ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 15, 2012

MH MEMBE AITAKIA KILA LA KHERI NA FANAKA CLOUDS MEDIA GROUP KWENYE SHAMRA SHAMRA ZAKE ZA KUTIMIZA MIAKAiza 13

Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano ya Kimataifa,Mh Bernard Membe pichani kulia akiagana na Ofisa Habari wa Clouds Media Group,Simalenga Saimon mapema leo mchana,kwenye viunga vya ofisi hizo zilizopo Mikocheni jijini Dar,Mh Membe alifika kwenye ofisi hizo kwa ajili ya kufanya mahojiano mafupi kuhusiana na mambo mbalimbali yanayoihusu wizara yake sambamba na kuitakia kheri na fanaka kampuni ya Clouds Media Group wakati ikiwa kwenye msimu wa sherehe na shamra shamra zake za kutimiza miaka 13 tangu kuanzishwa kwake.

NI MATAYARISHO YA LEO KUELEKEA SHOW YA KESHO YA MTU MZIMA KOFFI OLOMIDE MWANZA

Mnyama Dugu moja na wadhamini wetu wa show ya Koffi Olomide nchini Tanzania.

Ikiwa leo mpango mzima unasanukishwa ndani ya jiji la Dar upande wa pili lazima kuhakiki ubora wa stage la Mwanza uwanja wa tukio CCM Kirumba mahala ambapo itamwagwa show ya mtu mzima Koffi Olomide hiyo kesho.

Sound injinia wa Prime times Promotion Dee akifanya 'kalukulesheni' ndani ya dimba la CCM Kirumba jioni ya leo.

Muziki, lights na vimbanga vyose....

Mzigo..mpango

Ndani ya radio washirika Passion Fm 91.0 Mwanza mtangazaji Philbert Kabago akiwa na H. Baba na Ua lake pamoja na vijana wawili 'Hatari' katika dance.

Wapo Rock City ahadi kujumuika na wakazi wa Mwanza kushuhudia makali ya kesho jumapili CCM Kirumba na Mopao'

Friday, December 14, 2012

THIS WILL BE PLAYED LIVE TOMORROW AT THAI VILLAGE, MASAKI SO DON'T MISS OUT!

Mapenzi Sumu by Mad Ice
From new EP "Maisha"
Filmed & Directed by Joseph Bitar in Helsinki, Finland July 2011.

DIWANI KATA YA KIPAWA AANZISHA MRADI WA KUWASAIDIA WANAWAKE WA KATA YAKE.

Diwani wa Kata ya Kipawa,Bonnah Kaluwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza Uzinduzi wa Mradi wa Kuwaendeleza Wanawake na Wasichana wa Kata ya Kipawa kuwa Wajasiliamali na wanaoelewa biashara na Taaluma zao,unaofahamika kama WANAMA (Wamama na Maendeleo).Kulia ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Kipawa,Said Fundi.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Dalring Hair,Edward Shilla (kulia) ambao ni wadhamini wa Mafunzo ya Mradi huo wa WANAMA akizungumzia namna walivyoweza kujitokeza kudhamini Mradi huo utakaowawezesha Wanawake na Wasichana wa Kata ya Kipawa kuwa Wajasiliamali na wanaoelewa biashara na Taaluma zao.Kushoto ni Diwani wa Kata ya Kipawa,Bonnah Kaluwa ambaye ndie Mratibu mkuu wa Mradi.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Kipawa,Said Fundi (kushoto) akitoa shukrani kwa wadhamini wa Mradi wa Kuwaendeleza Wanawake na Wasichana wa Kata ya Kipawa kuwa Wajasiliamali na wanaoelewa biashara na Taaluma zao,unaofahamika kama WANAMA (Wamama na Maendeleo) ambao ni Kampuni ya Dalring Hair.Katikati ni Diwani wa Kata ya Kipawa,Bonnah Kaluwa na kulia ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya Dalring Hair,Edward Shilla.

