ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 25, 2019

Friday, May 24, 2019

TTHERESA MAY KUJIUZULU KAMA WAZIRI MKUU WA UINGEREZA JUNI 7


Theresa May kujiuzulu kama kiongozi wa chama cha Conservative tarehe 7 Juni na kutoa fursa kuidhinishwa mchakato wa kuchaguliwa waziri mkuu mpya Uingereza.

Katika taarifa iliojaa hisia alioitoa huko Downing Street, Bi May amesema amefanya "kila awezalo" kutekeleza matokeo ya kura ya maoni kuhusu EU ya mnamo 2016.

Ni jambo linalosalia kuwa "na majuto mengi" kwamba ameshindwa kutimiza Brexit - Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, ameongeza.

Lakini waziri mkuu mpya ndio suluhu " kwa manufaa ya taifa".

Bi May amesema ataendelea kuhudumu kama waziri mkuu wakati kukitarajiwa kuidhinishwa mchakato wa kumchagua kiongozi mpya wa chama cha Conservative.

Atajiuzulu kama kiongozi wa chama hicho Juni 7 na uteuzi wa waziri mkuu mpya unatarajiwa kuanza wiki inayoafuata baada ya hatua hiyo.

SEVILLA YAICHAPA SIMBA BAO 5-4, YACHUKUA KIKOMBE CHA URAFIKI


Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe, Harrison Mwakyembe (kulia) akitoa zawadi ya kikombe kwa mchezaji wa timu ya Sevilla mara baada ya kushinda mechi yao ya kirafiki na timu ya Simba SC uliofanyika May 23, 2019 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mechi hiyo ilikuwa imedhaminiwa na Kampuni ya SportPesa.
Wachezaji wa Simba SC na Sevilla ya Hispania wakifurahia pamoja mara baada ya kumaliza mechi yao ya kirafiki iliyochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Muonekano wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ukitokea kwa juu.

AIRPORT SIO UCHOCHORO WA KUPITISHA MAGENDO - IGP SirroMkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP,  Simon Sirro amesema kuwa, maeneo ya viwanja vya ndege hususani kiwanja cha ndege Dar es salaam kamwe hakitakuwa uchochoro wa kupitisha na kusafirisha magendo, biashara ya binadamu, nyara za serikali pamoja na dawa za kulevya.

IGP Sirro ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya ukaguzi katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) Terminal III kwa lengo la kujionea maendeleo ya ujenzi wa kiwanja hicho ambacho hadi sasa ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99.

Aidha, IGP Sirro, amesema kuwa, Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha hali ya usalama inakuwepo kiwanjani hapo na kwamba hakuna mtu atakaye jaribu kuutumia uwanja mpya wa ndege terminal III kwa vitendo vya kuhujumu uchumi wa taifa letu.

BREAKING: RAIS MAGUFULI AONDOKA NCHINI, AKIONGOZAN NA Dkt. KIKWETE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesafiri leo kuelekea nchini Afrika kusini huku akiongozana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.


Thursday, May 23, 2019

UMOJA WA VYAMA VYA WAANDISHI WA HABARI NCHINI TANZANIA UTPC WAMPA SHAVU JPM


UMOJA wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (Union of Tanzania Press Clubs -UTPC), umekamilisha taratibu za kulichukua Shirikisho la Klabu za Waandishi wa Habari katika nchi za Afrika na Karibiani (African and Caribbean Press Club-ACP) ambapo makao makuu yake yatakuwa jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan aliyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya sheria mbalimbali za habari kwa waandishi wa habari wa Vyombo vya Habari Mbadala (Alternative Media) yaliyofanyika Morena Hoteli jijini Dodoma kwa siku mbili kuanzia Mei 21, 2019 hadi Mei 22,2019.

“Waambieni watanzania jambo hilo, waambieni watu wasioijua UTPC jambo hilo, waambieni watu wenye mashaka na UTPC jambo hilo, kwamba sasa tunaisimamia “Federation” (shirikisho) ya nchi zaidi ya 160” alisema Karsan akisisitiza kwamba hilo si jambo dogo bali ni hatua kubwa.

