ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 28, 2011

"TAMASHA LA TIGO PESA MWANZA WA-CHAaa!!"

Kama kawaida yake Mwana Hip hop Roma alikisanukisha ile mbayaaa kwenye tamasha la kuitambulisha huduma ya Tigo Pesa, viwanja vya Furahisha Mwanza .

Kwa utilivu macho jukwaani..

Watoto hawa wanachungulia nini?

Alaaah Kumbe Nature!!!'

Sanaa ni kazi! chekshia mlume ndago.

Dj Ally Coco toka Stone Club ndiye aliyesimamia mzigo wa burudani on the one&two ya Nature na Kr Mura.

Kr. Mura aka Jibaba Cd700 akikamua kitu cha Push Up' kwenye songi 'Kamua'.

Msanii wa Bongo Flavour Dogo Baraka akikamua.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Tigo, Jackson Mbando akizitanabaisha Faida za huduma ya Tigo Pesa kwa wakazi wa Mwanza waliofurika kisawasawa kwenye viwanja vya furahisha.

Huduma ya Tigo pesa katika uwanja wa Furahisha Mwanza.

Mdau Mwananchi halisi wa Mwanza akiweka pesa live kwenye simu yake mara baada ya kujisajili Tigo Pesa katika viwanja hivyo.

AAAaah! jamani kuvalishwa raha!

'Fu-ngu-a tu-o-ne yaliyomo'

Wateja waliojiunga na huduma ya Tigo Pesa katika viwanja hivyo walizawadiwa simu kila mmoja.

Mwanza! Mwanza!!

Dj Maliz ndiye aliyesimamia mzigo awamu ya kwanza.

Wadau wa Tigo Mwanza.

KINA CHA MAJI ZIWA VICTORIA KIMEPUNGUA MITA 2.57 : WARSHA YA WADAU WA MAZINGIRA KUHUSU MABADILIKO YA TABIA NCHI ILIYOFANYIKA MWANZA YABAINISHA

Katibu Tawala msaidizi mkoa wa Mwanza Bi. Clesencia Joseph.
Mabadiliko ya Tabia nchi ndilo sasa tatizo linaloleta changamoto kubwa sana duniani hasa katika ukuaji wa uchumi, ustawi wa jamii na maendeleo endelevu kwa bara la Afrika.

Madhara yanazidi kuwa makubwa hasa kwa nchi changa na zenye uchumi unaotegemea hali ya hewa kama kilimo na uzalishaji wa umeme. Ambapo takribani asilimia 34 ya ardhi bara la Afrika ko katika hatari ya kugeuka jangwa.

Watu milioni 200 hawapati chakula cha kutosha ;
Asilimia 75 ya watoto wanaokufa kwa maralia inatokana na uchafuzi wa maralia;



Ripoti ya nne ya jopo la wana sayansi wanaofanya utafiti kuhusu mabadiliko ya tabia nchi (The Intergovernmental Panel on Climate-IPCC) iliyotolewa mwishoni mwa mwaka 2007 imeonyesha kuwa joto la dunia limeongezaka kwa wastani wa 0.74 sentigredi tangu mapinduzi ya viwanda.

Wadau wakibadilishana mawazo.
Kwa upande wa Tanzania tayari athari zimeanza kujitokeza, kina cha maji Ziwa Victoria kimepungua kwa mita 2.57, Ziwa Rukwa limepungua kwa kilomita 7 kwa kipindi cha takribani miaka 50 iliyopita. Kutokana na kuongezeka kwa kina cha bahari baadhi ya visima vya maji safi katika mwambao wa Pwani ya Bagamoyo na Pangani sasa vimeingiliwa na maji ya chumvi na vingine havitumiki kabisa hivyo kuathili upatikanaji wa maji safi na salama.

Nchi yetu pia inashuhudia kuenea zaidi kwa ugonjwa wa maralia katika maeneo ambayo haukuwa kawaida kama maeneo ya mkoa wa Kagera, Mbeya, Lushoto na Amani mkoani Tanga.

Picha ya pamoja ya Wanawarsha Mazingira.
Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, inaendelea kuelimisha umma na wataalamu katika sekta na taasisis za umma pamoja na sekta binafsi kuhusiana na tatizo la mabadiliko ya Tabianchi na kujiandaa vyema kukabiliana na tatizo kwa ujumla.

RWANDA YATAKA MAITI ZA WATU ZIFUKULIWE :::::: NI NDUGU ZA WALIOUAWA MWAKA 1994.

