Saturday, March 19, 2011
BANGO
Saturday, March 19, 2011
HABARI
'HahaaaaaAAAAAaaaa'
Ni time ya kuGONga cHiAZ MarA bAAda ya kUTOKa sAfARi kUPoKeA kikombe cHa bABu
USiuliZE nI wAPi 'STONE CLUB' tHe oNE aND oNLY.
Ukiwa Isamilo Lodge Mwanza na ukathubutu kuzama shimo la ladha chumba cha ngoma za raha makulaji na vinywaji utasikia--.. pRAkAtA tUMBa-tUMBa-TuMBA-tUMBa-tUMBa'''''''@@@@@##** !!!!!!!!!!!!!HuU ndO mPaNGo.
Frederick Katulanda ameandika...
Serikali ilieleza kuwa itashusha bei ya nishati Gass ili wanzania wote wamudu kuitumia na kuepukana na utumiaji wa mkaa kupunguza uharibifu wa mazingira. Je, ahadi hiyo imetekelezwa, na kama ni kweli ni watanzania wangapia wameacha kutumia mkaa na sasa wanatumia Gass?
Kuna taarifa zisizothibitishwa kwamba waziri wa ujenzi John Magufuli amejiuzulu wadhifa huo. Taarifa za kuaminika toka serikalini zimepasha kuwa waziri huyo amemuandikia barua Rais Jakaya Kikwete, akimtaarifu uamuzi wake wa kujiuzulu baada ya kufadhaishwa na hatua ya Waziri huyo, Mizengo Pinda kumuingilia katika utekelezaji wa majukumu ya wizara yake.
Vyanzo vimefafanua kuwa uamuzi huo umesababishwa zaidi na matukio ya hivi karibuni ya Pinda kukosoa hadharani kazi ya bomoa bomoa kwenye hifadhi ya barabara lililokuwa likitekelezwa na waziri huyo na kuagiza lisitishwe hadi hapo itakapo amuliwa vinginevyo na Baraza la Mawaziri.
JE NI KWELI?
Thursday, March 17, 2011
HABARI
Nchi zilizo wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimetakiwa kuendeleza ushirikiano kwa ajili ya kubambana na janga la maambukizi ya ugonjwa unaosababisha virusi vya ukimwi na baadaye kupata ufumbuzi wa tatizo hilo ambalo limeteketeza nguvu kazi miongoni mwa jamii ya nchi hizo. Hayo yalisemwa na Dk. Fatuma Mrisho, ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Kuthibiti Ukimwi nchini Tanzania, wakati akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa siku tatu wa wadau walio katika mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi kutoka nchi zilizo katika jumuiya hiyo ambazo ni Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi ambao uliofanyika katika hoteli ya Nyumbani jijini Mwanza.
Amesema kuwa mikakati iliyopo kwa sasa ya kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi, ni nchi zilizo katika jumuiya hiyo kuendeleza mipango ya kutokomeza tatizo hilo kwa ushirikiano wa karibu kwa nchi zilizo mwanachama ambazo ni Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi kwa kutoa semina, kongamano na mbinu zingine ambazo zitaweza kuwaelimisha wananchi ili kubadirisha tabia zao ambazo zinaleteleza maambukizo ya ugonjwa huo.
Dk. Mrisho amesema kuwa maambukizo mengi katika miongoni mwa wananchi walio katika Jumuiya hiyo yanatokana na ngono zembe miongoni mwa jamii, madereva wa magari makubwa yanayosafirisha bidhaa baina ya nchi hizo, wafanyakazi katika mabaa na sehemu zingine za starehe pamoja na maeneo yenye mlundikano wa watu wengi ambao huleteleza muingiliano usio rasmi.
Ameongeza kuwa endapo nchi zilizo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki zitafanya kazi kwa pamoja katika kutokomeza janga hilo, hadi kufikia mwishoni mwaka 2012, ugonjwa huo utakuwa umetokomezwa kabisa au kupungua kwa kiasi fulani iwapo jamii katika nchi husika itajikita katika kuthibiti maambukizo hayo.
