ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 7, 2012

UTALII JIMBO LA BUSEGA EH BANA WACHA TU!!

Sun set eneo tulivu.

Kutoka mbali moja ya hotel itakuelekeza macho yako kuona eneo hili la mbuga ya hifadhi...

Mbuni sawia kwenye hifadhi.

Mh. Mbunge Dk. Kamani wa jimbo la Busega eneo lililo na hifadhi hii ya Taifa.

Kila mmoja ana jukumu la kutangaza Utalii wa ndani wa nchi hii.


Makaribisho ya asubuhi na mapema.

Si wageni tu bali hata wenyeji hudhuru vivutio vya utalii jimbo la Busega linalopakana na mbuga mashuhuri ya Serengeti.

Swala.

Huwa nawachanganya majina wanyama hawa .... wengine huwaita Tumbili, wengine Nyani, wengine Kima na majina mengiiii.....

Sekta nzima ya Utalii jimbo la Busega imelenga.
1.Kuunganisha waendesha biashara ya utalii katika mkoa wa Mwanza ili kuweza kulitangaza eneo la ukanda huu kwa pamoja.
2.Kuongeza utangazaji wa utalii katika mwambao wa ziwa Victoria ili kuongeza biashara ya utalii katika eneo lililopo jimboni.
3.Kuvutia uwekezaji wa mahoteli katika mwambao wa ziwa Victoria na pembeni mwa vilima jimboni, na kuhamasisha michezo ya majina na meli za starehe.
4.Kubainisha mambo ya kale na shughuli za kiutamaduni zilizopo jimboni zinazofaa kutumika kama kivutio cha utalii.
5.Kufundisha wananchi ili waweze kushiriki katika biashara ya utalii.

WASIRA KUSIMAMIA HARAMBEE SHULE ALIYOSOMA WAZIRI MKUU MSTAAFU JOSEPH SINDE WARIOBA

Bw. Makongoro Mratibu wa mfuko huo.

HARAMBEE YA KUTUNISHA MFUKO WA MAENDELEO YA ELIMU KATA YA NYAMSWA ITAFANYIKA TAREHE 08,JAN 2012 KATIKA SHULE YA MSINGI IKIZU SHULE ALIYOSOMA WAZIRI MKUU MSTAAFU JAJI JOSEPH SINDE WARIOBA .

MGENI RASMI KATIKA HAFLA HIYO NI WAZIRI KATIKA OFISI YA RAIS MAHUSIANO MH. STEVEN WASSIRA - MBUNGE WA BUNDA.

WABUNGE WOTE WA MKOA WA MARA PIA WATAKUWEPO NA WAGENI WENGINE MAARUFU KAMA MAKAMU MKUU WA CHUO SAUT DK KITIMA, MENEJA WA PPF KANDA YA ZIWA NDG. MESHACK BANDAWE NA WENGINE WENGI.

Taarifa na mratibu wa mfuko huo
Bwana Makongoro.

Friday, January 6, 2012

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUFUNGULIWA KESI

MWANASHERIA wa kujitegemea wa jinini Mwanza Stephen Magaigwa amekusudia kufikisha hati yake ya mashitaka kuwafungulia kesi Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Mahakama kuu Maalum ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na wanasheria hao kuruhusu makosa muhimu manne yanayokinzana yaliyomo katika katiba ya Jamhuri na ile ya Mapinduzi.Mwanasheria Stephen Magaigwa.
Amesema kuwa Kupitia marekebisho ya katiba ya mwaka 1977 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Zanzibar ya mwaka 1984 tangu nchi hizi mbili zilipoungana kuna mambo walikubaliana kwamba haya ni ya Muungano lakini yamekiukwa kupitia marekebisho yaliyofanywa ya katiba ya Zanzibar.

"Baada ya kutumia taaluma yangu kifungu baada ya kifungu nimegundua kuwa marekebisho hayo yameingilia mambo ya Muungano na kuleta mkinzano au mkanganyiko katika shughuli za kila siku za utendaji wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania".

