ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 17, 2018

SERIKALI YASEMA ULAJI WA NYAMA NA MAYAI YA KUKU WA KISASA HAUNA MADHARA.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema kuwa ulaji wa mayai ya kuku wa kisasa hayana madhara kwa binadamu.

 Ulega alisema hayo akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Zainab Mndolwa (CUF). Alisema zipo aina mbili za ufugaji ambazo ni ufugaji wa kienyeji na ufugaji wa kisasa na kuongeza kuwa ufugaji wa kuku wa kisasa hutumia dawa nyingi sana katika ukuzaji na hutumia muda wa wiki tatu hadi nne ndio huliwa na binadamu.

Katika swali lake la msingi Zainab alitaka kufahamu iwapo kuku hao wana madhara gani kwa binadamu na je, Serikali inamkakati gani wa kuwasaidia wafugaji wa kuku kutumia njia bora ya kisasa ambayo haina mashaka kwa watumiaji? 
Akijibu swali hilo Ulega alisema, Napenda kulijulisha Bunge lako tukufu kwamba ulaji wa nyama ya kuku au mayai ya kuku wa kisasa hauna madhara. Aidha, ufugaji wa kuku wa kisasa hauendani na matumizi ya dawa kwa wingi.

Alisema vyakula vinavyotumika kwenye kulisha kuku wa kisasa huwa ni viini lishe kama madini, vitamin, protini na nishati pamoja na chanjo ambazo sio dawa ambayo ni muhimu kwa ukuaji na afya ya kuku na havina madhara kwa afya ya mlaji.

BENKI YA KILIMO YATOA BILIONI MBILI KWA WAKULIMA WA KOROSHO.


Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga,akizungumza na Waandishi wa Habari juu kiasi cha shilingi Bilioni mbili zilizotolewa katika awamu ya kwanza
Serikali Kupitia Benki ya kilimo Tanzania(TADB) imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 2 kwa wakulima wa korosho wa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma katika malipo ya kundi la kwanza la watu ambao wamehakikiwa kupitia vyama vya msingi na vyama vya ushirika.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 17, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, amesema TADB imeanza kulipa wakulima wote walioakikiwa katika mikoa tajwa kupitia vyama vyao vya Msingi na ushirika kwa kuhakikisha fedha hizo zinawafikia wakulima moja kwa moja kupitia akaunti zao.

“Zoezi la ulipaji limeanza jana na kwasasa tumewafikia wakulima zaidi ya 2168 kutoka mikoa mitatu tulionza nayo hivyo tunategemea kuendelea kulipa mpaka kufikia jumatatu tutakuwa tushalipwa wakulima wengi sana kama ilivyoagizwa na Rais Dk . John Pombe Magufuli kutaka fedha hizo ziende kwa wakulima moja kwa moja bila ya makato,”amesema Waziri Hasunga.

Katika hatua nyingine Waziri wa Kilimo ametangaza kuwa jumla ya Tani 20 za korosho zimekamatwa kutoka ghala la mtu binafsi la Olam lililoko mkoani Mtwara ambapo zilikuwa zinahamishwa kwenda kwenye eneo la ununuzi wakati zikiwa ni za mwaka jana.

Amesema korosho hizo zilikabidhiwa katika Chama cha Msingi cha Mnyawi kwa lengo la kuchanganywa kinyemela na zile zinazopelekwa kwenye maghala makuu.

“Jana (juzi) tulikamata tani 20 zilizokuwa zimepenyezwa katika vyama vya msingi, tusingependa lijirudie hivyo, wananchi wawe makini kuhakikisha korosho zinazoletwa katika vyama vya msingi ni zile za Watanzania ili korosho yetu peke yake iendelee kununuliwa na Serikali,” amesema Hasunga.

Amesema korosho zitakazokamatwa kutoka nje au kuingizwa kinyemela kwenye vyama vya msingi zitataifishwa na wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Jumanne wiki hii tani nyingine tisa zilikamatwa katika eneo la Newala baada ya kuingizwa kinyemela toka nchini Msumbiji.

Aidha juzi pia yalikamatwa magunia 152 ya korosho katika Wilaya ya Nanyumbu yaliyoingizwa nchini kutoka Msumbiji.

WAZIRI JAFO APIGA MARUFUKU MILA YA WAFIWA KUTAKASWA KWA KUFANYA TENDO LA NDOA.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),  selemani Jafo amekemea mila ya wafiwa kutakaswa kwa kufanya tendo la ndoa na mtu mwingine ili kuondoa mkosi kwenye kisiwa cha Ukara kwa kuwa wanaweza kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU) na ugonjwa wa Ini.

Waziri Jafo amekemea tabia hiyo inayoendelea kisiwani humo kwasasa baada ya watu wengi kufiwa na wenza wao kutokana na ajali ya kivuko cha MV. Nyerere kilichozama miezi michache iliyopita na kupoteza watu wengi.

Katika ziara yake maalum ya utekelezaji wa agizo la Rais Dk. John Magufuli la ujenzi wa majengo yenye hadhi ya  hospitali katika eneo la Ukara, Waziri Jafo amesema zoezi hilo limeanza rasmi leo na kuagiza  ujenzi huo ukamilike ndani ya miezi mitatu.

Amesema amepata taarifa kwamba wafiwa wanafanya mapenzi na watu wengine ili watolewe mikosi kitendo ambacho ametahadharisha kwamba kinaweza kusababisha maafa makubwa kisiwani humo kutokana na watu wao kuambukizwa nagonjwa yakiwepo gonjwa la UKIMWI na Ugonjwa wa Ini yaani Hepatitis B.

Jafo amewataka wale  ambao bado hawajafanya kitendo hicho cha kutakaswa wasijaribu kabisa kwani kinaweza kusababisha maafa makubwa kisiwani humo.

