Wadau mbalimbali wa muziki nchini watoa maoni yao juu ya adhabu aliyopewa msanii Shilole kufuatia kitendo kilichodaiwa kuwa ni kinyume na maadili.
Saturday, August 1, 2015
WANAAPOLO WAFIA MGODINI BAADA YA KIBERENGE KUKATIKA
Na Woinde Shizza wa libeneke la kaskazini blog
Wachimbaji wadogo wawili (wanaapolo) wanaofiwa kufa na wengine kadhaa
kujeruliwa katika mgodi wa madini ya Tanzanite uliopo Mererani
mkoani Manyara .
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo walieleza kuwa tukio hilo
lilitokea usiku wa kuamkia leo ambapo wachimbaji hao
waliangukiwa na kiberenge ndani ya mgodi huo uliopo block C unao
milikiwa na Said Nassor (mwarabu) walipo kuwa wakiendelea na kazi.
Shuhuda huyo aliyejitambulisha kwa jina la Edison Onyango alisema kuwa
kiberenge hicho kilikatika na kuporomoka na kisha kuwaangukia watu hao
na kusababisha vifo na majeruhi.
Akizungumza kwa njia ya simu mmiliki wa mgodi huo Said Nassor
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa wamepata maiti ya
mtu mmoja na wako katika harakati za kusafirisha mwili huo kwenda kwa
ndugu zao kwa ajili ya maziko.
Hata hivyo alieleza kuwa tukio hilo ni lakawaida na kwamba polisi
walifika kwa ajili ya uchunguzi wakiwemo maofisa wa idara ya madini
ili kuchunguza undani wa tukio hilo.
www.woindeshizza.blogspot.com
“kwakweli ndugu muandishi wa habari tukio hili ni kweli limetokea
katika mgodi wangu na alijasababishwa na uzembe ila ni tukio la
kawaida kutokea na linaweza kutokea katika mgodi wowote “alisema Said
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa aliyefariki dunia
ni mtu mmoja Joseph Kimati (27).
Aliongeza kuwa waliojeruliwa katika tukio hilo ni wawili ambao
aliwataja kwa majina ya Regan Rabiel(29) na Hussen Juma (25)na kueleza
kuwa chanzo cha tukio ni kiberenge kilichokatika na kupoteza
muhelekeo.
JESHI LA POLISI KAHAMA LAMKAMA MTUHUMIWA WA MAUAJI
KAHAMA
Jeshi la polisi wilayani Kahama mkoani shinyanga linamshikilia mtuhumiwa mmoja anayedaiwa kushiriki katika mauaji ya katibu wa Chama cha mapinduzi Kata ya Isagehe mauwaji ambayo yalitekelezwa mwaka jana.
Mkuu wa jeshi la polisi wilayani Kahama Leonard Nyandahu amemutaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Thomas Malenge miaka 35 mkazi wa kijiji cha Mwalugulu ambapo mtuhumiwa huyo akiwa na wenzake 5 walimuuwa katibu wa CCM marehemu Daud Mbatilo.
Amesema kuwa mtuhumiwa huyo na wenzake walikodiwa na mtu ambaye bado jeshi hilo linafanya uchunguzi kwa ujira wa kupatiwa kiasi cha shilingi milioni mbili na kabla ya mauwaji hayo walipatiwa kiasi cha shilingi laki 6 na kutekeleza mauwaji hayo Desemba 03 mwaka jana.
Aidha jeshi hilo tayari limewanasa watuhumiwa wote 6na kwamba watuhumiwa watano walikwisha kamatwa na kufikishwa mahakamani lakini mtuhumiwa huyo aliyekamatwa jana mala baada ya tukioalitoloka kusikojulikana hivyo juzi alilejea akidhani walisahau na kulialifu jeshi la polisi na kufanikiwa kumutia nguvuni.
Hata hivyo Jeshi la polisi linaendekea kumhoji mtuhumiwa ili kuweza kufanikiwa kumukamata mtu aliyefadhili mauwaji hayo ili wote waweze kufikishwa mahakamani kwa kosa la mauaji.
