ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 13, 2018

MBUNGE ANGELINA MABULA ATOA TAHADHARI KWA WANAODHARAU ZOEZI LA UTOAJI HATI YA UMILIKI ARDHI.



GSENGOtV
Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe. Angelina Mabula ametoa tahadhari kuwa hatokuwa tayari kumtetea mwananchi yeyote atakaye kosa haki yake ya umiliki wa ardhi kwa kudharau zoezi linaloendelea sasa la utoaji hati ya umiliki ardhi.

Mhe. Mabula ameyasema hayo alhamisi ya tarehe  12 July 2018 wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo lake katika viwanja vya Ofisi ya Kata ya Pasiansi wilayani humo kwenye ziara yake ya siku 4 kukagua shughuli za kimaendeleo pamoja na zungumza na wananchi kujadili changamoto na kuwakutanisha wananchi na wataalamu wa idara mbalimbali za Halmashauri.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe. Angelina Mabula.
Akizungumzia suala la upimaji shirikishi na zoezi la urasimishaji linaloendelea amesema zoezi hilo linaukomo ambapo muda wake ulikwishaisha toka tarehe 30 mwezi wa sita mwaka huu lakini Waziri Lukuvi aliongeza muda kutokana na hamasa kubwa ya watu kote nchini lakini pamoja na muda huo kuongezwa bado kuna baadhi ya wananchi wameonekana kudharau hatua hiyo. 

Aidha masuala mbalimbali yameweza kujadiliwa na kupatiwa majibu likiwemo suala la Ujenzi wa barabara mpya, Uboreshaji huduma za Afya, Miundombinu ya maji na umeme, Elimu, Ulinzi na Usalama. VIDEO INASEMA.







 ZIJUE FAIDA ZA KUMILIKI KIWANJA KILICHOPIMWA NA KUSAJILIWA;

Wengi wetu tunajua kuwa ardhi ndiyo nyenzo kuu ya uzalishaji hasa katika mfumo wa maisha ya kibepari (Capitalism).

Kwa wanahistoria mtakumbuka kuwa ardhi ilianza kuwa lulu tangu mfumo wa ukabaila (feudalism) ulipoanza kabla ya karne ya ishirini hapa Tanzania. 

Hata hivyo, mpaka leo ardhi imezidi kuwa lulu na ndio nyenzo muhimu zaidi ya uzalishaji.Hii inatokana na ukweli kwamba kila shughuli yoyote ya kiuchumi hutegemea ardhi kwa kiasi kikubwa. Na ndiyo maana katika sheria, ardhi hutambulika kama mali halisi (real property) kwa sababu ya upekee wake. 

Mathalani,huwezi kufanya kilimo bila ardhi, huwezi kufanya biashara bila ardhi na huwezi kujenga bila Kuwa na ardhi.Kwa hiyo kila shughuli hutegemea ardhi.Hata hivyo watanzania wengi wanapenda na wanamiliki ardhi na hili ni jambo zuri sana tu.Hata hivyo suala la msingi zaidi hapa ni je ardhi (kiwanja) chako kimepimwa kusajiliwa kisheria?

NINI FAIDA ZA KUMILIKI ARDHI (KIWANJA) KILICHOPIMWA NA KUSAJILIWA?

Kiwanja kilichopimwa na kusajiliwa hutolewa hati.Hiki ni cheti ambacho mmiliki halali wa kiwanja husika hupewa.
Zifuatazo ni faida chache za kumiliki kiwanja kilichopimwa na kusajiliwa;

1. Ni rahisi kuwekwa dhamana ya mkopo (mortgage). Dhamana ya kiwanja ndiyo dhamana ya uhakika na ya kuaminika.Hata hivyo kiwanja kilichopimwa na kusajiliwa ni muhimu zaidi na ndiyo pekee hupendelewa na maneno. Hii ni sababu kiwanja kilichosajiliwa huwa na hati inayoonesha mmiliki.Kwa hiyo mabenki hutoa mikopo kwa kushikilia hati ya mkopaji.

2. Ni rahisi kuuzika.Kununua kiwanja ni zoezi mtambuka sana.Ni shughuli inayohitaji umakini sana ili kujiridhisha kabla ya kuchukua maamuzi ya kiwanja. Hata hivyo kiwanja kilichosajiliwa hurahisisha zoezi kwani kila kitu kiko kwenye nyaraka na kwa msajili wa hati.Hivyo ni rahisi kuepuka utapeli ukilinganisha na kiwanja ambacho hakijapimwa na kusajiliwa.

3. Kiwanja kilichosajiliwa (chenye hati) ni rahisi kuonesha mmiliki halali kuliko kile kisichosajiliwa. Hii inatokana na ukweli kuwa hati ndiyo ushahidi mkubwa wa umiliki. Ndio maana ukitokea mgogoro wa umiliki, mwenye hati hupewa kipaumbele katika kumtafuta mmiliki sahihi wa kiwanja husika.

4. Kiwanja chenye hati hupunguza migogoro ya ardhi.Hii hutokana na kigezo cha nyaraka za umiliki na mipaka ya kiwanja husika.Si rahisi sana kutokea mgogoro wa umiliki kwa kiwanja kilichopimwa kama kile ambacho hakijapimwa.

5. Kiwanja kilichopimwa na kusajiliwa hupunguza ujenzi holela hivyo kupunguza Malawi ya uswahilini (slums).Hii ni Kwa sababu kila mwenye kiwanja hujenga Kwa kufuata ramani ya kiwanja chake na hivyo kuimarisha mipango miji.



Mpaka hapo kwa nini uendelee kumiliki kiwanja kisichosajiliwa? Ardhi ndiyo utajiri pekee.Kununua kiwanja ni hatua ya kwanza. Hakikisha unalinda umiliki wa kiwanja chako kwa kukisajili kikusaidie leo na kesho. 


UTAJIRI WA KWELI NI ARDHI.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.