ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, January 9, 2020

MBUNGE ATEKELEZA AHADI YA USAFIRI WA BAISKELI KWA VIONGOZI UWT UKEREWE




Mbunge atekeleza ahadi ya usafiri wa baiskeli kwa viongozi wa Jumuiya ya Wanawake(UWT) Wilaya ya Ukerewe ngazi ya Kata zote 25 ambazo wataxiyumia kusaka kura za Rais Dkt John Pombe Magufuli, Wabunge na Madiwani na kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo mwezi Oktoba mwaka huu. 

PICHA ZOTE NA PETER KATULANDA.

MFUMUKO WA BEI MWEI DISEMBA 2019 WABAKI KUWA ASILIMIA 3.8


Kaimu Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Bi. Ruth Minja akizungumza wakati akitangaza mfumuko wa bei wa mwezi Desemba 2019.
Na Mwandishi Wetu
Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2019 umebaki kuwa asilimia 3.8 kama ilivyokuwa  mwezi Novemba, 2019.
Akizungumza na waandishi wa habari  leo Jijini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa ya hali ya mfumuko wa bei, Kaimu mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Bi Ruth Minja amesema kuwa mfumuko wa Bei wa mwezi Desemba, 2019 umebaki kuwa sawa kama ilivyokuwa mwezi Novemba,2019 hali iliyochangiwa na kuongezeka na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia  Desemba, 2019 ikilinganishwa na mwezi Desemba 2018.
“Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizoongezeka bei kwa mwezi Desemba, 2019 zikilinganishwa na bei za mwezi Desemba 2018 ni pamoja na;mchele asilimia 7.0, mtama kwa asilimia 3.3, nyama kwa asilimia 2.3, maharage asilimia 7.7, na viazi mviringo kwa asilimia 2.7”; alisisitiza Minja
Akifafanua amesema kuwa bidhaa zisiszo za vyakula  kwa mwezi  Desemba 2019zilipungua bei ikilinganishwa na mwezi Desemba, 2018, Bidhaa hizo ni pamoja na gesi ya kupikia kwa asilimia 2.1, mafuta ya taa kwa asilimia 7.1,jiko la kupikia la gesi kwa asilimia 1.6, mafuta ya petrol I asilimia 8.7 na dizeli asilimia 8.7.
Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwaka unaoishia mwezi Desemba, 2019 umeongezeka kwa asilimia 6.3 kutoka asilimia 6.1 kwa mwaka unaoishia mwezi Novemba, 2019.
Aidha, Mfumuko wa Bei wa Taifa kutoka mwezi Januari 2019, umepungua hadi  asilimia 3.4 mwaka 2019 kutoka asilimia 3.5 mwaka 2018.
Kwa upande mwingine, Wastani wa Mfumuko wa Bei wa Bidhaa zisizo za vyakula kwa mwaka 2019 ulipungua hadi asilimia 4.0 kutoka asilimia4.3 ilivyokuwa mwaka 2018.
Kwa upande wa nchi ya Kenya mfumuko wa Bei kwa mwezi Desemba, 2019 umeongezeka hadi asilimia 5.82 kutoka asilimia 5.56 kwa mwaka ulioishia mwezi  Novemba,2019, Wakati nchini Uganda kwa mwezi unaoishia Desemba,2019 mfumuko wa bei umeongezeka hadi asilimia 3.6 kutoka asilimia 3.0 kwa mwaka unaoishia mwezi Novemba 2019.