Friday, November 16, 2018

MAJAMBAZI 7 WAUAWA NA POLISI MWANZA


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tumefanikiwa kuwaua Majambazi saba katika tukio la majibizano ya kurushiana risasi kati ya askari polisi na majambazi hao na kufanikiwa kukamata silaha mbili, silaha moja aina ya AK 47 yenye namba 56-3844714 ikiwa na magazine mbili na risasi 71 na silaha ya pili aina ya FN yenye namba 865895 ikiwa na magazine moja na risasi 5, huko katika maeneo ya milima uliopo karibu na shule ya msingi kishiri Wilayani Nyamagana.

Tukio hilo limetokea tarehe 15.11.2018 majira ya saa 22:00hrs usiku, hii ni baada kupatikana kwa taarifa za kiintelejensia kwamba katika Jiji la Mwanza wameingia majambazi wanaotaka kutenda uhalifu wakiwa na silaha za moto. Baada ya kupatikana kwa taarifa hizo Kikosi maalumu cha Makachero Mkoa Mwanza wakishirikiana na kikosi maalumu cha Makachero Mkoa wa Geita walifanya ufuatiliaji na kufanikiwa kumkamata jambazi mmoja aitwaye Hashim Said Abas, miaka 48, mkazi wa shamaliwa, akiwa anafuatilia eneo la kufanya uhalifu wa kutumia silaha na kupora mali katikati ya Jiji la Mwanza.

Baada ya jambazi huyo kukamatwa, askari walimhoji ndipo alikiri kwamba yeye ni miongoni mwa majambazi saba ambao wamekuwa wakifanya uhalifu wa kutumia silaha na kupora fedha na mali za watu katika mikoa ya Mwanza, Mara, Tabora, Shinyanga, Simiyu na Geita na kukiri kuhusika katika matukio yakiuhalifu yafuatayo;
        i.            MWS/IR/6108/2018 Kosa mauaji ya mfanyabiashara Richard Melkiadi Slaa Wilayani Nyamagana.
      ii.             BKR/IR/516/2018 Kosa unyang’anyi wa kutumia silaha Mkoani Geita.
    iii.            RNZ/IR/480/2018 Kosa unyang’anyi wa kutumia silaha Wilayani Bukombe.
  iv.            BWG/IR/643/2018 Kosa unyang’anyi wa kutumia silaha Wilayani Chato.
    v.            Tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha katika depot ya bia Mkoani Geita.
  vi.            Tukio la Unyang’anyi wa kutumia silaha kwa mfanyabiashara  wa dhahabu katika kijiji cha Pida Wilayani Bunda.
vii.            ITL/IR/261/2018 Kosa unyang’anyi wa kutumia silaha Wilayani Itilima.
viii.            BAR/IR/1246/2018 Kosa unyang’anyi wa kutumia silaha Wilayani Bariadi.
   ix.            MEA/IR/552/2018 Kosa mauaji Wilayani Meatu.
     x.            ITL/IR/523/2018 Kosa unyang’anyi wa kutumia silaha Wilayani Itilima
   xi.            ITL/1R/342/2018 Kosa unyang’anyi wa kutumia silaha Wilayani Itilima..
Pia jambazi huyo aliwaeleza askari kwamba ametumwa na wenzake ambao wapo katika mlima uliopo maeneo ya shule ya msingi kishiri ambako wameweka kambi kwa muda, kuangalia eneo la kufanya uhalifu katika Jiji la Mwanza haswaa eneo la Buzuruga ambapo kuna maduka mengi ya miamala ya fedha.

Kutokana na taarifa hizo Polisi tulijpanga vizuri kuelekea eneo hilo ambapo majambazi wenzake wameweka kambi kwa muda tukiongozwa na mtuhumiwa ndipo tulipofika karibu na eneo la tukio ghafla mtuhumiwa alitoa sauti ya neno “SHEMEJI” ishara ya kuwastua wenzake waliokuwa mafichoni ndipo walianza kufyatua risasi kuelekea kwa askari na kupelekea risasi hizo kumlenga mwenzao tuliyekua naye na kufariki dunia papo hapo. 

Askari tulichukua tahadhari ya kulala chini kisha tukaanza kujibu mashambulizi na baadae tuliwazidi nguvu majambazi hao na kufanikiwa kuwaua majambazi watatu waliokuwa wamejificha sehemu moja na kuendelea kuwafatilia wenzao watatu waliokuwa wakikimbia huku wakitufyatulia risasi lakini kwakuwa askari tulikuwa tumelizingira eneo lote vizuri tulifanikiwa kuwadhibiti na kuwaua.

Aidha katika eneo la tukio tumefanikiwa kukamata silaha mbili tajwa hapo juu zikiwa na risasi. Jambazi mmoja tu ndiye ametambuliwa jina aitwaye Hashim Said Abas, miaka 48, majambazi wengine bado hawajafahamika majina. Miili ya majambazi hao imehifadhiwa hospitali ya rufaa ya bugando kwa ajili ya utambuzi na uchunguzi, pindi uchunguzi ukikamilika itakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, tunatoa onyo kwa baadhi ya watu  hususani vijana wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu kuwa waache kwani vinaweza kuwapelekea kufungwa au kupoteza uhai hivyo wajihusishe na shughuli halali za kujipatia kipato. Sambamba na hilo tunawaomba wananchi waendelee kutupa ushirikiano wa kutuoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili wawezwe kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Imetolewa na;
Jonathan Shanna - ACP
Kamanda wa Polisi (M) Mwanza.
16 November, 2018

