ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 27, 2011

HAPA HAPA>>>>ARACHUGA

Hata mbuyu ulianza kama mchicha naskia kalikuwa kachupi kadogo TTuuu mwanawane miaka ikasonga kakawa kakubwa!

Haijalishi Kwa umeme wetu uchakarikaji unaendelea.

Kitu kinakuja.

Si mbugani wala porini ni mtaani kwetu Levolosi Arusha.

Bango.

Kituuuu au vituuu?.

Arusha Lutheran Medical Centre.

Biashara hiyo.

DJ ALLY ANAKUKARIBISHA MAWINGU DISCO CLUB ARUSHA EID MOSI NA EID PILI OF COZ NA MASIKU YOTE

Dj mkali kuliko wote Kanda ya Kaskazini Dj rafiki wa 'Timetables' DJ ALLY' anakukaribisha kwa moyo mkunjufu ndani ya Mawingu Disco Teque kuisherehekea sikukuu ya Eid El Fitri 2011. Menyu ya mchana itakuwa ni kwaajili ya Familia kisha "Baaenga' Mambo yetu yaleeeeeeEEEEE!!!!!

Ol weiz Mawingu kuna hapeni mowma!!!

Friday, August 26, 2011

KIKONGWE ALALA NA MAITI SIKU 6 AKIDAI ALIKUWA HAJUI LOLOTE, ARIPOTI MSIKITINI KUWA ANADHANI KUNA MAITI NYUMBANI MWAKE

KIKONGWE mwenye umri wa miaka 85 aliyefahamika kwa jina la Sadiki Salehe mkazi wa Ilolo kata ya Ruanda Jijini Mbeya amejikuta matatani kufuatia kulala na maiti ya mtoto wake pekee kwa siku sita. MAANDALIZI YA KUUTOA MWILI WA MAREHEMU

MASHUHUDA WA TUKIO HILO KATIKA MTAA WA ILOLOMAANDALIZI YA KUUZIKA MWILI WA MAREHEMU
.
MAANDALIZI YA KUUZIKA MWILI WA MAREHEMU AMBAE ALIKAA SIKU SITA NDANI YA NYUMBA


IBADA YA MAZISHI YA MAREHEMU SALEHE

IMAMU ELIASA SELEMANI WA MSIKITI WA SOWETO JIJINI MBEYA AKIMWOMBEA DUA MAREHEMU KWA MWENYEZI MUNGU

Habari za kuaminika kutoka kijijini hapo zimesema kuwa wakati harufu hiyo ikiendelea kuzagaa eneo la nyumba yake na majirani, Kikongwe huyo alikuwa akiendelea kuandaa futari karibu na mlango wa chumba cha marehemu hasa ukizingatia huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Mtoto wa kikongwe huyo alijulikana kwa jina la Salehe Sadiki(38) kwa mara ya mwisho alionekana Jumatano ya wiki liliopita(Agosti 17, 2011).

Kikongwe huyo alipohojiwa alisema kuwa Jumatano ya Agosti 24 mwaka huu akiwa nyumbani kwake alikuwa anahitaji dishi la kuogea ambalo lilikuwa katika chumba cha marehemu ambaye alikuwa akiishi nje ya nyumba ambayo ilikuwa ikitizama na ya baba yake umbali wa meta 1.5.
Na mara baada ya kuchukua hatua ya kutaka dishi hilo ndipo alipoenda na kugonga mlango wa chumba cha marehemu na kukuta mlango ukiwa umefungwa huku harufu ikitoka kwa mbali.

Harufu hiyo ilimshtua kikongwe huyo ambaye aliamua kwenda msikiti wa Soweto uliopo Jijini Mbeya kwa Imamu Eliasa Selemani ambaye naye alimtaarifu balozi wa mtaa huo Iddi Malole kuhusu tukio hilo.

Imamu Eliasa na Balozi Malole kwa pamoja walimtaarifu Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilolo Benson Mbwana kuhusu tukio hilo la kushangaza ambaye alimua kutoa taarifa katika kituo cha Polisi Mwanjelwa.

