ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 5, 2018

"KATIKA MUONEKANO MPYA WA KUVUTIA HII NDIYO VILLA PARK MWANZA"

  Baada ya ukarabati wa muda wa miezi miwili, kile kiunga chako chenye hadhi jijini Mwanza Villa Park Resort, hivi sasa kiko tayari tena kukuhudumia.
Sote tunapenda samaki fresh.....nao wanapatikana Villa Park Resort pekee.
Kuku choma, samaki banika hapa ndipo nyumbani kwake.
Sato, Sangara, Kamongo hadi Mumi wanapatikana hapa.
Chachandu ya hapa iko shkopa....
Usafi na huduma za jikoni.......mmmmmmH ni utamu tu!
Pishi hili laitwa Brenda Fasie....ukifika Villa Park Resort jaribu kuulizia, utamuwe utanambia.
Wali waliwa, Mchele wachelewa.
Karibu upate Ndizi za Bukoba, Ndizi Laini, Ndizi Mshale......
Twende mezani.....
Muonekano mpya wa VIP area ambayo haikugharimu chochote cha ziada kuitwa VIP, hapa nikimaanisha ukifika tu Villa Park Resort wewe una hadhi ya VIP.
Another shoot.
The muonekanoZ.
Ze angle at Villa Park Resort Mwanza Tanzania.
Jeh utakaa hapa ama pale?
Mazingira.
Haujifika Mwanza kama haujafika Villa Park Resort.

KUMBE MOURINHO ALITABIRI TIMU YAKE KUCHEZEA KICHAPO!

Anthony Knockaert akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Brighton & Hove Albion bao pekee dakika ya 57 ikiwalaza Manchester United 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja The American Express Community usiku wa Ijumaa.
 "Duh tumepigwa.......!"
Jose Mourinho na kauli yake: “It was not good enough,” he tells Sky Sports. “Wachezaji walio chukua nafasi katika mabadiriko hawakuwa katika kiwango kizuri. Mchezaji mmoja mmoja asipocheza katika kiwango kizuri, ni vigumu kwa timu kupata matokeo. "Hata wachezaji wangu ukiwauliza nilijua masaibu haya yatakwenda kutokea, na niliwaambia hata kabla ya mchezo nikawapa tahadhari" Alisema Mourinho 

 "My players will tell you that before the match I knew what was going to happen and I told them. At half-time I knew what was going to happen. I knew it and I told them.”

Friday, May 4, 2018

HIKI NDICHO ALICHOFANYA RAIS MAGUFULI LEO AKIWA MIKUMI.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempigia simu Katibu Mkuu wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo mbele ya wananchi wa kijiji cha kidodi , kumtaka kumchukulia hatua mkandarasi aliyepewa mradi wa maji na kutoukamilisha.


Akizungumza kwa sauti kubwa huku wananchi wa Kidodi wakiwa wanasikiliza 'live', Rais Magufuli amesema kwamba mkandarasi huyo alishapewa pesa za mradi milioni 800 lakini maji hayajafika kwa wananchi, hivyo ahakikishe amechukuliwa hatua za kisheria au awepo eneo la mradi kukamilisha.
Awali kabla ya kupiga simu hiyo, Rais Magufuli ametuma salamu kwa mkandarasi huyo kupitia wananchi wa kijiji cha Kidodi, kumtaka azirejeshe fedha alizopewa za mradi pasipo kutekeleza mradi huo muhimu kwa jamii.
“Nafahamu kuna mradi wa maji wa milioni 800 na mkandarasi alipewa, lakini maji hayajafika kwa wananchi, nilidhani mbunge wenu atauliza achukuliwe hatua gani lakini hajauliza, na mkandarasi kama alikula hela atazitapika, naomba mumfikishie huu ujumbe”, amesema Rais Magufuli.
Baada ya simu hiyo Profesa Mkumbo amesema anatarajia kuanza safari mchana huu kwenda kijijini hapo kushughulikia tatizo hilo, na mpaka kesho atakuwa ameshafika eneo la tukio na kutoa suluhu.


