ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 23, 2017

HAPA NDIPO LULU ANAPO LALA GEREZANI



Siku ya pili leo inakatika wakati ambapo mwigizaji nyota wa filamu nchini Tanzania Elizabeth Michael 'Lulu' akiwa nyuma ya nondo za gereza la Segerea jijini Dar es salaam, hii ikiwa ni mara baada ya maamuzi wa Mahakama dhidi yake yakimuamuru kutumikia kifungo cha miaka miwili baada ya kukutwa na kosa la kumuua bila kukusudia, aliyekuwa Nguli wa Filamu nchini Steven Kanumba 'The Greatest' Kanumba alifariki majira ya saa nane usiku,mnamo mwaka 2012 baada ya kutokea mzozo kati yake yake na Elizabeth Michael ambaye inaaminika kuwa walikuwa na uhusiano wa Kimapenzi. 

Moja ya maswali kati ya mengi yaliyotawala vichwa vya wengi:- 
 1. Maafisa magereza walimpokeaje Lulu huko gerezani? 
2. Jeh ni kweli kuwa watu maarufu wanapokuwa kifungoni huwa na maeneo yao spesheli yenye full service, Jeh msanii huyo baada ya kutupwa Segerea analala wapi? 
3. Mfungwa anapohukumiwa miaka yake kadhaa, Jeh hesabu ya miaka hiyo huwa kwa mtindo upi? ---Jeh Usiku na Mchana huhesabika kama siku mbili au imekaaje?
4. Jeh Lulu ana qualify kupata msamaha wa Rais? 

KAZI NA NGOMA ya Jembe Fm chini ya Mwenyekiti Albert G. Sengo naye Katibu Mansour Jumanne inamtafuta Afisa wa jeshi la Magereza ambaye ni Msemaji wa Jeshi hilo Lucas Mboje na kufanya naye mahojiano.

Rostam ft Maua Sama - Kiba_100 [Official Music Video]



Rostam (ROMA & STAMINA) - Kibamia. audio produced by Bea (Killi Records) From Original track SAUTI YA MTAA by Ramsoh Ratinho. video directed by NiCKLASS.

BREAKING NEWS: RAIS MAGUFULI AMTEUA DKT SLAA KUWA BALOZI.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amteua Dkt. Wilbrod Peter Slaa kuwa Balozi.

Uteuzi wa Dkt Wilbroad Slaa umefanyika leo Novemba 23 ambapo anategemea kuapishwa baada ya utaratibu kukamilika.

Dkt Slaa aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA na mwaka 2015 karibu na kipindi cha uchaguzi alitangaza kuachana na siasa.


10 YEARS ANNIVERSARY OF BANK OF AFRICA-TANZANIA

The guest of honor; Honorable Charles Mwijage, Minister of Industries, Trade and Investment giving out the speech at the Bank’s 10 years’ anniversary event, yesterday at Serena Hotel.

CEO and Managing Director of BANK OF AFRICA- TANZANIA, Mr. Ammishaddai Owusu-Amoah giving out his very exciting and energetic speech during the 10 years’ corporate anniversary event, which took place yesterday at Serena Hotel.

Deputy Managing Director of BANK OF AFRICA –TANZANIA, Mr. Wasia Mushi giving out his opening remarks and introducing the entire BANK OF AFRICA team present at the 10 years’ corporate anniversary event, which took place yesterday at Serena Hotel.

CEO and Managing Director of BANK OF AFRICA- TANZANIA, Mr. Ammishaddai Owusu-Amoah hands over a copy of his speech to the guest of honor; Honorable Charles Mwijage, Minister of Industries, Trade and Investment.

The guest of honor; Honorable Charles Mwijage, Minister of Industries, Trade and Investment in jovial moment while listening to the speech from CEO and Managing Director of BANK OF AFRICA- TANZANIA, Mr. Ammishaddai Owusu-Amoah. To his left hand side is the Board Chairperson of BANK OF AFRICA-TANZANIA, Ambassador Mwanaidi S. Maajar.

