|
Rais Ngowi akihutubia katika mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa BNSC |
Serikali ya Botswana
imeahidi kushirikiana na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) katika program
yake ya “Utalii wa Michezo” na kuifanya nchi hiyo kuwa moja ya mataifa
yanayong’ara kwenye medani ya masumbwi katika bara la Afrika. Ahadi hiyo
ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Michezo la Botswana bwana Persy
Raditladi alipofanya mazungumzo na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya
Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi katika ofisi za BNSC leo.
|
Rais Ngowi akiwa amesimama na Mkurugenzi Mtendaji wa BNSC bwana Persy Raditladi |
Rais Ngowi yuko nchini
Botswana kuutangaza mkanda wa ubingwa wa ngumi wa kimataifa ambao utashindaniwa
tarehe 5 July nchini Namibia kati
ya bondia wa Botswana Lesley Sekotswe na bondia kutoka Namibia Immanuel
Naidjala. Wawili hao walitoka sare katika mpambano wa kukata na shoka wa
kugombania mkanda huo tarehe 20 Machi mwaka huu katika jiji la Windhoek, nchini
Namibia.
Serikali ya Botswana
imeahidi kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa programu ya “Utalii wa
Micheazo ya IBF” inanufaisha nchi hii yenye vivutio kadhaa vya kitalii likiwamo
bonde la maarufu la “Okavango Delta”
Katika mazungumzo yao Rais Ngowi alieleza jinsi IBF
inavyozinufaisha nchi ambazo zimeingia katika programu hii na namna mabondia
wanaotoka katika nchi hizi wanavyonufaika na viwango vya kimataifa vya IBF.
Ngowi aliielezea Botswana kama nchi yenye neema ya vipaji vya mabondia wazuri
wa ridhaa na kuwashauri kuwa waweke mikakati ya mabondia wa ridhaa wanavyoweza
kujiunga na ngumni za kulipwa ili waweze kufaika na vipaji vyao.
Nchi ya Botswana ni moja
kati ya nchi zenye mabondia wazuri katika ngumi za ridhaa lakini kumekuweko na
pengo la kuwaendeleza wanapofikia kustaafu na kutokuwa na uwazi wa namna ya
kujiunga na ngumi za kulipwa. Ujio wa Rais wa IBF Afrika nchini Botswana
umefanyika wakati nchi hii inapokabiliwa na sintofahamu juu ya kuwaendeleza
mabondia wake wanapostaafu ngumi za ridhaa.
Mazungumzo ya Rais Ngowi na serikali ya Botswana yalitanguliwa na
mkutano wa waandishi wa habari pamoja na wadau kadhaa wa ngumi za kulipwa
uliofanyika katika ukumbi wa BNSC jijini Gaborone Botswana leo. Katika mkutano
huo Rasi Ngowi aliuonyesha mkanda wa IBF wa kimataifa katika uzito wa bantam utakaoshindaniwa
kati ya bondia wa Botswana Lesley Sekotswe na bondia kutoka Namibia Immanuel
Naidjala tarehe 5 July mwaka huu jijini Windhoek, Namibia.
Rais Ngowi aliwahakikishia wadau wa ngumi wa Botswana kuwa IBF
itafanya kila liwezalo kuhakikisha kuwa Botswana imejenga msingi mzuri wa ngumi
za kulipwa na kutumia vipaji vilivyonavyo katika ngumi za ridhaa. Rais Ngowi
aliondoka leo kwenda nchini Afrika ya Kusini ambako atakutana na wadau wa ngumi
na kutangaza mapambano kadhaa ya IBF yanayotarajiwa kufanyika nchini humo
kuanzia mwezi ujao!