Kituo cha Polisi cha Mwanjelwa kilishindwa kushughulikia suala hilo ambalo lilipelekwa katika kituo cha Polisi cha Kati (CENTRAL POLICE) ambacho kiliruhusu kuzikwa kwa mwili huo ambao ulikuwa umeharibika vibaya kwa kupasuka huku Polisi ikiendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Wakati Polisi wakitoa amri ya kuzikwa kwa mwili huo wakazi wa mtaa huo walipandwa na hasira kufuatia tukio hilo na walisikika wakisema kuwa sio mara ya kwanza kwa mzee huyo ambaye hapo awali alimuua mkewe na kumweka uvunguni mwa kitanda kwa zaidi ya siku nne hali iliyomfanya atumikie kifungo cha zaidi ya miaka 8 jela kutokana sakata hilo.

Polisi walipoona hayo ilimuondoa mzee huyo eneo la tukio kwa nguvu ili kunusuru maisha yake.

Wakati polisi ikiondoka na mzee huyo wakazi hao walisikika wakisema mzee huyu hatakiwi


PICHA ZAIDI TEMBELEA KAMANGA NA MATUKIO

Thursday, August 25, 2011

POZI NA MANJONJO YANAPO MPA MTU KULA

Jamaa sijui anaitwa nani vile aliniambia......? anaishi kwa kupiga mapozi yaliyo na manjonjo kedekede, anasakata muziki kinomanoma.

Ni uchumi tu ndiyo unafungua vichwa vya watu wakazama kwenye maubunifu, si hasara some times kujivika uchizi usipochunga utakula mawe.

Anapatikana katika viunga vya jiji la Arusha.

AIRTEL YATOA ML15 ROCK CITY MARATHON 2011

KAMPUNI ya Airtel Tanzania imetoa sh. mil 15/- kama udhamini wake katika mashindano ya riadha ya kilomita 21 yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon 2011’ yatakayofanyika Septemba 4 mwaka huu Jijini Mwanza. Akizungumzia udhamini huo Meneaja Uhusiano wa Kampuni hiyo Jackson Mbando alisema ni hatua inayothibitisha jinsi kampuni hiyo ilivyodhamiria kidhati kuinua michezo mbalimbali nchini.

Alisema pamoja na mambo mengine Airtel imekuwa na mikakati na programu mbalimbali zinazochangia kukua kwa sektta ya kichezo nchini na kwamba riadha ni sehemu ya michezo wanayoona inastahili kuwekewa nguvu na wadau.

“Wote mnajua tumekuwa na mchango mkubwa nchini katika kuinua michezo mbalimbali na udhamini wetu katika hili unadhihirisha dhamira ya dhati tuliyonayo katika hili na tutaendelea kufanya hivi kwa kadri uwezo utakavyokuwa unaruhusu”, alisema Mbando.

Wadhamini wengine ambao tayari wamejitosa katika mshindano ya mwaka huu ni pamoja na Geita Gold Mine, Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), New Africa Hotel, Mfuko wa Pensheni wa Taifa (PPF), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bank M, MOIL, New Mwanza Hotel, Shirika la Hifadhi ya Wanyapori Tanzania (TANAPA) na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Mratibu mashindano hayo kutoka Kampuni ya Capital Plus International (CPI) Zaituni Ituja alisema wanaandaa mshindano hayo kwa mara ya tatu mwaka huu na kwamba mbio hizo zitaanzia uwanja wa CCM Kirumba kuelekea njia tofauti za Jiji la Mwanza na kumalizia katika uwanja huo.

Kuhusu zawadi alisema alisema washindi wa kilometa 21 watapata sh.500,000/-kwa pande zote mbili za wanaume na wanawake huku yule atakayevunja rekodi ya mwaka huu ya dakika 59 atapata zawadi ya jumla ya sh. Milioni Moja na wale watakaoshika nafasi ya pili watapata sh. 300,000/-

Watakaoshika nafasi ya tatu watapata sh. 200,000/- huku nafasi ya nne hadi 12 kila mmoja atapata sh.90,000/- na wale watakaoangukia katika nafasi ya 13 hadi 50 kila mmoja atapatiwa kifuta jasho cha sh. 30,000/- wakati washindi 21 wa mbio za Kilometa 5, Kilometa 3 kwa Walemavu, Kilometa 3 za Wazee na Kilometa 2 kwa Watoto watapatiwa sh. 25,000/- kila mmoja kama kifuta jasho.

