ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 16, 2023

MAMA KOKA ATEMA CHECHE MAADHIMISHO YA MTOTO WA AFRIKA

 


Na Victor Masangu,Kibaha 


Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Selina Koka amehimiza wazazi na walezi kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri ya kuwalinda na kuwatunza watoto wao ikiwa sambamba na kuwapatia haki zao za msingi ikiwemo suala la  elimu.

Mama Koka ambaye pia ni mlezi wa jumuiya ya umoja wa wanawake Wilaya ya Kibaha mjini (UWT) ameyasema hayo leo ikiwa ni katika kilele Cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika duniani


Alisema kwamba jamii yote kwa kushirikiana na wazazi wanapaswa kubadilika kupitia siku hii na kuona umuhimu mkubwa wa kuwapa fursa sawa pamoja na ulinzi ili waweze kuishi katika mazingira mazuri.


"Siku hii ya maadhimisho ya mtoto wa afrika pia inatukumbusha sisi kama wazazi,na walezi kuwatupia macho zaidi watoto wetu katika kuwapatia fursa mbali mbali watoto wetu ikiwemo suala la fursa ya elimu pamoja na nahitaji muhimu ambayo yatawafanya watoto wapate furaha,"alisema Selina Koka.

Aidha aliongeza kuwa ana imani kwamba watoto pia wakilindwa na kupatiwa maadili mazuri yataweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuwa na heshima katika jamii na kuweza kutimiza malengo na ndoto zao waliojiwekea.


Katika hatua nyingine aliahidi kuweka mikakati madhubuti kwa kushirikiana na jumuiya ya umoja wa wanawake Wilaya ya Kibaha mjini katika kuwasaidia kwa hali na mali watoto yatima pamoja na wale ambao wanaishi katika mazingira rafiki kwa kuwasaidia mahitaji yao mbali mbali.


" Mimi nitaendelea kushirikiana bega kwa bega na wazazi pamoja na walezi katika kuwalinda na kuwatunza watoto wetu na  kitu kikubwa zaidi ninkuwapatia malezi bora na kuachanyana kabisa na na tabia ya kuwatumikisha kazi ngumu n vitendo vya ukatili hii sio nzuri hata kidogo kikubwa wote tushikamane,"alisema Selina Koka.

 Maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika ufanyika kila mwaka ifikapo Juni 16 ambapo kwa mwaka huu katika ngazi ya Mkoa wa Pwani yamefanyika katika Wilaya ya Kibiti na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali.

MWANAMKE AMKIRI BABAKE NI MZAZI HALISI WA WATOTO WAKE 3 WALA SI MUMEWE.


Mwanamke mmoja kutoka Ghana amesimulia hadithi yake tata ya mapenzi katika barua ambayo haikutajwa jina lake kwa kipindi maarufu cha uhusiano cha Citi FM/Citi cha Sister Sister.

Kulingana na mwanamke huyo kutoka Ghana, ameolewa na mume wake kwa miaka mingi na walijaliwa watoto watatu warembo lakini ukweli ni kwamba, hakuna mtoto ambaye ni wa mwanamume huyo. "Babangu huwa ananipeleka likizo, lakini mume wangu huwa halalamiki kwa sababu haoni ubaya. Nina umri wa miaka 35 sasa, nina watoto watatu warembo, na wote ni wa babangu, lakini hakuna mtu aliyewahi kushuku kwa sababu ninamfanana," alisema katika barua hiyo.

Mwanamke huyo alisema amekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na baba yake kwa miongo kadhaa, lakini sasa anaanza kuhisi vibaya.

 

Hadithi yake iliwashtua wengi mitandaoni na baadhi walikuwa na haya ya kusema:

 Ama Marfo alisema: "Baba yako? Watoto watatu! Wote wawili mko kwake kweli mna pepo. Mnamhitaji Yesu. Tafadhali mwache mume wako asiye na hatia nje ya laana hii."

Jackie Alex  alisema: "Siamini nilichokisoma!"

Akua Twumwah alitoa maoni yake: "Omba talaka. Inakuwaje nyinyi wawili mnafanya hivyo, si hii wanaiita dhambi au tuitaje?"

 Agnes Sarkodee-Adoo Tekyi alisema: "Tamaa ni kubwa na mahusiano haya ya kifamilia yanazidi kuendelea. Ungepaswa kuacha hili tangu mwanzo. Mungu aturehemu jamani."

 Racheal Muliwa alisema: "Maajabu haya! Babako wa kukuzaa, na wewe bado uko katika ndoa!!! Kuzaa watoto na babako!!! Wewe umelaaniwa."

