ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 23, 2016

HATIMAYE MWENYEKITI MPYA WA CCM APATIKANA HII HAPA KAULI YAKE YA KWANZA.

Hotuba ya mwenyekiti mpya wa CCM, Mhe. John Magufuli akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa mwenyekiti mpya wa CCM.


Mwenyekiti mpya wa CCM, Rais John Magufuli amezungumzia mambo manne atakayoshughulikia katika chama hicho, hasa kufanya mabadiliko makubwa ili chama kiweze kwenda na wakati.
Pia, Rais Magufuli amewaomba wana-CCM kumuombea ili awe na uvumilivu kama wa mtangulizi wake, Jakaya Kikwete katika kukabiliana na utovu wa nidhamu kwenye chama.
Hayo ni sehemu ya hotuba yake ya shukrani baada ya kupata kura zote 2,398, katika uchaguzi uliokuwa wa mgombea mmoja wa nafasi ya mwenyekiti wa CCM uliofanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa chama hicho uliopo mjini hapa.
Mwenyekiti huyo mpya alisema utendaji kazi ni suala muhimu, hivyo atajenga chama madhubuti ili kiweze kuisimamia Serikali.

RAIS MAGUFULI AKITANGAZWA KUWA MWENYEKITI WA CCM.

Mwenyeki wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Jakaya Kikwete akimtangaza  Rais Magufuli kushinda uenyekiti wa CCM kwa kura 2398 na kukabidhiwa Ilani ya CCM.

KOCHA Arsene Wenger awapa jeuri mashabiki wake.


Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameweka mkazo kwamba yupo tayari kutumia pesa kusajili mchezaji sahihi ambaye ni anaweza kufiti kwenye mfumo wake.
Mpaka sasa, Arsenal wamefanikiwa kutumia kitita kikubwa kumsajili Granit Xhaka na baadaye kuwachukua Mjapani Takumo Asano na Rob Holding
Wenger amekuwa akikosolewa kwa kushindwa kwake kusajili wachezaji wenye majina makubwa hasa kwenye nafasi ya beki wa kati na ushambuliaji licha ya wapinzani wake wengi kufanya hivyo.
Hata hivyo Wenger amesema kwamba bado hajamaliza kusajili ila anaangalia mtu sahihi wa kumleta kwenye timu yake.
“Tuna mwamko mkubwa. Kama tunapata mchezaji sahihi basi hatuwezi kusita kutumia pesa kumsajili,” Wenger aliimbia tovuti ya klabu baada ya sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Lens.
“Mpaka sasa tayari tumetumia pesa nyingi. Kwa ujumla tayari tumeimarisha kikosi chetu kwa kiasi kikubwa lakini hata hivyo bado yuko macho kwenye dirisha la usajili.
“Nisingeoenda kuangalia zaidi majina, kwasababu kama hujawapata, watu watakuuliza kwanini. Tuko makini, tena makini sana kila siku na hatujamaliza zoezi la usajili. Ndiyo kwanza tarehe 22 leo (jana) na dirisha la usajili linafungwa Agosti 31. Na unafahamu fika kwamba mambo mengi hutokea wiki ya mwisho. Hivyo bado kuna safari ndefu. Lakini tupo makini na tunalifanyia kazi suala hilo.
Mpaka leo hakuna aliumiapesa nyingi kutuzidi katika usajili nchini hapa. Hata kama [Paul] Pogba anataraji kuja hapa kutokea Italy, sijui….

TRAFIKI AUAWA JIJINI DAR.

Kutoka Jijini Dar es Salaam.

 Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Sajenti Mensah wa Kituo cha Polisi Oysterbay ameuawa usiku huu kwa kupigwa risasi akiwa kazini eneo la Sayansi Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Christopher Fuime amesema tukio hilo lilitokea majira ya saa mbili usiku huu na chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika.