ECO BANK YADHAMINI TAMASHA LA 'TOTO PARTY' LITAKALOFANYIKA CINE CLUB, DAR

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Glitz Entertainment Limited, ambao ni waandaaji wa tamasha la TOTO PARTY, Bw. Dennis Ssebo akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari juu ya tamasha hilo la watoto linalotarajia kufanyika tarehe 25 na 26 Desemba 2012 katika ufukwe wa Cine Club jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Masoko ya ECO Bank Bw. Andrew Lyimo.
Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Masoko ya ECO Bank Bw. Andrew Lyimo (wa kwanza kulia) akiongea kuelezea jinsi benki hiyo ilivyojitoa kudhamini tamasha la TOTO PARTY. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Glitz Entertainment Limited, ambao ni waandaaji wa tamasha la TOTO PARTY, Bw. Dennis Ssebo na Meneja wa Masuala ya Biashara Bw. Adenkule Adewaye.
Meneja wa Masuala ya Biashara Bw. Adenkule Adewaye (wa kwanza kushoto) akielezea machache yanayohusu benki yao.
 ---
Na Mwandishi Wetu
KATIKA kuhakikisha watoto nao wanapata nafasi ya kusheherekea vema sikukuu ya Krismasi vema, kampuni ya Giltz Limited ya jijini Dar es Salaam imeandaa tamasha maalumu kwa ajili kuwaburudisha maarufu kama “Toto Party”.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Glitz Entertainment Limited Bw. Dennis Ssebo alisema tamsaha hilo la Toto Party itafanyika katika ufukwe wa Cine Club uliopo Mikocheni ikiwa ni safari ni mara ya tatu mfululizo kufanywa kwa watoto wa Dar es Salaam.

“ Hii itakuwa ni mara yetu ya tatu kuandaa sherehe hizi kwa ajili ya watoto hapa Dar es Salaam na kwa mara ya kwanza itafanyika mara mbili tofauti na ilivyokuwa imezoeleka kwani sasa itafanyika Krismasi na Boxing Day hapo hapo Cine Club,” alisema Ssebo.

Katika sherehe hizo mbili watoto watapata nafasi ya kushiriki katika michezo mbalimbali kama soka la ufukweni, kuogelea, kusaka hazina (Treasure hunt) na kujipaka rangi usoni (Face painting) na mengine mengi. 

Aidha watoto hao pia wataweza kufunga akaunti ya benki kwa watoto inayojulikana kama ‘Pambazuka’ kupitia benki ya Ecobank.

Mbali na watoto kucheza na kufurahi michezo mbalimbali pia wazazi wao watachuana katika mchezo wa kuvuta kamba ambapo washindi katika michezo hiyo watazawadiwa zawadi mbalimbali na viingilio ni Sh 3,000 kwa watoto na wakubwa Sh 7,000.

Waratibu wa sherehe pia wamebainisha kuwa mwakani mbali na Dar es Salaam, sherehe hizo pia zitafanyika kwenye katika mikoa ya Arusha na Tanga.

KOFFI OLOMIDE NDANI YA SERENA TANZANIA


Mwanamuziki kutoka nchini DRC-Congo,Koffi Olomide akitia saini moja ya bango lenye kampeni inayowatahadharisha madereva wa magari kunywa pombe kupindukia,ikiwa ni hatari kwa afya na usalama wao kwa ujumla,pichani kulia ni Mkurugenzi wa kampuni ya bia ya Serengeti,Bwa.Steve Gannon akishuhudia tukio hilo,aidha katika tukio hilo Wanahabari mbalimbali walishuhudia tukio hilo ndani ya hotel ya Serena Inn mapema leo mchana.Koffi Olomide na skwadi lake la Quartie Latin wametua jana jijini Dar kwa ajili ya maonesho yao mawili yatakayofanyika jijini Dar ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni siku ya jumamosi na jijini Mwanza kwenye uwanja wa CCM-Kirumba siku ya jumapili kwa udhamini mkubwa wa kampuni ya SBL kupitia bia yake ya Tusker Lager.

Bango alilotia wino Koffi Olomide.
Koffi Olomide akitoa vionjo vya moja ya wimbo wake mbele ya wanahabari,kulia kwake ni Mkurugenzi wa Mahusiano Serengeti Breweries,Nandi Mwiyombela akinogesha
Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya SBL,Ephraim Mafuru akiuzumguza mbele ya Wanahabari mapema leo ndani ya hotel ya Serena Inn,kuhusiana na onesho la Mwanamuziki kutoka DRC-Congo,Koffi Olomide linalotarajiwa kufanyika kesho jumamosi kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.