Wednesday, May 22, 2019

GAVANA AAGIZA UTENDAJI MZURI MAKAZINI.

picha ikionyesha Mkurugenzi Mkuu wa Bodi yaTaifa ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu(NBAA),Pius Maneno akoongea na waandishi wa habari hii leo

picha ikionyesha baadhi ya washiriki pamoja na viongozi wakiwa katika picha ya pamoja

Na Woinde Shizza,Arusha
GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania(BOT)Florence Luoga,amewaagiza wahasibu na wakaguzi wa mahesabu hapa nchini kuhakikisha kuwa wanafanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya kazi ikiwa ni pamoja na kufanya kazi zao kwa weledi ili kuepuka malalamiko ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakiikumba kada hiyo
Aliyasema hayo leo alipokuwa akifungua mkutano wa bodi ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu hapa nchini(NBAA)unaondelea jijini hapa na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo kutaongeza imani ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu kwa jamii na taasisi wanazozihudumia.
“Ni vyema wahasibu kote nchini kuhakikisha kuwa malipo yote yanayofanyika yapitie katika taasisi za kifedha,ikiwemo mabenki taasisi hizo ziweze kujiendesha na serikali iweze kujiongezea kipato kwa lengo la kukuza pato la Taifa”alisema Luoga.
Ameongeza kuwa endapo watafuata utaratibu huo utasaidia kuondokana na changamoto ya malipo hewa pamoja na kukabiliana na tatizo kubwa la uingizwaji na uzagaaji wa fedha haramu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi yaTaifa ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu(NBAA),Pius Maneno amesema kuwa lengo la mkutano huo wa siku tatu ni kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu.
Ameongeza kuwa katika mkutano huo mada kumi na moja  zitawasilishwa na kujadiliwa zikiwemo za fedha,Tehama,uadilifu pamoja na muongozo wa wahasibu na wakaguzi wa mahesabu kuhusiana na suala zima la fedha haramu ikiwemo kanuni za nidhamu.
“Bodi ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu hapa nchini imeendelea kuwaelimisha wahasibu na wakaguzi wa mahesabu hapa nchini juu ya kufanya kuzingatia wajibu na weledi pindi watekelezapo majukumumu yao ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wale wote wanaokiuka maadili”alisema Mkurugenzi mtendaji huyo.
Mkurugenzi mtendaji huyo amesema kuwa bodi yake imetunga muongozo ulioanza kutumika tarehe 1aprili  mwaka huu kwa wafanyabiashara wadogo wadogo kuhakikisha kuwa wanakagua mahesabu yao lengo likiwa ni kuongeza kodi na tarehe 1 mei umeanza kutumika  muongozo wafedha hamu na tarehe 15juni zitaanzakutumika kanuni za uadilifu.
Amesema kuwa mkutano huu unashirikisha watu mia tatu ambao ni wahasibu na wakaguzi wa hesabu z kutoka taasisi na mashirika mbalimbali,maafisa kutoka Benki Kuu(BOT),nabenki nyinginezo,wataalamu wa fedha na taasisi za Bima.

Tuesday, May 21, 2019

MBUNGE AMWAGA SABABU KWANINI ATAKA KILIMO CHA BANGI KIRUHUSIWE.


Mbunge wa Kahama Mjini (CCM),   Jumanne Kishimba ameishauri Serikali ya Tanzania kuruhusu kilimo cha  bangi nchini kwa ajili ya utengenezaji wa dawa za binadamu.

"Amebainisha dawa nyingi za maumivu ya saratani asilimia 80 zinatokana na bangi, “Nashangaa wataalam wetu wa Mamlaka ya Chakula la Dawa (TFDA) wangekuwa wameshachukua sampuli na wangewajulisha kuwa dawa zilizo na bangi ndani yake,” amesema hayo Bungeni jijini Dodoma katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Kilimo mwaka 2019/2020.

“Wangemuuliza  msambazaji hiyo bangi anaitoa wapi? Spika sisi wenyewe tunayo bangi hiyo tunaona kila siku inakatwa ukweli nyingi sio kwa ajili ya kuvuta. Bangi hiyo imekuwa ikienda katika dawa za binadamu.”

“Bangi yote ya Tanzania inakwenda katika dawa za binadamu ambazo tunaletewa kutumia. Kuna ubaya gani ikaanza kutoa vibali kwenye maeneo mbalimbali na kuhalalisha watu waanze kulima bangi hiyo na kupata faida.” alihoji.

Amesema ana ushahidi Lesotho na Zimbabwe kuruhusu ulimaji wa bangi na kuna viwanda vya kutengeneza dawa za binadamu kwa kutumia bangi.

Aidha alisema kuwa nchi nne Barani Afrika zimeruhusu kilimo cha bangi kwa ajili ya matumizi ya dawa za binadamu.