SUKUMA DANCE YANOGILE - SONGA MBELE

 NA ALBERT G. SENGO/MAGU

"Katikati ya tamasha la utamaduni la watu wa sukuma (Bulabo) nakutana na ngoma hii ya asili ambapo uchezaji wake na milio ya ala zake inanivutia na kunisisimua, sijui wewe? " #samiasuluhuhassan #bulabo #kisesa #mwanza

PICHA ZA MATUKIO NHIF ILIVYOSHIRIKI MAONYESHO YA BIASHARA NA UTALII YA 10 YA JIJINI TANGA

 

Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Macrina Clemence kulia akitoa elimu kwa mmoja wa wananchi waliofika kwenye Banda lao wakati wa maonyesho  ya 10 ya Biashara na Utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga Wananchi wakiwa kwenye Banda ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakipatiwa huduma mbalimbali wakati wa maonyesho hayoWananchi wakiendelea kupata huduma kwenye Banda ya NHIF


KUTANA NA MADEREVA NA MAKONDAKTA WILAYA YA MAGU WALIOJIKITA PIA KWENYE UFUGAJI WA KISASA.

 NA ALBERT G. SENGO/KISESA/MAGU/MWANZA

Kujishughulisha huku na ufugaji na uwekezaji kwenye kilimo kuna uhitaji mwingi wa muda wa kutosha na ufuatiliaji, hamuoni kwamba mtakapoanza kufanikiwa huko mbele ya safari kundi kubwa mtaachana na shughuli zenu za usafiri na usafirishaji hivyo kuondoa maana au uhalisia wa jina lenu yaani Umoja wa Madereva na Makondakta Wafugaji wilaya ya Magu? Pata majibu ..........

Thursday, June 15, 2023

MV MWANZA KUKUZA UCHUMI

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Rais Samia Suluhu Hassan amesema ameridhika na maendeleo ya ujenzi wa meli ya MV. Mwanza, ambayo itasaidia kukuza biashara mkoani Mwanza, mikoa jirani na nchi jirani. Meli hiyo yenye uwezo wa kubeba mizigo hadi tani 400 kwa mara moja, itasaidia kwenye usafirisaji wa mazao katika nchi za Maziwa Makuu na hivyo kukuza uchumi wa nchi hizo. Aidha, Rais ameahidi kurudi kuizindua MV. Mwanza itakapokamilika na kuwataka Watanzania kuendelea kutunza amani na utulivu, kwani ndio chachu kwenye biashara za Kimataifa na uwekezaji. MV Mwanza itakuwa na madaraja sita ambayo ni VIP itakayokuwa maalum kwa viongozo wa kitaifa ambapo watakuwa wanakaa watu wawili tu pamoja na viongozi wa kitaifa wa nchi jirani kama watapata kibali cha kusafiri na meli hiyo. Daraja la VIP ambalo litabeba watu mashuhuri sehemu hii itakuwa na watu wanne yaani vyumba vinne, daraja la kwanza litakalokuwa na watu 60, daraja la biashara litakalokuwa na watu 100 daraja la pili litakalokuwa na watu 200.

MAMA KOKA AJIPANGA KUINUA UCHUMI WA JUMUIA YA WAZAZI KIBAHA MJI.

 


Na Victor Masangu,Kibaha


Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Selina Koka ameahidi kushirikiana bega kwa bega na jumuiya ya wazazi kwa lengo la kuwawezesha kiuchumi katika nyanja mbali mbali ili kuleta chachu ya maendeleo.

Selina ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya jumuiya ya wazazi Mkoa wa Pwani amebainiisha kuwa lengo lake kubwa ni kuendelea kufanya kazi kwa pamoja katika ngazi zote lengo ikiwa ni kuiimarisha jumuiya hiyo.

Aliyasema hayo wakati wa mkutano wa kuhitimisha ziara ya jumuiya ya wazazi Wilaya ya Kibaha mjini ambapo ilifanyika katika kata ya kongowe na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa chama pamoja na jjumuiya zake.


"Napenda kusema kwamba nitaendelea kushirikiana na nyinyi katika suala zima la kuweka misingi imara ya jumuiya hii ya wazazi inasonga mbele zaidi katika suala zima la kiuchumi na mimi nitaendelea kushirikiana katika kila nyanna,"alisema Selina Koka.

Kadhalika aliwapongeza viongozi wa jumuiya hiyo ya wazazi Wilaya ya Kibaha mjini kwa kumaliza ziara katika kata zote 14 za Jimbo la Kibaha mjini ambayo imeweza kuleta tija zaidi katika kuimarisha jumuiya kuanzia ngazi za chini.

"Nimefarijika kujumuika na nyinyi katika siku ya leo na wana chama wa CCM hasa jumuiya hii ya wazazi na kwamba mheshimiwa Mbunge anawasalimu Sana kwani kwa sasa yupo katika vikao vya bunge lakini yupo pamoja nanyi katika kuleta maendeleo.


Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Kibaha mjini imehitimisha ziara yake katika kata ya kongowe ambapo imeweza  kutembelea kata zote 14 za Jimbo la Kibaha mjini kwa ajili ya kuzungumza na wanachama kuangalia uhai wa chama na kutoa shukrani kwa wanachama.

MAELEZO ZAIDI UJENZI WA HOTELI YENYE HADHI YA NYOTA 5 JIJINI MWANZA

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Jengo la Hoteli itakayokuwa na hadhi ya Nyota tano ambayo inaendelea kujengwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF Mkoani Mwanza sasa kuendelezwa, likitarajiwa kukamilika mnamo mwezi Juni mwakani 2024. Baada ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kufanya ukaguzi wake katika ziara yake ya terehe 14 juni 2023 jijini hapa, Masha John Mshomba ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF anafunguka zaidi kuhusiana na uendelezwaji huo wa ujenzi ikiwa ni pamoja na mikakati iliyowekwa.

Wednesday, June 14, 2023

RAIS SAMIA ASISITIZA KASI UJENZI DARAJA LA JPM KIGONGO BUSISI AONYA WADOKOZI VIFAA VYA UJENZI.

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan hii leo amekagua maendeleo ya Ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi km 3) ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 75. Mhe. Rais Samia amekagua Daraja hilo ambalo Ujenzi wake unatarajiwa kukamilika Februari, 2024. Naye mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Misungwi Michael Masanja Smart akasimulia jinsi ujenzi wa daraja hilo walivyokuwa wakilichukulia kama hadithi za 'Abunuasi' lakini imekuwa kinyume na hatimaye ndoto hiyo inakwenda kutimia kupitia Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. #samiasuluhuhassan #mwanza #kaziiendelee

Tuesday, June 13, 2023

MCHUNGAJI AICHAMBUA HOTUBA YA RAIS SAMIA ALIYOITOA BUJORA JIJINI MWANZA

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Mchungaji Dr. Jacob Mutashi wa kanisa la EAGT Kiloleli jijini #Mwanza. #samiasuluhuhassan

WAZIRI PROFESA MBARAWA AFUNGUA KIKAO KAZI KATI YA MENEJIMENTI YA WIZARA YA UJENZI NA TAASISI ZAKE JIJINI TANGA

 

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa  akkizungumza wakati akifungua  kikao kazi kati ya Menejimenti ya Wizara (Ujenzi) na Menejimenti za Taasisi zake kinachofanyika kwa siku tatu chenye kauli mbiu ya Kuimarisha ari na morali katika utendaji kazi kilichofanyika Jijini Tanga

Katibu Mkuu Sekta ya Ujenzi Mhandisi Aisha Amour  akizungumza wakati wa kikao kazi hicho

Sehemu ya washiriki wa kikao hicho

Sehemu ya washiriki wa kikao hicho



Na Oscar Assenga, Tanga

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amefungua kikao kazi kati ya Menejimenti ya Wizara (Ujenzi) na Menejimenti za Taasisi zake kinachofanyika kwa siku tatu chenye kauli mbiu ya Kuimarisha ari na morali katika utendaji kazi

Akizungumza wakati wa kikao hicho Waziri Mbarawa amesema uwekezaji ambao Serikali imeingia ubia na Kampuni ya DP ya Nchini Dubai ni jambo lenye maslahi mapana kwa nchi kwa sababu itachangia kuiwezesha Bandari ongezeko la bajeti kwa nchi kutoka asilimia 37 hadi kufikia asilimia 67 kutokana na kwamba itawezesha kuongeza ufanisi mkubwa katika bandari ya Daresalaam.

Waziri Mbarawa alisema mkakati wa Serikali ni kuifanya Bandari ya Dar salaam ifanye kazi kwa ufanisi na mkakati mojawapo ni kuwapelekea kwenye viwango vya kimataifa ili waweze kushirikiana na TPA ili kuweza kuboresha bandari zao.

Aidha alisema miongoni mwa watu ambao wana viwango vya kimataifa ili kuweza kushirikiana na TPA kuboresha bandari zao ni DP World kutokana na kwamba ni kampuni kubwa kati ya makampuni 10 duniani yanayofanya mambo hayo.

Alizitaja kampuni nyengine ni Singapore Ports Authority ,Harshon ya Honkong,DP Word ,MPM sasa ni makampuni hayo makubwa ndio yanafanya kazi hiyo ya kupelekea mizigo na kutoa mizigo na wakaamua kuchukua kampuni uya DP Word .

Alisema wameamua kuchukua kampuni hiyo baada ya kufanya uchambuzi wa kina kwa sababu wanasifa za kipekee ukilinganisha na wengine ya kwanza ni anafanya kazi kwenye bandari sita Afrika ikiwemo kufanya kazi na Bandari 30 ulimwenguni kote lakini wanameli zaidi ya 100 za kuchukulia mzigo duniani.

