ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 14, 2018

MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU NSSF.



Profesa Godius Kahyarara 
Profesa Godius Kahyarara.

Rais  John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Profesa Godius Kahyarara na kumteua William Erio kuwa mkurugenzi mpya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Julai 14, 2018 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa inasema kabla ya uteuzi huo Erio alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF.
Taaifa hiyo imesema Profesa Kahyarara atapangiwa kazi nyingine.

SERIKALI YADHAMIRIA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA MJAMZITO NA MTOTO MCHANGA MWANZA

Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazaee na watoto Ummy Mwalimu amesema licha ya kuwepo kwa changamoto nyingi za upatikanaji wa huduma za afya nchini serikali imejipanga kupunguza magonjwa na vifo vya mama mjamzito na mtoto mchanga kwani sababu zinazochangia vifo hivyo zinaweza kuzuilika.

Akizindua mradi wa impact unaolenga kupunguza magonjwa na vifo vitokanavyo na uzazi kwa mama mjamzito na mtoto mchanga Waziri wa Afya, Jinsia wazee na watoto ummy mwalimu amesema sekta ya afya bado inakabiliwa na changamoto huku akiahidi kuendelea kushirikiana na wadau kuzitatua. BOFYA KUMSIKILIZA Ummy Mwalimu……Waziri wa Afya,Jinsia,Wazee na watoto



Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mary Tesha ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana na Mbunge wa Jimbo hilo Stanslaus Mabula wanaelezea taarifa ya utoaji wa huduma za Afya Mkoani Mwanza



Vifo vitokanavyo na uzazi bado ni tatizo,huku takwimu za kitaifa zikionyesha akina mama 556 hupoteza maisha katika kila vizazi  hai laki moja na kwa Mkoa wa Mwanza vifo vimeongezeka kutoka 150 hadi vifo 195 katika vizazi hai laki moja,Ambavyo husababishwa kupoteza damu nyingi kabla na baada ya kujifungua,kifafa cha mimba,uchungu pingamizi na vifo vya watoto njiti na wanaoshindwa kupumua.

Hapa Ummy Mwalimu anatoa onyo kwa waganga wakuu na kuelezea mikakati ya serikali katika kuboresha huduma ya mama na mtoto

Mradi huo wa miaka minne wa Afya ya uzazi mama mjamzito na mtoto mchanga unaofadhiliwa na serikali ya Canada pamoja na shirika la Aghakan utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 25.3 za kitanzania na unalenga kuwafikia wanawake wenye umri wa kuzaa 650,000.




















FEISAL 'FEI TOTO' SALUM NA JAFFAR MOHAMED 'WATAMBULISHWA YANGA SC'


Kiungo wa timu ya JKU na timu ya taifa ya Zanzibar Feisal Salum 'Toto' na kiungo wa Wanalizombe, Majimaji ya Songea Jaffar Mohamed wamekamilisha uhamisho wa kuziacha timu hizo na kujiunga na miamba ya soka ya Tanzania, Yanga SC.

Friday, July 13, 2018

MBUNGE ANGELINA MABULA ATOA TAHADHARI KWA WANAODHARAU ZOEZI LA UTOAJI HATI YA UMILIKI ARDHI.



GSENGOtV
Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe. Angelina Mabula ametoa tahadhari kuwa hatokuwa tayari kumtetea mwananchi yeyote atakaye kosa haki yake ya umiliki wa ardhi kwa kudharau zoezi linaloendelea sasa la utoaji hati ya umiliki ardhi.

Mhe. Mabula ameyasema hayo alhamisi ya tarehe  12 July 2018 wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo lake katika viwanja vya Ofisi ya Kata ya Pasiansi wilayani humo kwenye ziara yake ya siku 4 kukagua shughuli za kimaendeleo pamoja na zungumza na wananchi kujadili changamoto na kuwakutanisha wananchi na wataalamu wa idara mbalimbali za Halmashauri.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe. Angelina Mabula.
Akizungumzia suala la upimaji shirikishi na zoezi la urasimishaji linaloendelea amesema zoezi hilo linaukomo ambapo muda wake ulikwishaisha toka tarehe 30 mwezi wa sita mwaka huu lakini Waziri Lukuvi aliongeza muda kutokana na hamasa kubwa ya watu kote nchini lakini pamoja na muda huo kuongezwa bado kuna baadhi ya wananchi wameonekana kudharau hatua hiyo. 