 Baadhi ya wafanyakazi wa SBL wakifurahia jambo 
Mkurugenzi wa Mahusiano Serengeti Breweries,Nandi Mwiyombela akiwakaribisha wageni mbalimbali wakiwemo wanahabari kwenye mkutano uliohusu onesho la Mwanamuziki Koffi Olomide,ambalo limedhaminiwa na kampuni ya SBL kupitia kinywaji chake cha Tusker.
Mwanamuziki kutoka nchini DRC-Congo,Koffi Olomide akifafanua jambo mapema leo alipokuwa akizungumza na wanahabari (hawapo pichani),ndani ya hotel ya Serena kuhusiana na onesho lake atakalolifanya hapo kesho ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Koffi amewaomba washabiki na wapenzi wake waje wajionee kazi kubwa atakayokuwa akiifanya jukwaani akiwa na vipaji vipya kabisa katika tasnia ya muziki wa dansi nchini Congo.
 Mkurugenzi wa kampuni ya bia ya Serengeti,Bwa.Steve Gannon  akimkaribisha Koffi Olomide (hayupo pichani) na pia aliwataka mashabiki na wapenzi wa mwanamuziki huyo wajitokeze kwa wingi na kushuhudia tukio hilo adhimu hapo kesho.


Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akiwashukuru Wadhamini wa onesho la Koffi Olomide pamoja na Wanahabari kwa ushirikiano mkubwa walioutoa katika kuhakikisha jamii inapata taarifa mbalimbali kuhusiana na ujio wa mwanamuziki huyo pamoja na onesho lenyewe.
Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya SBL,Ephraim Mafuru akisalimiana mkono na Mwanamuziki wa Kimataifa Koffi Olomide.

Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga pichani shoto akiwa ameambata na mgeni wake Koffi Olomide sambamba na Mkurugenzi wa SBL,Steve Gannon wakiwasili ndani ya ukumbi wa mikutano,Serena Hotel kwa ajili ya kuzungumza na Wanahabari kuhusiana na onesho litakalofanyika kesho kwenye viwannja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.Picha na Michuzijr.Blogspot.com.

KOFFI OLOMIDE ATUA JIJINI DAR TAYARI KWA MAONESHO YAKE DAR NA MWANZA

Mwanamuziki nyota wa dansi kutoka nchini DRC-Kongo, Koffi Olomide akiwasalimia baadhi ya mashabiki wake waliofika kumlaki usiku huu mara baada ya kuwasili akiwa sambamba na skwadi lake zima la Quartier Latin kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), tayari kwa maonesho yake, la kwanza litafanyika siku ya jumamosi ndani ya viwanja vya Lidaz Club, Kinondoni jijini Dar na jumapili jijini Mwanza ndani ya uwanja wa CCM-Kirumba, Maonesho yote mawili yamedhaminiwa na kampuni ya bia ya Afrika Masharikia (EABL) kupitia kinywaji chake cha Tusker kiingilio kimepangwa kuwa ni shilingi 10,000/= kwa kichwa kama tiketi jijini Dar ikinunuliwa mapema na shilingi 15,000/= getini na kwa jijini Mwanza ni shilingi 5,000/= tu kama zawadi.

Pichani kushoto ni Mwenyeji wake kutoka kampuni ya Prime Time Promotions Ltd, Godfrey Kusaga

Watangazaji wa Clouds FM na Clouds TV pichan shoto ni Millard Ayo na Ben Kinyaiya pichani kulia wakifanya mahojiano mafupi na Mwanamuziki Koffi Olomide mara baada ya kuwasili usiku huu  kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),jijini Dar. Koffi Olomide alitanabaisha kuwa yeye amekuja nchini Tanzania kwa mara nyingine tena kuwaburudisha na kuwaonesha vipaji alivyo navyo sasa ndani ya kundi lake la Quartier Latin.

MAUAJI YA KUTISHA MARA,WATU WAKATWA VISHWA, SERIKALI YADAIWA KUTUMIA WAANDISHI UCHWARA NA WENYE NJAA KUKANUSHA UKATILI HUO


TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HII
Na George Marato,Musoma
Kufuatia mauji ya kinyama na kutisha kuibuka mkoani Mara, hatimaye jeshi la Polisi mkoani humo, limetoa tahadhari kubwa kwa wananchi wa Mkoa huo hasa  Wanawake wa maeneo ya vijijini kuwa makini  wakati wakiwa katika shughuli kilimo na utafutaji wa kuni.