SHEREHE YA KUWAKARIBISHA RASMI WASHIRIKI WA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA
Bw. Godia Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji cha Kasanga akiwakaribisha Washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula Shindano Linaloendeshwa na Oxfam Tanzania kupitia Kampeni ya Grow Kijijini kwake. |
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Kisalawe Bw. Ellioth Phillemon akiwakaribisha washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula Wilayani Kisalawe. |
Kikundi cha Burudani na sanaa cha Rumumba Theatre wakiendelea na Burudani wakati wa sherehe hizo za ukaribisho kijiji cha Makumbusho |
Eluka Kibona, Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam akielezea kwa ufupi juu ya Mchakato mzima wa Shindano la Mama shujaa wa chakula ambalo linalenga kuwawezesha wakina mama kutambulika katika kilimo na kueleza Matakwa yao juu ya kilimo endelevu. |
Bi. Mwanaidi Hamza ambaye anatoka katika Programu ya Big Result now akitoa ushuhuda jinsi gani alivyofanikiwa kulingana na Proramu hiyo na sasa anamaisha mazuri, na kuwasihi wakina mama wasikate tamaa katika kilimo. |
Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Jackson Samwel akiwapongeza Shirika la Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow kuanzisha shindano la Mama shujaa wa Chakula , kwa kutambua umuhimu wa ardhi katika kuzalisha chakula, ameshauri akinamama wabadilishane uzoefu pindi watakapokuwa kambini ili kuja na mbinu mpya za kilimo, ufugaji na uvuvi. |
Mmoja wa watoa Burudani, Mwanamke huyu akionesha kuhusu swala zima la Kilimo Endelevu. |
Stephen Mfuko aka Zero akitaja namba za washiriki na Jinsi ambavyo wanaweza Pigiwa Kura ambapo Programu mzima itaoneshwa katika Runinga ya ITV kila Siku kuanzia Tarehe 2.08.2015-21.08.2015 kuanzia saa 12 Jioni. |
Wageni waalikwa katika sherehe hiyo. |
Ofisa wa Programu ya Kampeni ya Grow Tanzania Suhaila Thawer akitoa maelezo mafupi ya Mchakato rasmi wa kumsaka Mshindi wa Mama shujaa wa Chakula |
Wanao onekana Mbele ni Baadhi ya wenyeji ambao ndio watakuwa wenyeji wa washiriki wa mama shujaa wa chakula pindi watakapokuwa kijijini. |
Washiriki wa Shindano la Mama shujaa wakiwa wanatambulishwa Tayari kuelekea Kisalawe Kijiji cha Kisanga kwa ajili ya kumsaka mshindi ambapo Programu mzima itaoneshwa katika Runinga ya ITV kila Siku kuanzia Tarehe 2.08.2015-21.08.2015 kuanzia saa 12 Jioni. |
Friday, July 31, 2015
BASATA YAMFUNGIA SHILOLE KWA UVUNJIFU WA MAADILI
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemfungia mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole kujihusisha na shughuli za sanaa kwa muda wa mwaka mmoja.
Mwanamuziki huyo anayejulikana pia kama Shishi Baby amekumbwa na dhahama hiyo baada ya kusambaa kwa picha zinazomuonesha akicheza jukwaani akiwa katika mavazi yanayokinzana na maadili ya Kitanzania akiwa nchini Ubelgiji.
Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza amezungumza na Mwananchi Digital kwa njia ya simu leo na kusema hatua hiyo imechukuliwa baada ya awali kumpa onyo kwa matukio ya kupanda jukwaani kufanya sanaa akiwa katika mavazi yasiyozingatia maadili ya Kitanzania.
“Awali tulimuonya kwa vitendo hivi, akakiri kosa na kuahidi kwa maandishi kuwa hatarudia kufanya hivyo” alisema na kuongeza: “Hata hivyo, wadau wa muziki watakumbuka alichokifanya nchini Ubelgiji. Lilikuwa tukio la aibu kwake kama msanii, aibu kama mwanamke na aibu kama Mtanzania” alisema.
Amewataka wasanii kujitathimini kabla ya kupanda jukwaani na kuonya kuwa Basata itaendelea kuchukua hatua kama hizo dhidi ya msanii yeyote atakayebainika kuvunja/kukiuka maadili ya nchi. Shilole amekiri kupokea barua kutoka Basata akisema, hivi sasa yuko kwenye majadiliano na mwanasheria wake na kusema anakusudia kukata rufaa kupinga kufungiwa huko. “Mashabiki wangu watulie kwani hii ni changamoto, tunaifanyia kazi kila kitu kitakuwa sawa hivi karibuni” alisema.
MSHINDI WA AIRTEL TRACE NALIMI MAYUNGA KUACHIA VIDEO YA KIBAO CHAKE CHA "NICE COUPLE" KWENYE CHANEL YA TRACE LEO
MSHINDI WA AIRTEL TRACE NALIMI MAYUNGA KUACHIA VIDEO YA KIBAO CHAKE
CHA "NICE COUPLE" KWENYE CHANEL YA TRACE LEO, 31/7/2015
Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Star Nalimi Mayunga ameachia kibao chake kipya cha " Nice Couple" video itakayorushwa kuanzia leo katika kituo cha DSTV chanel ya Trace Urban 325 Mwanzoni mwa mwezi huu.
