Kwa ujumla inakadiriwa watu 40,000 watashiriki katika Utafiti wa THIS 2022-2023.
Washiriki watakaohusika katika utafiti huu ni wanawake na wanaume wenye umri wa miaka 15 au zaidi, ambao kaya zao zimechaguliwa na wameridhia kushiriki.
Kwa umakini darasani.
SIMBACHAWENE KUZINDUA UTAFITI WA VIASHIRIA NA MATOKEO YA UKIMWI 2022-2023
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,George Simbachawene anatarajia kuzindua utafiti wa pili kitaifa wa Viashiria na Matokeo ya Virusi vya Ukimwi (VVU) Tanzania (TANZANIA HIV IMPACT SURVEY-THIS 2022-2023)
Simbachawene atazindua utafiti huo jijini Mwanza Septemba,29,2022 kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,ambapo utahudhuriwa na Naibu Waziri wa Afya,Dk.Godwin Mollel,Balozi wa Marekani nchini,Donald Wrigh,Mtakwimu Mkuu wa Serikali,TAMISEMI,wadau na sekta mbalimbali.
Mkurugenzi Mkazi wa ICAP,Haruka Maruyama akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu utafiti huo amesema kuwa uzinduzi utafanyika katika mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar,ukilenga kuzifikia kaya takribani 20,000 sawa na watu 40,000.
Amesema utafiti huo wa pili utatathmini kushamiri kwa maambukizi mapya ya VVU na matokeo ya huduma za VVU katika jamii na kuangalia malengo ya Umoja wa Mataif ya kudhibiti UKIMWI (UNAIDS) 95-95-95.
Mayaruma amesema THIS 2022-2023 utatumia dodoso la kukusanya taarifa za upimaji wa VVU,Homa ya Ini B na Homa ya Ini C kwa hiari,ukihusisha kaya takribani 20,000 sawa na watu 40,000 wenye umri wa miaka 15 na kuendelea ambao kaya zao zimechaguliwa na kuridhia kushiriki.
Pia fursa ya upimaji wa VVU itatolewa kwa hiari na usiri katika kaya,hivyo ni muhimu wanakaya kupima na kufahamu hali zao za maambukizi ya VVU ikiwemo Homa ya Ini B na C, watakaobaini wataunganishwa na huduma za tiba matunzo,hivyo kuisaidia serikali na wadau wengine kuboresha huduma za afya,sera na mipango ya kudhibiti maambukizi ya VVU nchini.
“THIS 2023-2023 ni utafiti uliofanywa na Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali (ICAP) lililopo Chuo Kikuu cha Columbia Marekani,kwa usaidizi wa kitaalamu wa kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa kwa ufadhili wa Serikali ya Marekani chini ya Mfuko wa Dharura wa Kupambana na UKIMWI unaolenga kutathmini matokeo ya afua mbalimbali za kinga,tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU' amesema Mayaruma na kuongeza;
“Utafiti huo utatoa mwongozo kwa serikali na wadau wengine kutekeleza malengo ya UNAIDS 95-95-95 ya kudhibiti janga la UKIMWI kufikia 95 asilimia ya watu wote wanaioshi na VVU kufahamu hali zao, 95 ya waliogundulika watapatiwa huduma za matibabu na asilimia 95 wanaoishi na VVU wajue kiwango cha VVU mwilini.”
Amesema taarifa za utafiti huo ni muhimu kwa kuwa zitasaidia Tanzania kufikia malengo ya 95-95-95 na kuweza kudhibiti VVU ifikapo 2030,pia utafiti utatumika kupima maambukizi ya homa ya ini B na homa ya ini C kwa hiari.
Mayaruma amesema THIS 2022-2023 ni mwendelezo wa ule wa awali wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi uliofanyika katika ngazi ya kaya Oktoba 2016 hadi Agosti 2017, hivyo utawapa viongozi wa serikali,wafanyakazi wa afya,asasi za kiraia na watafiti,mwongozo wa kipekee wa kufanya maamuzi juu ya sera ya VVU,programu,ufadhili na kuwezesha familia kuwa na afya bora na taifa lenye ustawi.
Imeelezwa kuwa utafiti huo wa kitaifa utahusisha kaya za maeneo mbalimbali ili kufahamu idadi ya maambukizi mpya ya VVU,ushamiri wa VVU/UKIMWI na waliopo katika matibabu ni miongoni mwa washiriki kuanzia umri wa miaka 15 na kuendelea.
Mkurugenzi huyo Mkazi wa ICAP ameleza kuwa ushauri nasaha utatolewa,watafiti watachukua sampuli ya damu kutoka mkononi kwa ajili ya kupima,majibu yatatolewa siku hiyo hiyo na watakaobainika kuwa maambukizi ya VVU watapewa rufaa katika vituo vya afya walivyochagua kwa usimamizi zaidi na usiri utazingatiwa.
Ameongeza THIS 2022-2023 itatoa mwongozo ngazi ya kitaifa katika kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa taarifa,kuongeza miundombinu ya maabara na uwezo wa rasilimali watu,taarifa za uelewa wa kina kuhusu mwitiko wa kitaifa katika kudhibiti VVU,mgawanyiko wa tabia hatarishi za VVU na utumiaji wa huduma za tiba na matunzo zitatolewa.
Kwa mujibu wa takwimu kiwango cha maambukizi ya VVU kitaifa ni kiwango cha 4.2 Tanzania Bara ambapo mkoa wa Njombe unaongoza kwa kuwa na kiwango cha 11.4,Iringa 11.3,Mbeya 9.3,Mwanza 7.2,Kagera ikiwa na kiwango cha 6.5 ambapo mgonjwa wa kwanza alipatikana hapa nchini 1981.
Takwimu za matumizi ya dawa za kufubaza (ARV’s) mkoa wa Lindi unaongoza kwa kiwango cha zaidi ya 100,Kilimanjaro 66.8,Kagera 66.0,Songwe 64.6,Pwani 63.5,Mara 63.4,Dodoma Njombe 60.5 huku mikoa inayobaki ikiwa chini ya kiwango cha 60 cha matumizi ya dawa hizo.
Kwa upande wa Zanzibar Mkoa wa Kaskazini Unguja, unaongoza kwa matumizi ya dawa za ARV’s ukiwa na kiwango cha 44.5 ikielezwa sababu ni mwingiliano wa watu kibiashara na utalii ambapo Mjini Magharibi una asilimia 21.0.
Maambukizi ya VVU Mkoa wa Kaskazini Unguja una kiwango cha 0.6 sawa na Mjini Magharibiki huku Kusini Pemba ikiwa na kiwango cha 0.3.