Pamoja na tahadhari hiyo pia wananchi hasa wanawake wameombwa kutoa taarifa polisi pindi tu wanaposhuku kuwepo kwa jambo lolote ambalo linahatarisha maisha yao ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mara SSP Japhet Lusingu,ametoa taadhari hiyo juzi ofisi kwake mjini hapa wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na matukio ya mauji ambayo yameibuka katika siku za hivi karibuni mkoani Mara hasa katika wilaya ya Butiama na Manispaa ya Musoma .

Alisema tayari jeshi la polisi linawashikiria watu sita kuhusiana na mauji ya Sabina Mkireri mkazi wa kijiji cha Kiemba ambaye aliuawa kwa kuchinjwa kisha wauji kuondoka na kichwa chake Desemba tatu mwaka huu.

“Nachukua nafasi hii kuwatoa hofu wananchi kuhusu mauji haya,lakini natoa taadhari kwa wakina mama hasa wa maeneo ya vijijini wanapokuwa katika shughuli za kilimo na utafutaji wa kuni wawe waangalifu na watoe taarifa mapema pindi tu wanaposhuku kuwapo kwa jambo lolote lisilo la kawaida”alisema kaimu kamanda huyo ambaye pia ni afisa mnadhimu wa jeshi la polisi mkoa wa Mara.

Aidha alisema Desemba mbili mwaka huu majira ya saa moja usiku Brandina Peru alikutwa polini akiwa amekufa baada ya kuchinjwa.

Kaimu kamanda huyo wa polisi mkoa wa Mara,alisema marehemu kabla ya kuuawa kikatili aliondoka nyumbani kwake desemba mosi mwaka huu akiwa peke yake kwenda porini kukata kuni na hakuweza kurudi nyumbani hadi alipokutwa amekufa kwa kuchinjwa.

Hata hivyo alisema kabla ya kuchinjwa wauaji hao walimvua nguo zote na kuweka kando kisha kumbaka na kwamba hakuna mtu yoyote aliyekamatwa hadi sasa na chanzo cha tukio bado kinachunguzwa.

Kwa sababu hiyo alisema jeshi la polisi limejipanga kikamilifu kwaajili ya kuwasaka watu wanahusika na vitendo hivyo huku akiwaamba waandishi wa habari na viongozi wa kisiasa kutowatia hofu wananchi kwa kutoa taarifa bila kuthibitishwa na vyombo vya dola.

Kuhusu taarifa za viungo hivyo vya binadamu kutumika kwa imani potofu kwa shughuli za uchimbaji wa madini na uvuvi wa samaki alisema jeshi hilo linachunguza ukweli wa taarifa hizo.

Wakati huo huo,kamanda Lusingu,alisema mwanafunzi mmoja Hamis Lazaro wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Etaro ameuawa kwa kushambuliwa,mawe na kukatwakatwa na mapanga katika sehemu mbalimbali za mwili wake.

Alisema tukio hilo lilitokea saa 11.30 katika kijiji cha Kwikerege kata ya Etaro wilaya Butiama baada ya kukutwa chini ya uvungu wa kitanda kilichokuwa kikitumiwa na Nyakongo Nyangata ambaye alikuwa na mahusiano ya kimapenzi.

Hata hivyo kamanda huyo alisema mbali na madai ya marehemu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi huyo mwenzake lakini wananchi walijichukulia sheria mkononi baada ya kuisi kuwa ni miongoni mwa watu ambao wamekuwa wakishiriki katika vitendo vya mauji ya kinyama katika eneo hilo.


UCHUNGUZI
 SAKATA la mauji ya kinyama mkoani Mara,imani za kishirikina ni moja ya sababu kubwa ambazo zimetajwa kuwa chanzo kikuu cha mauji hayo ambayo yameibuka kwa kasi kubwa katika mkoa huu hasa kwa wilaya za Butiama na Musoma mjini huku wauaji wakichukua baadhi ya viungo vya binadamu kwa madai ya kusadia shughuli za uvuvi wa samaki na uchimbaji wa dhahabu.

Imedaiwa kuwa wauji hao wengi wamekuwa wakitoka mkoa wa Kigoma wakiwa ni wenyeji wa nchi jirani ya Congo ambao wamekuwa wakishirikiana na wenyeji katika maeneo hayo kisha kufanya mipango ya mauji hayo ya kinyama.