“Kiujumla tumekuwa na maboresho makubwa katika zawadi kwa kuongeza wigo wa watu wanaozawadiwa na hii tumeifanya makusudi tukiwa na lengo la kuongeza hamasa kwa wote watakaoshiriki ili tuendelee kuamsha ari ya ushiriki na kuibua vipaji vya riadha nchini”, alisema.

Aliongeza kuwa tayari mikoa 14 imeonyesha nia ya kushiriki na ni faraja kwao na hiyo inathibitisha kukua kwa mashindano yenyewe mwaka hadi mwaka lakini pia inaonyesha ushindani utakuwa mkubwa zaidi.

“Tumeamua kuendelea kupanua wigo wa ushiriki mwaka huu kutokana na kutambua umuhimu wa michezo kwa rika mbalimbali lakini muhimu zaidi ni mapendekezo tofauti tuliyopokea kupitia wadau mbalimbali baada ya kumalizika kwa mashindano ya mwaka jana”, alisema Ituja.

Fedha zitakazopatikana kutokana na fomu za usajili zitaenda katika mfuko wa kuwasaidia watu wenye ulemavu mkoani Mwanza. Fomu kwa ajili ya kujisajili zitapatikana Ofisi za uwanja wa CCM Kirumba, Ofisi za CPI- DSM, Makao Makuu ya Chama cha Riadha

Tanzania (RT) Dar es Salaam, Ofisi za MRAA Mwanza. Fomu za usajili pia zinapatikana katika tovuti ya
www.rockcitymarathon.blogspot.com or info@capitalplus.co.tz.

FASHION STYLIST KOKUHILWA ROSEMARY OF FASHIONJUNKII EXCLUSIVE INTERVIEW WITH JESTINA GEORGE...!!!

FASHION STYLIST KOKUHILWA ROSEMARY OF FASHIONJUNKII EXCLUSIVE INTERVIEW WITH JESTINA GEORGE...!!!
FJ aka Kokuhilwa Rosemary


JG: Hi kokuhilwa Rosemary, Thank you for your time, straight away, let’s begin. Tell us about yourself, your history, family, education etc.

FJ: My name is Rosemary Kokuhilwa. I was born in Bukoba but grew up in Dar -es-salaam Tanzania. Right after high school I became a model and was managed by Faces International which was the first modelling agency in Tanzania back in the days. I am the eldest in my family, I have five siblings. I am currently in the States where I work and attend school at FIT (Fashion Institute Technology).

JG: Where did the name Fashionjunkii Stem from?

FJ: The name came about after playing around with diffferent names that fitted me as a fashion enthusiast. Then my sister and her boyfriend came up with Fashionjunkii because they thought I needed help because of my shopping habit. It was actually supposed to be fashionjunkie as in a "junkie" for fashion but instead I threw in "Junkii " thinking it would have a bit of swahili flavor.

JG: Where are you based NOW?

FJ: I am now based in New York

To read the full interview click on the link below:

FASHIONJUNKII EXCLUSIVE INTERVIEW WITH JESTINA GEORGE

KWA MARA NYINGINE ANNA LUKINDO AFANY KWELI NCHINI UINGEREZA

Anna Lukindo(katikati0 akiwa_na Mariam Kilumanga(kulia) pamoja na mamodo wake.
Salam

URBAN PULSE ikishirikiana na Miss Jestina Blog inakuletea matukio katika picha ya Mtanzania mbunifu wa kimataifa Anna Lukindo
(anaetumia jina la Anna Luks) alipoonyesha mavazi yake ya kibunifu mjini London.

