Saturday, February 6, 2016
DC MAKONDA ATOA SIKU 20 WENYEVITI WOTE WA SERIKALI ZA MITAA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM WAPEWE RAMANI ZA MITAA YAO
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akizungumza na Watendaji na Viongozi wa Serikali za Mitaa wa wilaya hiyo kwenye mkutano uliofanyika Dar es Salaam leo kuhusu jinsi ya kutatua na kukomesha kero za ardhi
Watendaji na Viongozi wa Serikali za Mitaa wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo, Paul Makonda (hayupo pichani)
Na Dotto Mwaibale
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ametoa siku 20 kwa Wenyeviti wote wa Serikali za Mitaa Manispaa hiyo kuwa na ramani ya mitaa ili kuyatambua maeneo ya wazi.
Makonda amewataka watendaji wa Manispaa hiyo kwenda na kasi ya serikali ya kuwatendea haki wananchi katika kumaliza migogoro ya ardhi.
Akizungumza Dar es Salaam leo mchana na Wenyeviti zaidi ya 100 wa Serikali za Mitaa ya9 Manispaa ya Kinondoni ,Makonda alisema baadhi ya watendaji wanatanguliza maslahi mbele kuliko mahitaji ya Wananchi na Taifa kwa ujumla.
Alisema migogoro ya ardhi ni kero kila sehemu misibani, harusini na kwenye mazishi suala kubwa ni la ardhi na kuongeza kuwa mabaraza ya ardhi ya Kata hayana uhalali wa kuamua kesi hizo kwa kuwa baadhi yao hata uelewa wa masuala hayo hawana na yamekuwa yakiongeza matatizo.
"Leo tumekutana hapa kwa sababu ya migogoro ya ardhi na kuanzia sasa ndani ya Wilaya ya Kinondoni nataka kurudisha heshima ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa nawaagiza kuanzia sasa mtu yeyote kutoka Wizarani,Manispaa au hata mwekezaji lazima apitie kwanza kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mitaa,"alisema.
Alisema watendaji wengi Manispaa ndio chanzo cha migogoro ya ardhi kwa kutotimiza wajibu wao na wameshindwa kuonyesha dira ya kuwasaidia wananchi.
"Kibaya zaidi ili kujitengenezea mazingira ya ulaji wenyeviti hawashirikishwi katika hatua za awali wanahusika zaidi pale kunapotokea mgogoro,"alisema.
Aliongeza kuwa "Sina hofu wala uoga wala sina sifa ya kupendwa wala kutafuta kupendwa hivyo nitahakikisha ninatumia Mamlaka niliyopewa kufanya migogoro hii ya ardhi Kinondoni na kuwa historia na nikitaka jambo huwa sishindwi"alisema.
Alisema baada ya wenyeviti hao kupewa ramani atahakikisha anakutana na Wazi ri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wilium Lukuvi na maofisa wa ardhi.
"Hapo sasa watakaobainika kuhusika katika michezo michafu na kuchochea migogoro basi Waziri Lukuvi aondoke nao maana wameshindwa kazi"alisema
Makonda aliwataka wenyeviti hao kuonesha maeneo ya wazi na yale yaliyovamiwa ili kuchukua hatua kwani wenye dhamana wapo ofisini huku wananchi wakiwa wanateseka na migogoro hiyo.
Mkuu wa Idara ya Mipango Miji Manispaa ya Kinondoni Juliana Letara alisema Wenyeviti wote watapewa ramani za mitaa yao ndani ya wiki mbili kwa kuwa zipo kwenye kompyuta ofisini hivyo atawapatia ramani hizo.
Alisema kutokana na migogoro mingi ya ardhi anapendekeza kufanyike mapendekezo ya mabadiliko ya sheria kwa kuwa kesi zote za mabaraza ya kata zinaigharimu serikali zaidi ya milioni tatu kwa siku.
Alizitaja kesi hizo kuwa ni za ardhi ya hifadhi,ardhi ya kawaida na ile ya kimila
"Tulikopa benki ya TIB mkopo kwa ajili ya kupima Viwanja likiwemo eneo la Mabwepande lakini kila siku tunatozwa riba ya sh.milioni tatu jambo ambalo ni gumu na ipo siku litashindikana na ndio maana tunauza Kiwanja hadi milioni 20 na 30,"alisema.