Baadhi ya wavuvi na wachimbaji wadogo wa madini,wamedai kuwa wauji hao wamekuwa wakiuza vichwa vya watu kwa imani za kishirikina kwaajili ya shughuli za uchimbaji wa dhahabu huku ndimi,matiti na sehemu za siri vikitumika kwaajili ya uvuvi katika ziwa Victoria.

Aidha imedaiwa kuwa baadhi ya Mangariba pia kutoka eneo la Tarime na Kiagata wamekuwa wakiwauzia wavuvi viungo vya mwanamke baada ya kuwakeketa jambo ambalo limetajwa kuwa chazo cha kusababisha wimbi la mauji ya watoto wa kike ambao wamekuwa wakiuawa kisha kunyofolewa viungo hivyo yakiwemo na matiti.

Hata hivyo baadhi ya wavuvi ambao wameomba kuhifadhiwa majina yao kutoka visiwa ndani ya ziwa victoria wakizungumza kwa njia ya simu na Nipashe Jumapili kwa nyakati tofauti,wamedai kuwa pamoja na matajiri wao kununua viungo hivyo kutoka kwa baadhi ya watu lakini hakuna mabadiliko yoyote ambayo wamekuwa wakiyapata.

“Kweli kuna wakati watu wanakuja eti ni waganga kisha wanakwenda ziwani usiku na matajiri na mwakilishi wa wavuvi kwa kila mtumbwi ili  kuonyesha nyavu zilipo wakifika wanachukua vitu kama nyama wanasugua kila mwesho wa nyavu lakini hatujawahi kuona mabadiliko ya kuongeza samaki”alisema mmoja ya wavuvi.

Wavuvi hao waliongeza kuwa watu hao wanaoisi kuwa ni waganga wamekuwa wakiwazuia kuongea kitu chochote wakati wa zoezi la kufanya mitambiko hiyo huku wao wakizungumza lugha na maneno wasio yaelewa hadi zoezi hilo linapo malizika.

Walipohojiwa ni kwanini wanashindwa kutoa taarifa hizo kwa vyombo vya dola wavuvi hao walidai kuwa wanashindwa kufanya hivyo kwa kuhofia maisha yao kwa vile wamiliki wengi wa zana hizo za uvuvi wana mahusiano makubwa na baadhi ya maafisa ambao wako katika vyombo vya dola.

Hata hivyo wachimbaji hao wa dhahabu wameshindwa kuwa wazi kila walipoulizwa ili kuthibitisha viungo hasa vichwa vya binadam vimekuwa vikitumika wakati gani na kwa maeneo yapi.

Kwa upande wake mbunge wa Musoma vijijini Nimrod Mkono,pamoja na kutoa pole kwa wote ambao wamekumbwa na janga hilo,lakini alisema jeshi la polisi linapaswa kuwachunguza wanasiasa kwani alisema wakati mwingine wamekuwa wakishiriki katika ushirikina huo kwaajili ya kujipatia fedha.

“Hali hii inatisha inawezekana vitu hivi vikatumika kwa ushirikina katika madini na uvuvi lakini miongoni mwetu wanasiasa ni vyema tukachunguzwa kwani wengini hawamuogopi mungu wanaweza kufanya mchezo huo mchafu kwaajili ya kupatafuta pesa za uchaguzi na wengine kufanyia mitambiko ya biashara zao”alisema Mkono kwa njia ya simu na kuongeza

“Hilo ni jambo kubwa haiwezekani mtu wa kawaida tu akaenda kumchinja mtu na kuondoka na kichwa chake bila ya kuwapo kwa mkono wa watu wenye uwezo,hivyo ni vyema jeshi la polisi likafanya uchunguzi wa kina kuhusu hali hii”alisema.

Juzi mbunge Musoma mjini Vicent Nyerere(Chadema) alimtaka mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP)Said Mwema kuchukua hatua sasa kuhusu mauji mauji ya kikatili ambavyo yameibuka katika Manispaa ya Musoma na wilaya ya Butiama.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu alisema katika kipindi cha mwezi mmoja tu zaidi ya watu kumi na saba wameuawa huku wengine wakichinjwa kicha waujia kuondoka na vichwa na viungo vyao vingine vya miili yao.

Alisema pamoja na hali hiyo ambayo imechangia hofu kubwa kwa wananchi lakini hakuna jitihada zozote zinazochukuwa kwaajili ya kukabiliana na vitendo hivyo vya kinyama.