"Nilitegemea kuwa wanasheria wa serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wangechukuwa hatuwa maalum kurekebisha hali hii tangu awali kabla ya kuipeleka katika utekelezaji lakini walikaa kimya kama wataalamu wa sheria wasiojuwa kazi yao.
Mambo manne aliyogundua"
Mbele ya wandishi wa habari.
1.Haki za binadamu:- "Katika marekebisho ya katiba ya Zanzibar suala la Haki za Binadamu katiba hiyo imezua kwamba haliwezi kuja katika Mahakama ya Rufaa –Wakati Ukisoma katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jedwali la 1 unagundua kuwa suala la Mahakama ya Rufaa ni suala la Muungano"

"Lakini Haitoshi linapokuja suala la haki za binadamu nchi inayohusika ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"
2.Ukisoma Marekebisho ya Katiba ya Zanzibar kifungu cha 2A Rais wa Zanzibar anaweza akaigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengine kadri atakavyojisikia – Lakini kifungu cha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2(2) Suala la Mipaka ya nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni suala la Muungano hivyo Rais akitaka kuigawa sehemu ya Jamhuri ya Muungano (Tz bara na Tz visiwani) ni lazima awasiliane na Rais wa Zanzibar  Lakini ya Zanzibar inasema anaweza kugawa bila kuwasiliana na Rais wa Tanzania, sasa tuna nchi moja ambayo imeungana kwenye mipaka lakini watu wawili wanaohusika kuigawa.

3.Majeshi ya Ulinzi:- "Katiba ya Jamhuri inasema kuwa nchi pekee ambayo imepewa mamlaka ya kuunda majeshi ya ulinzi au vikosi vya aina yeyote ile ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lakini Marekebisho ya kumi ya sheria namba 9 ya mwaka 2010 ya katiba ya Zanzibar yanasema sasa wanaweza kuunda vikosi kama KMKM na kadhalika … Swali ni nani Amri Jeshi Mkuu wa majeshi hayo? Kwani yanapoundwa lazima yawe na mtoa amri wake mkuu"
Katiba zinazokinzana.
4.Wakuu wa nchi wawili:- "Ukisoma katiba ya Zanzibar 26(1) na ile ya Muungano kifungu cha 33(2) utagundua kuwa sasa tuna wakuu wa nchi wawili, sasa tunapokuwa na wakuu wawili ile hali katika katiba hatua ruksa ya kuwa na ‘two head of state in one country’ hali hii inamaanisha nini?" "Nimefungua kesi hii Mwanza kwa mujibu wa Kifungu cha katiba ya Jamhuri 126-127 na 128, hivyo shauri langu litakapo sajiliwa na kupatiwa hati ya Mashitaka, Rais atapewa taarifa kuteuwa majaji wa kusikiliza kesi hii maalum ya katiba kwenye mahakama maalum ya katiba"

Lengo kuu:- Nitaomba Mahakama hiyo iamuru katiba ya Zanzibar irekebishwe kuondoa kasoro hizo haraka iwezekanavyo ili kuleta sifa ya Muungano.

NDIKILO AFUKUNYUA UPOTOSHAJI ULIOKITHIRI TAARIFA ZA FEDHA MKOANI MWANZA

MKUU wa Mkoa wa Mwanza Evalist Ndikilo amewaagiza wakurungenzi wote mkoani hapa kuwawajibisha kisheria maafisa watendaji wote wa vijiji wanalioshindwa kutoa taarifa za mapato na matumizi katika sehemu zao za kazi. Ndikilo ametoa agizo hilo katika kikao cha kamati cha ushauri mkoa kilichofanyika leo katika ukumbi wa chuo kikuu cha benki kufuati uzembe unaofanywa na watendaji hao wa kutokutoa taarifa kila baada ya miezi mitatu na badala yake wanatoa mwishoni wa mwaka tena kwa viwango hafifu.

Amesema kuwa watendaji wote wanafanya kazi kwa kutokana na sheria zilizowekwa, kwa wale walioshindwa kuwajibika wachukuliwe hatua kulingana na taratibu na sheria.


Dorice Mwanyika Katibu Tawala Jiji la Mwanza akitoa ufafanuzi.