Baadhi ya wenyeviti wa Serikali za Mitaa ambao walipata nafasi ya kuzungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo walimtaka Makonda kuondoa majipu sugu katika Manispaa hiyo likiwemo la maofisa mipango miji.
Alisema wako tayari kufanyazi na Makonda lakini sio wafanyakazi hao kitengo cha ardhi kwa kuwa wamekuwa chanzo cha migogoro mikubwa ya ardhi.
MAADHIMISHO YA MIAKA 39 YA CCM
Rais mstaafu Jakaya Kikwete aipongeza serikali ya awamu ya 5 kwa kutekeleza ilani ya CCM ndani ya siku chache za utawala wa rais Magufuli.
Rais Magufuli ameeleza kuwa serikali yake imedhamiria kufanya kazi na ametoa agizo kwa viongozi wote kuondoa kero za wananchi.
Rais Magufuli ameeleza kuwa serikali yake imedhamiria kufanya kazi na ametoa agizo kwa viongozi wote kuondoa kero za wananchi.
HII NDIYO KAMPUNI ILIYONUNUA TIKETI ZOTE ZA MICHUANO ZANZIBAR.
Makamu Mwenyekiti wa Balraza la Michezo Zanzibar BMZ akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi fedha kwa timu za JKU na Mafunzo za mchezo wao wa Kombe la CAF inayotarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Meneja wa Makampuni ya Hoteli za Ocean View Zanzibar Jacob Makundi akizungumza na Waandishi wa habari na Viongozi na Wachezaji wa Timu za JKU na Mafunzo wakati wa kukabidhi fedha za ununuzi wa tiketi wa michuano hiyo inayoandaliwa na CAF Championc Leagua na Confederation Cup 2016. na kuahidi kutowa gharama zote za michezo hiyo. inayotarajiwa kufanyika tarehe 13-2-2016 na 14-2-2016 katika uwanja wa amaan Zanzibar.
Viongozi wa Timu za JKU na Mafunzo wakimsikiliza Meneja wa Makampuni ya Zanzibar Ocean View Zanzibar akizungumza wakati wa hafla hiyo na kutoa ahadi kwa kilia Timun ikishinda mchezo wao huo wa awali itazawadiwa shilingin Milioni Tano kwa ushindi wowote ule,wakati wa hafla ya kukabidhi fedha za tiketi za mchezo huo Kampuni yake imenunua tiketi zote zenye thamani ya shilingi miliono tano kila moja na kutowa fursa kwa Wapenzi wa mchezo wa mpira Zanzibar kuona mapambano hayo bure bila ya kiingilio.
Wachezaji wa Timu za JKU na Mafunzo wakiwa katika hafla hiyo katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Wachezaji wa Timu za JKU na Mafunzo wakiwa katika hafla hiyo katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Mshauri wa Kisheria wa Makampuni ya Hoteli ya Zanzibar Ocean View Zanzibar Mhe Abdalla Juma akizungumza wakati wa hafla hiyo kwa niaba ya Kampuni hiyo kuhusiana na udhamini wa mchezo huo kwa timu za JKU na Mafunzo. na kutowa Salamu za Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni hayo Amani Ibrahim Makungu.