Aidha masuala mbalimbali yameweza kujadiliwa na kupatiwa majibu likiwemo suala la Ujenzi wa barabara mpya, Uboreshaji huduma za Afya, Miundombinu ya maji na umeme, Elimu, Ulinzi na Usalama. VIDEO INASEMA.







 ZIJUE FAIDA ZA KUMILIKI KIWANJA KILICHOPIMWA NA KUSAJILIWA;

Wengi wetu tunajua kuwa ardhi ndiyo nyenzo kuu ya uzalishaji hasa katika mfumo wa maisha ya kibepari (Capitalism).

Kwa wanahistoria mtakumbuka kuwa ardhi ilianza kuwa lulu tangu mfumo wa ukabaila (feudalism) ulipoanza kabla ya karne ya ishirini hapa Tanzania. 

Hata hivyo, mpaka leo ardhi imezidi kuwa lulu na ndio nyenzo muhimu zaidi ya uzalishaji.Hii inatokana na ukweli kwamba kila shughuli yoyote ya kiuchumi hutegemea ardhi kwa kiasi kikubwa. Na ndiyo maana katika sheria, ardhi hutambulika kama mali halisi (real property) kwa sababu ya upekee wake. 

Mathalani,huwezi kufanya kilimo bila ardhi, huwezi kufanya biashara bila ardhi na huwezi kujenga bila Kuwa na ardhi.Kwa hiyo kila shughuli hutegemea ardhi.Hata hivyo watanzania wengi wanapenda na wanamiliki ardhi na hili ni jambo zuri sana tu.Hata hivyo suala la msingi zaidi hapa ni je ardhi (kiwanja) chako kimepimwa kusajiliwa kisheria?

NINI FAIDA ZA KUMILIKI ARDHI (KIWANJA) KILICHOPIMWA NA KUSAJILIWA?

Kiwanja kilichopimwa na kusajiliwa hutolewa hati.Hiki ni cheti ambacho mmiliki halali wa kiwanja husika hupewa.
Zifuatazo ni faida chache za kumiliki kiwanja kilichopimwa na kusajiliwa;

1. Ni rahisi kuwekwa dhamana ya mkopo (mortgage). Dhamana ya kiwanja ndiyo dhamana ya uhakika na ya kuaminika.Hata hivyo kiwanja kilichopimwa na kusajiliwa ni muhimu zaidi na ndiyo pekee hupendelewa na maneno. Hii ni sababu kiwanja kilichosajiliwa huwa na hati inayoonesha mmiliki.Kwa hiyo mabenki hutoa mikopo kwa kushikilia hati ya mkopaji.

2. Ni rahisi kuuzika.Kununua kiwanja ni zoezi mtambuka sana.Ni shughuli inayohitaji umakini sana ili kujiridhisha kabla ya kuchukua maamuzi ya kiwanja. Hata hivyo kiwanja kilichosajiliwa hurahisisha zoezi kwani kila kitu kiko kwenye nyaraka na kwa msajili wa hati.Hivyo ni rahisi kuepuka utapeli ukilinganisha na kiwanja ambacho hakijapimwa na kusajiliwa.

3. Kiwanja kilichosajiliwa (chenye hati) ni rahisi kuonesha mmiliki halali kuliko kile kisichosajiliwa. Hii inatokana na ukweli kuwa hati ndiyo ushahidi mkubwa wa umiliki. Ndio maana ukitokea mgogoro wa umiliki, mwenye hati hupewa kipaumbele katika kumtafuta mmiliki sahihi wa kiwanja husika.

4. Kiwanja chenye hati hupunguza migogoro ya ardhi.Hii hutokana na kigezo cha nyaraka za umiliki na mipaka ya kiwanja husika.Si rahisi sana kutokea mgogoro wa umiliki kwa kiwanja kilichopimwa kama kile ambacho hakijapimwa.

5. Kiwanja kilichopimwa na kusajiliwa hupunguza ujenzi holela hivyo kupunguza Malawi ya uswahilini (slums).Hii ni Kwa sababu kila mwenye kiwanja hujenga Kwa kufuata ramani ya kiwanja chake na hivyo kuimarisha mipango miji.



