Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mpaka kifo kinamchukuwa ameacha vita ya wale maadui watatu ambao ni njaa, ujinga, umasikini. Ni miaka 12 sasa tangu alipotutoka nalo Taifa la Tanzania mwaka huu 2011 linakwenda sherehekea miaka yake 50 ya Uhuru likiwa na changamoto za kumwaga mpaka mchafuko wa kichefuchefu kwa kila siku tukibadili santuli za skendo.
Sasa kila mtu anavuna raslimali za taifa hili kadri anavyoweza, daraja kati ya masikini na tajiri linaongezeka urefu, huku masikini akiendelea kutwishwa mzigo wa ugumu ya maisha kila kukicha..... Nani kasema Tanzania ina amani? Watu wametulia tu, wananchi wana njaa, maisha magumu, bidhaa tunazozalisha wenyewe zinauzwa mara tano ya bei inayopaswa na pesa ya ongezeko inaenda kwa ‘mamasta plani’ wachache twawaita 'mafisadi', Amaniiiiii wakati Shida imekuwa wimbo wa taifa, halafu utasema huyo mtu ana amani kweli?
Nenda Mwalimu!, Nenda! Nasema Nenda kwani nahisi kuna jambo laja nami sitaki uweshuhuda ila sijajuwa litakuwa la faraja au huzuni …….
Inshahlah Mwenyezi Mungu ndiye ngome yetu.
Naomba kuwasilisha....!!!