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AZUNGUMZA NA BALOZI MPYA WA PALESTINE NA UJUMBE WA MADAKTARI KUTOKA NCHINI NORWAY CHUO CHA "HOUKELAND UNIVERSITY HOSPITAL"

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Balozi Mpya wa Palestine Nchini Tanzania. Mhe. Hamdi.M.H.Abuali, alipofika Ikulu Zanzibar, leo kwa mazungumzo na kujitambulisha.tarehe 16/11/2018.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi Mpya wa Palestine Nchini Tanzania Mhe. Hamdi M.H.Abuali, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha leo 16/11/2018, Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi Mpya wa Palestine Nchini Tanzania Mhe. Hamdi M.H.Abuali, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha, kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Issa Haji Ussi Gavu na Mshauri wa Rais Masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa Fedha na Uchumi Mhe.Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa.(Picha na Ikulu) 16/11/2018.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na mgeni wake Balozi Mpya wa Palestine Nchini Tanzania.Mr.Hamdi M.H.Abuali, baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Zanzibar leo kujitambulisha.tarehe 16/11/2018.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na CEO wa Chuo Kikuu cha "Houkeland University Hospital" Mr.Eivind Hamsen, alipofika Ikulu Zanzibar na Ujumbe wake wa Madaktari Bingwa kwa mazungumzo,leo tarehe 16/11/2018.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa Madaktari Bingwa kutoka Chuo cha "Houkeland University Hospital" kulia Mr. Eivind Hamsen -CEO,akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo.tarehe.16/11/2018.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa Madaktari Bingwa kutoka Norway Chuo Kikuu cha "Houkeland University Hospital" kulia Wairi wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed,anayefuata ni CEO Eivind Hamsen na John Wigum Dahil, wakifuatilia mazungumzo hayo wakiwa nje ya ukumbi baada ya mazungumzo yao leo Ikulu Zanzibar.terehe 16/11/2018.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa Madaktari Bingwa kutoka Norway Chuo Kikuu cha "Houkeland University Hospital" kulia Wairi wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed,anayefuata ni CEO Eivind Hamsen na John Wigum Dahil, wakifuatilia mazungumzo hayo wakiwa nje ya ukumbi baada ya mazungumzo yao leo Ikulu Zanzibar.terehe 16/11/2018.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Madaktari Bingwa kutoka Chuo Kikuu cha "Houkeland University Hospital" walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo.tarehe 16/11/2018.(Picha na Ikulu)    

Thursday, November 15, 2018

MSHINDI WA GARI YA 'TBL KUMENOGA, TUKUTANE BAA' AKABIDHIWA GARI ALILOSHINDA

Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya Wateja wa TBL,David Tarimo (kulia) akimkabidhi ufunguo wa gari aina ya mshindi wa kwanza wa promosheni ya TBL Kumenoga Tukutane baa. Julitha Kilawe . Kushoto ni Meneja Matukio wa TBL, Angela Mritaba. Mshindi wa kwanza wa gari kupitia promosheni ya TBL Kumenoga Tukutane Baa Julitha Kilawe,(katikati) akionyesha ufunguo wa gari alilojishindia baada ya kukabidhiwa na Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya Wateja wa TBL,David Tarimo (kulia)mwingine pichani Kushoto ni Meneja Matukio wa TBL, Angela Mritaba.
Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya Wateja wa TBL, David Tarimo ( mwenye shati jeupe) akimfungulia gari na kumuelekeza jinsi linavyotumika Mshindi wa kwanza wa gari kupitia promosheni ya TBL Kumenoga Tukutane Baa Julitha Kilawe.


Na Mwandishi Wetu.

Mkazi wa jiji la Dar es Salaam na mfanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Julitha Kilawe, ambaye wiki iliyopita aliibuka mshindi wa gari mpya aina ya Renault KWID kupitia droo ya kwanza ya promosheni ya TBL Kumenoga, Tukutane Baa’ leo amekabidhiwa rasmi gari lake katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya TBL, Ilala jijini Dar es Salaam.

Akiongea muda mfupi baada ya kukabidhiwa gari lake Julitha Kilawe, alisema “Ninayo furaha kubwa kwa kujishindia gari kupitia promosheni hii ya TBL Kumenoga tukutane baa, mpaka siamini macho yangu, naishukuru TBL kwa kuniwezesha kupata usafiri huu”.

Kilawe alisema gari hilo atalitumia kwa usafiri wa kwenda kazini na shughuli nyinginezo za kifamilia na aliwataka wateja wa bia kuchangamkia promosheni hii kutoka TBL ambayo imelenga kuboresha maisha ya wateja wake.

Akiongea wakati wa kumkabidhi zawadi hiyo, Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya wateja wa TBL, David Tarimo, kwa niaba ya kampuni ya TBL alimpongeza mshindi huyo na kutoa wito kwa wateja wote nchini kuendelea kuichangamkia promosheni hii ili kuweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi kubwa ya gari mpya aina ya Renault KWID.

“Mshindi wetu wa kwanza kupitia promosheni hii ya TBL Kumenoga tukutane baa ameshapatikana na leo ndio amekabidhiwa rasmi gari lake. Natoa wito kwa wateja wetu popote walipo kuendelea kushiriki promosheni hii ya miezi mitatu bado kuna magari 2 kwa ajili yao na zawadi nyinginezo nyingi”, alisema Tarimo.

Tarimo, aliongeza kuwa, promosheni hii inafanyika kwenye mabaa katika siku za mwisho wa juma yaani Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kupitia bia za chapa za Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite na Balimi Extra Lager.

Kwa upande wake, Meneja wa Ukuzaji wa Masoko wa TBL, Edith Bebwa, alisema promosheni inafanyika kwenye mabaa zaidi ya 5,000 nchini kote. “Wateja wetu wazidi kuitafuta bendera ya TBL Kumenoga, kwani ilipo bendera hii ndipo wateja na TBL wanapokutana katika promosheni.’