Mpaka hapo kwa nini uendelee kumiliki kiwanja kisichosajiliwa? Ardhi ndiyo utajiri pekee.Kununua kiwanja ni hatua ya kwanza. Hakikisha unalinda umiliki wa kiwanja chako kwa kukisajili kikusaidie leo na kesho. 


UTAJIRI WA KWELI NI ARDHI.

AZAM FC MABINGWA TENA KOMBE LA KAGAME, WAINYUMA SIMBA 2-1



TIMU ya Azam FC imefanikiwa kutetea taji lake la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Simba SC jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Shujaa wa Azam FC hii leo alikuwa ni Nahodha na beki, Aggrey Morris Ambroce aliyefunga bao la ushindi dakika ya 80 kwa shuti kali la mpira wa adhabu kutoka umbali wa mita 30, baada ya kumchungulia kipa Deogratius Munishi ‘Dida’. 

Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua, Azam FC ilitangulia kwa bao la mshambuliaji wake hodari, Shaaban Iddi Chilunda dakikaya 33 ambaye leo alikuwa anacheza mechi ya mwisho kabla ya kwenda kuanza kuutumikia mkataba wa mkopo Tenerife ya Daraja la Kwanza Hispania.

Shahban Iddi ambaye anatimiza miaka 20 Julai 20 Mwaka huu tangu azaliwe mwaka 1998, alifunga bao hilo akiunganisha kona maridadi iliyopigwa na winga wa zamani wa Simba SC, Ramadhani Singano ‘Messi’.

Chilunda aliyejiunga na akademi ya Azam FC Jumamosi ya Julai 21, mwaka 2012 kabla ya miaka miwili baadaye kupandishwa kikosi cha kwanza, ameibuka mfungaji bora wa michuano hiyo kwa mabao yake saba.

Lakini Simba SC ilifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 62 kupitia kwa mshambuliaji wake mpya, Meddie Kagere iliyemsajili mwezi uliopita kutoka Gor Mahia ya Kenya.

Mchezaji huyo raia wa Rwanda mwenye asili ya Uganda, alifunga bao hilo akimalizia pasi ya kiungo Said Hamisi Ndemla baada ya kazi nzuri ilitofanywa na mshambuliaji Rashid Juma.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Thierry Nkurunziza kutoka Burundi, Simba ilicharuka dakika za mwishoni katika kusaka bao la kusawazisha, lakini safu ya ulinzi ya Azam FC ilikuwa makini kuondosha hatari zote.

Mapema katika mchezo uliotangulia, Gor Mahia Mahia ya Kenya ilifanikiwa kumaliza katika nafasi ya tatu, baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya JKU, mabao ya Francis Mustafa na Samuel Onyango.

Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Razack Abalora, Aggrey Morris, Nicolas Wadada, Bruce Kangwa, Abdallah Kheri, Frank Domayo, Joseph Mahundi, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Shaaban Iddi/ Yahya Zayed dk87, Ditram Nchimbi na Ramadhani Singano ‘Messi’/ Oscar Masai dk77.

Simba SC: Deo Munishi, Mohammed Hussein, Nichoals Gyan, Paul Bukaba, Pascal Wawa, James Kotei, Mzamiru Yassin, Said Ndemla/ Moses Kitandu dk83, Meddie Kagere, Mohammed Rashid na Marcel Kaheza/Rashid Juma dk60.  