The guest of honor; Honorable Charles Mwijage, Minister of Industries, Trade and Investment, accompanied by the Board Chairperson of BANK OF AFRICA-TANZANIA, Ambassador Mwanaidi S. Maajar and CEO and Managing Director of BANK OF AFRICA- TANZANIA, Mr. Ammishaddai Owusu-Amoah to take part in a great spread of amazing foods available at the event yesterday.
The guest of honor; Honorable Charles Mwijage, Minister of Industries, Trade and Investment together with Board Chairperson of BANK OF AFRICA-TANZANIA, Ambassador Mwanaidi S. Maajar and CEO and Managing Director of BANK OF AFRICA- TANZANIA, Mr. Ammishaddai Owusu-Amoah; in group photo with a section of esteemed clients of the Bank who attended the corporate 10 years anniversary dinner gala.


HABARI KATIKA PICHA: MUENDELEZO WA ZIARA YA KUJITAMBULISHA YA RC DOM DKT. MAHENGE KWENYE WILAYA ZA MKOA WA DODOMA

Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. John Samwel Malecela (mwenye kofia ya njano) akimuonesha Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge mizabibu iliyopandwa kwenye shamba la Chinangali II Wilayani Chamwino wakati wa Ziara ya Dkt. Mahenge Wilayani humo
Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na ujumbe alioambatana nao wakipata maelezo juu ya mashine ya kusukumia maji kwa ajili ya umwagiliaji wa matone kwenye shamba la zabibu la Chinangali II Wilayani Chamwino wakati wa Ziara ya Dkt. Mahenge Wilayani humo.

Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na ujumbe alioambatana nao wakikagua bwawa la kutunzia maji kwa ajili ya umwagiliaji wa matone kwenye shamba la zabibu la Chinangali II Wilayani Chamwino wakati wa Ziara ya Dkt. Mahenge Wilayani humo.
 
Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akikagua nyaraka na kusikiliza kero za wananchi kwenye mkutano wa hadhara Kijiji cha Manzase  Wilayani Chamwino wakati wa ziara yake
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Manzase Wilayani Chamwino wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Mahenge (hayupo pichani) wakati alipofanya mkutano wa hadhara kusikiliza kero za wananchi Kijiji hapo.
 
Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akikagua mradi wa ujenzi wa jengo la Ghorofa moja la ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Chemba wakati wa ziara yake wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na ujumbe alioambatana nao akikagua chanzo cha chemichemi ya maji moto Mjini Kondoa, Chanzo hiko kwa sasa ndio kinategemewa kwa huduma ya maji Mjini Kondoa.
 (Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma Makao Makuu)