Maonyesho hayo ambayo yalifanyika Ijumaa tarehe 19 Agosti 2011 Chelsea Old Town Hall, King's Road, Chelsea London. SW3 5EE.
Maonyesho hayo yalienda sambamba na kusheherekea siku ya Ubinadamu duniani.

Anna ameonyesha ubunifu wake wa kipekee wa kutumia vitambaa asilia mfano gunia, kamba za katani na nyuzi mbalimbali ambazo anatumia ufundi maalum na kutengeneza vitambaa vyake mwenyewe. Wadau kadhaa kutoka katika nyanja tofauti walijitokeza kwa wingi kumuunga mkono na kuvutiwa zaidi kwa kazi zake.

Maonyesho haya yalitayarishwa na Mdoe ambaye ni Mkurugenzi Wa uchaguzi husika wa wasanii wenye vipaji vya maigizo jijini London. Mbali na shughuli nyingine za kidiplomasia yalikuwepo pia mashindano ya kutafuta mshindi wa Tuzo ya Uso wa mwaka 2012 yaliyoongozwa na mwonyeshaji urembo na mwanamichezo Rachel Christie. Baadaye yalifuatia maonyesho mawili ya mavazi "back to back" yaliyofanywa na wabunifu wawili wa mitindo Anna Lukindo wa Anna Luks na "Adopted Culture" msanifu wa rangi, Nana Antwi.

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Anna kwa kutembelea tovuti yake hapo chini
Pr/Media:Pauladpope@yahoo.co.uk
Web:annaluks.com
http://annaluks.blogspot.com/
Twitter:@AnnaLukindo


ASANTENI,

"CHEREKO CHEREKO UMEPONA MAZEEEE!!"

Jana katika ofisi za Nishati na Matini kulikuwa na furaha ya hali ya juu baada ya Mhe. Jairo kuwasiri katika kibarua chake kilicho ponea chupu chupu kutiwa mchanga na wabunge

KATTIBU MKUU KIONGOZI, Phillemon Luhanjo(kulia) alitangaza uamuzi huo katika mkutano wake na waandishi uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam juzi akisema Jairo hana hatia na jana anapaswa kurejea kazini mara moja.

Alisema matokeo ya uchunguzi dhidi yake yamebainisha kwamba hakuwa na hatia hivyo kusema kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Sheria namba 8 ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002 na kanuni zake za mwaka 2003, anamrejesha kazini Jairo... “Ninaamuru David Jairo arejee kazini kuanzia siku ya Jumatano (jana).”

KUMBUKA kuwa..... tuhuma hizo zilitolewa na Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo na hata kumfanya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuzitolea maelezo Bungeni akisema akama angekuwa na mamlaka, angelitolea uamuzi (kumwajibisha mhusika) lakini akaahidi kulifikisha kwa Rais ambaye alisema ndiye mwenye mamlaka ya uteuzi.

Tehe! mwisho wa siku shangwe kama kawaiiiida'


Wednesday, August 24, 2011

GADDAFI AAPA KUPAMBANA HADI KIFO

Kanali Muammar Gaddafi ameapa kupigana na waasi hadi kifo au ushindi, ripoti zimesema, baada ya waasi kudhibiti makazi yake mjini Tripoli.

Televisheni inayomuunga mkono Kanali Gaddafi, al-Urubah, imesema Kanali Gaddafi ambaye bado hajulikani alipo, ametoa hotuba akisema kuondoka kutoka kwa makazi yake kulikuwa ni ''mpango''.

Makazi hayo ndiyo yaliyokuwa maeneo ya mwisho chini ya udhibiti wa Kanali Gaddafi mjini Tripoli. Waasi wamekuwa wakisheherekea mafanikio yao katika bustani ya Green Square, mjini Tripoli.

Picha za televisheni pia zimeonyesha wapiganaji wakivunja sanamu ya kiongozi huyo na kuipiga mateka baada ya kuuteka Bab al-Aziziya siku ya Jumanne. Waasi hao pia walichukua vifaa mbalimbali katika makazi hayo ya Kanali Gaddafi.

Hata hivyo bado mapambano yanaripotiwa katika mji huo, mkiwemo katika maeneo ya Abu Salim na Hadba na karibu na hoteli ya Rixos, ambapo waandishi wa kigeni wanapoishi.