TUNATENGENEZA TAIFA LA KESHO LA AINA GANI?MOJA ya mbinu za kutatua changamoto mbalimbali za vitendo vya ukatili  (hasa zile zilizofichika) zilizopo kwa watoto na wasichana ni kuwashirikisha katika kutafuta ufumbuzi wake, wengi wetu hudhani kuwa kupitia uchunguzi tu na hatua zetu za maamuzi kama wazazi na wadau wa sheria ndiyo suluhu la kumaliza masahibu yanayowakuta kumbe la-hasha, kwa hatua hiyo tunakuwa tumekataza tu lakini hatujaondoa mzizi wa changamoto.

Hebu safiri nasi hadi Shule ya Sekondari Kilabela iliyopo wilayani Senerema mkoani Mwanza kujionea jinsi wadau wa Maendeleo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO wakishirikiana na FAWE Tanzania kupitia ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Korea ya Kusini (KOICA) wanachofanya......

Monday, May 20, 2019

UTPC YAWASILISHA MPANGO KAZI WA UTETEZI WA HAKI ZA BINADAMU KWA BLOGGERS.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) umewasilisha mpango kazi wa mradi wa Utetezi na Ushawishi wa kutumia Takwimu (Data Driven Advocacy-DDA), unaotekelezwa kwa ushirikiano wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Arusha (APC) kupitia waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media).

Mpango kazi huo umewasilishwa leo Mei 20, 2019 jijini Dodoma kupitia kikao kazi kilichowajumuisha waandishi wa habari wa mitandaoni 23 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani.

Akiwasilisha mpango kazi huo, Victor Maleko ambaye ni Afisa Programu kutoka UTPC amesema pamoja na mambo mengine, umelenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa mitandaoni kuzifahamu sheria mbalimbali za habari ikiwemo Sheria ya Takwimu 2015, Sheria za Huduma za Vyombo vya Habari 2016 pamoja na Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 ili kuripoti kwa weledi habari za utetezi na ushawishi wa haki za binadamu kwa kutumia takwimu.

Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Arusha (APC), Claude Gwandu amewataka washiriki wa mradi huo kuwajibika ipasavyo ili kuhakikisha unafikia malengo yaliyokusudiwa na kwamba klabu hiyo hakitakuwa tayari kuona mradi unakwama kutokana na baadhi ya washiriki kutowajibika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kundi la waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala kupitia mradi huo, Midraji Ibrahim amesema ili vyombo hivyo viendelee kuwa na manufaa katika jamii, lazima waandishi wake waweke habari zenye maudhui bora yakiwemo yanayogusa utetezi na ushawishi wa kutumia takwimu sahihi.

Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa kutumia takwimu (Data Driven Advocacy-DDA), unafadhiliwa na taasisi ya Freedom House ambapo ulianza mwaka jana 2018 ukitarajiwa kufikia tamati mwaka 2022.
Afisa Program kutoka UTPC, Victor Maleko akifafanua jambo kwenye kikao kazi hicho kilichofanyika jijini Dodoma.
Afisa Program kutoka UTPC, Victor Maleko akiwasilisha mpango kazi wa utekelezaji wa Utetezi na Ushawishi wa kutumia Takwimu (Data Driven Advocacy-DDA) kupitia kundi namba tatu linalowajumuisha waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Altenative Media).
Mwenyekiti wa Arusha Press Club (APC), Claude Gwandu akizungumza kwenye kikao kazi hicho.
Washiriki wakimsikiliza Mwenyekiti wa Arusha Pres Club (APC), Claude Gwandu kwenye kikao kazi hicho.
Meneja Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa kutumia takwimu (DDA) nchini Tanzania, Wakili Daniel Lema akifafanua jambo kwenye kikao kazi hicho.
Washiriki wakimsikiliza Meneja Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa kutumia takwimu (DDA) nchini Tanzania, Wakili Daniel Lema.
Mwenyekiti wa kundi namba tatu linalowajumuisha waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media),  Midraji Ibrahim (aliyesimama) akizungumza kwenye kikao kazi hicho.
Washiriki wa kikao kazi hicho wakifuatilia mada.
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi hicho.
Washiriki wa kikao kazi hicho.
Kikao kazi hicho kimewajumuisha washiriki 23 kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani.
Washiriki wakifuatilia mada kwenye kikao kazi hicho.
Washiriki wakiwa kwenye kikao kazi hicho.
Washiriki wakifuatilia kikao kazi hicho.
Washiriki wakifuatilia mpango kazi wa utekelezaji Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa kutumia takwimu (Data Driven Advocacy-DDA), kupitia kundi namba tatu linalowajumuisha waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Altenative Media) nchini Tanzania.
Washiriki wa kikao kazi hicho kilichofanyika jijini Dodoma.
Walioshiriki kikao kazi hicho ni pamoja na Kadama Malunde (Malunde Blog), William Bundala (Kijukuu Blog), Merina Makasi (Ngasa TV), Mohamed Zengwa (Global TV), Eliya Mbonea (Mtanzania Digital), Midraji Ibrahim (Sub Editor Mwananchi Digital), Mika Ndaba (Ayo TV), James Range (Sub Editor/ Programme Manager Global TV), Frankius Cleophace (Cleo24 News and Dar Mpya), Asha Shabani (Asha Shabani TV), George Binagi (Binagi Media Group), Albert G. Sengo (GSengo Blog).