Aidha mbunge huyo alimtaka pia Rais Jakaya Kikwete kuchukua hatua kwa wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama wa wilaya hizo ambao amedai baadhi yao wameshindwa kusimamia majukumu yao na kubaki kuendesha siasa wakati wananchi wakizidi kuawa kinyama na wengine kuachwa na vilema vya maisha.

“Ni tatizo kubwa ndani ya mwezi mmoja tu watu kumi na saba wameuawa kinyama na wengine kuchinjwa lakini mbali na vyombo vya dola kukaa kimya hata nyinyi waandishi mmeshindwa kujulisha umma kuhusu ukatili huu”alisema Nyerere na kuongeza.

“Rais mtoe mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya(DC) hapo Musoma amekalia siasa na kuacha majukumui ya serikali katika kulinda raia na mali zao hii ni hatari kubwa”aliongeza.

Hata hivyo wakati mbunge huyo akitoa kauli hiyo,mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Butiama Angelina Mabula,ameliagiza jeshi la polisi kufanya kazi usiku na mchana katika kuhakikisha linawatia mbaloni watu wote ambao wanahusika na mauji ya kikatili ya raia.

Mabula ambaye ni mkuu wa wilaya ya Butiama,alitoa agizo hilo juzi jioni baada ya kuokotwa kwa mama mmoja Sabina Mkereri (46)ambaye alichinjwa na wauji kuondoka na kichwa chake katika kijiji cha Kabegi kata kata ya Nyakatende.

“Nawaomba wananchi mtoe ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha wahusika wote wanasakwa na kuanzia sasa naagiza kuanza kwa vikundi vya ulinzi shirikishi kwaajili ya kufanya kazi ya kuwasaka watu hawa usiku na mchana…jamani tunaipeleka wapi Tanzania yetu yenye amani kwa kufanya matendo haya ya kinyama”alisema DC Mabula.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mara SSP Japhet Lusingu,akizungumza na gazeti hili pamoja na kukiri baadhi ya watu kuchinjwa na viungo vyao kuchukuliwa lakini alisema idadi inayotajwa si sahihi.

Alisema tayari jeshi la polisi limechukua hatua mbalimbali za kukabiliana na vitendo hivyo vya kinyama huku akisema jeshi lake linachunguza kuhusu viungo hivyo kutumika kwa shughuli za uvuvi na ushirikiana.

Hata hivyo aliwaomba waandishi na viongozi wa siasa kuacha kutoa taarifa ambazo si sahihi bila kuthibitishwa na jeshi hilo ili kutowaweka katika hali ya hofu wananchi. 

Thursday, December 13, 2012

AIRTEL YALETA KINGINE CHA KWANZA KUPOKEA SIMU BILA GHARAMA YOYOTE INDIA

Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Bw Sam Elanagaloor akielezea huduma ya 'One network' kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)ambapo leo airtel imezidua huduma itakayowaweze wateja wa airtel wanaosafiri kwenda India, Srilanka na Bangladesh kusafiri na laini zao za Airtel Tanzania na watafaidi kupokea simu bila malipo yoyote na kufurahia kupiga simu kwa viwango nafuu zaidi wakiwa katika shughuli zao za kusherehekea kumaliza mwaka, biashara au matibabu (leo) katika ofisi kuu ya Airtel Tanzania




Airtel  yaleta kingine cha kwanza kupokea simu bila gharama yoyote  India
*       Wateja wa Airtel kupokea simu bure wakiwa nchini India
*       Huduma hii pia itapatikana  Srilanka and Bangladesh