Aidha alisema kwamba kampuni ya DP Word wana uwezo wa meli nyengine za kuchukulia watalii,kuhamasisha mnyororo mzima wa mizigo toka unapotoka mpaka unafika kwa mteja wa mwisho ikiwemo uwezo wa kujenga bandari kavu maeneo mbalimbali.

“Lakini pia wana uwezo wa kujenga maeneo kwa ajili ya logistiki paki kwa mfano Rwanda wamejenga logistika paki kubwa maana ayke mzigo wa wqafanyabiashara wa Rwanda lazima upitie Dar es Salaam na DRC wana mpango wa kujenga logistic paki kubwa na wenyewe wataweza kuitumia vizuri kupata mzigo mkubwa utakaokwenda Kongo”Alisema

Hata hivyo alisema wakifanya maboresha hayo yataweza kuisaidia Bandari ya Dar kwenye makubaliano watakayoyafanya yamejigawa miradi ya sehemu mbili ambazo ni ya kwanza itaangalia Bandari Dar es Saalaam itaangalia gati namba 1 mpaka 7 wataenda kuangalia gati ya majahazi pamoja na abiria na wataangalia maeneo mawili ya kwanza ni operesheni.

Waziri alisema kwa sababu shida moja ya bandari ya Dar ni wamewekeza karibia trilioni 1 kutoka Gati namba moja mpaka 7 lakini bado utendaji wa kazi hauridhishi kwa sababu hakuna vifaa vya kisasa,miundombinu ikiwemo vifaa vya Tehama vya kisasa sio vizuri.

Hata hivyo alisema kwamba hata utendaji wenyewe wanafanya kazi kwa mazoea hivyo wakimpata DP wanaamini wataona mabadiliko makubwa kwenye Bandari ya Dar hivyo wanawatoa hofu watanzania.

Awali akizungumzia kuhusu kikao hicho alisema kwamba kitachochea utendaji kazi kwa uwazi ikiwemo pamoja na kubuni za kiutendaji zinazolenga kuweka mazingira yenye kuchochea morali kwa watumishi wanaowasimamia.

“Hivyo ni mategemeo yangu kwamba mtakuwa huru katika ,kujadiliana masuala ya kiutendaji kwqa uwazi lengo likiwa kupata mwelekeo mmoja utakaohakikisha wizara na taasisi zake zinatimiza malengo yake vizuri”Alisema

Hata hivyo aliwataka washiriki wa kikao hicho kuhakikisha wanatoa mitazamo yao mbalimbali na wasipofanya hivyo maana ya mkutano huo itakuwa haipo.

Awali akizungumza katika kikao hicho Katibu Mkuu Sekta ya Ujenzi Mhandisi Aisha Amour alisema pamoja na mengine kitakuwa na fursa ya kipekee watendaji kujipanga na kuweka mipango ya kutekeleza malengo waliojiwekea

Alisema sekta ya ujenzi imeendelea kutekeleza majukumu yake katika kuchangia maendeleo ya Taifa kwa kuzingatia viwango vya ubora vya ujenzi na ukaribati wa barabara ,madaraja na nyumba za serikali pamoja na vivuko,ujenzi na upanuzi wa viwanja vya ndege na matengezo ya magari ya serikali.

Katika kutekeleza majukumu hayo leo tumekutana hapa kwa lengo la kuweka mipango na kutafakari nini kifanye ili kuweza kuongeza kasi ya utrekelezajoi wa majukumu yao .

Mwishoi.

Monday, June 12, 2023

"TANZANIA NI MOJA HAIUZIKI WALA HAIGAWANYIKI MIMI NI MTANZANIA" KAULI YA KWANZA YA RAIS SAMIA AKITUA JIJINI MWANZA

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi ya siku nne huku akisisitiza umoja katika ujenzi wa Taifa. Akisalimia na umati wa wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kumpokea eneo la uwanja wa Ndege (Air Port Mwanza) katika siku ya kwanza ya ziara hiyo, Mkuu huyo wa nchi amesema Tanzania ni nchi moja isiyogawanyika na kuwataka Watanzania kila mmoja kwa eneo lake kutimiza wajibu wa kujenga uchumi wa nchi, kisha akatia msisitizo kwa kusema "TANZANIA NI MOJA HAIUZIKI WALA HAIGAWANYIKI MIMI NI MTANZANIA"

Sunday, June 11, 2023

TAMKO LA MKUU WA MKOA WA MWANZA ZIARA YA RAIS SAMIA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA KIMKAKATI.

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwasili Mkoani Mwanza Jumatatu juni 12 Mwaka huu kwaajili ya uzinduzi wa Tamasha la BULABO ambalo limeandaliwa na kituo cha utamaduni cha Bujora pamoja na watemi Mkoani hapa kisha ratiba rasmi itafuata.