Hata hivyo, Dk. Mrisho amesema kuwa nchi zilizo katika jumuiya hiyo kwa kupitia taasisi zilizo katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo zitakutana mara kwa mara ili kubadirishana uzoefu wao, itakuwa ni rahisi kutambua matatizo yaliyo katika nchi husika na kuweza kushirikiana katika kuyatatua ili kuweza kuwa na malengo ya pamoja katika kubambana na ugonjwa huo.
Mkutano huo ambao umeanza Machi 16 utahitimishwa kesho Machi, 18 ambapo kwa mujibu wa Dk. Mrisho ambaye ni mwenyeji katika mkutano huo, wajumbe wataweza kutoa maamuzi ya jumla ambayo yatalenga kutokomeza maambukizi ya ugonjwa huo.
Thursday, March 17, 2011
ARUSHA
Madereva wa pikipiki nchini Pakistan ni mafundi kwelikweli linapokuja suala la kusaidia mteja kuminimaizi cost za maisha, Hebu cheki na picha hii iliyopigwa katika barabara kuu nchini humo.
Mbona patatosha tuu...!
side a.
side b
Wednesday, March 16, 2011
HABARI
Waziri wa Maji,Prof. Mark Mwandosya (kulia) pamoja na Mkuu wa Jumuia ya Ulaya Nchini Balozi,Tom Clarke (pili kushoto) wakimsikiliza kwa makini mwandisi mshauri wa maradi wa maji taka katika eneo la Butuja alipokuwa akitoa maelezo ya mradi huo leo jijini Mwanza.
Waziri Wa Maji Mh. Mark Mwandosya leo amefungua wiki ya Maji mjini hapa kwa kuzindua mradi mkubwa wa Maji taka katika eneo la Butuja Wilayani Ilemela Mwanza.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mradi huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mwanza (MWAUASA) Bw. Mashaka Sitta alisema kuwa mradi huo utakaogharimu karibu Billioni 29 ulibuniwa mwaka 2002 na kuanza kutekelezwa tangu mwaka 2009.Alieleza kuwa miradi itakayojumuisha katika mradi huo ni pamoja na ujenzi wa bomba kubwa la kipenyo cha mm 700 kwa umbali wa mita 140,ujenzi wa mabwawa mapya matatu, ukarabati wa mabwawa kumi ya zamani, ujenzi wa matanki mapya ya kuhifadhia Maji taka pamoja na ununuzi wa vifaa vya maabara.
‘’ Tunatarajia kuwa kukamilika kwa mradi huu itatuwezesha kujenga pia mtandao wa Maji taka kwa kilomota 24, kujenga mashimo ya maji taka (manhole chambers) zipatazo 880 itakayounganisha karibu nyumba 5000 kwenye mtandao wa majitaka’’ alisema Mkurugenzi huyo.
Akizungumza baada ya uzinduzi huo, Mh Waziri alisisitiza umuhimu wa kutunza miradi hii kwani Wafadhili wanatumia fedha nyingi kugharamia miradi hii. ‘’Nisingependa baada ya ufunguzi huu wa leo, tuwaombe tena Wafadhili kutukarabatia miundominu yetu nitashukuru kama kutakuwa na kazi ya mamna hii katika Nchi moja ya jirani basi kazi hiyo ifanywe na MWAUSA’’ alisisitiza Mwandosya.
Pamoja na uzinduzi huo Mh.Waziri alipokea pia magari 4 ya kubebea maji taka yatakayotumika na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka jiji Mwanza.Sherehe ya UzinduzI wa mradi huu mkubwa maji taka ulihudhuriwa pia na Mwakilishi mkuu wa Jumiya ya Ulaya hapa Tanzania Balozi Tom Clarke, Balozi Mdojo wa Ujerumani hapa Nchini pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya maendeleo ya Ujerumaini (KWF) Dr Wolfgang.
Maadhimisho ya wiki ya Maji yanafanyika katika viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza na yatafikia kilele chake tarehe 22 Machi kwa kufungwa rasmi na Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Gharib Bilal.
Wednesday, March 16, 2011
huzuni
Tuesday, March 15, 2011
ARUSHA
Tuesday, March 15, 2011
HABARI