Mbunge wa jimbo la Busega mh. Titus Kamani ni mmoja kati ya waliohudhuria kikao hicho.

Kuhusu majibu yanayotolewa kuwa wananchi hawahudhurii mikutano ya adhara kwa ajili ya kupokea taarifa za mapato na matumizi, mkuu huyo amesema kuwa hizo sio hoja ya msingi na kama wananchi wameshindwa kuhudhuria vikao hivyo ni wazi kuwa watendaji hao wameshindwa kutawala.

Aidha Ndikilo ametoa onyo kwa watendaji wote kuanzia leo kubandika taarifa hizo kwenye vibao vya matangazo na ameahidi kufanya ukaguzi wa taarifa hizo kwa vijiji vyote kupitia ziara yake anayotegemea kuifanya hivi karibuni.

Wakuu kutoka idara mbalimbali kikaoni.

Pia mkuu huyo amewaonya na kuahidi kuwachukulia hatua watu binafsi, vikundi, wanasiasa na wale wote watakaokwamisha zoezi hilo pamoja na ukusanyaji michango muhimu ya maendeleo kwa sababu zao binafsi.

Joyce Masunga Katibu mpya wa CCM Mkoa wa Mwanza aliyechukuwa nafasi ya Alhaji Mwangi Rajab Kundya aliyehamishiwa jimbo la Mjini Magharibi.

Wajumbe wa kikao.

Kwa ujumla ya halmashauri nyingi za mkoa wa Mwanza zimeshindwa kuwasilisha taarifa zake za mapato na matumizi.

Thursday, January 5, 2012

KUANZIA LEO HARAMU MWANAUME KUUZA CHUPI NCHINI SAUDIA

Sheria mpya inayowapiga marufuku wanaume kuuza nguo za ndani za wanawake kama vile chupi na sidiria inaanza kutekelezwa hii leo nchini Saudi Arabia.

Wanaharakati wa kike katika Ufalme huo wa kiislamu wanatumai kuwa agizo hilo lililotolewa na mfalme Abdulla mwaka wa 2006, utamaliza mfadhaiko ulipo wakati wanawake wanauziwa nguo zao za wasaidizi wanaume madukani.

Ajira kwa wanawake
Hatua hiyo itawapa fursa adimu zaidi ya wanawake 40,000 kuchukua nafasi za kazi zitakazoaachwa wazi.

Maafisa wa kidini wasiopendelea mabadiliko wamepinga vikali hatua hiyo ya wanawake kufanya kazi nje ya nyumba zao.

Serikali imepanga kupeleka waangalizi katika vituo vya biashara kote nchini kuhakikisha kwamba wasaidizi wanawake madukani hawabughudhiwi na maafisa wa polisi wa kidini.

MABONDIA WA KLABU YA AMANA WAENDELEA KUJIFUA KWA MAPAMBANO YAJAYO MWISHONI MWA MWEZI.

Baadhi ya mabondia wakifanya mazoezi katika klabu ya Amana CCM jijini Dar es salaam jana kwa ajili ya mashindano mbalimbali yatakayowakabili mwishoni mwa mwezi huu. (Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

TAFAKARI YA LEO.......

Ukishindwa nipe mji.....

Wednesday, January 4, 2012

BREAKING NEWS: HAMAD RASHID ATIMULIWA CUF

Hamad Rashid na wenzie wame- timuliwa uanachama kwa chama cha Wananchi CUF, hivyo kiongozi huyo mahiri mwenye ushawishi mkubwa ndani ya chama kukosa sifa za kuendelea kuwa Mbunge wa chama hicho kwa jimbo la Wawi.

Hivi karibuni Mbunge huyo alifika kwenye Kata ya Manzese jijini Dar es salaam ili kufanya mkutano na wanachama lakini ghafla watu wanaodaiwa kutoka makao makuu ya chama hicho, walifika Manzese na kufanya vurugu wakizuia asifanye mkutano.