DKT TIZEBA AWAPIGA MSASA WATAFITI MARUKU-BUKOBA

Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza kwenye kikao kazi kilichowakutanisha watendaji wa Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kituo cha Maruku, Taasisi ya utafiti wa kahawa (TACRI) na Uongozi wa chuo cha mafunzo ya kilimo MARUKU katika kijiji cha Butairuka Kata ya Maruku Wilayani Bukoba vijijini, Leo 13 Julai 2018. (Picha zote Na Mathias Canal-WK)
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba mbegu za maharege zinazofanyiwa utafiti na Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kituo cha Maruku, wakati akiwa katika ziara ya kikazi katika kijiji cha Butairuka Kata ya Maruku Wilayani Bukoba vijijini, Leo 13 Julai 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza kwenye kikao kazi kilichowakutanisha watendaji wa Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kituo cha Maruku, Taasisi ya utafiti wa kahawa (TACRI) na Uongozi wa chuo cha mafunzo ya kilimo MARUKU katika kijiji cha Butairuka Kata ya Maruku Wilayani Bukoba vijijini, Leo 13 Julai 2018. 
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba mbegu za maharege zinazofanyiwa utafiti na Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kituo cha Maruku, wakati akiwa katika ziara ya kikazi katika kijiji cha Butairuka Kata ya Maruku Wilayani Bukoba vijijini, Leo 13 Julai 2018.


Na Mathias Canal-WK, Bukoba-Kagera

UONGOZI wa Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kituo cha Maruku, Taasisi ya utafiti wa kahawa (TACRI) umetakiwa kuongeza ufanisi katika utaalamu wao ili kuwanufaisha wakulima kote nchini kwani kwa sasa Benki ya Tafiti zilizopo hazijatumika ipasavyo.


Wataalamu wa utafiti wamepaswa kufanya vizuri pia katika eneo la kutangaza tafiti zao ikiwemo Kuongeza ujuzi katika Utafiti wa Mazao mbalimbali ikiwa ni pamoja na zao la kahawa ili kuongeza uwezo wa uzalishaji wa miche.

Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao kazi kilichowakutanisha watendaji wa taasisi hizo za utafiti sambamba na uongozi wa chuo cha mafunzo ya Kilimo MARUKU katika kijiji cha Butairuka Kata ya Maruku Wilayani Bukoba vijijini.


Waziri huyo wa kilimo aliwasihi watafiti hao Kuendelea kufanya juhudi kubwa kuandika miradi mbalimbali (Reseach Proposals) kwa ajili ya kusaidia shughuli za uendelezaji wa utafiti kwani bajeti ya serikali pekee haiwezi kutosha kukamilisha kila changamoto zinazowakabili.

Alisema wataalamu hao wanapaswa kufanya tafiti kwa kuendana na matakwa ya sekta ya kilimo na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ili kuongeza tija katika uzalishaji wa Kahawa nchini sambamba na Mazao mengine.

Aliwasihi kuongeza ushirikiano ili kuendelea na utafiti kuhusu njia bora za uzalishaji mazao, urutubishaji udongo, mfumo wa usambazaji wa teknolojia, masoko yenye tija, tathmini ya uenezaji wa teknolojia na mchango wa matokeo ya utafiti katika kuboresha hali ya maisha ya wananchi na uchumi wa taifa kwa ujumla.

Alisema kuwa kituo cha utafiti wa kilimo kinapaswa kuendelea na juhudi za uzalishaji wa mbegu bora za mazao mbalimbali kama vile maharage, viazi vitamu, muhogo na mengineyo.

Kituo cha utafiti wa kilimo cha Maruku (TARI-MARUKU) ni kati ya vituo viwili vya utafiti wa kilimo katika Kanda ya ziwa ambapo makao makuu yake yapo Ukiriguru-Mwanza ambapo kinatoa mafunzo na ushauri kwa wakulima na wadau mbalimbali wa kilimo juu ya teknolojia mbalimbali za kilimo.

Katika hatua nyingine Waziri Tizeba amemuagiza Mkuu wa chuo cha mafunzo ya kilimo Maruku Ndg Laurent Mathew Luhembe ndani ya mwaka mmoja kutatua changamoto ya ukosefu wa bweni la chakula.

Aliongeza kuwa chuo hicho kinapaswa kubuni mbinu mbadala za mapato ikiwa ni pamoja na kujenga kitalu nyumba (Green House) kwani itasaidia kuongeza kipato mahususi na hatimaye chuo kujiendesha badala ya kutaka changamoto zote zitatuliwe na serikali.

Aidha, Taasisi hizo za utafiti ikiwa ni pamoja na Chuo cha Maendeleo ya kilimo Maruku zimetakiwa kuhakikisha wanatunza ardhi yao ili kuondosha hofu ya uvamizi wa maeneo.