Alisema ili kuingia kwenye droo ya magari mapya ya ‘TBL Kumenoga, Tukutane Baa’ wateja watatakiwa kununua bia tatu kati ya Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite au Balimi Extra Lager kwenye promosheni ambapo watapatiwa kuponi yenye namba, kisha watatuma namba hiyo kwa meseji kwenda 15451, hii ni kwa wale wenye mitandao ya VODACOM, TIGO na AIRTEL. Kwa wateja wa mitandao mingine watatuma namba iliyo kwenye kuponi kupitia tovuti ya http://www.tblkumenoga.co.tz/">www.tblkumenoga.co.tz

SERIKALI YAPUNGUZA UDUMAVU, VIFO VYA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO KWA ASILIMIA 50

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza wakati alipomwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango katika uzinduzi wa machapisho ya uchambuzi wa bajeti katika sekta ya jamii iliofanyika leo jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria ufunguzi huo wakisikiliza hotuba kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa machapisho ya uchambuzi wa bajeti katika sekta ya jamii iliofanyika leo jijini Dodoma.

Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
Serikali imeweza kufanya tahtmini na kubaini kuwa jitihada zilizofanyika zimeweza kupunguza udumavu na vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kwa asilimia 50.

Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alipokuwa akimuwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango katika uzinduzi wa machapisho ya uchambuzi wa bajeti katika sekta ya jamii.

Waziri Ummy amesema kuwa katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na upungufu wa viwango vya matatizo ya lishe kwa baadhi ya viashiria ambapo moja ya viashiria vya kupungua kwa matatizo ya lishe ni kushuka kwa tatizo la udumavu, uzito pungufu pamoja na ukondefu wa mwili miongoni mwa watoto.

“Kama tunavyofahamu udumavu huathiri ukuaji wa mtoto kimwili na kiakili na kupunguza uwezo wa kufanya vizuri shuleni pamoja na kupunguza ufanisi wake katika maisha ya utu uzima, hivyo kutokana na juhudi za Serikali na wadau mbalimbali tumeweza kupunguza udumavu kwa kiwango cha asilimia 50 ambapo kwa sasa kuna wastani wa watoto watatu wenye udumavu kati ya watoto 10 walio chini ya umri wa miaka mitano,” alisema Waziri Ummy.

Waziri Ummy ameongeza  kuwa ingawa bado kuna changamoto kubwa miongoni mwa kundi la watoto kwa sababu ya idadi yao kuwa kubwa, kushuka kwa kiwango cha udumavu ni jambo la kujivunia kwani  hali hiyo inaonesha kuwa jitihada za kupambana na tatizo hilo zimezaa matunda.

Akizungumzia kuhusu machapisho hayo, Waziri Ummy amefafanua kuwa  Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na UNICEF walifanya uchambuzi wa bajeti katika sekta mtambuka ya jamii hususan katika Elimu, Afya, Virusi vya Ukimwi, Maji na Usafi wa mazingira na lishe kwa lengo la kuboresha upangaji na utekelezaji wa masuala ya Mama na Mtoto katika mipango na Bajeti.

Akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa za Michezo, Susan Mlawa amesema kuwa machapisho hayo yanatoaMuhtasari wa Bajeti katika sekta mtambuka ya maendeleo ya jamii kwa kipindi cha kati ya mwaka wa fedha 2013/2014 na 2017/2018.

“Machapisho hayo yameelezea kuhusu kubaini kiasi cha fedha zilizotengwa na kutolewa katika bajeti kwamaeneo muhimu ya sekta ya jamii ambayo ni Elimu, Afya, Virusi vya Ukimwi na Ukimwi, Lishe, Maji na Usafi wa mazingira, kutoa Muhtasari wa Bajeti, kuishauri Serikali katika Sera, Mipango na bajeti yenye kuzingatia kuwapatia watoto makuzi bora na ulinzi kwa Mama na watoto katika jamii pamoja na kutoa elimu kwa wadau mbalimbali,” alisema Susan.

Akiwawakilisha wadau wengine, Mwakilishi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF), Maniza Zaman amesema kuwa shirika hilo limekuwa likifuatilia kwa karibu matumizi ya fedha za Umma zinazoelekezwa kwa watoto.

Zaman amefafanua kuwa katika kutekeleza na kuzingatia dira ya Serikali 2025 inayolenga ukuaji wa viwanda na kufikia uchumi wa kati, kumekuwa na hitaji la kuboresha huduma za afya, elimu pamoja na kuondoa changamoto zinazowakabili watoto na vijana nchini ili waweze kuimarisha afya zao pamoja na kuchangia katika maendeleo ya taifa hivyo mapendekezo yaliyotolewa katika machapisho hayo yanalenga kutekeleza lengo hilo.

Machapisho hayo yameandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikisha Wizara za Kisekta; Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Tume ya UKIMWI Tanzania (TACAIDS) na Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC).

WAFANYABIASHARA ENDELEENI KULIPA KODI:- DKT ABBASSI

Mkurugenzi   wa   Idara   ya   habari  Maelezo   na   msemaji  Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbassi 

Na Grace Semfuko-MAELEZO

Wafanyabiashara   nchini   wametakiwa   kuendelea   kulipa   kodi   na   kuzingatia   matumizi   yamashine za kielektroniki za kukusanyia mapato (EFD) ili wasiingie katika migogoro isiyo yalazima na serikali. 

Hayo   yamesemwa   jana na  Mkurugenzi   wa   Idara   ya   habari  Maelezo   na   msemaji  Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbassi katika mahojiano maalum na redio Uhuru ya Jijini Dar es Salaa,kuelezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha miaka mitatu tangu iingiemadarakani.