KITUO CHA PILI NCHINI CHA KUPIMA NA KUHAKIKI MATENKI YA MALORI YA MAFUTA CHAANZA KUFANYA KAZI MWANZA



WAMILIKI wa Malori ya kubeba mafuta kwa mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Kagera, Simiyu, Geita na mikoa jirani na Kanda ya Ziwa sasa hawato ingia gharama ya kuchoma mafuta kusafirisha maroli yao hadi jijini dar es salaam kwaajili ya kupata huduma ya upimaji na uhakiki matenki yao kila mwaka mara baada ya Serikali kusimika kituo cha kisasa cha upimaji katika eneo .la Nyamhongolo wilayani Nyamagana jijini Mwanza. Hiki ni kituo cha pili cha upimaji matenki ya magari ya kubebea mafuta nchini kikitanguliwa na kile cha jijini Dar es salaam. Meneja wa wakala wa vipimo mkoani Mwanza Arobogast Kajungu anasema malengo ya Serikali katika kuwahudumia wafanyabiashara wa mafuta Kanda ya Ziwa yametimia.

Wednesday, January 8, 2020

WHO: UGONJWA WA SURUA ULIUA WATU 6000 NCHINI DRC, 2019.

WHO: Ugonjwa wa surua uliua watu 6000 nchini DRC, 2019

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, watu 6,000 walipoteza maisha kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa surua (measles) nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mwaka uliomalizika 2019.

WHO imetoa mwito wa kupatiwa fedha zaidi ili kupambana na mlipuko huo unaoaminika kuwa mkubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kufikia sasa, WHO imeweza kupokea dola milioni 27.6 za Marekani, ingawaje inahitaji dola milioni 40 zaidi ili kupanua shughuli ya kutoa chanjo kwa watoto kati ya miaka 6 na 14, katika kipindi cha miezi sita ijayo.

Dakta Amedee Prosper Djiguimde, afisa wa Shirika la Afya Duniani nchini Kongo DR amesema, "Maelfu ya familia za Wakongomani wanahitaji misaada yetu ili kuzikwamua kutoka kwenye mgogoro huo wa kiafya. Hatuwezi kufanya chochote iwapo hatuna fedha."

Chanjo ya surua
Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), asilimia 74 ya wagonjwa hao wa surua ni watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano na mbaya zaidi ni kuwa, takribani asilimia 90 ya vifo ni watoto wa umri huo.
Takwimu zinaonyesha kuwa katika mwaka uliomalizika wa 2019, takribani maambukizi laki 3 yanayodhaniwa kuwa ni ya surua yaliripotiwa.

KIONGOZI MUADHAMU : TUMEMPIGA KIBAO TU ADUI, ANACHOPASWA MAREKANI NI KUONDOKA ENEO HILI.

Kiongozi Muadhamu: Tumempiga kibao tu adui, anachopaswa kufanya Marekani ni kuondoka eneo hili
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, mashambulio ya makombora yaliyofanywa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH katika kambi mbili za Marekani nchini Iraq ni kibao cha uso tu alichopigwa adui huyo.
Amesema, majibu ya Iran hayatoishia hapo kwani kinachotakiwa hasa ni kuangamizwa kikamilifu uwepo wa kifisadi na kiharibifu wa Marekani katika eneo hili zima.
Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo asubuhi (Jumatano) wakati alipoonana na maelfu ya wananchi wa Qum na huku akitilia mkazo uhakika kwamba mataifa ya eneo hili na tawala zilizotokana na wananchi, bila ya shaka yoyote hazitaki kuona Marekani inaendelea kuwepo katika eneo lao, amesema, kuwepo Wamarekani kwenye eneo hili na katika sehemu yoyote ile duniani hakuna matokeo mengine isipokuwa vita, ugomvi, fitna na kuharibiwa miundombinu ya eneo hilo.

Vile vile amezungumzia nafasi ya kipekee isiyo na mbadala ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani katika kufelisha njama za Marekani huko Palestina, Iraq na Lebanon na kuongeza kuwa, shahid Luteni Jenerali Soleimani alifanikiwa kuvunja na kufelisha njama zote za Marekani zilizotumia fedha nyingi, mabavu, uchochezi wa kisiasa na uundaji wa makundi mbalimbali.
Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa, tunaposema "adui" tunakusudia Marekani, utawala wa Kizayuni na majimui ya vibaraka wao na kuongeza kuwa, baadhi ya tawala za ndani na nje ya eneo hili hazipaswi kuingizwa kwenye kundi hilo la adui hadi pale zitakapochukua hatua ya kumtumikia adui.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amesisitiza kuwa, muswada uliopasishwa na bunge la Iraq wa kufukuzwa wanajeshi wa Marekani nchini humo ni hatua nzuri sana na tunamuomba Mwenyezi Mungu alete taufiki ya kuendelea jambo hilo katika nchi nyinginezo.