Mshindi huyo wa Airtel Trace Music star alitua mjini Johannesburg South Afrika akitokea nchini Tanzania ili kuanza safari yake kujiendeleza kimuziki na kufikia ndoto zake mara baada ya kuibuka mshindi wa mashindano makubwa yaliyoshirikisha nchi 13 barani Afrika yaliyofanyika tarehe 18 April 2015,
Mayunga alitangazwa mshindi na mwanamuziki wa kimataifa wa miondoko ya R&B wa nchini Marekeni , Akon and kupata zawadi nono ikiwemo deli ya kurekodi single ambapo Mayunga alishuka nchini South Afrika na kuredoki nyimbo yake ya "Nice Couple" katika maeneo ya Orlando East.
Wimbo huo tayari umeshaanza kupigwa katika vyombo vya habari na sehemu mbalimbali nchini Afrika ya Kusini.
MATOKEO YA MASHINDANO YA AFRIKA MASHARIKI TIMU YA TAIFA YA NGUMI
Taarifa kwa vyombo vya
habari.
Yah:
Timu ya Taifa ya ngumi yaanza vema katika mashindano ya kimataifa kwa nchi za
Afrika Mashariki Mombasa Kenya.
Wachezaji wa timu ya Taifa
ya ngumi waliokwenda Mombasa Kenya kuwakilisha Taifa katika mashindano ya
kimataifa ya nchi za Afrika Mashariki wameanza vizuri kupeperusha bendera ya
Tanzania katika mashindano yaliyoanza leo tarehe 30/07/2015 jijini Mombasa kwa
kushirikisha nchi za Tanzania, Uganda na wenyeji Kenya, Timu hiyo yenye jumla ya mabondia
wanne na kocha Saidi Omari iliondoka juzi kwa udhamini wa viongozi wa juu wa
shirikisho la masumbwi Tanzania.
Matokeo kwa michezo
waliyocheza mabondia kutoka Tanzania yalikuwa kama ifuatavyo:-
·
Katika uzito wa 49 Kgs Gerevas
Logasian(TAN) alishindwa na Mwinyifiki Kombo wa (Kenya) kwa majaji 3.0,
·
52 Kgs. Said Hofu (TAN) alimshinda Sajabi
Yassini (Kenya) kwa majaji 2,1
·
56 Kgs Hamadi Furahisha
(TAN) alimshinda Denis Ochieng (Kenya) kwa majaji 3.0 kwa
·
60 KGS Ismail Issack
(TAN) alimshinda Mava Johnboscow (Uganda) kwa TKO
Mashindano hayo yataendelea
kesho tarehe 31/07/2015 kwa hatua ya nusu fainali na fainali za mashindano hayo
zitafanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 01.08.2015 na timu kurejea nyumbani
02.08,2015.
Lengo la mashindano ni kuziandaa timu za kutoka ukanda wa
Afrika mashariki vizuri kabla ya
kwenda kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa hususani Mashindano ya
Afrika (All African Games). Shirikisho la ngumi Tanzania linawatakia mafanikio
zaidi ili kutangaza vema Tanzania kupitia mchezo wa ngumi
Habari hizi zinaletwa kwenu na

Makore Mashaga
KATIBU MKUU.
Thursday, July 30, 2015
SAKATA LA LOWASSA KUHAMIA UKAWA LITAITIKISA CCM KWA KIPINDI KIFUPI ASEMA MCHAMBUZI WA MASUALA YA SIASA SAUTI
Mhadhiri na mchambuzi wa siasa toka chuo cha St.Augustino azungumzia sakata la Lowassa kuhamia UKAWA.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA KIA-MERERANI JIJINI ARUSHA
![]() |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi. Picha na OMR |
![]() |
Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal. Picha na OMR |
![]() |
Magufuli, akikabidhiwa fimbo ya heshima ya kabila la Kimasai. |
KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI KUDHAMINI UZINDUZI WA VIDEO MPYA YA MSANII “LINAH"
KAMPUNI ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Jebel Coconut imetangaza rasmi siku ya leo dhamira yake ya kudhamini uzinduzi wa video mpya ya msanii Estelinah Sanga maarufu kwa jina la kisanii “Linah” itakayo kwenda kwa jina la “No Stress”.
