ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 31, 2015

MSHINDI WA AIRTEL TRACE NALIMI MAYUNGA KUACHIA VIDEO YA KIBAO CHAKE CHA "NICE COUPLE" KWENYE CHANEL YA TRACE LEO

MSHINDI WA AIRTEL TRACE NALIMI MAYUNGA KUACHIA VIDEO YA KIBAO CHAKE CHA "NICE COUPLE" KWENYE CHANEL YA TRACE LEO, 31/7/2015 

Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Star Nalimi Mayunga ameachia kibao chake kipya cha " Nice Couple" video itakayorushwa kuanzia leo katika kituo cha DSTV chanel ya Trace Urban 325 Mwanzoni mwa mwezi huu.

Mshindi huyo wa Airtel Trace Music star alitua mjini Johannesburg South Afrika akitokea nchini Tanzania ili kuanza safari yake kujiendeleza kimuziki na kufikia ndoto zake mara baada ya kuibuka mshindi wa mashindano makubwa yaliyoshirikisha nchi 13 barani Afrika yaliyofanyika tarehe 18 April 2015, 

Mayunga alitangazwa mshindi na mwanamuziki wa kimataifa wa miondoko ya R&B wa nchini Marekeni , Akon and kupata zawadi nono ikiwemo deli ya kurekodi single ambapo Mayunga alishuka nchini South Afrika na kuredoki nyimbo yake ya "Nice Couple" katika maeneo ya Orlando East.

 Wimbo huo tayari umeshaanza kupigwa katika vyombo vya habari na sehemu mbalimbali nchini Afrika ya Kusini.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.