“Wafanyabiashara wale wanaokwepa kulipa kodi, tutawafikia, ni mkuhimu ulipe kodi ili iwezekufanya kazi za kuwahudumia watanzania, na kwa  mawakala wa kukusanya kodi wahakikishewanaifikisha kodi hizo serikalini kwa wakati” alisema. 

Dkt Abbasi amesema Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Magufuli  inafanya kazi kubwa  yakuhakikisha Watanzania wanapata maisha bora, hivyo ulipaji wa kodi ni muhimu sana ili fedhahizo ziwezeshe kupatikana kwa huduma bora zaidi kwa watanzania. 

Aidha  Dkt. Abbassi amewataka watendaji kwenye taasisi za umma kufanya kazi kwa weledina  kwa  kujituma   pia   kuzingatia   majukumu   yao   yaliyopo   kwenye   mikataba  yao   ya   kazi   ilikuleta ufanisi  kwenye taasisi zao. Alisema  Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kinidhamu watendaji wote wa umma ambaohawawajibiki ipasavyo  kwani  wamekuwa  ni  mzigo kwa Serikali, na wanakwamisha  jitihadakubwa zinazofanywa na Rais Magufuli.

“Mmeona   wenyewe   juzi   tu   Mheshimiwa   Rais   amefanya   maamuzi   magumu   lakini   ni   sahihikabisa ya kuwaondoa baadhi ya watendaji wasiowajibika Serikalini,haiishii kwenye ngazi yajuu tu hii ni kwa kila mtendaji wa Serikali kuanzia ngazi za chini” alisema Dkt. Abbassi. 

Dkt.Abbasi   alisema  kuna   mjadala   mkubwa   duniani   unaendelea   kuhusu   maendeleo   na   ninimaana ya kuwekeza, ambapo Tanzania imewekeza kwenye miradi mbalimbali ya maendeleona  miundombinu pamoja na watu kwa maana ya watumiaji wakuu wa miradi hiyo.

Kuhusu elimu amesema serikali inatoa shilingi bilioni 23.85 kila mwezi ili kugharamia elimukwenye shule za Serikali ikiwa ni mojawapo ya mkakati wa kuimarisha elimu nchini na hasakatika utekelezaji wa sera ya Serikali ya elimu bure kuanzia ngazi ya awali mpaka kidato channe.

Fedha hizo zinapelekwa moja kwa moja kwenya akaunti za shule badala ya kupelekwa kwenyeHalmashauri za Wilaya na Manispaa ambazo zilikuwa zikichelewesha fedha hizo kufika shuleniama kutumiwa kwa matumizi yaliyokusudiwa.

Serikali pia imeongeza  fedha za mikopo ya  wanafunzi wa elimu ya juu   katika  kipindi chamiaka mitatu  ya  utawala   wa  Rais  Magufuli kutoka  shilingi  Bilioni  380  mwaka 2015  mpakakufikia zaidi ya bilioni 500 mwaka 2018.Hatua hiyo ya Serikali inalenga kuimarisha sekta ya elimu nchini ambayo inatajwa kuwa nimsingi mkuu wa maendeleo endelevu kwenye Taifa lolote Duniani.MWISHO

PALE WANANCHI WANAPOJITUTUMUA SERIKALI INAWAPIGA TAFU.


 GSENGOtV

Shule ya Msingi Sumbuka ni kati ya shule 139 za msingi zilizojengwa kwa nguvu za wananchi (mafundi, wasombaji maji na nguvu ya mkono kwa mkono)

Shule hii ni moja kati ya shule zilizo na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu, ambapo mahitaji ya vyumba 08 vya madarasa na nyumba za walimu 08.

Mradi wa wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na ofisi moja ya walimu ulianza kutekelezwa mwezi Octoba 2018 na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 3 tangu tarehe ya kuanza. 

Mradi huo utakapokamilika unatarajiwa kupunguza tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa ambao umekuwa hauendani na kasi ya uandikishwaji wanafunzi wapya vilevile utakuwa umeondoa adha kwa wanafunzi waliyokuwa wakiipata kila siku kutembea umbali mrefu kwenda kwenye kata nyingine kupata nafasi jambo ambalo limekuwa chanzo kwa baadhi ya wanafunzi kukatisha masomo.

Serikali kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imetoa ufadhili wa Tshs 60,000,000/= kugharamikia ujenzi huo.

KIZAMBULI 🔥 🔥 VIDEO IS OUT


🔥 KIZAMBULI 🔥 🔥 🔥 VIDEO IS OUT 🔥 
Habari mdau na mpenzi wa muziki.
Kundi la muziki linalotamba kutoka jiji la Mwanza LAKEZONIA tunapenda kutoa shukrani zetu kwa kuendelea kutuamini na kutupatia support pale tunapotoa Kazi zetu.

Tunapenda kukualika kuangalia VIDEO ya wimbo wetu unaotamba kwa sasa KIZAMBULI  uliotengenezwa chini ya muongozaji makini@@vippertz
Ahsante sana
@@lakezoniatz@@lakezoniabloodfun
@@vippertz

DC MURO AZISAKA MILIONI 400


Na Imma Msumba, Arumeru 

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro Kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wilayani Arumeru linamsaka aliyekuwa mweka hazina ( Muhasibu ) wa halmashauri ya meru Ndg. Emmanueli  Joram na Michael Palanjo aliyekuwa mhudumu wa kawaida akapewa kazi ya wakala wa kukusanya mapato ya halmashauri  kwa tuhuma za ubadhilifu wa ya shilingi Milioni 364 Fedha Za Miradi ya TASAF kwa halmashauri ya Meru, uku Shilingi milioni 119,674,285 zikiwa pia hazionekani katika akaunti ya halmashauri ya Meru zikiwa ni fedha za makusanyo ya ndani ambazo hazijapelekwa benki na hazijulikani zilipo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Halmashauri hiyo Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. JERRY MURO ambapo amefanya ziara yake ya kushtukiza katika Halmashauri hiyo na kubaini kiasi hicho cha fedha kupotea na ameshangazwa na upotevu huo kuchukua muda mrefu bila uchunguzi.