“Tukipata chanzo itakuwa tayari upelelezi wetu umetimia, hivyo kwa sasa tunalifanyia kazi ili kubaini wahusika wa mauaji hayo,” amesema Fuime.

MH. MKUU WA WILAYA AKABIDHI MADAWATI 200 SHULE YA MSINGI GONGOLAMBOTO

 Mh. Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akizungumza jambo wakati wa hafla hiyo 
 Mh. Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akipokelwa na viongozi mbalimbali 
 Diwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Ukonga, Juma Mwipopo (kulia) akimsalimia  Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mh. Sophia Mjema wakati wa hafla ya kukabidhi madawati katika  Shule ya Msingi Gongolamboto Jeshini ambapo  hafla hiyo ya Harambee ya madawati inaongozwa na Kituo cha Televishen cha Channel ten kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mh. Paul Makonda

 Mhariri Mkuu Afrika, Media Chanenl Ten, Dina Chahali akimkaribisha kwa kumpokea Mh, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mh. Sophia Mjema katika hafla ya kukabidhi madawati katika Shule ya Msingi Gongolamboto Jeshini

   Mwenyekiti wa kamati ya Mkoa Madawati, Hamid Abdulrahman akimkadhi madawati mia mbili  Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (kushoto)  ambapo hafla hiyo ya Harambee ya madawati inaongozwa na Kituo cha Televishen cha Channel ten kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mh. Paul Makonda , hafla hiyo imefanyika  Dar es Salaam  jana

Mh. Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (kushoto) akimkabidhi madawati mia mbili, Mwalimu  Mkuu wa  Shule ya Msingi Gongolamboto Jeshini, Joel Balua, ambapo hafla hiyo ya Harambee ya madawati inaongozwa na Channel ten kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa , hafla hiyo imefanyika  Dar es Salaam  jana, wakwanza kulia ni Mwenyekiti Kamati ya Shule Benjamin Wasonge
 Mh. Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (katikati) katika picha ya pamoja na Waalimu wa Shule hiyo.
 Mjumbe wa Kamati ya Uchangiaji madawati Mkoa wa Dar es Salaam Sakina Yusuphali akimpatia kinywaji mmoja wa  wanafunzi  hao

  Mh. Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (katikati) katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi hao wa Shule hiyo


 Muonekano wa baadhi ya madarasa katika hatua ya mwisho
 Muonekano wa baadhi ya madarasa katika hatua ilipofikia
 Wakitoka katika kuangalia vyumba vilivyokuwa tayari na vikiwa vinamadawati 
 Baadhi ya wanafunzi wakiwa wameinua mikono baada ya kuulizwa swali na  Mh. Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, niwangapi wanao fuatilia kuangalia Tv na niwangapi hua wakiona tangazo gani? (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

PROF J AWATAJA DIAMOND PLATNUMZ, NAVY KENZO, JOH MAKINI KUWA NI WASANII WANAOCHIPUKIA, AWASHAURI PIA AISIFIA SINGELI, KULIKO KUMUIGA LIL WAYNE NI BORA KUCHUKUWA VIONJO VYA ASILI YETU.

13722247_1241942852482968_737225465_nHivi karibuni Profesa ameishoot video ya wimbo wake mpya aliomshirikisha staa wa Singeli, Sharo Mwamba.

Akijibu swali la mtangazaji wa Jembe FM, Jackson Joseph aka JJ,  kupitia kipindi cha HOT STAGE kinachoruka kila siku za jumatatu hadi alhamisi saa moja usiku hadi saa tatu, kwamba '....ni Ujumbe gani anao wapa wasanii wanavuma sasa kwenye game' Profesa amesema " sasa hivi hatutizami tena maslahi ya Profesa Jay, tunatizama maslahi ya muziki wetu, tumeleta mapinduzi makubwa kwenye muziki huu kwa nyimbo kama Chemsha bongo kuwaaminisha wazazi kuwa huu muziki si wakihuni ingawa kunawahuni wachache huu muziki wanaufanya.