Wachunguzi wa karibu wa sakata hili na chanzo cha kutemwa kwa Hamad Rashid, wananyetisha kuwa hili limetokea kutokana na kumekuwepo kwa malumbano ya sera na madaraka baina ya Maalim Seif na Hamad ambaye alitangaza hadharani kwamba atawania nafasi ya Katibu Mkuu wa CUF inayoshikiliwa na Maalim Seif.

Nia ya Hamad kuwania nafasi hiyo imeonyesha dhahiri kumtikisa Maalim Seif ambaye kwa siku za hivi karibuni alinukuliwa akijibu kauli hiyo kwa kusema kama ana ubavu asubiri uchaguzi.

Jeh! picha litaendeleaje...?

YOUSSOU N'DOUR ATANGAZA KUWANIA UPREZIDA'H

Mwanamuziki mashuhuri nchini Senegal na mwanaharakati wa kisiasa,Youssou N'dour, ametangaza kuwa atawania kiti cha urais katika uchaguzi wa mwezi Februari nchini humo. Mwanamuziki huyo amesema kuwa anaitikia wito wa kumtaka agombee kiti hicho dhidi ya rais wa sasa Abdoulaye Wade, ambaye anapania kuwania kiti hicho kwa muhula wa tatu.

Youssou N'dour amehusika na maswala ya kibinadamu kwa siku nyingi na pia ni balozi wa shirika la umoja wa matataifa kuhusu maswala ya watoto (UNICEF).

Mwandishi wa BBC mjini Dakar, Thomas Fessy, anasema hatua ya bwana Youssou N'dour kutangaza kuwa atawania kiti cha urais, haijawashangaza wengi. Hii ni kufuatia tangazo alilotoa mwisho wa mwaka uliopita kuwa atajitosa katika ulingo wa kisiasa.

Katika hotuba iliyopeperushwa kupitia kituo chake cha redio na televisheni, mwanamuziki huyo amesema atapunguza matuzi ya serikali na kuahidi kuzalisha chakula na umeme kwa wote iwapo atachaguliwa kuwa rais wa Senegal.

''kuwa rais ni kazi sio taaluma''Youssou N'dour anakubali kuwa yeye sio msomi lakini anaelezea wadhifa wa rais kama ''kazi na sio taaluma''.

Youssou N'dour alikuwa rafiki wa karibu wa rais Abdoulaye Wade, lakini baada ya Wade kutangaza nia ya kuwania kiti cha urais kwa muhula wa tatu, aligeuka na kuwa mpinzani wake mkuu. Lakini haitakuwa kazi rahisi kwa Bw. Youssou Ndour kuwabadili maelfu ya wafuasi wake wa muziki kumpigia kura.

Aidha, Youssou N'dour amewahi kuwashutumu viongozi wa nchi za Afrika kuhusu jinsi walivyoshughulikia janga la njaa nchini Somalia.


CHANZO bbc swahili.

Tuesday, January 3, 2012

WAWILI WAFARIKI LEO AJALI YA BASI MOROGORO

Ajali mbaya ya basi la Upendo Coach imeripotiwa kutokea leo mkoani Morogoro na kusababisha vifo vya watu WAWILI papo hapo na ZAIDI ya abiria 23 kujeruhiwa,

Kwa mujibu wa moja wa manusura wa ajali hiyo bw. Stanley Amanzi aliyehojiwa na Radio ya watu Clouds Fm majira ya alasili wakati akielekea hospitali ya mkoa wa Morogoro kupatiwa matibabu, amesimulia kuwa akiwa ndani ya basi hilo roli lilitokea upande wa pili likiovateki bila kuchukuwa tahadhari nalo basi lao likiwa katika mwendo kasi ilibidi kujinusuru kukwepa roli hilo kugongana uso kwa uso kwa dereva kukimbilia pembezoni mwa barabara hali iliyopelekea basi hilo kukosa uelekeo na kupinduka.

Taarifa hii imefanyiwa masahihisho…..

PARTY ya Urban Pulse na Miss Jestina George Blog ilikua Noumer!!!!!!!!!!!!