Kwa upande wake msimamizi wa mfuko wa Tasaf Ndg. Bonifasi Mwilanga mbali na kukiri  kufahamu kwa ubatilifu huo amekiri pesa hizo zimetumika kinyume cha utaratibu katika matumizi yake.

Pia kwa upande wao baadhi ya viongozi wa Halmashauri hiyo akiwemo Mkurugenzi Ndg. Emmanueli Mkongo na Mwenyekiti  wa halmashauri hiyo  Ndg. Wille Njau wamelezea jitihada walizozichukua ikiwa ni pamoja na kuunda kwa tume ya uchunguzi juu ya upotevu wa fedha hizo.

Dc Muro amewaagiza wakuu wa idara zote katika Halmashauri hiyo kutosubiri taarifa za fedha za idara zao na badala yake ni kufatilia kila Juma kimaandishi ili kutotoa mwanya wa upotevu wa pesa za umma.

LIVERPOOL WAWEKA MEZANI KITITA KUMNASA DEMBELE.



Klabu ya Liverpool inajianda kuweka mezani kitita cha pauni milioni 85 kwaajili ya kumsajili nyota wa Barcelona, Ousmane Dembele dirisha lijalo la mwezi wa Januari.

Mfaransa huyo ameshindwa kabisa kuendana na mfumo ndani ya Nou Camp hali inayopelekea kushindwa kuwa na nafasi ya uhakika ya kucheza tangu aliposajiliwa kutoka Borussia Dortmund  kwa dau nono lililoweka rekodi ya dunia ya pauni milioni 135.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka ndani ya Liverpool meneja wa timu hiyo Jurgen Klopp yupo tayari kuweka kitita cha fedha kwaajili ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21.

Klopp anaamini kuwa usajili wa nyota huyo utasaidia kuongeza nguvu ndani ya kikosi chake kwenye mbio za kuwania ubingwa.

Hata hivyo kwa sasa Majogoo hao wa Uingereza wapo vizuri hasa kutokana na uwepo wa Mohamed Salah, Sadio Mane, Roberto Firmino na Daniel Sturridge.

BREAKING NEWS:- MBUNGE WA CUF ABDALAH MTOLEA AJIUZULU.


Mbunge wa Jimbo la Tememe kupitia Chama cha Wananchi CUF Abdallah Mtolea ametangaza kujiuzulu nafasi zake zote ndani ya Chama hicho.

Mtolea ameyasema hayo hii leo Bungeni jijini Dodoma na bado haijajulikana atahamia kwenye Chama gani.

DC MURO AKABIDHI MBUZI 100 KWA KINA MAMA WAJANE



GSENGOtV

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mh Jerry Muro AMEFANIKIWA kupata msaada wa mbuzi mia moja ( 100) wa Kisasa wa maziwa kutoka IRELAND 🇮🇪  kwa ajili ya kinamama Jane wanaotoka katika kaya Maskini wilayani humo ambao ni Msaada  kutoka kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Teknolojia za kilimo na ufugaji ECHO Ndugu Erwin Kinsey ambaye ameshirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo kutoka nchini Ireland.

Dc Muro ambae ameazimia kuwakomboa kina kama Kwa kuwatafutia misaada mbalimbali ya kujikombe  amewataka wakinamama hao kutumia msaada huo kuwa kama mbegu katika kujiendeleza katika jamii zao na kuowaongezea kipato waweze kuendesha Familia zao na kutoa Ombi Kwa kina mama hao kutothubutu kuwauza mbuzi hao wala kuwafanyia matumizi mengine tofauti na ufugaji ili waweze kutimiza malengo yaliyokusudiwa Kutokana na  msaada huo

Pia  Mhe. Muro amemshukuru Mkuu wa Jimbo la Arusha Magharibi dayosisiya Kaskazini kati ya Kanisa la kuingilia la Kilutheri Tanzania KKKT Mchungaji Philemon Mollel * kwa kushirikiana na Ndg. *Erwin Kinsey wa Kituo cha ECO Katika kuongeza jitihada zake kwa kushirikiana na  serikali kupitia shirika la Tasaf  kusaidia kaya masikini kwa kuwaletea mbuzi hao ambao watawasaidia baadhi ya kina mama hao kuleta maendeleo katika Wilaya ya Arumeru.

Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru

Tuesday, November 13, 2018

VIDEO:- HUU NDIYO MRADI WA MAJI UTAKAO TATUA TATIZO LA MAJI MISUNGWI.



GSENGOtV/MISUNGWI

HEBU vuta kumbukumbu hadi mwaka 2015 aliyekuwa mgombea mwenza wa urais, sasa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan alizunguka nchi nzima kuendesha kampeni ya kuingia akiangia ikulu akitumia kaulimbiu ya ‘Kumtua mama ndoo kichwani’ akiahidi Serikali ya chama hicho ingemaliza kero hiyo endapo ingeichaguliwa.

Kama haitoshi, aliyekuwa mgombea urais ambaye baadaye aliibuka kidedea, John Magufuli mbali na kampeni, alipoingia madarakani alitamka bungeni akiahidi kuwatua akina mama ndoo vichwani.