Kisha akaongeza "Lakini pia tumetaka kuwaambia wazazi kwamba muziki unaweza kuleta ajira, wengi mmeona kwamba wasanii wengi wanajiajiri na kuajiri watu wengi katika sanaa na tasnia ya muziki..........."Nawashukuru wasanii chipukizi kama Diamond Platnumz, Ali Kiba, Vanessa, akina Joh Makini wako wengi wanao Re-Present kwa kweli Aika, Navy Kenzo wanafanya vizuri kwa kweli kuupeleka muziki kwenye levo nyingine lakini wanahitaji sapoti inabidi tushambulie kama Barcelona, tunashambulia pamoja tunakaba pamoja"
ZAIDI BOFYA UPATE KUSIKILIZA KILICHOTOKEA.Aidha Prof Jay amedai kuwa Singeli ni muziki unaoweza kulipeleka taifa hili mbali kwani unaojumuisha ladha nyingi za asili ya Tanzania .

“Sisi watanzania tumekuwa na muziki ambao haueleweki, hata hip hop tunayoifanya inayoweza kumuonesha huyu ni mtanzania ni Kiswahili tu,” amesema Jay.

“Nimefanya hip hop singeli kwaajili ya kuupeleka muziki huo mbali lakini pia kuitengeneza hip hop tofauti. Kuliko kuwakopi akina Lil Wayne wanafanyaje basi tufanye muziki ambao tutakopi muziki wa nyumbani,” ameongeza.

“Nadhani ni muda sasa hivi wasanii wa hip hop kutanua, wasikopi vya Marekani, wako vya Tanzania ili kuifanya hip hop yetu ibadilike kila siku.”

Friday, July 22, 2016

AMANA BANK TANZANIA WAZINDUA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA

Juma Msabaha ambaye ni senior costomer service manager wa Bank Ya AMANA nchini Tanzania akifafanua jambo kwa wanahabari wakati Bank Hiyo ikizindua Rasmi Kituo cha Huduma kwa wateja ambacho ni mahsusi kwa kuwasaidia wateja wake kuzifikia na kuzipata Huduma Zao kiurahisi zaidi


Benki ya kwanza ya Kiislam nchini Tanzania Amana benki leo imezindua kituo chake cha huduma kwa wateja ambacho kitakuwa kikiwasaidia wateja wake kuweza kupata taarifa mbalimbali kuhusu huduma zao kama maulizo kuhusu bidhaa za amana, Atms,huduma za mitandao (simu banking) na amana banki mtaani n.k.

Kituo hicho kitakuwa kikifanya kazi kuanzia saa 2  asubuhi mpaka saa 4 na watakuwa wanapatikana kwa nambari 0657980000 ambapo amana Bank ni miongoni mwa benki zinazofanya vizuri kwa sasa wana matawi saba matano yakiwa Dar es salaam,Arusha,Mwanza na wanatarajia kufungua matawi mengine mikoa mingi zaidi ila waliyoipa kipaumbele zaidi ni Zanzibar na Tanga

Akizungumza na waadishi wa habari meneja mfawidhi na huduma kwa wateja Juma Msabaha Amesema kuwa utaratibu wanaotumia  kuweza kuwapata mawakala ni kwamba wakala lazima awe na leseni ya biashara pia awe na tin namba ya biashara kuonyesha kuwa ni mlipa kodi  pia awe amefanya kazi zaidi ya miaka miwili na pia anaweza kuomba uwakala kwa namba zao ambazo ni 0657980000 au info@ amanabank.co.tz na maombi yake yatapelekwa BOT kuweza kujadiliwa na kama amekidhi vigezo atapewa uwakala ambapo amesema kuwa kwa sasa wana mawakala kwa mikoa kama tabora ,bukoba,na mtwara na bado wanaendelea kupokea maombi kutoka kwa watu mbalimbali.