Asha Baraka na Miss jestina George wakila pozi
Asha Baraka Akisherekea mwaka mpya 2012
Pit Stop London Palikua hapatoshi
Mdau akila pozi
Dj Q akijiachia
Frank akisherekea Mwaka Mpya na Wadau
Dada'Zz wakila pozi
Wazungu nao walikuja kula bata.
Urban Pulse Creative na Miss Jestina George Blog wanapenda kuwashukuru wadau wote waliojitokeza kuja siku ya Jumamosi tarehe 31.12.2011 kusherekea nasi ndani ya kiota kipya cha maraha The Pit Stop 'Uwanja wa Nyumbani' bila ya kumsahau mkurugenzi wa ASET Asha Baraka katika party ya kuuga mwaka 2011 na kuukaribisha mwaka 2012 hapa jijini London. Kwa picha zaidi za bofya hapo chini
http://www.jestina-george.com/2012/01/kodak-moments-of-urban-pulse-jestina.html

Tunawatakia kila la kheri katika mafanikio mema na changamoto mbalimbali ndani ya mwaka huu mpya tuliouanza 2012. Kaeni mkao wa kula kwa burudani na vipindi mbalimbali vipya kutoka Urban Pulse na Miss Jestina George Blog.

Wote Mbarikiwe.

Asanteni,

HOT NYUZI ZA MAGAZETI YA LEO

KAULI ya Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli kwamba watakaoshindwa kulipa nauli mpya ya Sh200 kuvuka Kigamboni ni vyema wakapiga mbizi kuvuka bahari, imewakera wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao sasa wanamtaka aombe radhi.

Juzi, Dk Magufuli akiwa katika ziara eneo la Kivukoni alijaribu kuzungumza na wananchi wa Kigamboni kuhusu ongezeko hilo la nauli lakini badala ya wananchi hao kumsikiliza, walizomea ndipo alipowaambia kuwa watakaoshindwa ni vyema wakapiga mbizi baharini, kuzunguka Kongowe kuingia katikati ya jiji au warudi kijijini wakalime.jana, wabunge hao licha ya kumtaka Dk Magufuli aombe radhi, wameitaka Serikali kusitisha mara moja amri ya ongezeko hilo la nauli katika kivuko hicho kutokana na uamuzi huo kufikiwa bila ya kuwashirikisha wananchi.....

BAADHI ya madiwani, wenyeviti wa serikali za vijiji kupitia NCCR MAGEUZI katika Jimbo la Kigoma Kusini pamoja na wanachama, wamesema watajiuzulu nyadhifa zao zote za serikali na kurudisha kadi ikiwa mbunge wa jimbo hilo, David Kafulila, atavuliwa uanachama na kupoteza ubunge.

Katika Jimbo la Kigoma Kusini, NCCR-Mageuzi inaongoza vijiji nane na ina madiwani wanne katika kata za Nguruka, Itebula, Mgaza na Kandaga.......

MVUA NEEMA - MVUA KARAHA

Mashamba katika vijiji vingi kanda ya ziwa yamejaa maji wakulima wanasema ni neema, kwani eneo kubwa la ardhi hutumika kwa kilimo cha mpunga.

Mpunga ni moja kati ya mazao yanayohitaji maji mengi katika ukuaji.

Shamba la mpunga lililooteshwa vyema, mavuno ya mwaka huu 2012 kuna kila dalili ya kupata mchele wa kutosha.

Huku Mvua zikiendelea kunyesha katika maeneo mengi changamoto iliyo kubwa ni kwamba bado wakulima wengi wanalima kwa kusuasua kutokana na kukosa mitaji ya pembejeo, mbegu na fedha kwa ajili ya utayarishaji wa mashamba kulingana na wakati, wengi mvua hizi imekuwa kama zimewashtukiza (hawakuzitegemea).

Changamoto ni kwa miundombinu ya barabara zetu wilayani na vijijini kwani nyingi si za kiwango cha lami.

Kivuko cha Mv Sengerema kunachofanya safari zake kutoka Kigongo ferry kuelekea Busisi.

Athari za mvua na ukuta wa 'Kibandaumiza' Igoma Mwanza.

Halmashauri ya jiji la Mwanza inaendelea na harakati zake kusafisha mifereji ya kandokando ya barabara ili kujizatiti kimiundo mbinu.