Ikiwa ni miaka mitatu sasa kwa Rais John Pombe Magufuli kuwa madarakani hayawi hayawi ndoto hiyo sasa inakwenda kutimia, kwani hapa Mhe.Mongella anakagua chanzo cha mradi wa maji Nyahiti-Misungwi ambao hadi kukamilika kwake mwakani, utaondoa adha ya uhaba wa maji safi na salama kwa wakazi wa Wilaya Misungwi.

Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe. John Mongella ambaye leo ameanza ziara ya siku mbili wilayani hapa kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo afya, maji na elimu, inayo tekelezwa na fedha za Serikali ya awamu ya 5, amesimamia hatua kwa hatua ikiwa ni sanjari na kuwaweka kitimoto wakandarasi na wasimamizi pale alipokuwa akipatilia shaka kwenye miradi husika.

Mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira Misungwi unatekelezwa na kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) kwa gharama ya shilingi bilioni tisa.

RC SONGWE ATOA SULUHU MGOGORO WA UCHIMBAJI MADINI

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus E. Mwangela akikagua shughuli za wachimbaji wadogo wa madini Wilayani Songwe ambapo ameagiza Ofisi ya Madini kuwatembelea wachimbaji na kuwapa elimu kuhusu sheria na taratibu za uchimbaji wa madini.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus E. Mwangela akiwa na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wamesuluhisha mgogoro baina ya wakazi wawili wa kijiji cha Saza Wilaya ya Songwe kuhusu eneo la uchimbaji wa madini.
Brig. Jen. Mwangela amesema Suzan Karan amebainika kisheria kuwa ni mmiliki halali wa eneo lililokuwa likigombewa kwa kuwa ana leseni halali huku Elimbotwa Naftari ambaye hana leseni na amekuwa akidai umiliki wa eneo hilo amebainika kuendesha shughuli za uchimbali kinyume na sheria.
“Sheria inamtambua Suzan kama mmliki halaki kwakuwa anayo leseni na amefuata taratibu na sheria za uchimbaji madini, tunashauri Elimbotwa kama atataka kuendelea kuchimba madini katika eneo hilo basi akubaliane na Suzan kufanya naye kazi”, amesisitiza.
Ameongeza kuwa serikali za vijiji hazina mamlaka ya kuwapa vibali vya uchimbaji wawekezaji wa madini bali leseni na vibali vyote vya uchimbaji wa madini hutolewa na ofisi za madini Wilaya, mkoa au kanda, hii inatokana na kuwa serikali ya kijiji ilimtambua Elimbotwa kama mmiliki wa eneo la uchimbaji kinyume na sheria.
Kwa upande wake Elimbotwa amesema anamtambua Suzan kama mmliki halali wa eneo walilokuwa wakiligombania isipokuwa sasa anadai fidia ya zaidi ya shilingi milioni 190 ikiwa ni gharama ya vitu alivyowekeza kabla ya Suzan kupewa leseni ya eneo hilo.
Naye Suzan ameupongeza uongozi wa Mkoa kwa kutoa suluhu ya mgogoro huo kutokana na kuwa ulipelekea kusimama kwa shughuli za uchimbaji na hivyo kuathiri uchumi wake.
Aidha Brig. Jen. Mwangela ameagiza Takukuru, TRA na taasisi zinazoweza kufanya ukaguzi, zihakiki madai ya Elimbotwa kama ni halisi ili Suzan aweze kuyalipa.
Imeelezwa kuwa baadhi ya migogoro ya haki ya kumiliki maeneo ya uchimbaji wa madini mkoani Songwe inasababishwa na ukiukwaji wa taratibu na sheria za madini unaofanywa na baadhi ya watendaji na wachimbaji.

MBATIA AELEZA ALICHOZUNGUMZA NA RAIS MAGUFULI IKULU LEO


Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) amesema kuwa Rais Magufulia amewapokea vizuri na amekubali kuzungumza mambo ya msingi kwa Taifa kwa kuwa waliombwa tangu mwaka juzi.

Mbatia ameyasema hayo mara baada ya kutoka kufanya mazungumzo na Rais Magufu ambapo amesema kuwa wamezungumza masuala ya elimu,afya na Tanzania iwe ya nchi gani.

"Tumezungumza na Mh. mambo ya msingi kwa Taifa letu tulikuwa tumeombwa tangu mwaka jana mwaka juzi sisi ndani ya TCD mimi ni mwenyekiti wao vile vyama vilivyo na uwakilishi Bungeni na vile vyama vile wanaalikwa washirika na kwa kuwa Tanzania ni yetu sote, Tanzania tunashirikiana soteTanzania iliyo njema," amesema Mbatia.

Aidha Mbatia ameongeza kuwa "Rais ametupokea vizuri na kutuhakikishia kwamba yeye yuko tayari tuzungumze vyama vya siasa na Watanzania kwa ujumla, pamoja na viongozi wa dini  ni taasisi ambazo ni sehemu ya Tanzania kwahiyo tukiwa na meza ya mazungumzo na maridhiano ya Kitaifa Tanzania yetu itasonga mbele zaidi na itapata baraka zaidi."

ROSTAM AZIZ:- NIMEKUJA KUMPONGEZA RAIS MAGUFULI


Mfanyabiashara maarufu Tanzania Rostam Aziz ametinga IKULU kuonana, kuzungumza na Rais Magufuli ambapo baada ya mazungumzo yao Rostam ameongea yafuatayo.

WALICHOJADILI WADAU WA PAMBA MWANZA6


 Katika Mwaka wa Fedha 2018/19, uzalishaji wa zao la pamba umefikia tani 221,600 ambazo ni sawa na ongezeko la asilimia 67 kutoka tani 133,000 zilizozalishwa mwaka 2017/18.