Munir Rajab – mkuu wa idarara ya biashara amana benki amisema kuanzishwa kituo hicho kuna lengo la kuhitaji kuwa karibu na na wateja wao huku akitanabaisha  kuwa huduma za kibenki huwa zinafanana lakini kinachoweza kuwatofautisha ni ubora wa huduma kwa wateja na kwamba wao wamejipanga vizuri kuingia kwenye ushindani huo ambapo wameamua kuwa mwaka huu ni mwaka wa mawakala kwa sababu wanahitaji kuweza kuwafikia wateja wao mpaka mahali ambapo hakuna matawi na wataweza kutumia huduma za kibenki kupitia mawakala wao .
 Mkuu wa biashara wa Bank ya AMANA nchini Tanzania Munir rajab akieleza mambo mbalimbali kwa wanahabari kuhusu huduma hiyo mpya kutoka kwao
Bw. Juma Msabaha akijibu swali wa muandishi wa habari Alisema kuwa utaratibu wanaotumia  kuweza kuwapata mawakala ni kwamba wakala lazima awe na leseni ya biashara pia awena tin namba ya biashara kuonyesha kuwa ni mlipa kodi  pia aweamefanya kazi zaidi ya miaka miwili na pia anaweza kuomba uwakala kwa namba zao ambazo ni 0657980000 au info@ amanabank.co.tz na maombi yake yatapelekwa BOT kuweza kujadiliwa na kana amekidhi vigezo atapewa uwakala . na kwa sasa wana mawakala kwa mikoa kama Tabora ,Bukoba,na Mtwara na bado wanaendelea kupokea maombi kutoka kwa watu mbalimbali.

TBL YAZINDUA BIA MPYA YA NDOVU RED MALT JIJINI DAR ES SALAAM.

Meneja wa Bia ya Ndovu Red Malt, Nicolas John (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Mkurugenzi wa Masoko TBL Kushila Thomas pamoja na Meneja Masoko wa vinywaji wa kampuni ya TBL Vimal Vaghmaria (wa kwanza kulia) wakionyesha kinywaji cha Ndovu Red Malt mara baada ya kuzindua kinywaji hicho jana katika mgahawa wa 305 The Boks uliopo Kinondoni jijini Dar e Salaam ambapo wateja zaidi ya 50 walihudhuria katika hafla ya uzinduzi wake. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. Meneja wa Bia ya Ndovu Red Malt, Nicolas John akiongea wakati wa Uzinduzi wa bia ya Ndovu Red Malt uliofanyika jana katika mgahawa wa 305 The Boks uliopo Kinondoni jijini Dar e Salaam ambapo wateja zaidi ya 50 walihudhuria katika hafla ya uzinduzi wake. Meneja Masoko wa vinywaji wa kampuni ya TBL Vimal Vaghmaria amesema: “Ubunifu wa kila bidhaa yetu unalenga kukidhi matakwa ya watumiaji wake ambao ni wateja wetu ambao wanahitaji kutumia bia zilizo bora na zinazokwenda na wakati katika soko”. Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Damian Soul akitoa burudani katika uzinduzi wa bia ya Ndovu Red Malt uliofanyika jana katika mgahawa wa 305 The Boks uliopo Kinondoni jijini Dar e Salaam. Mkurugenzi wa Masoko TBL, Kushila Thomas (wa kwanza kushoto) akijadiliana jambo na Meneja wa Bia ya Ndovu Red Malt, Nicolas John (katikati) pamoja na mgeni mwaliko aliyefika katika uzinduzi wa bia ya Ndovu Red Malt uliofanyika mgahawa wa 305 The Boks uliopo Kinondoni jijini Dar e Salaam. Wageni waalikwa wakijipatia bia ya Ndovu Red Malt. Wageni waaalikwa wakibadilisha nawazo huku wakijipatia kinywaji cha Ndovu Red Malt. Wageni waliohudhuria uzinduzi wa bia ya Ndovu Red Malt uliofanyika mgahawa wa 305 The Boks uliopo Kinondoni jijini Dar e Salaam. Kinywaji cha Ndovu Red Malt. Meneja wa Bia ya Ndovu Red Malt, Nicolas John(kushoto) akiwa na Msanii wa Kuchora Picha Bwana Lute (katikati) wakionyesha furaha yao mara baada ya uzinduzi wa bia hiyo. Maua yaliyohudumia tukio hilo. --- Katika mkakati wake wa kuendelea kuwaletea wateja wake bidhaa zenye bora wa hali ya juu, kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) imezindua bia mpya inayojulikana kama Ndovu Red Malt, bia ambayo imetengenezwa kwa kimea kwa asilimia 100 na ikiwa ni mwendelezo wa ubunifu wenye ubora wa bia ya Ndovu Special Malt inayoongoza kwa ubora na bia pendwa kwa watumiaji wengi wa bia nchini.