Chama cha upinzani nchini Rwanda kimeishutumu serikali ya nchi hiyo kwa kuwalazimisha watu kufukua miili ya ndugu zao waliouawa wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ili iwekwe kwenye eneo la maonyesho ya kumbukumbu.Serikali imesema mabaki ya miili iwekwe pamoja katika maeneo hayo ili watu waisahau mauaji ya maelfu ya Watutsi na Wahutu waliokuwa wakifuata siasa za wastani.

Mwakilishi wa chama cha upinzani cha Rwandan National Congress, Jonathan Musonera amesema yeye binafsi ameathiriwa na amri hiyo ya serikali. Alisema serikali iliamrisha wafukue miili ya jamaa zao na ipelekwe katika makumbusho ya mauaji ya kimbari.

Familia yangu ilikataa lakini serikali ilitishia kuamrisha wafungwa waifukue miili hiyo, hatukuwa na la kufanya isipokuwa kwa jamaa zetu kufukua miili hiyo na kuipeleka katika makumbusho ya mauaji ya kimbari.


Raia wa nchi hiyo toka kabila la Tutsi akionyesha makovu yakutisha aliyopata kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Bw Musonera aliongeza kwamba familia yake imesononeshwa sana na amri hiyo akisema walipoteza ndugu zao kwa njia ya kikatili.

Walistahili kupewa mazishi ya heshima, kilichotokea hakiaminiki, kwani alikuwa na uhusiano wa upendo wa hali ya juu kwa wazazi, ndugu, dada na marafiki waliopotea wakati wa mauaji, na kwamba hawezi tena kustahamili kuona mifupa yao ikining'inia maeneo ya makumbusho.

Hata hivyo chama cha manusura wa mauaji ya kimbari ambacho kina fungamano kubwa na serikali kinaunga mkono sera hiyo ya kufukua miili. Jean Pierre Dusingizemungu mkuu wa chama hicho anasema miili ya watu hao inapaswa kuwekwa katika maeneo hayo ili kuonyesha kilichotokea wakati wa mauaji.


Aliongeza miili hiyo inapaswa kuhifadhiwa vizuri ili iweze kuonyeshwa kwa muda mrefu. Kuna maeneo kadhaa ya kumbukumbu za mauaji ya kimbari nchini Rwanda, kubwa zaidi mjini Kigali ambako kuna mifupa na mafuvu ya watu lakini mawili yanaonyeshwa hadharani.

Serikali ya Rwanda inataka miili ya kila muathiriwa wa mauaji ya kimbari yaonyeshwe hadharani ili kubainisha kiwango cha ukatili wa mauaji hayo.

Lakini wengi wanaoambiwa kufukua miili hiyo ya jamaa zao waliouwawa miaka 17 iliyopita, wangependelea wapumzike kwa amani mahali walikozikwa.

WAYDAD USO KWA USO NA SIMBA LEO MISRI.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Misri kuchezesha pambano la mkondo mmoja kati ya Simba ya Tanzania na Wydad Casablanca ya Morocco litakalofanyika LEO Mei 28 2011 Uwanja wa Petrosport jijini Cairo, Misri.Simba Sc mazoezini.

Mechi hiyo ya kutafuta timu ya kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya MabingwaAfrika itaanza saa 12 kamili jioni kwa saa za Cairo. Waamuzi hao ni Farouk Mohamed atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake ni Mohamed Waleed na Hassan Sherif. Mwamuzi wa mezani (fourth official) ni OmarFahim wakati Kamishna wa mchezo huo ni Magdy Shams El Din kutoka Sudan.

Wydad Casablanca.

Mshindi wa mchezo wa leo atacheza kundi B pamoja na timu za Al Ahly ya Misri, Esperance ya Tunisia na Moloudia Club d’Alger ya Algeria.

Timu itakayoshindwa itaingia katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho ambapo itacheza mechi ya kwanza nyumbani dhidi ya Daring Club Motema Pembe ya DRC kati ya Juni 10, 11 na 12 mwaka huu.

Friday, May 27, 2011

CHAGUA MOJA KESHO :: KULIA AU KUCHEKA!!

Hayawi hayawi sasa yamekuwa! kile KiputeezZ cha Ukweli baina ya Mafahari wawili wenye mashabiki wengi' wengi' wengi' sana duniani na maadui wengi' wengi' wengi' duniani, Barcelona na Machester United kesho wanakutana uso kwa uso. Ingawa Manchester United inacheza katika ardhi ya Nyumbani (England), Barcelona kwa mujibu wa UEFA ndiyo watakuwa wenyeji wa mchezo huo kuikaribisha 'Man Yu'.

<--Messi katika dimba la Arsenal jana mara baada ya mazoezi.