Video ya wimbo huo imefanyika nchini Kenya na Afrika ya kusini ambapo kwa kushirikiana na menejimenti ya msanii huyo, SBL imeweza kudhamini utengenezaji wa video hiyo ambayo hadi sasa imeshakamilika huku Kampuni hiyo ikisubiria kuizindua rasmi kwa wananchi.
Hatua ya SBL kudhamini video ya wimbo huo ni njia mojawapo ya Kampuni hiyo kutambua sanaa ya muziki hapa nchini ambapo pia hapo awali Kampuni hiyo iliahidi kumsapoti msanii huyo mara baada ya kupata mkataba wa mwaka mmoja wa kuwa balozi wa kinywaji cha Kampuni hiyo cha Jebel coconut.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utoaji wa taarifa hiyo kwa umma, Meneja Uvumbuzi wa kampuni hiyo Attu Mynah alisema “Kampuni ya bia ya Serengeti inatambua umuhimu wa Sanaa ya muziki hapa nchini na siku zote inalenga kumuwezesha msanii aweze kufikia malengo ya ndoto zake. Tumeamua kudhamini utengenezaji na uzinduzi wa video ya wimbo wa msanii Linah kwa kuwa tunatambua uwezo wake na tungependa afike mbali zaidi kimuziki”.
, alisema “Tunafuraha kwa kuwa Kinywaji chetu cha Jebel coconut kinaendelea kujizolea mashabiki wengi kupitia ubalozi wake ambapo ameendelea kuitangaza chapa hii sehemu mbalimbali za Tanzania. Kama SBL tunajivunia kudhamini baadhi ya kazi zake na ni matumaini yetu kuwa kupitia udhamini huu ataendelea kufanya vizuri zaidi katika ngazi za kimataifa”.
Jebel coconut ni aina ya pombe kali yenye ujazo wa 250ml inayotengenezwa nchini Tanzania na Kampuni ya bia ya Serengeti ambayo imebuniwa na kutengenezwa kwa ladha ya nazi ambazo zinapatikana kwa wingi hapa nchini. Jebel pia ni kati ya pombe kali zaidi ya 10 za kimataifa zinazosambazwa na kampuni ya bia ya Serengeti huku walengwa wa kinywaji hiki wakiwa ni watu wazima na wenye umri wa kati.
AIRTEL SMARTPHONE BAZAAR NDANI YA NANENANE MOROGORO
Baadhi ya wateja wakiwa ndani ya Airtel smartphone Bazaar ili
kusmartiphonica na simu za kisasa kwa bei poa.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza offa kabambe ya simu za kisasa itakayopatikana katika viwanja vya nane nane kuanzia siku ya Ijumaa tarehe 31 julai 2015, kwa muda wa siku 10.
Akiongea kuhusu ofa hiyo Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga amesema, Airtel inaendelea kuwapati wateja wake mawasiliano bora na kuwaunganisha na simu za kisasa zilizounganishwa na vifurushi vya bure vya internet katika msimu huu wa nanenane".
" Napenda kuwajulisha watanzania wote na wakazi wa Morogoro kuwa Airtel sasa tumewafikia na kusogeza huduma zetu karibu nao katika viwanja vya nanenane ambapo tutakuwa na offa nyingi ikiwemo simu za kisasa ya aina ya Airtel red itakayounganishwa na huduma za internet bure kwa mwaka mzima kwa gharama ya shilingi 75,000.
Sambamba na Airtel Red pia tunazo simu za aina nyingi ambazo ni pamoja na simu ya Huawei , Techno, Samsaung. Simu hizi zinamuwezesha mteja kuzitumia katika kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kutunza rekodi zao, inatumika kama kamera ya kupiga picha pamoja na mambo mengine mengi.
Tunatoa wito kwa wateja wetu watembelee banda la Airtel katika viwanja ya Nanenane na kupata nafasi ya kununua simu hizi za kijanja kwa gharama nafuu "aliongeza Muga Airtel Smartphone Bazaar bado pia iko jijini Dar es Salaam katika maduka yote ya Airtel.
Khalikadhalika wateja wote bado pia wananafasi ya kusmatiphonica kwa kutembelea maduka ya Airtel nchi nzima.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza offa kabambe ya simu za kisasa itakayopatikana katika viwanja vya nane nane kuanzia siku ya Ijumaa tarehe 31 julai 2015, kwa muda wa siku 10.
Akiongea kuhusu ofa hiyo Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga amesema, Airtel inaendelea kuwapati wateja wake mawasiliano bora na kuwaunganisha na simu za kisasa zilizounganishwa na vifurushi vya bure vya internet katika msimu huu wa nanenane".