NECTA YAZUIA MATOKEO YA WATAHINIWA 13


Baraza la Mtihani la Tanzania (NECTA) limezuia matokeo ya watahiniwa kumi na tatu kutokana na sababu kadhaa na wengine nane kufutiwa kabisa matokeo kwa sababu ya udanganyifu.

Akitaja sababu za kuzuiwa kwa matokeo hayo, Katibu mtendaji wa baraza hilo Dkt. Charles Msonde wakati akitangaza matokeo hayo leo visiwani Zanzibar, amesema kuwa kuna baadhi ya watahiniwa walishindwa kukamilisha mitihani yao kutokana na sababu za kiafya na hivyo kufanya mitihani nusu, watapewa nafasi ya kurudia mwaka unaofuata.

Licha ya hiyo, Dkt. Msonde amesema kuwa ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 96.06% mwaka 2017 hadi 97.12% mwaka huu, huku ufaulu katika masomo ya sayansi umeshuka ukilinganishwa na masomo ya sanaa na biashara.

“Jumla ya watahiniwa 83,581 sawa na asilimia 97.58 ya watahiniwa waliofanya mitihani ya kidato cha sita Mei mwaka huu wamefaulu huku wasichana wakiwa ni 34,358, na wavulana waliofaulu ni 49,223 pekee”, amesema Dkt. Msonde.

Dkt. Msonde ameongeza kuwa tathmini ya hali ya matokeo imeonesha kuimarika kwa ufaulu katika madaraja ya I,II na III ikiwemo kupanda kwa asilimia 1.80 kutoka 93.72 mwaka 2017 na kuwa asilimia 95.52 mwaka 2018.

Shule zilizofanya vizuri zimetajwa kuwa ni Kibaha, Kisimiri, Kemebos na Mzumbe, Feza Boys, Marian Boys, AHMES, St Mary's Mazinde Juu, Marian Girls & Feza Girls.

ZAIDI YA BILIONI 23 ZAHAWILISHWA KWA WALENGWA WA KAYA MASKINI GEITA.

 Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Mhandisi Robert Gabriel, ameendesha kikao cha Tatu cha Tathimini ya Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini TASAF Awamu ya Tatu ambacho hufanyika mara moja kila mwaka tangu kuanza kwa mpango huo.


Akiongea na wajumbe wa kikao hicho, Mhe. Mhandisi Gabriel alianza kwa kuwapongeza waandishi wa habari kwa kuendelea kutoa taarifa sahihi, lakini pia kuwashukuru waratibu wa mpango huo kuanzia ngazi ya Sekretarieti ya Mkoa hadi ngazi za Halmashauri na kusema kuwa, ni imani yake kikao hicho kitaweka mikakati thabiti ili kupata matokeo chanya. Ni baada ya kusomewa taarifa ya utekelezaji wa mpango huo, ndani ya ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Geita tarehe 12.07.2018.

Mkuu wa Mkoa aliendelea kwa kusema “nimeona mabadiliko makubwa ,nimefurahishwa na mashamba ya pamba ambayo yanamilikiwa na walengwa wa mpango. Nawashukuru sana viongozi kwa usimamizi mzuri, hivyo ni vyema viongozi kuendelea kuzitembelea kaya hizi na kila mmoja kwa nafasi yake, kwenye eneo lake, ahakikishe TASAF awamu hii inakuwa yenye manufaa kwenye eneo husika lakini walengwa wanaondokana na umasikini kupitia ufuatiliaji wa karibu ili nia ya Serikali ya Awamu ya Tano iendelee kufanikiwa”.
 Akisoma taarifa ya utekelezaji, Mratibu wa TASAF ngazi ya Mkoa Bw. Elikana J. Harun alieleza kuwa, Mkoa wa Geita umehawilisha jumla ya Shilingi Bilioni Ishirini na Tatu, Mia Sita Themanini Milioni, Sitini na Nane Elfu na Hamsini na Nane  (Tshs.23,680,068,058) sawa na asilimia 98.32 ya fedha zilizopokelewa ili kutekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini – TASAF awamu ya Tatu kuanzia Julai 2015/2016 hadi Juni, 2017/2018, kazi iliyofanyika kwa vipindi 18 katika Mitaa 27 na Vijiji 321 vilivyoingizwa kwenye mpango huo kwenye halmashauri sita za Mkoa wa Geita, Bw. Harun aliyataja mafanikio mbalimbali waliyoyapata kaya hizo yakiwemo kuongezeka idadi ya wazazi na walezi wanaopeleka watoto kliniki, kaya kupata uwezo wa kununua chakula na mahitaji mengine tofauti na awali na baadhi yao kuanzisha miradi midogo midogo ya uzalishaji mali. 