Jumatano 12 Desemba 2012, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel katika msimu huu wa sikukuu imewawezesha wateja wote nchini kuendelea kutumia laini zao za Airtel Tanzania wakiwa India na kufurahia kupokea simu bila makato yeyote  na kuwahakikishia uhuru wa kuongea wakati wa msimu huu wa sikukuu.
Akitoa ufafanuzi juu ya huduma hii ijulikanayo kama "One Network Asia" Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bw Sam Elanagaloor alisema" wateja wetu kutoka Tanzania wanaosafiri kwenda India, Srilanka na Bangladesh wataweza kusafiri na laini zao za Airtel Tanzania na watafaidi kupokea simu bila malipo yoyote na kufurahia kupiga simu kwa viwango nafuu zaidi wakiwa katika shughuli zao za kusherehekea kumaliza mwaka au biashara
"Tunafahamu kuna watanzania wengi wanapata matibabu nchini India, kuna watanzania wengi wanasoma nchini India, Tunaamini kwa kupitia huduma hii tutawawezesha watanzania wengi wanaotembelea na wale wenye ndugu nchini India kuwasiliana bila gharama yeyote sio tu katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu ila na siku za usoni.  Mteja anachotakiwa kufanya ni kuongeza muda wa maongezi kwenye laini yake ya Airtel Tanzania na kufurahia huduma za Airtel" aliongeza Elangalloor.
Mbali na kuzinduliwa kwa huduma hii inayota unafuu kwa wateja wa Airtel watakaofanya safari zao kwenda India Srilanka na Bangladesh, wateja wa Airtel wote pia wataendelea kufurahia huduma huduma ya 'One network' (kutumia laini zao za nyumbani)  katika nchi 17 za Afrika ikiwemo: Kenya, Uganda, Malawi, DRC, CongoB, Madagascar, Nigeria, Ghana, Rwanda, Zambia, Niger, Gabon, Burkina, Sierra L,Chad, Tanzania
"Hili ni la uhakika kabisa  kwa kuwa mtandao wetu ni mpana, wateja wa Airtel wanaposafiri kwenye nchi hizo wanaunganishwa na kupiga simu kwa bei nafuu, kuongeza salio kwa kutumia vocha za nchi walizotoka wakiwa popote, pamoja na kuunganishwa na huduma ya internet" alimaliza kwa kusema Elangalloor
Mwisho

"HONGERA WAHITIMU LAKINI?"

Kila msimu BODI ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini pamoja na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) hupokea maelfu ya majina ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu wanao omba mikopo, na kila msimu wa mwaka wanafunzi maelfu wanahitimu... Kuhitimu ni mwanzo wa kulipa madeni...
Jeh ndoto zitafikiwa?

Wednesday, December 12, 2012

MBIO ZA SERENGETI MARATHON 2012 ZAFANA MKOANI SIMIYU

Mshindi wa kwanza wa Serengeti marathon 2012 Dickson Marwa kutoka mkoani Mara, akihitimisha ukimbiaji mbio za nyika mita 21 zilizofanyika jana kwenye mbuga za Serengeti mkoani Simiyu.

Mashindano hato ya kwanza yamevuka malengo kutoka washiriki 80 waliojiandikisha awali hadi kufikia washiriki 207 waliojitokeza mapema asubuhi kabla ya mbio hizo kuanza kutimua vumbi.

Big up sana kwa Mshiriki mwenye ulemavu wa mkono mmoja Edward Joseph aliyemaliza mbio hizo kwa upande wa wanaume akiwa nafasi ya 14.

Mshindi wa kwanza wa Serengeti marathon 2012 Dickson Marwa kutoka mkoani Mara akiwa ameshikilia medali yake ya dhahabu na fedha kiasi cha shilingi laki 5 alichonyakuwa kwenye mbio za kwanza za nyika za Serengeti Marathon.

Hawa ndiyo washindi kumi wa kumi bora upande wa wanaume ukimbiaji mbio za nyika mita 21 zilizofanyika jana kwenye mbuga za Serengeti mkoani Simiyu, mbele ni mshindi wa kumi akifuatia wa tisa hadi wa kwanza nyuma, wakiwa kwenye mstari kwaajili ya kutunukishwa zawadi zao.

Wakuu mbalimbali waliohudhuria michuano ya kwanza ya Serengeti Marathon.

Mshindi wa kwanza wanawake katika Serengeti marathon 2012 Failuna Mohamed kutoka mkoani Arumeru akiwa ameshikilia medali yake ya dhahabu na fedha kiasi cha shilingi laki 5 alichonyakuwa kwenye mbio za kwanza za nyika za Serengeti Marathon.

Maafisa wanyamapori kutoka mbuga ya hifadhi ya taifa ya Serengeti wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati wa utoaji wa zawadi kwa watimua vumbi wa mbio hizo, hawa ndio waliosimamia zoezi la kuhakikisha barabara ni salama kwa wakimbiaji  ili wasishambuliwe na wanyama wakali.