TRA YAANZA RASMI ZOEZI LA KUSAJILI WAMACHINGA MWANZA.


NA ZEPHANIA MANDIA WA G.SENGO TV
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, ameziagiza halmashauri zote mkoani hapa kuhakikisha asilimia tano za wanawake na vijana, zilizokuwa zikitolewa katika makundi hayo,  zianze kutolewa kwa wafanyabiashara ndogo ndogo (Machinga) ambao wamesajiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) 

Mongella ametoa agizo hilo wakati wa zoezi la ugawaji wa vitambulisho maalumu kwa wafanyabiashara ndogo ndogo jijini Mwanza waliojiunga katika vikundi mbalimbali vya wajasliamali, ambapo amesema atashangazwa kuona vikundi  ambavyo sio rasmi vikipewa mikopo.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Charles Kichere, amewaomba wafanyabiashara wadogo wadogo (Machinga) kujiunga katika vikundi vidogo vidogo ili waweze kunufaika na mikopo mbalimbali inayotolewa na Taasisi za kifedha.

Naibu Kamishna wa kondi za ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Michael Mhoja, amesema mamlaka hiyo tayari imesajili vikundi 30 vya wafanyabiashara ndogo ndogo vyenye jumla ya wafanyabiashara 1,110 huku akidai mpango wao ni kusajili vikundi 130.

Nae Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire akatoa neno kwa wajasliamali hao huku baadhi ya wafanyabiashara hao nao wakazungumzia zoezi hilo.
PIGA KAMBI YA UTALII NDANI YA NGORO NGORO CRATER.

IMG-20180502-WA0026 1
LISA FICKENSCHER ADVENTURES presents PIGA KAMBI UTALII WA NDANI in NGORO NGORO CRATER from 11th to 13th may, Trip starts From Dar - es- salaam only for 395000/= price includes -:
Transport
Accommodation two nights
Park Fee
Game Drive
Snake park
Masai village

For more Information contacts us: ±255712711111 / ±255768288898
Email : Lisafickenscher02@gmail.com
or Visit our Instagram page : @utaliiwandani @lisa_fickenscher

UHAMIAJI WAWATAKA RAIA WOTE WA KIGENI WANAOISHI MKOANI MWANZA KUJIORODHESHA KATIKA DAFTARI LA WAGENI.

NA ZEPHANIA MANDIA G.SENGO TV
Idara ya uhamiaji mkoani  Mwanza imewataka raia wote wa kigeni wanaoishi katika jiji la Mwanza kuhakikisha wanajiorodhesha katika daftari la orodha ya wageni wanaoishi hapa nchini ambayo yametolewa katika ofisi za watendaji wa kata na mitaa katika jiji hilo.

Agizo hilo limetolewa na Afisa uhamiaji mkoa wa mwanza, Naibu kamishna wa uhamiaji, Paul Eranga wakati akitoa elimu ya uraia na wajibu wa viongozi wa serikali katika kukabiliana na wimbi kubwa la wahamiaji haramu  kwa wenyeviti, watendaji wa kata na mitaa zaidi ya 60 kutoka kata 18 za wilaya ya nyamagana mkoani Mwanza ambapo amesema raia yeyote wa kigeni ambaye atakaidi agizo hilo atachukuliwa hatua zakisheria kwa atakayebainika. 

Aidha naibu afisa uhamiaji wa mkoa huo na afisa uhamiaji wa wilaya ya nyamagana moses mutash wamewataka watendaji na wenyeviti hao kufuata sheria na taratibu zinazoelekeza hatua za kufuatwa katika kufanya maamuzi na kuidhinisha maombi ya uraia ambayo yanawasilishwa kwao na raia wa kigeni.