Alianisha baadhi ya changamoto zikiwemo upungufu wa magari unaopelekea shughuli hiyo kuchelewa lakini pia baadhi ya walengwa kutohudhuria wakati wa uhawilishaji fedha kutokana na kuhama, safari za mbali n.k. jambo lililopelekea asilimia mia kutofikiwa.
 Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Bw. Selestine Gesimba aliwaasa Wajumbe wa kikao kujitahidi kuwasaidia walengwa hao ili hata mpango unapokoma basi waweze kuwa wamejikwamua. Alimaliza kwa mfano wa biblia wa mpanzi akisema, “mbegu imeshapandwa, sasa wajumbe tujihoji kama je, zimeanguka kwenye mwamba, kwenye magugu, kwenye miiba au udongo mzuri utakaowezesha mti kuzaa matunda?.
 Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe. Shaaban Ntarambe Kwaniaba ya viongozi waliohudhuria yaani Wahe.Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa mwongozo mzuri alioutoa na kuahidi utekelezaji wake kufanyika kwa kusema, “yote aliyosema Mkuu wa Mkoa yanatuhusu viongozi na watendaji na katika awamu hii ya tano tunatakiwa kuwa eyes on and hands on” alimaliza.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu TASAF Bw. Zacharia Ngoma alipongeza kasi ya Geita baada ya michango iliyotoka kwa waheshmiwa wakuu wa Wilaya za Geita ambao pia walihudhulia akiamini kama viongozi wana uelewa mzuri wa mpango huo, basi utafanikiwa; kisha kuwakumbusha kuzitembelea kaya maskini vijijini ili kujifunza mengi zaidi.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Waratibu, Wahasibu na Maafisa Ufuatiliaji wa TASAF ngazi ya Halmashauri na Wilaya bila kusahau Sekretarieti ya Mkoa.

MABONDIA SHOMARI MILUNDI RAMADHANI MIGWEDE WASAINI KUZIPIGA DAR LIVE SIKU YA NANENANE

Promota wa mpambano wa ngumi Zahoro Maganga katikati akiwanuwa mikono juu kuwatambulisha mabondia Ramadhani Migwede 'kushoto' na Shomari Milundi kulia kwa ajili ya mpambano wao wa agost 8 utakaofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Ramadhani Migwede Kushoto akitunishiana misuli na Sgomari Milundi baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga Agost 8 katika ukumbi wa Dar Live Mbagala katikati ni Promota wa mpambano uho Zahoro Maganga Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Ramadhani Migwede Kushoto akitunishiana misuli na Sgomari Milundi baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga Agost 8 katika ukumbi wa Dar Live Mbagala katikati ni Promota wa mpambano uho Zahoro Maganga Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Sgomari Milundi akisaini mkataba kwa ajili ya kuzipiga na Ramadhani Migwede siku ya nane nane Mabondia atika  Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Ramadhani Migwede akisaini mkaraba wa kuzipiga na Shomari Milundi siku ya nanenane katika ukumbi wa Dar Live Mbagala  Picha na SUPER D BOXING NEWS


Na Mwandishi Wetu

MABONDIA  Shomari Milundi na Ramadhani Migwede wamesaini kuzipiga Agost 8 katika ukumbi wa Dar live Mbagala mpambano wa raundi sita mabondia hawo wenye mashabiki lukuki watapanda ulingoni kusindikiza mpambano wa mahasimu wawili litakalopigwa siku hiyo.

Watakutana bondia Abdallah Pazi 'Dulla Mbabe' na Saidi Mbelwa 'Moto wa Gesi' watazipiga kwa raundi kumi zisizo na ubingwa mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mbalimbali ya ngumi pamoja na burudani mbalimbali zitakazo kuwepo siku hiyo

Akizungumza kuhusu mpambano huo Promota Zahoro Maganga amesema siku hiyo kutakuwa na burudani za kutosha hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kuja kushidia mpambano uho uliokuwa unasubiliwa kwa hamu kubwa sana na mashabiki wa mchezo wa ngumi.