SADIO MANE ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA AFRIKA 2019 🏆 JUU YA SALAH NA MEHREZ



Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane amenyakuwa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2019, katika sherehe iliyofanyika usiku uliopita nchini Misri katika eneo la ufukwe wa Hurghada.
.
Mane amemshinda mchezaji mwenzake wanayekiputa klabu moja Mohamed Salah wa Misri na Mahrez aliyeiongoza Algeria akiwa nahodha katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika yakiyofanyika mwaka jana nchini Misri na anayekiputa katika klabu ya #ManchesterCity 

✂HII HAPA ORODHA YA WACHEZAJI WANAOUNDA KIKOSI CHA FifPro Africa Best XI  FOR 2019

Andre Onana (GK) 🇨🇲
Serge Aurier 🇨🇮
Joel Matip 🇨🇲
Kalidou Koulibaly 🇸🇳
Achraf Hakimi 🇲🇦
Idrissa Gana Gueye 🇸🇳
Riyad Mahrez 🇩🇿
Hakim Ziyech 🇲🇦
Mohamed Salah 🇪🇬
Pierre-Emerick Aubameyang 🇬🇦 
Sadio Mané 🇸🇳

#CAFAwards2019

Tuesday, January 7, 2020

MKWASA ATANGAZWA KUWA KOCHA BORA MWEZI DISEMBA


Kaimu Kocha wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, ametangazwa kuwa kocha bora kwa mwezi uliopita.


Mkwasa ametwaa tuzo ya ukocha bora ikiwa ni muda mchache tangu achukue nafasi hiyo Yanga baada ya kuondoka kwa Mwinyi Zahera ambaye alikuwa anaiona timu hiyo.

MAOFISA FEKI WA IKULU WANASWA NA POLISI WAKIWA NA AMBULANCE

🔴Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limefanikiwa kuwakamata watu saba kwa tuhuma za kujifanya maofisa usalama wa Taifa kutoka Ikulu, ambao wamekuwa wakiwatapeli wananchi na baadhi ya watumishi wa serikali katika Jiji la Mwanza.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza ACP Muliro Muliro, amesema matukio hayo yametokea kati ya Desemba 27, mwaka jana na Januari 2, mwaka huu, Nyakato wilayani Nyamagana, walipokuwa wanatumia gari lenye NA. T.751 BNL, aina ya Toyota Ambulance, ambalo walidai ni sehemu ya msafara wa viongozi wakuu.

Kamanda aliwataja Watuhumiwa waliokamatwa ni Chalanga Chalanga (45) Mkazi wa Pasiansi na Arusha Hamis Mwalimu (25) Fundi magari, kujifanya bodygurd wà Chalanga Chalanga, Philipo Petro (35), Mkazi wa Usagara Misungwi, pia dereva wa Chalanga Chalanga, Elia Gunda (30) anayedai yeye ni mchungaji wa Kanisa la EAGT liliopo Kisesa pia Mkazi wa Kisesa. Hassan Juma (29) Mkazi wa Mkolani Fundi wa IT, Seleman Karanga (25), anajifanya Mlinzi Mkuu wa Chalanga Chalanga na Afisa Mkuu wa Ikulu Michael Mazige Mkazi wa Morogoro.

Monday, January 6, 2020

KIVUKO KIPYA CHA MV ILEMELA CHASHUSHWA ZIWA VICTORIA KWA MARA YA KWANZA.


