ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 11, 2016

WAKURUGENZI MWANZA WAKALIA KUTI KAVU.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella .
Wakurugenzi wa halmashauri za Mkoa wa Mwanza ambao hawajatimiza hata nusu ya idadi ya madawati yanayohitajika, wameagizwa kuhakikisha wanakamilisha  kabla ya mwisho wa mwezi huu.

Akizungumza na madiwani wa Manispaa ya Ilemela juzi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema ameunda kamati kufuatilia utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la ifikapo mwisho wa mwezi huu wanafunzi wawe wanakaa kwenye madawati

“Anayependa kuendelea kushikilia nafasi yake ahakikishe halmashauri inafanya kazi usiku na mchana, ili kukamilisha idadi ya madawati,” alisema Mongella na kuongeza:

“Ole wake mkurugenzi ambaye tutakuta watoto wanakaa chini kwenye shule za halmashauri yake.”

DONDOO ZA MAGAZETI: MKUTANO MKUU WA CCM WAOTA MBAWA. TAKUKURU KUANZA NA VIGOGO KESI MAHAKAMA YA MAFISADI. JWTZ KORTINI KWA UJANGILI.


Ukawa warudi na bajeti ya JK. Zitto awachokoza tena wabunge. Sakata la Kitilya latinga bungeni. Aua mama kisa mlo. 


Mkutano mkuu maalum wa CCM waota mbawa. Takukuru kuanza na vigogo kesi mahakama ya mafisadi. JWTZ kortini kwa ujangili.

KERI HILSON ATUA NCHINI NIGERIA KWA FINALI ZA MASHINDANO AIRTEL TRACE MUSIC STARS AFRIKA (2)

Mwanamuziki nguli wa nchini Marekani na jaji mkuu wa shindano la Airtel Trace Music Stars, Keri Hilson akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari ulifanyika lagos nchini Nigeria
Mwanamuziki nguli wa nchini Marekani na jaji mkuu wa shindano la Airtel Trace Music Stars, Keri Hilson akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari ulifanyika lagos nchini Nigeria. Akishuhudia ni Mkurugenzi wa Masoko Airtel Afrika, Dia Ezzaoudi
Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika 2015, Nalimi Mayunga akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Lagos nchini Nigeria. 
Mwanamuziki nguli wa nchini Marekani na jaji mkuu wa shindano la Airtel Trace Music Stars, Keri Hilson akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari
Mwanamuziki nguli wa nchini Marekani na jaji mkuu wa shindano la Airtel Trace Music Stars, Keri Hilson akiwa katika picha  pamoja na Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika 2015, Nalimi Mayunga
Wafanyakazi wa Airtel kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika picha pamoja na Mwanamuziki nguli wa nchini Marekani na jaji mkuu wa shindano la Airtel Trace Music Stars, Keri Hilson mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari. Pichani (wa pili kushot) Afisa uhusiano wa Airtel Tanzania , Bi Jane Matinde

Mwanamuziki nguli nchini Marekani, Keri Hilson ameingi nchini Nigeria ili kushiriki  katika shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika linaloshiriksha nchi 9 barani Afrika ambapo Tanzania inawakilishwa na mwanadada Melisa John.

Keri Hilson atashirikiana pamoja na majaji wengine katika kumtafuta mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika kwa mwaka 2016. Ambapo Taji la ushindi wa Airtel Trace Music Stars 2015 linashikiriwa na Nalimi Mayunga kutoka Tanzania

Siku moja baada ya kuwasili , Keri Hilson ameshiriki katika mkutano na waandishi wa habari ambapo alihainisha kuvutiwa kwake na washiriki na kukiri kwamba bara la Afrika lina  vipaji vingi vya muziki na kuwapongeza Airtel na Trace kwa kuanzisha mpango huu wenye lengo la kuinua vipaji na kuwawezesha vijana kuvifikia ndoto zao

“ naamini finali itakuwa na mvuto sana nimekutana na washiriki  na kushuhudia vipaji vya kutosha.  Mambo makuu tutakayoangali wakati wa  fainali ni pamoja na  uwezo wa mshiriki kuweza kutoa burdani , uwezo wa sauti yake na jinsi gani anaweza kutoa burdani kwa mashabiki. Naamini mashindano ya kesho yatakuwa na mvuto nanimejiandaa vyema kufanya kazi na mshiriki atakayeshinda kwa mwaka huu”

Friday, June 10, 2016

SAFARI YANGU YA UTALII AFRIKA YA KUSINI PART ONE.

Tungali ndani ya chombo cha usafiri na mwenyeji wetu hapa Afrika ya kusini ni bibie Fezeka na kushoto kwake mbele yuko mke wangu mupenzi Oliver.
Mitaa ya wenzetu kuelekea Sunnyside nchini Afrika ya Kusini.
Yanayojiri barabarani.
Hii ni moja ya barabara kuelekea eneo la kihistoria nchini Afrika ya Kusini Union Buildings.
Gsengo at the area.
Niliambatana na my wife Oliver ikiwa ni safari ya mapumziko kuadhimisha miaka 10 ya ndoa yetu.
My Queen.
We.
Gsengo.
Here we come again.
Eneo hili la kihistoria hutumiwa pia na wenyeji pamoja na wageni katika zile picha za kumbukumbu kwa maharusi na mahafali mbalimbali.
Maharusi eneo la kihistoria 
Union Buildings.
Kinachoonekana juu ya mnara wa nyuma. 
The Union Buildings (AfrikaansDie Uniegebou) mahala hapa ndipo zilipo ofisi za viongozi wa taifa la Afrika ya Kusini na pia ofisi kuu ya Rais wa nchi hiyo. Mjengo huu uko Pretoria Pretoria, katika kilima cha kitongoji cha mji wa Meintjieskop katika ncha ya kaskazini ya Arcadia, karibu kabisa na kanisa la kihistoria linalojulikana kwa jina la Church Square.
Ni mnara wa sanamu ya Rais wa kwanza Mweusi mzalendo wa taifa la wana wa Afrika ya Kusini Nelson Mandela, mnara wenye urefu wa mita 9 ulioko Pretoria. 
Muonekano wa barabara na majengo ya ofisi pamoja na makazi ya watu kutoka kituo cha usafiri wa reli mji wa Sandton na Marlboro nchini Afrika ya Kusini.
Juu kiduchu.....
Treni ya mizigo.
Makazi ya watu.
Parking ni suala ambalo limezingatiwa kila mji.
Moja ya minara.
Safari kwa njia ya picha bado inaendelea hivyo endelea kutupia jicho lako hapa Gsengo blog kwa pix zaidi na zipate simulizi kupitia Kazi na Ngoma ya 93.7 Jembe Fm Mwanza hadi tutakapofika nyumbani kwa Nelson Mandela.