ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, January 6, 2020

KOCHA WA MANCHESTER UNITED AMPIGA BITI MCHEZAJI WAKE KUHUSU MITANDAO YA KIJAMII.

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer alimemueleza mshambuliaji wake Jesse Lingard aachane na matumizi ya mtandao ya kijamii ili arudishe kiwango chake kilichozorota hivi karibuni.

Jesse Lingard amekuwa na kiwango kibovu hivi sasa ndani ya klabu hiyo, akiwa hajafunga bao lolote au kutoa 'assist' katika ligi kuu ndani ya mwaka 2019, huku pia akiachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza.


Akizungumza kuelekea mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Kombe la Carabao kesho Januari 7, Solskjaer amesema, "tunamuhitaji Lingard kwenye ufungaji na kutoa 'assist'. Sidhani kama Jesse anaonekana sana kwenye mitandao kwa sasa kama mlivyokuwa mkimuona hapo nyuma, anajituma kwa nguvu ili aweze kurejea yule Jesse niliyemjua".


Alipoulizwa kuhusu matumizi ya mitandao kwa wachezaji, Solskjaer amesema, "ni moja ya majukumu ya kuwa mchezaji wa Man United, ninaongea sana na wachezaji juu ya namna ya kuishi katika mitandao. Mimi sina mambo haya ya mitandao lakini kumbuka hiki ni kizazi tofauti".

Man United itawakaribisha mahasimu wao wa mji mmoja, Manchester City katika dimba la Old Trafford Jumanne hii kwenye mchezo wa kwanza wa kombe la Carabao, ikiwa na majeraha kadhaa mpaka sasa akiwemo Jesse Lingard, Anthony Martial na Luke Shaw ambao walikosekana kwenye mchezo uliopita dhidi ya Wolves, ambapo amesema mpaka kufikia mapema Jumanne atajua kama ataweza kuwatumia baadhi yao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.