Mwandishi wa BBC Rana Jawad mjini Tripoli amesema kuwa kuna hisia kuwa huu ndio mwisho wa utawala wa Kanali Gaddafi, lakini sherehe kamili hajitaanza hadi pale yeye na jamaa wake watakapo kamatwa.
Akizungumza na redio moja mjini Tripoli, Kanali Gaddafi ameahidi''kifo au ushindi'' katika mapigano dhidi ya majeshi ya NATO na waasi wa Libya, redio ya al-Urubah ilisema.

Kanali Gaddafi aidha amesema makazi yake yameharibiwa na mashambulio 64 ya angalini ya NATO. Jumanne asubuhi, wapiganaji wa waasi waliokuwa wamejihami vilivyo walimiminika katika mji mkuu kushiriki katika mashambulio ya Bab al-Aziziya.


Baada ya saa tano ya mapigano makali, walivunja lango kuu na kuvamia makazi hayo. Waasi walionekana wakiharibu masanamu, mkiwemo sanamu ya dhahabu, ya mkono unaovunja ndege ya kivita ya Marekani. Hema ya Kanali Gaddafi ambayo aliitumia kupokea wageni pia iliteketezwa.

Wametoroka kama panya.
''Tumeshinda makabiliano'' Abdul Hakim Belhaj, kamanda wa ngazi ya juu wa waasi mjini Tripoli aliliambia shirika la al-Jazeera.''Wametoroka kama panya''.

Haijulikani iwapo kanali Gaddafi na jamaa wake walikuwa katika makazi hayo ya Bab al-Aziziya, lakini inaripotiwa kuwa ina mahandaki ya chini kwa chini, yanayounganisha na maeneo mengine ya mji.

Hali sio wazi katika katika mji wa Sirte, alikozaliwa Kanali Gaddafi, ambayo imekuwa ngome ya maafisa wanaomuunga mkono. Ripoti zinasema wanajeshi waliorudishwa nyuma wanaelekea huko.

Tuesday, August 23, 2011

KUMBUKUMBU

Edward Joseph Magongo (1977 – 1992)
Ilikuwa siku, wiki, mwezi na leo tarehe 24/08/2011 ni miaka kumi na tisa tangu ututoke na kurejea kwenye makazi ya usalama.

Tulikupenda sana ila Mungu alikupenda zaidi.

Unakumbukwa sana na wazazi wako Joseph na Clementina Magongo, Dada, kaka, wadogo zako, mashemeji, wajomba, ndugu jamaa na marafiki.

Raha ya milele umpe ee Bwana, na mwanga wa milele umwangazie, apumzike kwa amani.

AMINA

DWIGHT HOWARD WA ORLANDO MAGIC AKUTANA NA RAIS KIKWETE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Mchezaji maarufu wa mpira wa Kikapu duniani Dwight Howard akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete zawadi ya jezi wakati nyota huyo alipomtembelea Rais ikulu jijini Dar es Salaam jana.Dwight Howard ni mchezaji nyota wa timu ya kikapu ya Orlando Magic ya nchini Marekani.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(kulia),Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso Lenhardt (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na nyota wa mchezo wa kikapu nchini Marekani Dwight Howard (Katikati)wakati nyota huyo alipomtembelea Rais ikulu jijini Dar es Salaam jana.Nyota huyo anachezea klabu ya Orlando Magic.

Nyota mchezo wa kikapu nchini Marekani Dwight Howard akimwangalia Simba aliyekaushwa kitaalamu na kupamba lango la ikulu jijini Dar es Salaam huku akifurahia jambo na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati nyota huyo alipokwenda ikulu kumsalimia Rais na kutoa ahadi ya kutoa msaada ili kukuza vipaji vya mchezo huo nchini. (Picha na Freddy Maro).