 Bia ya Ndovu Red Malt imegundulika na kutengenezwa hapa nchini Tanzania ili kukidhi ladha ya wanywaji wa bia ikiwa na ubora wa kiwango cha juu na yenye ladha ya pekee kwa kulinganisha na aina nyinginezo za bia zilizopo kwenye soko.

 Uzinduzi wa bia ya Ndovu Red Malt umefanyika katika mgahawa wa 305 The Boks uliopo Kinondoni jijini Dar e Salaam Julai 20 mwaka huu ambapo wateja zaidi ya 50 walihudhuria katika hafla ya uzinduzi wake. 

 Mbali na kuwa na ladha ya aina yake inayoleta burudani kwa watumiaji wake kutokana na kutengenezwa kwa Shahiri kwa asilimia kubwa pia bia ya Ndovu Red Malt inavutia kwa mwonekano wake wa rangi kuwa na rangi ya uwekundu kwa mbali. Meneja Masoko wa vinywaji wa kampuni ya TBL Vimal Vaghmaria amesema: “Ubunifu wa kila bidhaa yetu unalenga kukidhi matakwa ya watumiaji wake ambao ni wateja wetu ambao wanahitaji kutumia bia zilizo bora na zinazokwenda na wakati katika soko”. 

 Alisema utengenezwaji wa bia ya Ndovu Red Malt kwa kutumia Shahiri kwa asilimia asilimia100 kunaleta upekee wa bia hii kwa kulinganisha na bia zingine kwenye soko na ina ladha tamu na mwonekano wake wa kuvutia ambao unaiongezea thamani. 

 Kwa upande wake, Mpishi Mkuu wa Bia wa Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Cavin Nkya, alisema kuwa bia hii mpya ya Ndovu Red Malt inazinduliwa ikiwa ni uthibitisho wa uwezo wa kampuni katika kuwapatia watanzania kinywaji chenye kiwango cha kimataifa na chenye ubora wa hali ya juu. “Ndovu Red Malt ni bia ya daraja la kwanza inayodhihirisha dhamira yetu ya kuwapatia wateja kinywaji ambacho daima wametamani kukipata kikiwa kimesheheni radha murua naya kipekee,” alisema Nkya. 

 Nkya alimalizia kwa kusema kwamba matokeo mazuri katika utayarishaji kinywaji hiki ni kutokana na uchanganyaji mahiri na wa umakini wa nafaka bora zinazozalisha hapa nchini ambazo zinazotumika kutengeneza bia Ndovu Red Malt. 

Bia hii ina kiasi cha kilevi cha asilimia asilimia 4 na inapatikana katika chupa zenye muundo maridhawa zenye ujazo wa mililita 375 ,kama zilivyo aina nyingi za bia zinazozalishwa na kampuni ya TBL zilizopo sokoni. Sasa, bia ya Ndovu Red Malt itaanza kupatikana sehemu zote nchini ambako kampuni inasambaza bidhaa zake kuanzia wiki hii kwa gharama ya shilingi 2,000/ kwa bei ya reja reja.