UOKOAJI KARIAKOO
NA ALBERT G SENGO
RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amemuelekeza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa kuongeza saa 24 za uokoaji katika jengo lililoporomoka eneo la Kariakoo. Akiwa eneo la tukio, Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Thobias Makoba amefunguka haya.......Ninakupa maelekezo ya kutositisha zoezi la uokoaji na kuongeza muda wa saa 24 zaidi ili kuwapambania ndugu zetu ambao tunaamini bado wako hai.” Aidha, Rais Dkt. Samia pia ameongeza kusema kuwa: “Kwa vikosi vyetu vyote na wananchi wote wanaopambana kuokoa maisha ya ndugu zetu katika zoezi hilo ninaomba ufikishe salamu zangu na uwaeleze kuwa natambua na nina wathamini sana. Wameonyesha utu, uzalendo mkubwa na uchapakazi wa hali ya juu sana. Hivyo nawatia moyo na kuwapa nguvu ya kuendelea kuwapambania ndugu zetu kwani ninyi ni mashujaa wa taifa letu.” Rais Dk. Samia anawaombea kwa Mungu awalinde na kuwapa nguvu muda wote wakiwa wanateleleza jukumu hilo kubwa na la kizalendo.
Kwa upande mwingine, Rais Dk. Samia amewasihi wananchi, ndugu na jamaa kuendelea kuwa na subira na kama taifa tuendelee kuwaombea ndugu zetu na wapiganaji wetu ili kufanikishe zoezi hilo kwa mafanikio makubwa. “Mwenyezi Mungu tunakuomba utufanyie wepesi kwenye zoezi hili. Amin,” amesema Rais Dk. Samia.
WAZIRI BASHUNGWA AWASHA MOTO KWA TANRODS AWAAGIZA KUFUNGA MIZANI MITATU YA MAGARI TUNDUMA
NA MWANDISHI WETU
WAZIRI AWESO ATOA SIKU 60 KWA MAMENEJA WA MAMLAKA ZA MAJI KILINDI
WAFANYABIASHARA ZINGA BAGAMOYO WATEMA CHECHE JUU YA KUJENGEWA VYOO NA MACHINJIO YA KISASA
NA VICTOR MASANGU,BAGAMOYO