DC GONDWE AWATAKA WANANCHI WASICHOKE KUCHANGIA KATIKA MAENDELEO YA AFYA

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akiongea na wananchi wa Kata ya Kwamgwe wakati akikabidhiwa zahanati iliyojengwa kwa hisani ya shirika la maendeleo la World Vision Tanzania kwa kushirikiana na nguvu za wananchi, mkuu wa wilaya aliwaomba wananchi waendelee na moyo wa kujitokea katika kuchangia kazi za maendeleo ili kijiji kiweze kujikwamua kimaendeleo. PICHA NA KAJUNASON/MMG - HANDENI, TANGA.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akimsaidia Diwani wa Kata ya Kwamgwe, Sharifa Abebe alipokuwa akitoa machozi ya shukrani kwa shirika la maendeleo la World Vision Tanzania kwa kuweza kushirikiana na wananchi kuwajengea jengo la zahanati lililoweza kugharimu shilingi milioni 190 ambapo wao World Vision Tanzania waliweza kutoa Milioni 100 na wao wananchi waliweza kujitoa kwa nguvu zao kwa thamani ya milioni 90. Hafla hiyo ilifanyika katika Kata ya Kwamgwe ambapo ndipo jengo hilo lilipojegwa.
Mwezeshaji wa mradi Mkumburu ADP wa World Vision Tanzania,  Humphrey Bernard akisoma risala ya mradi wa ujenzi wa zahanati iliyojengwa katika Kata ya Kwamgwe ambapo aliwashukuru wananchi wa kata ya Kwamgwe kwa kuweza kujitoa kufanikisha ujenzi wa jengo la zahanati.
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akikabidhiwa mikataba wa zahanati na mwezeshaji wa mradi Mkumburu ADP wa World Vision Tanzania, Humphrey Bernard (kushoto) ambao ndiyo waliojenga kwa kushirikiana na wananchi waliojitoa kwa hali na mali.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Handeni, William Makufwe akitoa ufafanuzi jinsi wananchi walivyoweza kujitoa ujenzi wa zahanati.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Dokta Credianus akitoa nasaha zake kwa wananchi wa Handeni waweze kujua umuhimu wa kuwekeza katika afya. Jengo la zahanati iliyojengwa katika Kata ya Kwangwe, Wilayani Handeni.
Wakati huo huo, mkuu wa wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akipokea zawadi ya kuku kutoka wa mwenyekiti wa kitongoji cha Migombani, Michungwani-Segera Bi. Amina Njama ambaye amekuwa msitari wa mbele katika uhamasishaji wa kukusanya matofali ili yaweze kusaidia katika ujenzi wa madarasa na zahanati.
 Mkuu wa Wilaya akifurahi na viongozi.
 Mkuu wilaya akipata maelezo machache kutoka kwa wananchi waliitikia wito wa kuchangia maendeleo kwa kuchimba msingi wa zahanati ya  Migombani, Michungwani - Segera.
Mkuu wa Wilaya akiwashukuru wananchi kwa moyo wao wa kujitolea katika maendeleo. Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe amewataka wananchi wa Kata ya Kwamgwe kuendelea kujitoa kikamilifu katika kuchangia shughuli za kijamii ili kuendana na kasi ya rais Dkt. John Magufuli katika kuleta maendeleo endelevu. 

Akizungumza na wakazi wa Kata ya Kwamgwe wakati akikabidhiwa zahanati iliyojengwa kwa hisani ya shirika la maendeleo la World Vision Tanzania, mkuu wa wilaya aliwaomba wananchi waendelee na moyo wa kujitolea katika kuchangia kazi za maendeleo ili kijiji kiweze kujikwamua. "Nawaomba ndugu zangu, sisi wote ni wanaKwamngwe, lazima tuamue kuchangua mambo muhimu matatu, kutambaa, kutembea au kukimbia. 

Jambo la msingi ni lazima tuwe katika mwendo, tuendelee kujitoa tuzidi kuleta maendeleo kijijini kwetu," alisema Gondwe. Awali akikabidhi mradi huo wa zahanati hiyo, Mwezeshaji wa mradi Mkumburu ADP, Humphrey Bernard aliwashukuru wananchi wa kata ya Kwamgwe kwa kuweza kujitoa kufanikisha ujenzi wa jengo la zahanati. 

Wakati huo huo, Mkuu wa wilaya Handeni aliweza kutembelea ujenzi wa kituo cha afya cha Michungwani, Segera ambapo ujenzi wake unaanza hivi karibuni kwa nguvu za wananchi kupitia kampeni ya mkuu huyo ya kuongeza zahanati na madarasa.

WAZIRI HARRISON MWAKYEMBE AZINDUA MICHUANO YA SHIMUTA IRINGA

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akiwa pamoja na mkuu wa mkoa wa Iringa bi Amina Masenza jukwaa kuu akiwahutubia wanamichezo waliojitokeza kushiriki michuano ya SHIMUTA

 Baadhi ya wanamichezo walikuwa wakifurahia jambo baada ya waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kuzindua rasmi mashindano hayo


Michuano ya SHIMUTA inayohusisha wafanyakazi wa mashirika ya umma, kampuni za watu binafsi na taasisi zilizopo hapa nchini imezinduliwa rasmi mkoani Iringa huku washiriki wakiwataka waajiri kuwaruhusu wafanyakazi kushiriki katika michezo huku waziri mwenye dhamana ya michezo akitoa onyo kwa mamluki.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amezionya timu ambazo zinashiriki kwenye michuano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Kampuni Binafsi Nchini (SHIMUTA) kuacha kuchukua wachezaji ambao sio wafanyakazi  kwani kufanya hivyo kunapunguza ladha ya mashindano hayo.                                