TANGU dunia kuumbwa hata nchi yetu kupata Uhuru Wananchi wa Kisiwa cha Bezi mkoani Mwanza hawajawahi kuwa na kivuko au usafiri wa uhakika wa meli zaidi ya kutumia mitumbwi na boti ndogo kusafiri na kusafirisha mizigo yao kusaka huduma muhimu toka maeneo tofautitofauti hali ambayo imesababisha mara kadhaa wananchi hao wasafiri kukumbwa na madhila mbalimbali yaliyoletwa na ajali.

Hatimaye Leo tarehe 6 mwezi Januari 2020 Ahadi ya Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt. Angeline Mabula ya kutatua kero ya usafiri wa uhakika kwa wananchi wa visiwa hivyo aliyoitoa kipindi cha uchaguzi mkuu 2015 imetimia baada ya serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kujenga kivuko chenye uwezo wa kubeba abiria 200, tani 10 za mizigo na magari 10 na kukiingiza majini ziwani Victoria tayari kuanza kutoa huduma ya usafiri. 

 Akizungumza na wananchi hao wakati wa kukiingiza kivuko hicho katika ziwa Victoria, Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditie amesema kivuko hicho kimejengwa baada ya wananchi kuwasilisha vilio vyao.

Mradi huo umetekelezwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano chini ya usimamizi wa Wakala wa Ufundi na Umeme TAMESA baada ya kampuni ya ujenzi na utengenezaji meli ya Songora Marine kushinda zabuni ya utengenezaji wa kivuko hicho.

Mbunge wa Jimbo la Ilemela Angeline Mabula ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesema kituo hicho kitafuta machozi ya wananchi huku Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akiipongeza Serikali kwa ukamilishaji wa ujenzi wa kivuko hicho.

Kukamilika kwa kivuko hicho kunakwenda sambamba  na ujenzi wa vivuko vingine viwili vya Mv Chato na Mv Ukara vinavyotarajiwa kukamilika Februari Mwaka huu ili kuanza kuhudumia wananchi.











 Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni iliyotengeneza kivuko hicho ya Songoro Marine Ltd ya jijini Mwanza, Meja Songoro ameishukuru Serikali kwa kuiamini kampuni yake na kuikabidhi tenda kadhaa ikiwemo ya ujenzi wa meli hiyo na nyinginezo nchini kwani kwa mfumo huo, serikali inazidi kuvijengea uwezo viwanda vyake vya ndani.

Awali, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle, akisoma taarifa kwa mgeni rasmi katika tukio hilo alisema serikali kupitia TEMESA inaendelea na ujenzi wa vivuko vingine vipya kwa ajili ya Mafia Nyamisati kwa gharama ya shilingi bilioni 5.3, Bugorola Ukara kwa gharama ya shilingi bilioni 4.2 pamoja na Chato Nkome kwa gharama ya shilingi bilioni 3.1.


Ujenzi wa kivuko cha Mv Ilemela umegharimu kiasi cha bilioni 2.7. 

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA VITUO VYA KISAYANSI PEMBA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Viongozi na Wananchi wa Pujini katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Pujini Wilaya ya Chakechake Kisiwani Pembalepo Januari 06,2020 baada ya kuweka Jiwe la Msingi Kituo cha Ubunifu wa Kisayansi kwa niaba ya Vituo 22 vya Unguja na Pemba  ikiwa ni moja ya Shamrashamra za kuelekea kwenye Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yanayotegemewa kuadhimishwa tarehe 12 January 2020 katika Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.