Tayari Timu ya Barcelona imekwisha wasili nchini Uingereza kwaajili ya mpambano huo unao subiri masaa tu kuanza huku wakipewa hifadhi ya kutosha toka kwa Club ya Arsenal iliyotoa kiwanja chake kwaajili ya mazoezi ya wakali hao wanaohitaji kudhihirisha kuwa ndiyo wanaotisha dunia muzima kwa sasa.

Mchezo huo umepangwa kuanza saa 3:45 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.


"KIFAA hiki tutakitumbukiza ndani ya kombe na kusepa" Ni kama wanazungumza vile Gerard Pique and Carles Puyol walipoiteua picha ya Fabregas katika ofisi za uwanja wa mazoezi wa Arsenal.

Ikumbukwe kuwa ni hawa hawa Pique na mwenzake Puyol ndiyo waliomlazimisha Fabregas kuvaa jezi ya Barca wakisherekea kombe la dunia mara baada ya kulitwaa pamoja kama timu ya taifa la Hispania.

Tayari kocha wa Machester United, Sir Alex Ferguson kasema kuwa atakitumia kikosi kilichoibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Schalke 04 kwenye nusu fainali ya michuano hiyo.


SWALI NI MAN U ama BARCA?
@g sengo

Thursday, May 26, 2011

KARIBU TTCL MWANZA

TTCL Mwanza wapo barabara ya Posta karibu kabisa na uwanja wa michezo wa Nyamagana, yaani kwa nyuma ya jengo hili ndimo uwanjani.

Tuzo ilizoshinda kwa tawi lake la Mwanza kutoka kushoto
#5thMwanza E.A Trade Fair Information and Com..Technology.
#Trade in Service Sector Exhibitors 1st Winner.
#Best Tanzanian Exhibitors 2nd Winner.
#Best Service Exhibitors 2nd Winner.
#Information and Communication Technology 1st Winner 2010


Wafanyakazi wa TTCL Mwanza Kikazi zaidi aliyetabasamu ni Abel Ngusa (kaka yake Alex Ngusa yule mtangazaji) kisha anayefuata ni Pius Ningo.

Wateja wakipatiwa huduma.

Wateja wakitoka mjengoni mara baada ya kupata huduma.

THE BEAT FESTIVAL 27MAY2011.

The Beat is a monthly festival (usually on the last friday of the month) showcasing the best live music from Tanzania and abroad. The festival is hosted by Mzungu Kichaa and features some of the best local and international talent passing through Tanzania.

powered by CARAVAN RECORDS
www.myspace.com/caravanrec

LISSU NA WENZAKE MARUFUKU NYAMONGO

Tundu Lissu akionyesha shati lake analodai kuchaniwa na polisi baada ya kumpa kichapo akiwa nje ya Mahakama ya Wilaya ya Tarime, baada ya kupata dhamana jana. Picha na Anthony Mayunga

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, na wenzake saba ambao juzi walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime na kusomewa mashtaka matatu ya kuingia eneo la hospitali bila kibali, kufanya mkutano na kuzuia watu kufanya kazi, wamepata dhamana lakini wamezuiwa kutembelea maeneo ya Nyamongo hadi kesi inayowakabili itakapokwisha.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya hiyo, Yusto Roboroga alitoa uamuzi huo akisema ni kwa mujibu wa kifungu cha Sheria Namba 148 cha Makosa ya Jinai, kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002, ambacho kinatoa haki kwa watuhumiwa kupata dhamana. Alitoa uamuzi huo baada ya kupitia pingamizi lililowekwa na upande wa mashtaka kutaka wasipewe dhamana. Hata hivyo, alisema: “Washtakiwa wanazuiwa kutembelea maeneo ya Nyamongo mpaka kesi hiyo itakapokuwa imekwisha."

Hakimu Ruboroga alitaja masharti ya dhamana hiyo kuwa ni kusaini mkataba wa dhamana wa Sh5 milioni kwa wadhamini wawili wanaoaminika. Kwa wasio wakazi wa Tarime, alisema watatakiwa kupeleka mahakamani hati za mali isiyohamishika. Washtakiwa wote walikidhi masharti na kuachiwa kwa dhamana hadi Juni 26, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

Juzi, Lissu na wenzake, Waitara Mwita Mwikwabe, Stanslaus Nyembea, Anderson Deogratias Chacha, Andrew Andalu Nyandu, Mwita Marwa Maswi, Bashiri Abdalllah Selemani na Ibrahimu Juma Kimu walifikishwa mbele ya mahakama hiyo na kusomewa mashtaka hayo matatu na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Casmir Kiria ambaye alisema, waliyatenda Mei 23, majira ya saa nne usiku. Wote walikana mashtaka hayo.