 Wengine ni Francis Godwin (Dar Mpya Blog/ Matukio Daima Blog), Abubakar Kisandu (Kisandu Zenji Blog), Rashid Said Rukungu (Rukungutz Blog CG Online Tv), Edither Karo (Correspondent (Michuzi Blog and Malunde Blog), Joseph Mwaisango (Mbeya Yetu Online TV), Bakari Chilumba (Correspondent Dar Mpya Blog, Millard Ayo, Mpekuzi na Muungwana), Abdulaziz Ahmed (Lindi Yetu Blog na Lindi yetu Online TV), Gabriel Kilamlya (Dar 24 Blog), Ibrahim Said Limala (Correspondent Global TV online), Clavery Christian (Muungwana Blog) pamoja na Hamza Mashore (Ruvuma TV).
Maafisa Programu wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) nchini Tanzania wakiwa kwenye kikao kazi hicho.
Picha na Kadama Malunde, Malunde 1 Blog

MAFUNZO YA JINSIA KWA WANAHABARI KANDA YA ZIWA YAFIKIA TAMATI JIJINI MWANZA.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa (Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu na Geita) ili kuandika habari za kijinsia kwa weledi yamefikia tamati jijini Mwanza.

Mafunzo hayo ya siku mbili kuanzia jumamosi Mei 18, 2019 yaliandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa kushirikiana na ile ya Vyombo vya Habari nchini Finland VIKES.

Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa alitumia fursa hiyo kuwahimiza waandishi wa habari Tanzania kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, misingi na miiko ya uandishi wa habari huku wakitoa usawa wa vyanzo vyao vya habari kwa kuzingatia jinsia.

"Bado vyanzo vingi vya habari vinawahusisha wanaume huku wanawake wakisahaulika hivyo mafunzo haya yawe chachu ya kuleta mabadiliko kwenye kazi zenu kwa kuibua na kutangaza masuala mbalimbali yanayowahusisha wanawake pia" alisema Gasirigwa.

Naye Maridhia Ngemela kutoka Radio Iqra FM ya jijini Mwanza aliyeshiriki kwenye mafunzo hayo alisema changamoto kubwa katika uandaaji wa habari na makala kwa kuzingatia jinsia ni baadhi ya wanawake kutokuwa tayari kutoa ushirikiano kama ilivyo kwa wanaume hivyo ni vyema elimu ikaendelea kutolewa ili kuondoa hali hiyo..

Hata hivyo mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo, Alex Mchomvu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino jijini Mwanza alisema suala la imani, mila na tamaduni mbalimbali linakwamisha usawa wa kijinsia hapa nchini hivyo waandishi wa habari ni vyema wakatumia nyenzo zao kutoa elimu ili kubadili fikra hizo na hivyo kuleta usawa wa kijinsia baina ya wanawake na wanaume.
Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa (wa tatu kulia) na Mkufunzi Kenneth Simbaya ambaye ni Mwenyekiti Mtandao wa Waandishi wa Habari za Afya Tanzania (wa pili kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzio hayo.
Mmoja wa wakufunzi, Alex Mchomvu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino jijini Mwanza akiwasilisha mada kwenye mafunzi hayo.
Washiriki waki-refesh viungo vya miili yao kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakimsikiliza Mkufunzi, Kenneth Simbaya wakati akiwasilisha mada.
Mkufunzi, Kenneth Simbaya akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada kwenye mafunzo hayo.
Baadhi ya washirikiwa wakiwa kwenye majadiliano kupitia makundi.
Mwanahabari mkongwe, Florah Magabe (kushoto) pamoja na mwanahabari chipukizi, Sefroza Joseph (kulia) wote kutoka jijini Mwanza, wakifurahia jambo kwenye mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia jambo kwenye mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wakisikiliza kwa umakini jambo kwenye mafunzo hayo.