 Viongozi na Wananchi wa Pujini kisiwani Pemba wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassa wakati alipokuwa akihutubia Wananchi wa Pujini Wilaya ya Chakechake Kisiwani Pemba baada ya kuweka Jiwe la Msingi Kituo cha Ubunifu wa Kisayansi kwa niaba ya Vituo 22 vya Unguja na Pemba leo tarehe 06 Januari 2020 ikiwa ni moja ya Shamrashamra za kuelekea kwenye Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yanayotegemewa kuadhimishwa tarehe 12 January 2020 katika Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo ya Ujenzi cha Kituo cha Ubunifu wa Kisayansi kwa niaba ya Vituo 22 vya Unguja na Pemba katika Kijiji cha Pujini Wilaya Chake chake Mkoa wa kusini Pemba baada ya kuweka Jiwe la msingi  ujenzi wa Vituo hivyo leo tarehe 06 Januari 2020  ikiwa ni moja ya Shamrashamra za kuelekea kwenye Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yanayotegemewa kuadhimishwa tarehe 12 January 2020 katika Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.Kulia ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Simai Mohammed Said.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba Mhe. Hemedi Suleiman Abdalla alipowasili Uwanja wa Ndege wa Chakechake kisiwani Pemba leo tarehe 06 Januari 2020  kwa ajili ya kuweka  Jiwe la Msingi Kituo cha Ubunifu wa Kisayansi kwa niaba ya Vituo 22 vya Unguja na Pemba katika Kijiji cha Pujini Wilaya Chake chake Mkoa wa kusini Pemba  ikiwa ni moja ya Shamrashamra za kuelekea kwenye Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yanayotegemewa kuadhimishwa tarehe 12 January 2020 katika Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.

(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

KOCHA WA MANCHESTER UNITED AMPIGA BITI MCHEZAJI WAKE KUHUSU MITANDAO YA KIJAMII.

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer alimemueleza mshambuliaji wake Jesse Lingard aachane na matumizi ya mtandao ya kijamii ili arudishe kiwango chake kilichozorota hivi karibuni.

Jesse Lingard amekuwa na kiwango kibovu hivi sasa ndani ya klabu hiyo, akiwa hajafunga bao lolote au kutoa 'assist' katika ligi kuu ndani ya mwaka 2019, huku pia akiachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza.


Akizungumza kuelekea mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Kombe la Carabao kesho Januari 7, Solskjaer amesema, "tunamuhitaji Lingard kwenye ufungaji na kutoa 'assist'. Sidhani kama Jesse anaonekana sana kwenye mitandao kwa sasa kama mlivyokuwa mkimuona hapo nyuma, anajituma kwa nguvu ili aweze kurejea yule Jesse niliyemjua".


Alipoulizwa kuhusu matumizi ya mitandao kwa wachezaji, Solskjaer amesema, "ni moja ya majukumu ya kuwa mchezaji wa Man United, ninaongea sana na wachezaji juu ya namna ya kuishi katika mitandao. Mimi sina mambo haya ya mitandao lakini kumbuka hiki ni kizazi tofauti".

Man United itawakaribisha mahasimu wao wa mji mmoja, Manchester City katika dimba la Old Trafford Jumanne hii kwenye mchezo wa kwanza wa kombe la Carabao, ikiwa na majeraha kadhaa mpaka sasa akiwemo Jesse Lingard, Anthony Martial na Luke Shaw ambao walikosekana kwenye mchezo uliopita dhidi ya Wolves, ambapo amesema mpaka kufikia mapema Jumanne atajua kama ataweza kuwatumia baadhi yao.

AGIZO LA JPM SHULE YA ISENI B KASI YA UTEKELEZAJI WAKE YAMSHANGAZA JAFO.


AGIZO la Rais John Magufuli alialolitoa Desemba 7, mwaka jana (2019) na kuutaka uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, kujenga madarasa matano katika Shule ya Msingi Iseni B katika Halmashauri hiyo, limetekelezwa kwa zaidi ya asilimia 90.

Akizungumza mwishoni mwa wiki akiwa shuleni hapo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo ameupongeza uongozi wa mkoa na jiji la Mwanza kwa utekelezaji wa agizo hilo uliofanyika ndani ya mwezi mmoja na sasa umefikia hatua ya upauaji.

Sunday, January 5, 2020

MWANZA IMEJIPANGA HIVI KUFIKIA MALENGO SEKTA YA ELIMU



Ni katika Tamasha la utoaji TUZO ZA UMAHIRI KATIKA ELIMU MKOA WA MWANZA zilizoanzishwa na wadau wa elimu mkoa huo kama sehemu ya mkakati wa kuimarisha na kuongeza kiwango cha ufaulu kimkoa ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Serikali za Mitaa TAMISEMI, Selemani Jafo.