SIKIA HII>>>>


Millard Ayo kanitumishia ujumba anaronga hivi:-

"Nilifanya interview saa nne na dakika 40 USIKU na familia ya aliyekua mchezaji wa AFRICAN LYON, Yusuf Soka ambae anadaiwa KUZAMIA nchini SWEDEN baada ya kwenda kujaribiwa kucheza soka la KULIPWA, katika picha nikiwa na wajomba zake pamoja na mama yake mzazi. vyombo vya habari vimekua vikiripoti HABARI ZA KUZAMIA kwake na HAJULIKANI ALIKO, sasa familia imezungumza. tukutane sa1 usiku - 3 kwenye AMPPLIFAYA on CLOUD'S FM"

VILIVYONIVUTIA ''''''KUVIDADISI''''''

Sawa imeandikwa 'asiye fanya kazi na asile' lakini pia imeandikwa 'ombeni mtapewa'.

Taja jina chukuwa mzigo...!
Naitwaaaa....

From school....

Waponda kokoto eneo la majengo Arachuga.

Wanazipatia hao...!!..

GAMBUTI aka 'Gum-boot'

Mishemishe.

Bei ya madafu leo.

Monday, August 22, 2011

AIRTEL YAMWAGA MSAADA WA VITABU SUA SEKONDARI

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekabidhi msaada wa vitabu vya kiada na ziada kwa shule za sekondari nne za mkoani Morogoro, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kusaidia jamii hapa nchini. Meneja Mauzo Kanda ya Pwani wa kampuni ya simu ya Airtel, Aluta Kweka (kushoto), akikabidhi sehemu ya msaada wa vitabu kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Alfred Shayo vilivyotolewa na kampuni hiyo kwa Shule za Sekondari za SUA, Mwembesengo, Mji Mpya na Mgulasi Mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Sekondari ya SUA, Khalfan Millongo, Meneja Huduma za Jamii wa Airtel Tunu Kavishe na Diwani wa Kata ya Mbuyuni, Samuel Msuya. Vitabu hivyo vina thamani ya shs milioni 4

Meneja Huduma za Jamii wa Airtel Tanzania, Tunu Kavishe (wa tatu kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada wa vitabu kwa mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari SUA, Rogers Shempemba vilivyotolewa na kampuni hiyo kwa Shule za Sekondari za SUA, Mwembesengo, Mji Mpya na Mgulasi Mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki.

Meneja Mauzo Kanda ya Pwani wa kampuni ya simu ya Airtel, Aluta Kweka (kushoto), akikabidhi sehemu ya msaada wa vitabu kwa mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari SUA, Happiness Makundi vilivyotolewa na kampuni hiyo kwa Shule za Sekondari za SUA, Wa pili kushoto ni Meneja Huduma za Jamii wa Airtel, Tunu Kavishe na kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Alfred Shayo. Vitabu hivyo vina thamani ya shs milioni 4.

Meneja Huduma za Jamii wa Airtel Tanzania, Tunu Kavishe (wa tatukushoto) akikabidhi sehemu ya msaada wa vitabu kwa mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari SUA.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Alfred Shayo (kulia) akimshukuru Meneja Huduma za Jamii wa Airtel Tanzania, Tunu Kavishe (kushoto) katika hafla ambayo Airtel ilikabidhi msaada wa vitabu vyenye thamani ya shs milioni 4 kwa Shule za Sekondari za SUA, Mwembesengo, Mji Mpya na Mgulasi Mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mkuu wa Shule ya Sekondari SUA, Khalfan Millongo.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Alfred Shayo, akihutubia katika hafla hiyo.

Shule zilizopata msaada wa vitabu ni shule za sekondari ya Mwembesongo, Mji mpya, SUA na Mgulasi.