Dr. Mtiro akitoa Huduma ya Kwanza kwa moja ya washiriki wa mbio hizo mara baada ya kumalizika kwa mashindano. 

Vitita na Medali mezani kabla ya kumilikishwa kwa washindi....

Serebuka ya wafukuza upepo.

Mkuu wa wilaya ya Busega Paul Mzindakaya (katikati) akipata picha ya pamoja na washindi watatu watatu kutoka kwa kila pande, Kutoka kushoto ni Ndege Stephen (Nyamagana Mwanza) aliyeshika No. 3, Said Makula (Arumeru ) aliyeshika No. 2 na Dickson Marwa (Mara) mshindi nafasi ya kwanza, Upande wa pili baada ya mweshimiwa ni mwanadada Failuna Mohamed (Arumeru) aliyeshika nafasi ya kwanza wanawake, Grace Jackson (Bariadi mkoani Simiyu) No. 2 na Neema Mathius (Magu mkoani Mwanza) No. 3. 

ALLIANCE MWANZA YATWAA UBINGWA WA AFRIKA MASHARIKI ACADEMY

Alliance Academy ya jijini mwanza imeweza kujinyakulia vikombe viwili vya vijana chini ya miaka 12 na 14 pamoja na medali mbili za wafungaji bora kati ya michuano ya Afrika Mashariki ya Academy (nyumba ya vipaji) iliyokuwa ikitimua vumbi jijini Arusha. 

michuano hiyo iliyodumu kwa siku tatu tangu Disemba 7 na kukamilika Disemba 9 mwaka huu iliandaliwa na Academy ya features ya jijiji Arusha na kushirikisha nchi za Kenya, Uganda, Burundi, Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo ambao ni waalikwa pamoja na Tanzania ambao ni wenyeji.

Akizungumza mara baada ya kuwasili, katibu wa Alliance, Kessy mziray alisema ushindi wao ulitokana na kuzifunga timu za Burka mabao 3-0, Mambas ya uganda mabao 2-0, Olduvai ya Arusha mabao 3-0 na kufanikiwa kuingia fainali na Stars waliowakamua mabao 3-0 kwa vijana wenye umri chini ya miaka 14.

Mziray aliongeza kuwa kwa upande wa vijana wenye umri chini ya miaka 12 waliweza kuzifunga timu za Tacoda mabao 6-0, Olduvai ya Kenya mabao 2-0 na kufanikiwa kuingia fainali na Younglife  waliyoibanjua bao 1-0, hivyo kuibuka washindi wa michuano hiyo.


CORAL BEACH MASAKI HAPATOSHI JUMAMOSI HII!!



CORAL BEACH MASAKI HAPATOSHI JUMAMOSI HII!!
Karibu kwenye Wine testingya WINE 25 za Distell, kuanzia saa tisa jioni hadi saa moja na nusu usiku, Kiingilio kinahusisha Bites Na Snacks pia! Kuletewa ticket piga simu…. 0717 03 66 40.

KABLA YA MWAKA HAUJAISHA MJUE MBUNIFU HUYU


Salim Ali ndiye huyoo (kulia) akitambulishwa na mwanamitindo Ritcha Adhia.


Name is Salim Ali, a Tanzanian fashion designer designer based in Dar-es-salaam, My whose been involved in the fashion industry for a couple of years now, i love art in different forms, music,fashion,dance, and etc, i was inspired to join the industry after seeing the amount of potentials our country has, and the rise of
more African designers so i decided to put in my touch so as to add
more flavour  in the industry.

I am happy and proud to have released four collections since i started, which is a very big achievement for me as a young man, my last collection “MNG’AO” was a success because the response i got from people was great, though it’s hard work but it still kept me going and managed to come up with another collection this year known as “Brown Sugar” which i managed to showcase at the Swahili fashion week festival which  happened on the 6th of December to 8th.  

Brown sugar stands for the  proud African brown skin which stands for hard work,
resilience, happiness and success,  embracing the African style and charm.

Thanks to the almighty Allah i have managed to achieve a couple of things this year, by dressing up alot of  big names in the industry, either for their shows, or video roles.

Very happy to have received an award as the best upcoming dBrown sugar stands for the  proud African brown skin which stands for hard work, resilience, happiness
and success, embracing the African style and charm.

Designer  of the year in the lady in red  Fashion show , with that it was more like a platform for me to step up my game and work harder so as to achieve more in life.  INSHALLAH