Hisani ya gazeti la Mwananchi

OBAMA AKA 'CHALAQUE'

Rais Barack Obama aliwasili rasmi jumanne Ulaya kuanza ziara yake ya siku tatu akianzia mjini Durban, nchini Ireland ambako alikwenda katika kijiji jidogo ambacho wanatokea mababu zake wa upande wa mama yake, pia alihudhuria mkutano wa kundi la mataifa yenye utajiri wa viwanda G8 uliofanyika Ufaransa.

Rais Barack Obama, shoto, na first lady Michelle Obama, kulia, wakisalimiana na waziri mkuu wa Ireland, Enda Kenny, wa pili kulia, na mkewe Fionnuala Kenny mara baada ya kuwasili ikulu ya Dublin, May 23, 2011

Katika safari yake kuitembelea Uingereza amepewa jina la kificho (codename) na wana usalama wa Uingereza 'Chalaque' neno toka kabila la Punjabi lenye maana Mjanja mwenye akili kupita kiasi, hii ni kwa ajili ya ulinzi wake. Kwahiyo walinzi hao wakitaka kupeana taarifa zozote kuhusu yeye hawamtaji kwa jina lake halisi bali wanatumia jina hilo mbadala.

THE IRISH connection:
TO AMERICANS, Barack Obama will always be known as their country’s first black president. For that reason, many Americans were surprised by his visit to his ancestral home in Moneygall on Monday.

For Obama, choosing to be Irish ensured an enthusiastic welcome in Ireland and may have brought some political benefits back in the US. But it also spoke to his appeal as an individual who offers hope for a post-racial future in which Americans can hold multiple identities (black and Irish) and can choose which identities to adopt and in what circumstances.


Yet, while most white Americans today can choose their ethnic identities, most non-white Americans do not have the same options.Obama knows this well. Indeed, he wrote perceptively in his autobiography, Dreams from my Father, about his adolescent confusion over his own racial identity. Even though he barely knew his Kenyan father, most other Americans treated him only as “black”.

In choosing to embrace his Irish roots along with his African ones, Obama is more the exception among African Americans than the rule. And his choice is more easily accepted in Ireland than in the US, where the Washington Post expressed surprise over “his Irish – yes, Irish – roots”.


Ziara kwa malkia Uingereza

Obama’s ability to choose Irishness also reflects the fact that he can embrace an ancestor through his white mother. For many African Americans with Irish roots, the story is different.

Lost in the discussions over Barack Obama’s Irish roots was the fact that Michelle Obama too could trace her ancestry back to Ireland. While Barack’s roots go back to Falmouth Kearney, who emigrated from Moneygall to seek a better life in America, Michelle’s can most likely be traced to Henry Shields, an Irish-American slaveowner who had children with a slave he purchased named Melvinia. (Megan Smolenyak, the same genealogist that traced Barack’s roots to Ireland did the same for Michelle. While the available evidence points to Henry Shields as her ancestor, it has not been confirmed by DNA testing).


Rais Barack Obama akiwa na Malkia Elizabeth wakati wimbo wa Taifa la marekeni.

Rais Barack Obama na first lady Michelle Obama walipokutana na Prince William and Catherine, the Duchess of Cambridge, at Buckingham Palace in London, May 24, 2011.

HISANI YA www.irishtimes.com

Wednesday, May 25, 2011

KIWEWE CHA KUSHUKA DARAJA ZIARA YA BIRMINGHAM CITY NCHINI TANZANIA YAYEYUKA

Birmingham City wameamua kufuta safari yao ya Tanzania.

City, ambao wameshuka daraja katika ligi kuu ya England msimu huu walikuwa wasafiri kuja Tanzania kupambana na Simba ya Yanga katika mechi za kirafiki.

Hata hivyo watayarishaji walishindwa kuthibitisha utaratibu wa safari hiyo katika muda waliopewa.

Mabingwa hao wa kombe la Carling walioshuka daraja wanatafuta nchi ya kwenda kucheza mechi za kabla ya kuanza kwa msimu wa ligi daraja la kwanza kuisaka tiketi ya kurejea ligi kuu.

TWENDE KAZzzz...

Kula kwangu - Jasho langu.

Sagula sagula ya Mashatiz.

"Magimbi wala? Chukuwa basi na maparachichi!"

Vitengez na pale kwa mbele matundaz

Siyo kapeti ni Postaz kwaajili ya kupamba kuta zauzwa.

Ubize wote huu unatoka katika barabara hii ya Pamba jijini Mwanza hasa nyakati za jioni.