Kwa upande wao baadhi ya watendaji hao wametoa hisia zao kuhusiana na elimu ya uraia na wajibu wao katika kukabiliana na wimbi kubwa la wahamiaji haramu katika maeneo yao na kuomba ushirikiano kutoka kwa maafisa uhamiaji punde wanapowabaini wahamiaji haramu katika maeneo yao ukizingatia jiji la Mwanza ni lango kubwa kwa nchi jirani UGANDA, RWANDA, BURUNDI, DR CONGO NA KENYA. 

VIDEO: BABU SEYA NA BENDI YAKE WAKARIBISHWA DINNER NA DIAMOND LOUNGE MWANZA


Baada ya ya kutinga jijini Mwanza marafiki wa kiota cha burudani kilicho maarufu jijini hapa kinachopatikana kona ya Bwiru wilayani Ilemela, Diamond Lounge wamesema katu lazima wa-show love na Babu Seya na Mwanae.

Hapa ni sehemu ya hafla kimya kimya ya chakula cha jioni ambapo uongozi wa eneo hilo umehaidi mara baada ya kumaliza show zao kwa mikoa ya Geita (leo ijumaa) na Mwanza (kesho jumamosi) watawazawadia ndoo za samaki wanamuziki hao wakati wakirejea jijini Dar es salaam.
Ujio wa mwanamuziki Nguli wa muziki wa Dansi nchini Tanzania Nguza Viking al maarufu Babu Seya akiwa na mwanaye Papii Kocha unakuja  ikiwa ni kwaajili ya kuikata ile kiu ya muda mrefu ya burudani ya muziki wa ukweli waliyoikosa kwa takribani miaka 14 wakati wakali hao walipokuwa wametupwa gerezani.

HISTORIA
Mnamo Tarehe 9 Mwezi Disemba 2016 msamaha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli uliwajumuisha mwanamziki maarufu nchini Tanzania Nguza Viking, maarufu kama Babu Seya aliyehukumiwa kifungo cha maisha jela.
Msamaha huu unatajwa kuwa historia na hasa kuwasamehe wafungwa wa maisha na wale wa kunyongwa ambapo kwa wakunyongwa waliachiwa huru ni 61 na wengine walioachiwa huru kutokana na makosa mbali mbali ni 1,821 huku wengine 8157 wamepunguziwa adhabu zao.

WATU WENYE SILAHA WAVAMIA OFISI ZA SHIRIKA LA MSALABA MWEKUNDU MJINI MOGADISHU SOMALIA.

Watu wenye silaha wavamia ofisi za shirika la Msalaba Mwekundu mjini Mogadishu SomaliaWatu wenye silaha jana walizivamia ofisi za Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu za Mogadishu, mji mkuu wa Somalia na kumteka nyara muuguzi mmoja wa kike, raia wa Ujerumaini.
CHANZO/PARStODAY
Jeshi la polisi linaendelea na operesheni ya kumtafuta Bi Sonja Nientiet aliyetekwa nyara na watu wennye silaha katika ofisi wa shirika la Msalaba Mwekundu mjini Mogadishu.
Tukio hilo lilitokea Jumatano jioni baada ya watu wenye silaha kuvamia eneo hilo na kumteka nyara muuguzi huyo na kutoroka naye mlango wa nyuma ili kukwepa kuonekana na walinzi wa ofisi hizo. 

Ofisi za shirika la Msalaba Mwekundu mjini Mogadishu Somalia
Muuguzi huyo amekuwa akilifanyia kazi Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu tangu mwaka 2014 katika maeneo yenye vita ikiwemo Syria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 
Utekaji nyara huo ni tukio la pili kubwa lililowahusisha wafanyakazi wa afya nchini Somalia wiki hii baada ya mfanyakazi mwingine wa Shirika la Afya Duniani WHO, Mariam Abdullahi kutekwa nyara siku ya Jumanne.
Msaidizi wa shirika la Msalaba Mwekundu, nchini Somalia, Daniel O’Malley, amesema: "Tuna wasiwasi mkubwa na usalama wa mwenzetu huyo."
"Ni muuguzi ambaye amejitolewa kuokoa maisha ya watu kila siku na kuboresha kiwango cha afya katika baadhi ya maeneo yenye matatizo mengi zaidi nchini Somalia."
Hadi hivi sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na uvamizi huo, ingawa matukio kama hayo mara nyingi hufanywa na genge la kigaidi la ukufurishaji la al Shabaab.