Mwakyembe alisema kuwa michezo hujenga undugu na furaha baina ya wanamichezo hivyo kuwaingiza wachezaji ambao sio wafanyakazi kwenye mashindano hayo wataondoa maana halisi ya mashindano hayo jambo ambalo linaweza kuwafanya kushindwa kufikia malengo yao waliojiwekea. 

  “Mashindano haya ni ya wanamichezo wafanyakazi…kuna wale wanamichezo ambao sio wafanyakazi ambao wanajulikana kama mamluki au wavamizi kwamba hapa sio mahala pao nawasihi tuchezeshe wafanyakazi halisi ili mshindi apatikane kihalali na sio vyenginevyo….. kwa sababu ni hatari sana kumleta mwanamichezo ambaye sio mfanyakazi kwenye michezo hii anaweza kuvunjika mguu au akifa kwa mfano hatuombei itokee hiyo itakuwaje “Alisema Mwakyembe

Aidha Mwakyembe alizitaka timu hizo kuacha kuwatumia wachezaji wa aina hiyo kwani wana madhara makubwa hasa pale yanapokuwa yakijitokeza kwa kuzitaka timu zenye utamaduni huo kuhakikisha wanaondokana nao. 

Hata hivyo waziri Mwakyembe alionekana kukerekwa na baadhi ya menejimenti za Taasisi,Mashirika na makampuni mbalimbali kuwa na utashi wa kutokupenda michezo na wengine kwa kisingizio cha ukosefu wa fedha kuacha kufanya hivyo badala yake wamuunge mkono Rais Jakaya Kikwete katika jitihada zake za kuinua na kuendeleza michezo hapa nchini. 

Akizungumzia waamuzi wanaochezesha mashindano hayo, Mwakyembe aliwataka kuchezesha kwa haki bila upendeleo kwa kufuata sheria za mchezo husika ili mshindi aweze kupatikana kihalali kwa sababu wakienda kunyume chake wanaweza kusababisha tafrani na manung’uniko kwa baadhi ya timu shiriki. 

Hali kadhalika aliwataka kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ya hali ya juu wakati wote wa mashindano ikiwemo kukubaliana na matokeo pindi watakapojikuta wamefungwa wakati wa mashindano hayo. 

Naye Mwenyekiti wa Shimuta, Khamis Mkanachi alisema kuwa kupungua kwa idadi ya timu shiriki kunatokana na baadhi ya mashirika kubinafsishwa hali ambayo imepelekea timu nyingi kushindwa kupata nafasi ya kupeleka washiriki wake lakini pamoja na kuwepo hali hiyo shirikisho hilo limendelea na jitihada za ziada kuhakikisha idadi ya timu hizo haipungui bali kuongezeka. 

Nao baadhi ya washiriki wameeleza sababu ya baadhi ya waajiri wasio na mapenzi na michezo kushindwa kutoa hamasa sehemu za kazi kwa kutokujua faida zitokanazo na michezo.

 Ni wajibu wa viongozi kuinua na kuendeleza michezo mahala pa kazi “ni kauli mbiu yenye lengo la kuhamasisha ushiriki wa michezo kwa watumishi kwa lengo la kukutanisha wafanyakazi wa idara tofauti na kubadilishana uzoefu wa kikazi lakini kubwa zaidi ni kujenga afya kwa kupitia michezo.

SHIMUTA ni Shirikisho la Michezo la mashirika ya Umma Taasisi, na kampuni binafsi hapa nchini, lililoanzishwa na serikali ili kuhimiza michezo mahala pa kazi.