Meneja wa Makampuni ya Hoteli ya Zanzibar Ocean View Zanzibar Jacob Makundi akimkabidhiwa Tiketi ya Mchezo wa JKU na Gaborone United Club na Kiongozi wa Timu ya JKU Khamis Mohammed, mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar, Kampuni ya Zanzibar Ocean View Imenunua tiketi hizo zote za mchezo huo na kutowa fursa kwa Wananchi na Wapenzi wa Michezo Zanzibar kujionea Michuano hiyo ya CAF kujionea bure. makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa hoteli hiyo Kilimani Zanzibar
Meneja wa Makampuni ya Hoteli ya Zanzibar Ocean View Zanzibar Jacob Makundi akimkabidhi Milioni tano fedha za mauzo ya Tiketi ya Mchezo wa JKU na Timu ya Gaborone United Club Kiongozi wa Timu ya JKU Khamis Mohammed, mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar, Kampuni ya Zanzibar Ocean View Imenunua tiketi hizo zote za mchezo huo na kutowa fursa kwa Wananchi na Wapenzi wa Michezo Zanzibar kujionea Michuano hiyo ya CAF kujionea bure. makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa hoteli hiyo Kilimani Zanzibar
Meneja wa Makampuni ya Hoteli ya Zanzibar Ocean View Zanzibar Jacob Makundi akimkabidhi Milioni tano fedha za mauzo ya Tiketi ya Mchezo wa Mafunzo na AS Vita Club ya Congo Kiongozi wa Timu hiyo Khamis Ali Machenga, mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar, Kampuni ya Zanzibar Ocean View Imenunua tiketi hizo zote za mchezo huo na kutowa fursa kwa Wananchi na Wapenzi wa Michezo Zanzibar kujionea Michuano hiyo ya CAF kujionea bure. makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa hoteli hiyo Kilimani Zanzibar
Meneja wa Makampuni ya Hoteli ya Zanzibar Ocean View Zanzibar Jacob Makundi akimkabidhi Milioni tano fedha za mauzo ya Tiketi ya Mchezo wa Mafunzo na AS Vita Club ya Congo Kiongozi wa Timu hiyo Khamis Ali Machenga, mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar, Kampuni ya Zanzibar Ocean View Imenunua tiketi hizo zote za mchezo huo na kutowa fursa kwa Wananchi na Wapenzi wa Michezo Zanzibar kujionea Michuano hiyo ya CAF kujionea bure. makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa hoteli hiyo Kilimani Zanzibar
Msemaji wa ZFA Ali Cheupe akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi fedha za mauzo ya tiketi ya mchezo wa JKU na Mafunzo, uliofadiliwac na Makampuni ya Hoteli ya Ocean View Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa hoteli hiyo kilimani Zanzibar.
Kiongozi wa Timu ya JKU akitowa shukrani kwa Timu za JKU na Mafunzo kwa ufadhili wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View kudhamini Michuano hiyo kwa kununua tiketi zote za michuano hiyo na kutowa fursa kwa wananchi kuona mchezo huo bila ya kulipa kiingilio wakati wa michuano hiyo inayotarajiwa kufanyika wiki ijayo kuazia tarehe 13-2-2016 na 14-2-2016 yatakayofanyika katika uwanja wa Amaan Zanzibar na kuwataka Wafanyabiashara wengine kujitokeza kudhamini michuano mbalimbali Zanzibar ili kukuza kiwango cha Mpira Zanzibar.
Imetayarioshwa na OthmanMapara.Blogspot
Zanzinews.com
othmanmaulid@gmail.com.
TAMASHA LA PASAKA MWAKA HUU KUFANYIKA MACHI 28 WILAYANI KAHAMA
Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani), jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Tamasha la Pasaka litakalofanyika Mkoani Shinyanga Wilayani Kahama Machi 28 mwaka huu ambapo Tamasha la Pasaka mwaka huu halitafanyika jijini Dar es Salaam na baadala yake kufanyika mikoani.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama wakati akizungumza nao leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
TAMASHA la Pasaka mwaka huu kufanyika Machi 28 Mkoani Shinyanga katika viwanja kahama wilaya ya Kahama, ambapo tamasha hilo limewapa kipaumbele waimbaji wa ndani ya nchi yetu.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Msama amesema kuwa Kauli mbiu ya Tamasha la Pasaka mwaka huu ni "UMOJA NA UPENDO HUDUMISHA AMANI KATIKA NCHI YETU". ambayo itatawala katika tamasha hilo hapa nchini.
Msama amesema kuwa Mwimbaji wa nyimbo za Injiri Bonfasi Mwaitege amethibisha kutumbuiza katika tamasha hilo pamoja na Mwimbaji wa nyimbo za Injiri Rose Mhando.
Aidha Msama amelishukuru Balaza la Sanaa Tanzinia(BASATA) kwa kuruhusu kufanyika Tamasha la Pasaka wilayani Kahama pia amewaomba wananchi wajitokeze kwa wingi katika tamasha hilo mkoani humo.
JPM HANA MAMLAKA UCHAGUZI ZANZIBAR: MWANASHERIA MKUU.