HUENDA MLANGO WA SERIKALI UMEFUNGULIWA SASA KWA WANAHABARI?

Waziri wa Habari, Utamaduni na michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema Serikali imefungua milango ya majadiliano na wanahabari kuhusu changamoto zao.

Waziri Mwakyembe amesema hayo leo katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ambapo ameweka wazi kwamba Serikali imetoa haki ya kupelekwa mahakamani mashauri mbalimbali kuhusiana na sheria ambazo zimepitishwa lakini bado kuna fursa nzuri ya kufanya mazungumzo na wadau.

“Serikali itaendelea kusimamia sheria zilizotungwa katika kuhakikisha wanahabari na wamiliki wa mitandao ya kijamii wanafanyakazi kwa weledi na kujali maslahi ya taifa na tamaduni,” amesema.

Amesema Serikali itahakikisha inasimamia kuundwa kwa vyombo vitatu katika kutekeleza sheria ya huduma za habari, ambavyo ni baraza huru la habari, Bodi ya Ithibati na kuwepo kwa mfuko wa kusaidia wanahabari.

Thursday, May 3, 2018

UCHAGUZI MKUU YANGA KUFANYIKA JUNI 7.

UONGOZI na Kamati ya Maandalizi Klabu ya Yanga SC wamefanya mabadiliko kwa kusogeza mbele tarehe ya Mkutano Mkuu wao.

Mkutano Mkuu wa klabu hiyo ulikuwa ufanyike Mei 5 mwaka huu lakini sasa unatarajia kufanyika Juni 7 mwaka huu katika Bwalo la Polisi Oyestabey jijini Dar es Salaam kuanzia saa tatu asubuhi.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga Charles Boniphase Mkwasa amesema kamati imekaa na kujadiliana, hivyo wameona wasogeze mbele tarehe ya mkutano huo kwa sababu za kimsingi zilizojitokeza.

"Tuna mechi nyingi za Ligi zitakazokuwa zinaendelea  hapa katikati pamoja na hilo baadhi ya  viongozi watakuwa nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wetu wa kwanza katika hatua ya makundi katika Shirikisho Barani Afrika dhidi ya  USM Alger, "amesema Mkwasa.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Makundi ya WhatsApp ya Yanga Tanzania Bakili Makele amewataka wanachama wote wa klabu hiyo nchini kulipi kadi zao.

"Ni muhimu kwa kila mwanachama kulipia kadi yake ya uanachama iwe ya Benki au ya kawaida ili auhudhurie mkutano huo ili kila mmoja apate haki yake ya kuchangia  na hatimaye kuondoa changamoto zilizopo na tusonge mbele,”amesema Makele.

ALI KIBA, DIAMOND NA BEN PAUL WATAJWA WAKATI BABU SEYA NA MWANAE WAKIIBUSU ARDHI YA MWANZAAli Kiba, Diamond Platnumz pamoja na Ben Paul wamehusishwa kwenye majibu ya maswali aliyoulizwa na waaandishi wa habari yaliyoelekezwa kwake mwanamuziki Papii Kocha wakati akitua kwa mara ya kwanza katika uwanja wa ndege jijini Mwanza.

Ndani ya abiria waliotua hii leo majira ya saa 5:20 asubuhi kwa kutumia ndege ya shirika la Precision Air,  yumo mwanamuziki Nguli wa muziki wa Dansi nchini Tanzania Nguza Viking al maarufu Babu Seya akiwa na mwanaye Papii Kocha ambao ujio wao unakuja  kwaajili ya kuikata ile kiu ya muda mrefu ya burudani ya muziki wa ukweli waliyoikosa kwa takribani miaka 14 wakazi wa Kanda ya Ziwa miji ya Mwanza na Geita.