" Napenda kuwajulisha watanzania wote na wakazi wa Morogoro kuwa Airtel sasa tumewafikia na kusogeza huduma zetu karibu nao katika viwanja vya nanenane ambapo tutakuwa na offa nyingi ikiwemo simu za kisasa ya aina ya Airtel red itakayounganishwa na huduma za internet bure kwa mwaka mzima kwa gharama ya shilingi 75,000.
Sambamba na Airtel Red pia tunazo simu za aina nyingi ambazo ni pamoja na simu ya Huawei , Techno, Samsaung. Simu hizi zinamuwezesha mteja kuzitumia katika kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kutunza rekodi zao, inatumika kama kamera ya kupiga picha pamoja na mambo mengine mengi.
Tunatoa wito kwa wateja wetu watembelee banda la Airtel katika viwanja ya Nanenane na kupata nafasi ya kununua simu hizi za kijanja kwa gharama nafuu "aliongeza Muga Airtel Smartphone Bazaar bado pia iko jijini Dar es Salaam katika maduka yote ya Airtel.
Khalikadhalika wateja wote bado pia wananafasi ya kusmatiphonica kwa kutembelea maduka ya Airtel nchi nzima.
LEMBELI KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAHAMA KUPITIA CHADEMA
![]() |
James Lembeli |
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kahama mkoani Shinyanga James Lembeli amechaguliwa kutetea nafasi hiyo kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA baada ya kuwashinda wagombea wengine 13.
Akitangaza matokeo msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni mratibu wa zoezi hilo kanda ya Serengeti Haile Sizza amesema kati ya kura 262 zilizopigwa na wajumbe Lembeli ameshinda kwa kura 168 sawa na zaidi ya asilimia 80 ya kura zote zilizopigwa.
SAUTI YA Haile KUWAJIA PUNDE.
Lembeli ametangazwa kutetea nafasi ya ubunge katika jimbo hilo kwa tiketi ya CHADEMA ikiwa ni siku chache baada ya kutangaza kujiunga na chama hicho akitokea chama cha Mapinduzi CCM.
Mara baada ya kutangazwa kukiwakilisha chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA katika uchaguzi mkuu mwezi Oktoba Lembeli amewashukuru wajumbe na kuomba ushirikiano na mshikamano ndani ya chama kwa maendeleo ya jimbo hilo.
SAUTI YA Lembeli KUWAJIA PUNDE.
Katika hatua nyingine Winfrida Mwinura amechaguliwa kuwania ubunge viti maalumu baada ya kuwashinda wagombea wengine wanne kwa kura 34 kati ya kura 77 zilizopigwa na wajumbe wa baraza la wanawake wa chama hicho(BAVICHA).
LOWASSA KUPEPERUSHA BENDERA YA CHADEMA UCHAGUZI 2015
Wednesday, July 29, 2015
TFF YAUTOSA UWANJA WA NYAMAGANA?
HATIMAYE ndoto za wakazi wa Manispaa ya Bukoba kufaidi michezo ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu ujao zitatimia sasa, baada ya Serikali nchini kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania TFF kuruhusu nyasi zilizokuwa zimekwama bandarini kwa muda mrefu kuwasili katika uwanja wa kaitaba.
Viwanja vya Nyamagana (Mwanza) na Kaitaba (Bukoba mkoani Kagera) viko katika mchakato wa kuwekewa nyasi bandia kwa msaada wa Fifa na Serikali.
Viwanja vya Nyamagana (Mwanza) na Kaitaba (Bukoba mkoani Kagera) viko katika mchakato wa kuwekewa nyasi bandia kwa msaada wa Fifa na Serikali.
Lakini wakati uwanja wa Kaitaba wa mkoani Kagera ukipokea nyasi zake uwanja wa Nyamagana wenyewe bado nyasi zake ziko bandarini suala ambalo Chama cha soka mkoa wa Mwanza MZFA kupitia kwa katibu wake Nassib Mabruk amesema kuwa tayari wamewakumbusha TFF ili suala la Nyamagana nalo lipatiwe ufumbuzi ukizingatia umuhimu wa uwanja huo mkongwe jijini Mwanza katika Maendeleo ya Michezo hapa nchini.
Nyamagana ndiyo ilikuwa plani ya kwanza, baadaye ikifuatia Kaitaba. Swali ni je 'Kwanini Kaitaba Kwanza na siyo Nyamagana?'
RAIS KIKWETE ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA CHUO KIKUU CHA NEWCASTLE, AUSTRALIA
PICHA NA IKULU
Subscribe to:
Posts (Atom)