|
Meneja Mauzo na Usambazaji wa TBL, Kanda ya Ziwa , Malaki Sitaki(kulia) akimkabidhi kikombe Mwenyekiti wa Chama cha mbio za Mitumbwi Taifa, Richard Mgabo ikiwa ni zawadi ya mshindi wa kwanza wanaume katika fainali za mashindano ya mbio za mitumbwi yanayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki katika ufukwe wa Mwaloni jijini Mwanza kwaudhamini wa Bia ya Balimi Extra Lager.Kushoto ni Mratibu wa Mashindano hayo, Peter Zacharia. |
Mwanza.
KAMPUNI ya Bia Tanzania(TBL) kupitia Bia yake ya Balimi Extra Lager, leo imetangaza Zawadi za washindi wa mashindano ya mbio za mitumbwi zinazotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki, Desemba 7,2013, katika Ufukwe wa Mwaloni jijini Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja mauzo na usambazaji wa Kanda ya Ziwa, Malaki Sitaki alisema bingwa wa mashindano hayo wa mwaka 2013 upande wa wanaume ataibuka na kitita chafedha taslimu shilingi 2,700,000/=, Kikombe pamoja na medali za dhahabu.
Mshindi wa pili atazawadiwa fedha taslimu shilingi 2,300,000/=,mshindi wa tatu, 1,700,000/=, mshindi wa nne 900,000/= na washindi wa 5 hadi wa kumi watapatiwa kifuta jasho cha fedha taslimu shilingi 400,000/= kila kikundi.
Wakati upande wa wanawake bingwa ataibuka na zawadi ya fedha taslimu shilingi 2,300,000/=, Kikombe na medali za dhahabu, mshindi wa pili 1,700,000/=, mshindi wa tatu 900,000/=, mshindi wan ne 700,000/= na washindi wa 5 hadi 10 watapewa kifuta jasho cha fedha taslimu shilingi 250,000/=
Malaki alisema jumla ya timu 16 za wanaume na timu 11 za wanawake ziatarajia kuchuana siku hiyo na hatimaye kuwapata mabingwa wa mwaka 2013.
Aidha Malaki alivitaja vikundi vilivyotinga fainali upande wa wanaume kuwa ni Beach Boys Kigongo kutoka Kigoma, Dautius Kiiza kutoka Kagera, Katonga A kutoka Kigoma, Costantine Lusalago kutoka Mwanza, Leonard Kasunzu kutoka Mwanza, Toto Sebastian kutoka Ukerewe, Simon Fundi kutoka Ukerewe, J.J.Buna kutoka Mara, Makila Camp kutoka Kigoma, Zaidock Kaiza kutoka Kagera, Daniel Mgenha kutoka Mwanza, Totoji Mazige kutoka Mara, Benidicto Chamba kutoka Mara, Bernadr Charles kutoka Mara, Emanuel Petro kutoka Kagera na mabingwa watetezi kikundi cha Eliud Prosper kutoka Kagera
Wakati upande wa wanawake ni kikundi cha Elizabeth Manoni kutoka Mara,Nyamiti Juma kutoka Mara,Muhate Mwocha kutoka Ukerewe,Jenifer Elias kutoka Ukerewe,Tabu Daudi kutoka Mwanza, Regina Kazungu kutoka Mwanza, Levina Costantine kutoka Kagera, Salome Ernest kutoka Kagera, Mwangongo Star kutoka Kigoma,Akina Mama Lemba kutoka Kigoma na mabingwa watetezi kikundi cha Nyamizi Deo kutoka Mara.
Mwenyekiti wa Chama cha wakimbia mbio za mitumbwi Taifa, Richard Mgabo aliishukuru kampuni ya Bia Tanzania kupitia Bia yake ya Balimi Extra Lager kwa kudhamini mashindano hayo na kuwaomba waendelee kudhamini kwani hamasa yake inazidi kukua mwaka hadi mwaka.
Aidha Mwenyekiti alimtaja Mkuu wa Mkoa wa jiji la Mwanza, Injinia Everisto Ndikilo ndiye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika fainali hizo zitakazoanza kwa maandamano na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa huyo.
Nae mratibu wa mashindano ya mbio za mitumbwi, Peter Zacharia aliwaomba wapenzi, mashabi hususani wakazi wa Mwanza waje siku hiyo kushuhudia fainali hizo zitakazo sindikizwa na burudani lukuki ikiwemo Ngoma ya Bugobogobo ya Mang’ombe ga Kijiji kutoka Misungwi.