Takwimu hizo zimetolewa leo Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo,  Omary Mgumba alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Igunga, Dkt. Dalaly Kafumu lililohoji ni lini Serikali itashughulikia changamoto za wakulima hasa kwa kupewa mbegu bure.

Mgumba amesema kuwa mojawapo ya changamoto za wakulima wa pamba katika kuongeza tija na uzalishaji ni upatikanaji wa pembejeo kwa wakati, wakulima kutotumia kikamilifu pembejeo pamoja na uzingatiaji wa kanuni za kilimo bora cha zao hilo.

Hata hivyo Mgumba amefafanua kuwa pamoja na changamoto hizo Serikali imeendelea kudhibiti ubora wa pembejeo kupitia Mamlaka mbalimbali ikiwemo Taasisi ya TPRI na Mamlaka ya Udhibiti wa ubora wa mbegu kwa kufanya majaribio ya mbegu za pamba kabla ya kupeleka kwa wakulima kwa ajili ya kupanda ili kuboresha uzalishaji wa zao hilo.

“Kutokana na mikakati ya Serikali katika kuboresha pembejeo hasa kwa kuelekeza wakulima kutumia mbegu aina ya UKM08 na iliyoondolewa manyoya kuanzia msimu wa 2018/19, uzalishaji wa pamba umeongezeka kufikia tani 221.600 kutoka tani 133,000”, alisema Mgumba.

Mhe. Mgumba ameongeza kuwa utaratibu wa zamani haukuwa kuwapatia wakulima mbegu bure bali wakulima wa pamba waliwekewa utaratibu wa kukopeshwa kupitia Vyama Vikuu vya Ushirika na vya Msingi na kukatwa wakati wa kuuza pamba yao.

Aidha, mpango wa Serikali ni kuweka mazingira wezeshi ili wakulima waweze kufanya shughuli zao kwa ufanisi na kupata faida ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa mitaji kwa ajili kwa ajili ya kuendeleza kilimo ikiwemo ununuzi wa pembejeo.

Vile vile, katika kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo, Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ilidhamini mkopo  kwa wakulima kwa kutumia ushuru wake unaotokana na pamba ambapo wakulima hao walipata fursa ya kukopeshwa jumla ya shilingi 1,567,698,000 katika msimu uliopita.

MAMLAKA YA MAJI MWANZA WAPIGWA MSASA NA JUMUIYA YA KIMATAIFA YA MAJI

 Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga (kulia) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uandaaji wa Mpango wa Usalama wa Maji yanayotolewa kwa wafanyakazi wa MWAUWASA na  Jumuiya ya Kimataifa ya Maji (IWA)
 Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa Mpango wa Usalama wa Maji yanayotolewa na  Jumuiya ya Kimataifa ya Maji (IWA) wakimsikiliza Mhandisi Anthony Sanga (hayupo pichani). Wa pili kulia ni Mkufunzi kutoka IWA, Kizito Masinde.
 Washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa Mpango wa Usalama wa Maji yanayotolewa na  Jumuiya ya Kimataifa ya Maji (IWA) wakifuatilia mafunzo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa Mpango wa Usalama wa Maji yanayotolewa na  Jumuiya ya Kimataifa ya Maji (IWA) wakimsikiliza Mkufunzi Kizito Masinde (hayupo pichani).

Washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa Mpango wa Usalama wa Maji yanayotolewa na  Jumuiya ya Kimataifa ya Maji (IWA) katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Anthony Sanga (mbele katikati)  mara baada ya ufunguzi wa mafunzo.


Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA) wametakiwa kuzingatia  Mpango wa Usalama wa Maji kila wanapotekeleza shughuli zao ili kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama kwa ubora unaotakiwa.

Wito huo umetolewa Novemba 12, 2018 na Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uandaaji wa Mpango wa Usalama wa Maji yanayotolewa kwa wafanyakazi wa MWAUWASA na  Jumuiya ya Kimataifa ya Maji (IWA). 

Mhandisi Sanga alisisitiza umakini kwenye usimamizi wa mnyororo mzima wa utoaji huduma ya maji kuanzia kwenye chanzo, uzalishaji hadi yanapomfikia mtumiaji ambapo alisema ni wajibu wa kila mtumishi kuhakikisha maji yanayozalishwa yana ubora unaokubalika Kitaifa na Kimataifa.

Aliongeza kuwa suala la usalama wa maji ni nyeti na linapaswa kupewa kipaumbele cha kipekee na kila mtumishi ili kutimiza wajibu wa kuwapatia wananchi huduma wanayostahili kupata.

"Watumishi mliopata nafasi ya kuhudhuria mafunzo haya, mkitoka hapa hakikisheni mnawaelimisha na wale ambao hawakufanikiwa kushiriki," alisema Mhandisi Sanga.

Aliwataka waliohudhuria mafunzo hayo kuuliza maswali na kufuatilia kwa umakini ili mara baada ya mafunzo hayo waboreshe Mpango wa Usalama wa Maji uliopo.

Mafunzo hayo ya siku Tano yameanza Tarehe 12 na yatamalizika Tarehe 16 Novemba, 2018 lengo likiwa ni kuwawezesha wataalam wa Mamlaka kuhakikisha ubora wa maji wanayosambaza kwa wananchi kuanzia mahala yanapozalishwa hadi yanapofika kwa mtumiaji.

Kwa mujibu wa Mkufunzi kutoka IWA, Bwana Kizito Masinde alisema MWAUWASA ndiyo Mamlaka pekee miongoni mwa Mamlaka za Maji Nchini ambayo imepewa kipaumbele cha mafunzo hayo.

Kizito aliongeza kwamba matarajio ya IWA ni kuona wataalam wa MWAUWASA wakitoa mafunzo ya namna hiyo kwa Mamlaka zingine kote nchini.