ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 3, 2023

WAZEE VISIGA WAMFAGILIA MBUNGE KOKA KWA KUTOA ENEO LA UJENZI WA KITUO CHA MATIBABU

 

NA VICTOR MASANGU,KIBAHA

Baàdhi ya wazee katika kata ya Visiga iliyopo halmashauri ya mji Kibaha mkoani Pwani wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kwa kuwa karibu nao na  kuwajali kwa hali na mali katika kusikiliza changamoto zao mbali mbali zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi.

Wazee hao wametoa pongezi hizo wakati wa halfa maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwakabidhi kadi zao rasmi zaidi ya 300 ambazo  watazitumia katika kupata  matibabu kwa urahisi  pindi wanapoumwa ili kuondoka na na usumbufu ambao waliokuwa wanaupata.

Walibainisha kwamba kitendo cha Mhe.Mbunge wao kwa kuwaahidi kuwasaidia kwa hali na mali ikiwemo katika suala zima la huduma ya afya litakuwa ni msaada mkubwa kwa upañde wao.
Kadhalika wazee hao waliongeza kwamba wana Imani kubwa na Mbunge Koka ataweza kuleta mabadiliko mbali mbali kutokana na msaada wake wa kutoa eneo la kiwanja kwa gharama zake ili liweze kutumika kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kuwasaidia wazee.

"Kwa kweli sisi Kama wazee leo tumefarijika sana kupata fursa ya kupatiwa kadi zetu ambazo kiukweli zitaweza kutusaidia katika kupata matibabu kwa urahisi zaidi kuliko ilivyokuwa kipindi cha nyuma na pia tunashukuru shirika la Videa ambao wamewezesha upatikanaji wa kadi hizi bila kumsahau  Mbunge kwa kutoa kiwanja"walisema.

Kwa upañde wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka alisema kwamba kwa kuwa lengo lake kubwa ni kuboresha sekta ya afya ameamua kuwatafutia eneo la kiwanja kwa lengo la kujenga kituo cha kudumu kwa ajili ya kuwasaidia wazee kupata huduma mbali mbali hususan za matibabu na mambo mengine.

Mhe.Koka alifafanua kuwa wazee ni watu muhimu sana katika jamii hivyo wanapaswa kuwekewa mazingira bora na rafiki ikiwemo kuwajali kwa kuwapatia vifaa tiba ambavyo vitaweza kuwa ni mkombozi katika matibabu pamoja na mahitaji mengine ya msingi.

"Nimeisikiliza risala yenu na kikubwa ili Jambo nimelichukua kwa mikono miwili na kikubwa kwa kuwa na mimi nina marafiki zao nina imani baadhi ya vitu wataweza kutusaidia kwa kushirikiana na ofisi yangu lengo ni kuwasaidia wazee wetu kwani na sisi lazima tutakuwa wazee ili alikwepeki,"alisema Mhe.Koka.

Mbunge huyo aliongeza kuwa katika kufanikisha azma ya shirika hilo la Videa pia atashirikiana na wadau mbali mbali ikiwemo wa ndani na nje ya nchi ili mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha kudumu uweze kutimia na kuleta mabadiliko chanya kwa wazee hasa katika kuwatimizia mahitaji yao mbali mbali.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilokuwa la kiserikali la Videa Social Service Organization Tumaini Msheika alisema kwa sasa kituo hicho kinaendesha kazi zake za kuwahudumia wananchi katika majengo ya kupanga hivyo msada wa kiwanja walioupata kutoka kwa Mbunge Koka kwa ajili ya ujenzi utakuwa mkombozi mkubwa.

  Mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi (CCM) Kibaha mjini mwalimu Mwajuma Nyamka alisema juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya afya ni utekelezaji wa ilani hivyo hivyo ana Imani wazee hao wataendelea kusikilizwa na kupata matibabu kwa upendeleo maalumu kwani ni haki yao.

Sunday, October 1, 2023

MTEMBEZI MARATHON 2023 KUVUMBUA VIVUTIO VIPYA MWANZA

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Miongoni mwa vitu ambavyo jamii yetu haijajua, haijakubali au pengine haina huo uelewa wa kutosha kuhusu suala la utalii ni kwamba utalii siyo kufanya ziara mbugani au kutembelea sehemu zenye vivutio vya kale, dhana ya utalii ni kubwa na inazama ikishirikisha masuala mengi sana ndani ya jamii na yanayoizunguka jamii ikiwemo utamaduni, ngoma, majengo mapya, miundombinu ya usafiri na usafirishaji yakiwemo madaraja mapya, maziwa na bahari. Vilevile dhana ya utalii inaingia hadi kwenye mavazi ya asili, viunga vya burudani aka bata na hata mito na milima inayopatikana mahali flani, ambapo safari hii Mtembezi Marathon inakuja kuvumbua na kuainisha maeneo mapya ya utalii Kkatika jiji la miamba (Rock City) Mtembezi Marathon tayari imeshafanyika katika mikoa ya Dar es salaam, Kigoma, Tabora na Dodoma na sasa inaenda kufanyika mkoani Mwanza. #mwanza #samiasuluhuhassan #royaltour #tanzania

UWT KATA YA MISUGUSU WAMPA HEKO MAMA KOKA KWA KUWAKOMBOA WANAWAKE



Na Victor Masangu,Kibaha 

Katika kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya michezo mke wa Mbunge la Jimbo la Kibaha mjini Selina Koka ameanzisha  rasmi mashindano ya mchezo wa netiboli kwa wanawake wa jumuiya ya umoja wanawake (UWT) kata ya Misugusugu.


Mama Koka amezindua michuano hiyo ikiwa ni moja ya ahadi yake kubwa ambayo aliitoa ya kukuza na kuinua vipaji vya mchezo huo kwa wanawake wa kata zote 14 zilizopo katika Jimbo la Kibaha mjini ili kuweza kupata fursa ya wanawake kushiriki kikamilifu katika kukuza vipaji vyao.

Alibainisha kwamba hivi karibuni aliweza kufanya ziara yake katika kata mbali mbali akiwa Kama mlezi wa UWT Kibaha mji na alitoa na kukabidhi vifaa mbali mbali kwa timu husika ikiwemo mipira pamoja na jezi lengo ikiwa ni kila kata kuweza kuunda timu yao ya netiboli.
 

"Kwa kweli nimefarijika sana leo kuwepo hapa katika kata ya Misugusugu ikiwa nimekuja kuonana na wanawake wenzangu sambamba na kuzindua mashandano haya ambayo tumeyapa jina la Selina Cup na mm lengo langu ni kukuza vipaji zaidi katika mchezo huu wa netiboli,"alisema Mama Koka.

Kadhalika aliwahimiza wanawake wote wa UWT kuwa na mshikamano katika kushiriki katika mambo mbali mbali ikiwemo suala zima la michezo pamoja na  kukiimarisha chama Cha mapinduzi kuanzia ngazi za chini kabisa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha mji Elina Mgonja alimpongeza Mke wa Mbunge kwa ushirikiano wake wa kujitolea na kuwa karibu na jamii katika nyanja mbali mbali ikiwemo sekta ya michezo hususan netiboli kwa wanawake.




Hivi karibuni Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mji alipokuwa katika ziara ya Mwenyekiti wa UWT Kibaha mji aligawa vifaa mbali mbali vya mchezo wa netiboli katika kata 14 kwa lengo la kukuza na kuinua na kukuza vipaji vya wanawake wa Jimbo la Kibaha mjini.