Ujue mabondia hawa walikuwa wakitafutana mda mrefu na walitaka kupigana ila mpambano wao aujafanyika sasa mimi nikamuwa kuwakutanisha ili wazipige kwa ajili ya kujua nani zaidi katika mpambano wa masumbwi alisema Maganga.

Siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatuampaka kujua kitu kamili katikamchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani.

DKT TIZEBA AITAKA CRDB KULIPA FEDHA ZA USHIRIKA (KCU)

Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza na wadau wa Kahawa Wilayani Muleba wakati wa ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani Kagera, Jana 12 Julai 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Muleba kusini Mhe. Prof Anna Tibaijuka kabla ya mkutano na wadau wa Kahawa Wilayani Muleba wakati wa ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani Kagera, Jana 12 Julai 2018.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage akimakabidhi muongozo wa ujenzi wa viwanda Mkuu wa Wilayani ya Muleba Mhe Richard Ruyango mara baada ya kuwasili Wilayani humo kwa ajili ya mkutano wa wadau wa Kahawa wakati wa ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani Kagera, Jana 12 Julai 2018. Mwingine pichani ni Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt Consolata Ishebali.
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza na wadau wa Kahawa Wilayani Muleba wakati wa ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani Kagera, Jana 12 Julai 2018. 

Na Mathias Canal-WK, Muleba-Kagera

Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba Jana 12 Julai 2018 ameitaka Benki ya CRDB kulipa haraka malipo ya fedha za Ushirika za Chama Kikuu cha Kagera (KCU) kulingana na hatma ya kesi iliyokuwa mahakamani mwaka 2003 ambapo wakulima walikuwa wakikatwa kiasi cha shilingi 10 kwa kila kilo moja ya Kahawa ili kujenga mfuko wa Mazao kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 1990 hadi 1993.

Dkt Tizeba ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye mkutano uliowakutanisha wadau wa Kahawa Wilayani Muleba ikiwa ni siku ya tatu ya ziara ya kikazi mkoani Kagera iliyoanza Juzi 10 Julai 2018 na kuhudhuriwa pia na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage.

Swala la madai hayo katika mkutano huo liliibuka baada ya baadhi ya wakulima kuonyesha vitabu vya mfuko huo ambapo makato hayo ya shilingi 10 kwa kilo kwa kipindi cha miaka mitatu jinsi ambavyo yalikuwa yakifanyika.

Madai ya wakulima hao yamekuwa yakilalamikiwa kwa kipindi kirefu na kuchangia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa imani ya wakulima kwa chama kikuu cha ushirika Kagera (KCU).

Chanzo cha kesi hiyo ni baada ya Benki ya CRDB kuzuia fedha za malipo yaliyotokana na mauzo ya Kahawa ili kulipia deni la msimu wa mwaka 1997/1998.

Hukumu ya kesi iliyotolewa tarehe 28 Octoba 2009 na mfuko wa Mazao wa wakulima Mkoani Kagera kupewa tahfifu ulizoomba ambapo tangu wakati huo Benki ya CRDB iliweza kulipa fedha za mfuko ilizochukua kiasi cha shilingi milioni 525 na fedha zilizobaki bado hazijalipwa kwa kisingizio cha kuwa na nia ya kukata rufaa ambayo bado haijakatwa ambapo hata hivyo hawawezi kukata rufaa kutokana na muda kuwa umepita.

Dkt Tizeba alisema kuwa Jumla ya madai hayo sambamba na riba ni shilingi Bilioni sita za kitanzania huku akisisitiza kuwa Benki hiyo ya CRDB inapaswa kuwa mfano wa Benki zingine nchini hivyo kushindwa kuwalipa wakulima kwa wakati ni kushindwa kwenda na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

Wakati huo huo Waziri Tizeba aliagiza Halmashauri zote nchini zinazolima Kahawa kusimamia ukusanyaji wa Kahawa kwenda vya Msingi (AMCOS) kwani kutokana na usimamizi huo ndio hupata ushuru wa Halmshauri.