Hii
ni kauli ya pili kutolewa ndani ya wiki moja ikieleza hali hiyo, baada
ya ile ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Luvuba
aliyoitoa wiki iliyopita baada ya kufanya mazungumzo na Rais Magufuli,
Ikulu, Dar es Salaam.
Akizungumza
bungeni juzi, Masaju alisema: “Katiba ya Zanzibar si ya Muungano,
masuala ya ulinzi na usalama ndiyo ya Muungano na ndiyo sababu ulinzi
umeimarishwa visiwani humo kuhakikisha nchi hiyo inakuwa salama.
Alitoa
kauli hiyo juzi jioni wakati akifafanua mambo mbalimbali
yaliyozungumzwa na wabunge wakati wa mjadala wa mwongozo wa mpango wa
Bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha wa 2016/17 na Mapendekezo ya Mpango
wa Taifa wa Maendeleo wa mwaka 2016/17.
Tangu
kuibuka kwa mgogoro Zanzibar watu wa kada mbalimbali wamekuwa wakisema
mwarobaini wa mgogoro huo kwa kutumia jitihada za ndani, ufanywe na Rais
Magufuli baada ya jitihada za viongozi wa kisiasa visiwani kukwama.
Mgogoro
huo, ambao umekuwa kawaida kuibuka kila baada ya Uchaguzi Mkuu,
uliibuka baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salum
Jecha kufuta matokeo Oktoba 28 na baadaye kuuitisha upya, kitendo
ambacho CUF inakipinga.
Tangu
wakati huo, Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, Rais wa
Zanzibar, Dk Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd
na marais wa zamani wa Zanzibar, Dk Salmin Amour, Ali Hassan Mwinyi na
Amani Karume wamekuwa kwenye mazungumzo ambayo hayakuzaa muafaka.
“Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua uwepo wa Serikali mbili.
Hizi Serikali uwepo wake ni Katiba ya Muungano na Katiba ya Zanzibar.
Ukisoma Ibara ya nne ya Katiba si tu kwamba inaweka mgawanyo wa madaraka
katika mihimili mitatu ya Dola, bali inaweka mgawanyo wa madaraka kati
ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar.”
Ibara
ya 4 ya Katiba inasema (1) Shughuli zote za Mamlaka ya nchi katika
Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kudhibitiwa na vyombo viwili vyenye
mamlaka ya utendaji, vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji
haki na pia vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia
utekelezaji wa shughuli za umma.
(2)
Vyombo vyenye mamlaka ya utendaji vitakuwa ni Serikali ya Jamhuri ya
Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, vyombo vyenye mamlaka ya
kutekeleza utoaji haki vitakuwa ni Idara ya Mahakama ya Serikali ya
Jamhuri ya Muungano na Idara ya Mahakama ya Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, na vyombo vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia
utekelezaji wa shughuli za umma vitakuwa ni Bunge na Baraza la
Wawakilishi.
(3)
Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za umma katika Jamhuri ya
Muungano, na kwa ajili ya mgawanyo wa madaraka juu ya shughuli hizo
baina ya vyombo vilivyotajwa katika ibara hii, kutakuwa na mambo ya
Muungano kama alivyoorodheshwa katika nyongeza ya Kwanza iliyoko
mwishoni mwa Katiba hii, na pia kutakuwa na mambo yasiyo ya Muungano
ambayo ni mambo mengine yote yasiyo ya Muungano.
(4)
Kila chombo kilichotajwa katika ibara hii kitaundwa na kutekeleza
majukumu yake kwa kufuata masharti mengine yaliyomo katika Katiba hii.
Masaju alisema Katiba ya Zanzibar ndio inayozaa ZEC.
“Kile
ambacho baadhi ya wabunge wamekisema hapa ni kama kuitaka Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuingilia mamlaka ya Zanzibar na tafsiri
yake ni kama unataka kuleta hoja ya kujenga Serikali moja,” alisema.
RAIS MAGUFULI ATANGAZA VITA MPYA KWA WAFANYABIASHARA.
Rais Magufuli atangaza vita mpya kwa waliomilikishwa mashamba na viwanda
huku akidai hatamuonea mtu haya bila kujali chama chake.