Hizi ni kauli za wasemaji mbalimbali waliopata nafasi ya kuwasilisha mapendekezo yao mbele ya Waziri wa OR TAMISEMI pamoja na halaiki ya hafla hiyo ya tuzo iliyotanguliwa na michezo mbalimbali ya ufunguzi kama chachu ya kujenga mahusiano.

MHUBIRI AMUUA MKEWE WAKATI WA IBADA


Mhubiri Elisha Misiko wa kanisa la Ground for Jesus, lililoko mjini Mombasa nchini Kenya, amemuua mke wake kwa kumchoma na kisu na kisha yeye kujikata koo lake na kufariki papo hapo, wakati wa ibada ya Jumapili ikiendelea kanisani hapo.

Tukio hilo limetoa leo Januari 5, 2020, ambapo kwa mujibu wa waumini wa kanisa hilo wamesema kuwa mhubiri huyo alitekeleza unyama huo kwa haraka sana na kwamba juhudi za kuwanusuru wawili hao hazikuzaa matunda.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa eneo la Kisauni, Julius Kiragu, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea majira ya saa 4:00 asubuhi ya leo na kwamba Jeshi la Polisi mjini Mombasa, limekwishaanza kufanya uchunguzi ili kubaini nini chanzo kilichopelekea mume kumuua mkewe na kisha yeye naye kujikata koromeo.

Aidha Kamanda Kiragu amesema kuwa ndani ya mfuko wa suruali wa mhubiri huyo wakati wakiondoa mwili wake na kuupeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti, wamekuta barua yenye kurasa 17, iliyokuwa ikieleza chanzo cha mauaji hayo kuwa ni migogoro ya kifamilia.

PROF PLO LUMUMBA SPEAKS TO AFRICAN LEADERS.


Patrick Loch Otieno Lumumba (alizaliwa 17 Julai 1962) ni Mkenya aliyekuwa Mkurugenzi wa Tume ya Kupambana na Rushwa ya Kenya kutoka Septemba 2010 hadi Agosti 2011 na sasa ni Mkurugenzi wa Shule ya Sheria ya Kenya tangu mwaka 2014.

Lumumba ni mwanasheria mwenye ujuzi wa kuzungumza hadharani, na ana shahada ya Udaktari wa Falsafa katika sheria za bahari kutoka Chuo Kikuu cha Ghen nchini Ubelgiji.

MMILIKI MABASI YA SAHARA AKUTWA AMEKUFA KWENYE NYUMBA YA WAGENI.

 Mfanyabiashara na mmiliki wa mabasi ya Sahara, Abdalah Msangi (47) mkazi wa Usangi Mkoani Kilimanjaro, amekutwa amekufa kwenye moja ya nyumba ya wageni iliyopo Mtaa Dar es Salaam Mjini Moshi.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumapili Januari 5, 2020, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Tanzania, James Manyama amethibitisha kutokea kwa kifo hicho.

Amesema mfanyabiashara huyo alikuwa na rafiki yake wa kike chumbani, lakini baada ya kuona mwenzake anaishiwa nguvu na kuanza kutokwa na povu puani na mdomoni akakimbia.

“Huyu Mfanyabiashara alikuwa na rafiki yake wa kike kwenye chumba cha wageni huko Dar es Salaam street, baada ya kuona ameishiwa nguvu na kuanza kutokwa na povu mdomoni alitoroka, amedai Kamanda Manyama.

Aidha, amesema baada ya kupata taarifa na kufika eneo la tukio na kulipekua gari la Msangi kulikutwa dawa ya kienyeji ambayo imechukuliwa kwa uchunguzi.

Amesema Mwili wa marehemu umepelekwa Hospitali ya Mkoa Mawenzi  kwa uchunguzi zaidi.