MSONDO YATWAA TUZO ya the Best Rhumba Group katika East Africa Music

BENDI ya muziki wa dansi nchini Msondo ngoma imepata TUZO ya the Best Rhumba Group katika East Africa Music Awards mashindano yaliyofanyika Nairobi Kenya na kukusanyika kwa bendi za Afrika Mashariki na bendi ya msondo kuibuka Kidedea katika mashindano hayo akithibitisha ushindi huo meneja wa bendi Saidi Kibiriti alipokuwa akiongea na Msemaji wa Bendi hiyo, Rajabu Mhamila , Super D Alisema wameshinda tuzo hiyo na watahakikisha wanaionesha kwa mashabiki wa bendi hiyo ili kudhirisha kuwa bendi hiyo ipo ngangari popote duniani mana bendi imekamilika kila idara alisema Super D (pichani)

Bendi hiyo itanza mazoezi siku ya jumatatu kwa ajili ya kujiandaa na sikukuu ya Iddi inayotarajia kufanyika wiki ijayo ambapo wanaingia kambini kusuka vibao vipya ikiwemo na kuvifanyia kazi vile vya Zamani

Super D alisema bendi hiyo siku ya Iddi Mosi itapiga katika viwanja vya TTC Chang'ombe ambapo mashabiki watapata kuona tuzo hiyo ya Afrika Mashariki walioitwaa hivi karibuni na kupata fulsa ya kupiga nayo picha katika viwanja hivyo

Bendi hiyo inayotamba na vibao vyake vipya vya Suluu utunzi wake Shabani Dede na Nadhili ya Mapenzi uliotungwa na Juma Katundu


Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
Mob;+255787 406930
+255774406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

Sunday, August 21, 2011

KILIMO KWANZA KIUTEKELEZAJI INAWEZEKANA: SIYO BLA-BLA MAJUKWAANI

Wakulima mbalimbali wanaojishughulisha na kilimo cha umwagiliaji mkoani arusha walipata ugeni wa wataalamu wa kilimo toka nchini Misri (Egypt) kufundisha na kuwaongezea ujuzi wakulima hao wakubwa kwa wadogo, Arusha Bloom ni moja kati ya mashamba makubwa yaliyotembelewa na wataalam hao.

Masanduku ya kuhifadhia mbogamboga kwaajili ya upangwaji katika madaraja ya ubora husafishwa kwa uangalifu wa hali ya juu toka kwa wakulima wa shamba hili.

Shughuli ya uchambuaji.

Uchumaji Nyanya kwenye shamba hili ni wa manufaa kweli hebu fikiri kwa kipindi cha miezi 6 hadi 8 we unachuma tu nyanya babake! kisha mashina hung'olewa na kupandwa mbegu upya.

Mzigo wenyewe.

Masalia ya makopo ya dawa za kuulia wadudu hutobolewa, tobolewa ili kuepusha wananchi kuyaokota makopo hayo kwa matumizi ya nyumbani, kwani si wote wanaweza kuyasafisha yanavyopaswa kuondoa sumu iliyosalia.

Shamba la matango na uvunaji.

Haya ndiyo matango yanayozalishwa hapa na Arusha Bloom.

Bendera nyekundu (tahadhari) kielelezo kuwa usipige dawa bila maelekezo au kuchuma mazao yanaweza kuwa yamenyunyiziwa dawa.

Kuna baadhi ya mazao ambayo hayachavushwi kwa upepo isipokuwa kupitia wadudu, moja ya mazao hayo ni matango hivyo kutokana na ukubwa wa mashamba haya kuna mizinga mingi ya nyuki ya kutosha maalum iliyojegwa sehemu mbalimbali ndani ya shamba hili kama unavyoona pichani.

Uvunaji maharagwe machanga.

Maharagwe katika daraja.

Shamba la maharagwe na kingo zake kuzuia wadudu washambualiao mazao na kuaharibu ubora.

Chakufurahisha zaidi wageni wataalamu kutoka Misri huja mara kwa mara kuwakutanisha wakulima wakubwa na wadogo kutoa semina ya kilimo bora. Pichani Wakulima wadogo wadogo wakiagana na wataalamu wa kilimo mara baada ya kupewa darasa juu ya namna bora za kilimo cha manufaa ili kufikia malengo ya kuuza mazao kwenye soko la kimataifa kwa kiwango cha juu.

Much Thanks to CCP for facilitating this event and TAHA support on the same, it now the turn of the 17 Participants to use the education gained from this event by training many farmers who are in the industry in order to see that more Tanzania Farmers are awarded Global GAP certificates and be in position to export their produce.