|
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga wa pili kulia pamoja na Mkurugenzi wa Duka la vifaa vya ujenzi la Bw. Zuri Nanji wa kwanza kulia wakikabidhi mifuko 50 kwa uongozi wa shule ya msingi Butimba Mazoezi A na B iliyopo Kata ya Butimba kwaajili ya ujenzi wa vyoo vya shule hiyo. |
MKUU wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga jana alikabidhi jumla ya mifuko 200 ya saruji kwa shule nne za msingi katika Kata nne za Wilaya hiyo ikiwa ni mkakati wake wa kuchangia, kuhamasisha mendeleo na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa vitendo.
Konisaga ambaye amekuwa akihamasisha mkubwawa maendeleo na kuhakikisha kero mbalimbali za kijamii zinatafutiwa ufumbuzi wa haraka kwenye sekta zote ambapo katika msaada huo alioukabidhi kwa lengo la kupunguza upungufu wa matundu ya vyoo kwenye baadhi ya shule hizo zinazokabiliwa na changamoto hiyo kutokana na wingi wa wanafunzi.
“Msaada huu wa saruji mifuko 200 umetolewa kwangu na mfanyabiashara maarufu Jijini Mwanza Zuri Nanji maarufu kwa jina la ‘Mwanza Huduma’ ambaye alikuja ofisini kwangu na kuniahidi kunisaidia kwenye sekta ya Elimu lakini kwa shule za msingi na eneo alilopendekeza ni kwenye ujenzi wa vyoo ili kusaidia kuongeza matundu ya vyoo jambo ambalo litasaidia kupunguza msongamano kwa wanafunzi wakihitaji kujisaidia”alisema
Mkuu huyo wa Wilaya alisema kwamba kutokana na msaada huo aliamua kuugawa kwenye shule za msingi nne kati ya 81 zilizopo katika Wilaya hiyo ambapo shule zilizonufaika na msaada huo ni Butimba Mazoezi A na B iliyopo Kata ya Butimba, Ibanda iliyopo Kata ya Mkolani, Igogo B iliyopo Kata ya Igogo na Igoma iliyopo Kata ya Igoma.
|
Pamoja na makabidhiano hayo yaliyofanywa shule ya msingi Butimba imeendeleza juhudi zake za ujenzi wa vyoo ili kupunguza makali ya changamoto iliyopo. |
|
Msafara wa Mkuu wa wilaya ya Nyamagana na wadau wake ukirejea toka kwenye ukaguzi shule ya msingi Butimba Mazoezi A na B iliyopo Kata ya Butimba.. |
|
Konisaga pia alipata fursa fupi ya kuzungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Butimba Mazoezi A na B iliyopo Kata ya Butimba. |
|
Makabidhiano ya Mifuko 50 ya saruji kwa shule ya Msingi Mkolani. |
|
Waalimu na wanafunzi shule ya msingi mkolani. |
|
Saruji ikishushwa shule ya msingi Mkolani. |
|
Mifuko 50 ya Saruji kwa shule ya msingi Mkolani. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akizungumza na waalimu, wanafunzi na uongozi wa kamati shule ya msingi Igogo ambapo alikabidhi mifuko 50 kwaajili ya ujenzi wa vyoo vya shule hiyo. |
|
Vyoo vya shule ya msingi Igogo ambavyo tayari vimejengwa. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akikabidhi Naibu Meya John Minja mifuko 50 ya saruji huku akishuhudiwa na viongozi wa kamati na waalimu wa shule ya msingi Igogo B iliyopo Kata ya Igogo wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza kwaajili ya ujenzi wa vyoo vya shule hiyo. |
|
Kabla ya makabidhiano kwa shule ya msingi Igoma waalimu na wanafunzi walikutanishwa katika ukumbi wa shule hii kwaajili ya kupata changamoto zilizopo. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga (wa pili kutoka kushoto) akikabidhi mifuko 50 kwa uongozi wa shule ya msingi Igoma kwaajili ya ujenzi wa vyoo vya shule hiyo. |
“Hali
ya vyoo kwenye shule hizi si nzuri sana hivyo Mudau huyu ‘Mwanza Huduma’ ameguswa
na hali hiyo na kuonyesha umuhimu wake kutokana na shughuli zake nyingi
kuzifanyia Wilayani kwetu kweli ni mfano wa kuigwa kwani shule hizi ni mali ya
wazazi ambao wanatakiwa kuchangia uboreshaji wake ikiwemo ujenzi wa vyumba vya
madarasa, nyumba za walimu, madawati na matundu ya vyoo” alisisitiza.
Konisaga
alisema kwamba wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule za msingi na sekondariwanao wajibu mkubwa kwa
kushirikiana na walimu na kamati zao za shule hizo kuboresha miundombinu kwa
kushirikiana na Halmashauri ya Jiji na Serikali kwa kuchangia fedha ili
kupunguza aidha kuondoa kero mbalimbali kwenye miradi ya maendeleo inayotoa
huduma za kijamii kwenye sekta zote kwenye maeneo yao.
“Viongozi
wa serikali ni kusimamia ulinzi na amani ya wananchi na kuwahamasisha pia kuchangia
miradi ya maendeleo kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji na serikali Kuu
ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ili kuwawezesha
kupatiwa huduma bora kama inavyokusudiwa na wananchi kuwaepuka wanasiasa
wanaowahamasisha kutochangia miradi hiyo eti ni jukumu lake hao hawafai na wasiwaunge mkono”alisema Mkuu huyo.
Konisaga
aliwataka viongozi wa Kamati za shule hizo zilizokabidhiwa msaada huo kuacha
tabia ya kuweka mafundi na kuwaacha wakichakachua na kufanya ujenzi hafifu na
kusababisha majengo hayo kuwa chini ya kiwango na hata kuharibika kwa wakati
mfupi jambo ambalo limekuwa likiwakatisha tamaa baadhi ya wadau,
wafanyabiashara na wafadhili kuendelea kuchangia tena kwenye miradi mbalimbali
ya kijamii.
Naye
kwa upande wake Zuri Nanji ‘Mwanza
Huduma’ alisema kwamba hali ni mbaya sana kwenye shule za msingi ambapo
kuna watoto wengi (wanafunzi) ambao kutokana na matundu ya vyoo kuwa machache
husababisha wanafunzi hao kujisaidia holela na kuharibu mazingira na kuwa
hatarishi kwa afya zao ikiwemo kukumbwa na magonjwa ya kuambukiza hali
iliyomfanya kusaidi kwa kutoa msaada huo.
“Nitaendelea
kuwa mdau wa kuchangia saruji na vifaa
vingine vya ujenzi kwenye shule za msingi na sekondari ili kuhakikisha juhudi
za kushirikiana na Jamii na kuiunga mkono serikali kutoa huduma kwa wananchi
inatekelezwa kwa wakati kupitia pia sekta binafisi ili kuwapatia huduma zinazositaili kwenye
maeneo yao bila kuwabagua kutokana na tofauti ya kipato”alisema
Kwa
mujibu wa maelezo ya kitaalamu ya mafundi wa Ujenzi wa majengo na Mwanza Huduma
alieleza kuwa kila Shule hizo zilizopatiwa kila moja mifuko ya saruji 50 yenye
uwezo wa kutoa tofari 1400 kwa kila mfuko mmoja wa kilo 50 unaouwezo wa kutoa
tofari 28 hadi 32 na kuhitaji maji mengi hali inayoimarisha kuta za majengo na
kuwa imara na bora baada ya kukamilika huku vyoo vya matundu 8 vya kisasa
vikitumia tofari 450 tu .