Imeelezwa kwamba licha ya serikali kuendelea kutoa kipaumbele katika sekta ya elimu bado sekta hiyo imeendelea kukumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa miundombinu.
Imeelezwa kwamba licha ya serikali kuendelea kutoa kipaumbele katika sekta ya elimu bado sekta hiyo imeendelea kukumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa miundombinu.
KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AWATEMBELEA WAHADZABE NA KUSHIRIKI SHUGHULI ZA MAENDELEO KWA JAMII HIYO.
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukikatisha misitu na mabonde wakati ukielekea kata ya Mwangeza kijiji cha Kibampa ambako jamii hiyo inaishi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia Sola zinazosukuma maji kwenye kisima cha mradi wa maji yanayotumika kwenye kijiji pamoja na shule ya msingi ya Munguli iliyopo wilaya ya Mkalama mkoani Singida.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya mradi wa maji wa kijiji cha Munguli kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Ndugu Christopher Ngubiagai.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa ndani ya hosteli ya shule ya msingi Munguli ambayo wanasoma watoto wa Kihadzabe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakulima wakati akiwa njiani kuelekea kata ya Mwangeza kijiji cha Kibampa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakulima wakati akiwa njiani kuelekea kata ya Mwangeza kijiji cha Kibampa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikaribishwa kijiji cha Kibampa na wakazi wa hapo amabao ni Wahadzabe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akifurahia jambo na kijana wa kabila la Kihadzabe
Wahadzabe wakiwa kwenye kikao maalum kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakishiriki kupanda mihogo kwenye shamba ya la Wahadzabe kwenye kijiji cha Kibampa wilaya ya Mkalama.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Ndugu Christopher Ngubiagai akimuelekeza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana namna Wahadzabe wanavyosaga mtama kwa kutumia jiwe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana leo ameweka historia ya kuwa kiongozi wa nne mkubwa wa Kitaifa kufika kwenye kijiji cha Munguli na Kibampa ambavyo wanaishi jamii ya Wahadzabe .Kijiji cha Munguli kilitembelewa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kamabarage Nyerere, akifuatiwa na aliyekuwa Makamu wake Abdu Jumbe na Mama Sofia Kawawa.
Jamii ya Wahadzabe inaishi kwa kutegemea uwindaji,kula matunda ya porini,mizizi ,wadudu na miti hata hivyo juhudi kubwa zimefanyika kuanza kuwafundisha kilimo, kuwapeleka watoto shule ,zaidi ya Wahadzabe 305 wanasoma kwenye shule ya msingi Munguli, pamoja na vijana zaidi ya 50 kupelekwa kujiunga na JKT.
Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone kwa jitihada zake za kuwasaidia jamii ya Wahadzabe ikiwa pamoja na kuhakikisha wanapata elimu, wanajifunza kilimo lakini pia uamuzi wa kupima maeneo ya Wahadzabe ili wamiliki ardhi yao wenyewe.
PICHA NA MICHUZI JR-MMG-SINGIDA
PICHA NA MICHUZI JR-MMG-SINGIDA
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akiwa kwenye nyumba maalum ya chifu wa wahadzabe pamoja na Mwenyekiti wa Wahadzabe Edward Mashimba na Mama Sarah Philipo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakitoka kwenye nyumba ya Chifu wa Wahadzabe iliyopo kijiji cha Kibampa kata ya Mwangeza wilaya ya Mkalama mkoani Singida
wakazi wa kijiji cha Kibampa ambaco wakazi wake ni jamii ndogo yenye kaya 300 ya Wahadzabe wakishangilia jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Kibampa ambako wakazi wake ni jamii ndogo yenye kaya 300 ya Wahadzabe,kushoto ni Mwenyekiti wa Wahadzabe Ndugu Edward Mashimba (kushoto) ambaye alikuwa akitafsiri kwa lugha ya Kihadzabe
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Kibampa ambako wakazi wake ni jamii ndogo yenye kaya 300 ya Wahadzabe,kushoto ni Mwenyekiti wa Wahadzabe Ndugu Edward Mashimba (kushoto) ambaye alikuwa akitafsiri kwa lugha ya Kihadzabe
Subscribe to:
Posts (Atom)