WANANCHI KATA ZA LUDETE, KAKUBILO WAMKOSHA RC GEITA UJENZI WA ZAHANATI NA MADARASA ACHANGIA TOFALI 2000,MIFUKO 420 YA SARUJI

 Mhandisi Robert Gabriel akishirikiana na mafundi kupandisha ndoo yenye zege kwa ajili ya uwagaji wa leta katika majengo 10 ya vyumba vya madarasa shule ya Msingi Ludete Wilayani Geita.
 Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akifuatilia kwa karibu maendeleo ya wanafunzi wa kidato cha Tatu shule ya Sekondari Kakubilo Halmashauri ya Geita baada ya kutembelea shule hiyo na kutoa swali la Hisabati kwa wanafunzi hao.
 Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa Geita akikabidhi fedha shilingi 2,400,000/= kwa Diwani wa Kata ya Ludete Sebastian Mranda kwa ajili ya ujenzi wa boma la Zahanati ya Kijiji na Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari katika hiyo.
 Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akishirikiana na wananchi wa Kata ya Ludete Wilayani Geita kumwaga zege kwa ajili ya lenta kwenye ujenzi wa madarasa 10 ya shule ya msingi Ludete yenye wanafunzi 6,616  alipokwenda kuzindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.
 Wananchi wa kijiji cha Ludete Kata ya Ludete Wilayani Geita wakishiriki katika uchimbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati katika kijiji hicho kwa lengo la kuunga mkono jitihada za mkuu wa mkoa wa Geita za kila kijiji kuwa na Zahanati.
 Wananchi wa kijiji cha Ludete Kata ya Ludete Wilayani Geita wakishiriki katika uchimbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati katika kijiji hicho kwa lengo la kuunga mkono jitihada za mkuu wa mkoa wa Geita za kila kijiji kuwa na Zahanati.


Mheshimiwa Herman Kapufi Mkuu wa Wilaya ya Geita akitoa maelekezo kwa viongozi wa Halmashauri ya Geita na kata ya kakubilo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel katika Halmashauri hiyo kuhamasisha ujenzi wa Zahanati na vyumba vya madarasa.



WANANCHI KATA ZA LUDETE, KAKUBILO WAMKOSHA RC GEITA UJENZI WA ZAHANATI NA MADARASA ACHANGIA TOFALI  2000,MIFUKO 420 YA SARUJI
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel ameunga mkono jitihada za ujenzi wa Zahanati na Shule kata za Ludete na Kakubilo Halmashauri ya Geita kwa kuchangia matofali yenye thamani ya shilingi 2,400,000/= na kufanikisha harambee ya mifuko ya Saruji zaidi ya 420.

Mhandisi Robert Gabriel ameunga mkono jitihada za wananchi  baada ya kutembelea kata hizo na kuridhishwa na kazi za ujenzi wa Zahanati za vijiji na Shule zinazofanywa na wananchi kwa kujitolea kufanya kazi bila malipo, kuchangia vifaa mbalimbali vya ujenzi na kuchimba misingi.

Akiwa Kata ya Ludete Mkuu wa Mkoa amesema " Nimefurahi sana kuona namna mnavyoshiriki katika utekelezaji wa miradi hii niwaombe mshiriki kuanzia mwanzo hadi mwisho na msikubali mtu yeyote kuwavunja moyo kwa kuwa maendeleo ya Ludete yataletwa na wananchi wenyewe hivyo mimi ninawachangia matofali 1000 kwa ajili ya Zahanati na mengine 1000 ya kujenga vyumba vya madarasa shule ya Sekondari Ludete".

Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa Diwani wa Kata ya Ludete Sebastian Benedicto Mranda amesema kuwa wananchi wameamua kujitolea kushiriki  ujenzi wa Shule mpya ya msingi baada ya shule ya Msingi Ludete kuwa na Idadi ya wanafunzi 6,616  huku kukiwa na madarasa 20 yenye mikondo 108 ambao unasababisha msongamano wa wanafunzi darasani. 

Marando ameongeza kusema kuwa Kata ya Ludete haina Zahanati kwa muda mrefu hivyo wananchi wamejihamasisha kujenga ili wapate huduma katika maeneo yaliyo jirani pia kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Geita kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na Zahanati na shule ya msingi na Sekondari kwa Kata, Kata ya ludete ina wanafunzi 900 wanaotarajia kujiunga na elimu ya Sekondari ikiwa na uhaba wa zaidi ya vyumba vya madarasa 20.

