
HAPA NDO KWAAANZA NGOMA IMEANZA SHIMO JIPYA KUSAKA MADINI, ALIYEPEMBENI NI MMILIKI WA SHIMO AKISIMAMIA SHUGHULI.

KAMA NI SUALA LA AFYA HIKI NI MOJA YA VYOO KATIKA KUJISITIRI WANA MIGODISTI. KWA WAPENDA CHABOOZ! UKIWA JUU YA VILIMA VYA MALUNDO YA UDONGO ALIYEKO NDANI WAMCHORA FRESH... UTAIPENDA

KAZI INAENDELEA BUSINESS INAFANYIKA HILI NI MOJA KATI YA ENEO LA BONDE LENYE MASHIMO MANNE WAMILIKI TOFAUTI NA HAWAINGILIANI

ENEO HUBAKI NA MASHIMO MAKUBWA SAMBAMBA NA VILIMA VYA UDONGO, NA HII NI KUTOKANA NA UTARATIBU MBOVU WA WACHIMBAJI KWANI MARA WAMALIZAPO SHUGHULI ZA USAKAJI MADINI YA ALMASI MASHIMO HUYAACHA BILA KUYAFUKIA. TENA WENGINE WAKISHATUSUA YAANI WANAPOTEA KABISA.

NALO ENEO HILI LILIKUWA TAMBARARE TENA MAKAZI YA WATU.