Katika ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa amefanya harambee ambayo imefanikisha upatikanaji wa mifuko ya Saruji zaidi ya 420 na kuziagiza Halmashauri kutumia vikundi vya mafundi waliokatika maeneo ya miradi ili kupunguza gharama na kusimamia matumizi ya fedha za miradi hiyo.

Kutokana na Mkoa wa Geita kuwa na uhaba wa vyumba vya madarasa na Zahanati Serikali imeamua kushirikiana na wananchi kufanya kampeni ya mkoa mzima kuhamasisha wananchi kujitokeza kushiriki na kuchangia ujenzi wa miradi ya maendeleo ili wananchi wapate huduma katika majengo bora na mazingira salama.

ZAIDI YA RAIA 800 KUTOKA CONGO WAKIMBILIA KIGOMA KUHOFIA AMANI

 Mkuu   wa   Mkoa   wa   Kigoma   Brig.   Jen.   Emannuel   Maganga   (mwenye   kofia) akikagua makazi ya raia waomba hifadhi kutoka Congo DRC  katika kituo cha Kigadye Wilayani Kasulu.
  Baadhi ya raia kutoka Jamuri ya Kidemokrasia ya Congo DCR wakifuatilia ujio wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kigoma ilipowasili kukagua  kituo cha Kigadye Wilayani Kasulu.

   Baadhi ya raia kutoka Jamuri ya Kidemokrasia ya Congo DCR wakifuatilia ujio wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kigoma ilipowasili kukagua  kituo cha Kigadye Wilayani Kasulu.
 
    Mmoja wa waomba hifadhi akieleza mbele ya Kamati ya Ulinzi ya Mkoa sababu zilizo wafanya wakimbilie Tanzania

    Mwakilishi wa Shirika la kuhudumia wakimbizi  UNHCR Kigoma(mwenye kofia ya bluu)   akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Kigoma hali ya kituo cha kupokelea Wakimbizi Kigadye.

ZAIDI YA RAIA 800 KUTO CONGO WAKIMBILIA KIGOMA KUHOFIA AMANI
    Takribani   raia  800   kutoka   Jamhuri   ya   Kidemokrasia   ya   Kongo,   wamekimbilia
    Nchini Tanzania kuomba hifadhi ya ukimbizi katika kijiji cha Kigadye Wilayani
    Kasulu, Mkoani Kigoma wakihofia machafuko.

    Raia hao ambao wengi wao wanatoka maeneo ya Fizi na misisi Kivu kusini mwa
    Congo wamedai kuwa Vikosi na wapiganaji wa maimai nchi Congo na vikundi
    mbalimbali vya waasi vinavyoendelea kupigana nchini vimewatia hofu na  hivyo
    kuanza kukimbia nchini Tanzania kuomba hifadhi ya ukimbizi.

    Wakizungumza   mbele   ya   kamati   ya   ulinzi   na   usalama   ya   Mkoa   wa   Kigoma
    iliyotembelea katika kituo cha kupokelea waomba hifadhi kijiji cha Kigadye raia
    hao walisema sababu iliyowafanya kukimbilia Tanzania ni hofu ya usalama wa
    maisha yao kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya vikundi vya waasi na
    Serikali iliyopo madarakani.

    Mkuu   wa   Mkoa   wa   Kigoma   Brigedia   Jenerali   (mst.)   Emannuel   Maganga
    akiongoza kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa amesema tayari Mkoa umefika
    kuwaona   raia   hao   na   wanafana   jitihada   za   kuhakikishah   wanapatiwa   huduma
    muimu   za   kibinadamu   zinaboresha  katika   eneo   hilo wakati   kamati   ya  taifa   ya
    kusikiliza maombi ya ukimbizi inajiadaa kuwasikiiza raia hao.

    Kutokakana na wimbi kubwa hilo huduma za kibinadamu ikiwemo chakula, malazi
    zinahitajika haraka ili kuwahudumia raia hao ambao wengi wao ni kinamama na
    watoto.                  

    Baadhi   ya   raia   waliokimbilia   nchini   Tanzaia   wamedai   kuwa   kutokana   na
    kuahirishwa Uchaguzi Mkuu uliopaswa kufanika Desemba, 2017 dalili za kuzuka
    kwa mzozo wa mapigano uenda ukawaathiri amani nchini Congowa,  Vyama vya
    upinzanu   vimeanza   kuonesha   dalili   za   kupinga   kusitishwa   kwa   uchaguzi,
    wamehofia amani.

    Kituo cha kigadye wilayani kasulu, huenda kikashindwa kimili idadi kubwa ya raia
    wa Congo wanaoendelea kfika kituoni hapo kwa madai ya kukimbia vita nchini
    mwao. Kusini mwa Congo kumekuwa na matukio ya hivi karibuni mashambulio
    ya mara kwa mara yanayosabisha hofu ya machafuko kwa wananchi.


 
    Habari na Picha zimeandaliwa na.
    Gabriel Ng’honoli
    Afisa Habari
    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kigoma


Wednesday, November 22, 2017

HECHE ATOKA KWA DHAMANA, KURIPOTI DESEMBA NNE



Baada ya kuhojiwa kwa siku mbili mfululizo katika kituo cha polisi Morogoro Mbunge wa Tarime vijijini kupitia Chadema John Heche Novemba 21 ameachiwa kwa dhamana hadi desemba 4 atakapotakiwa kuripoti.

KWANINI WA-ZIMBABWE WANANCHUKIA GRACE MUGABE.

Grace Mugabe

Wakati mwisho wa utawala wa miaka 37 wa mume wake Aliyekuwa Rais Robart Mugabe wa Zimbabwe ukiwa wa aibu, sababu tano za wananchi wa taifa hilo kumchukia Grace Mugabe zimeanikwa.
Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya kijamii na magazeti ya nchi hiyo, Grace Mugabe alisababisha watu kumchukia kutokana na tabia yake ya kupenda kufanya manunuzi ya gharama ambayo yalisababisha kupewa jina la utani la First Shopper, badala ya first Lady. Manunuzi hayo yanadhaniwa kutumia fedha za umma.

Sababu nyingine inayotajwa kumfanya achukiwe ni ubabe, ambao aliounyesha katika matukio mbalimbali ya hadhara, alipokuwa akiongozana na mume wake katika shughuli za kisiasa. Katika hafla nyingi, Grace aliweza kuwafokea maofisa wa serikali hadharani na kumfanya kuogopwa kupita kiasi.
Licha ya sifa hizo, pia mwanamke huyo aliyezaa na Mugabe akiwa bado kwenye ndoa yake, anadaiwa kuwa mgomvi, kwani mara kadhaa ameripotiwa kuwapiga watu, wakiwemo waandishi wa habari na watu wa kawaida, kama ilivyokuwa mapema mwaka huu, alipompiga na kumuumiza msichana mmoja wa miaka 20 nchini Afrika Kusini, baada ya kumkuta akiwa na watoto wake wa kiume hotelini.

Jambo lingine lililomfanya kuchukiwa na wananchi wengi wa nchi hiyo ni tamaa yake ya madaraka, kwani licha ya kuwa kiongozi wa Jumuia ya wanawake wa Zanu PF, pia kwa nyakati tofauti alionyesha kutamani kuchukua nafasi ya mume wake, kitu kilichofanya wananchi wake kuona kama nchi inataka kuendeshwa kifamilia.

Inadaiwa hata kuondolewa kwa Makamu wa Rais Emmerson Mnangangwa, kulifanywa na Mugabe kwa shinikizo lake. Kitu kingine kinachowaudhi wananchi wa nchi hiyo ambayo fedha yake haina thamani kutokana na vikwazo kutoka nchi za Magharibi, ni kitendo chake cha kukosa heshima za kike, hasa tabia yake ya kuropoka hovyo katika hafla mbalimbali zinazohitaji staha kwa wanawake.

Hadi wakati gazeti hili likienda mtaani, bado haikujulikana alipo mwanamke huyo mzaliwa wa Afrika Kusini, baadhi ya habari zikisema amekimbilia Namibia, lakini wengine wakisema amedhibitiwa nchini Zimbabwe