ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 24, 2023

KITANDULA ATOA MSAADA WA VYAKULA NA FEDHA KWA WALIOKUMBWA NA MAFURIKO JIMBONI KWAKE

 

 





Na Oscar Assenga, MKINGA.

MBUNGE wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula ametoa msaada wa Vyakula na Fedha kwa Kaya 36 zilizopo kwenye Kata ya Manza na Mtimbwani wananchi katika Kijiji cha Msimbazi ambao walikumbwa na kadhia ya mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali hapa nchini

Kitandula ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii aliamua kutoa msaada huo wakati akiwa kwenye ziara ya Jimbo hilo ili kuhakikisha wananchi hao wanaaondokana na changamoto ambazo wamekumbana nazo kutokana na uwepo wa mafuriko hayo

Akizungumza wakati akiwa kwenye ziara hiyo pamoja alipokwenda kushuhudia zoezi la ukoaji wa wananachi katika Kijiji cha Msimbazi Kata ya Manza kutokana na mvua kubwa zinazoendelea katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Kitandula aliwaeleza wananchi hapo kwamba yupo pamoja nao na kuhaidia kuendelea kuwasaidia kuhakikisha wanaondokana na changamoto mbalimbali ili kuweza kujikwamua kiuchumi

Katika hatua nyengine Mbunge Kitandula alitoa msaada wa Pikipiki kwa kikundi cha wafugaji kwa ajili ya kukusanya maziwa kutoka kwa wafugaji wadogo wilayani humo.

Baada ya kuwakabidhi Pikipiki hiyo alimshukuru Mkuu wa wilaya hiyo Kanali Maulid Surumbu kwa kumshirikisha kwenye jambo hili ni kazi kubwa na nzuri ambazo zimekuwa zikifanywa kwa ajili ya kuwakwamua kiuchumi wafugaji hao

“Nimeona niwaunge mkono kwa kuwapatia pikipiki hii naamini utakuwa chachu kwenu lakini pia niwaambie kwamba tupo pamoja na tutaendelea kushirikiana “Alisema

Awali akizungumza mmoja wa wanakikundi hao Abdala Mwajasi alimshukuru Mbunge huyo kwa msaada aliowasaidia huku akieleza mbunge huyo ni mahiri sana kuwasaidia wananchi hasa wanapokuwa wamekumbana na changamoto mbalimbali.

“Tunakushuru Mhe Mbunge Wetu kwa kutusaidia jambo hilo la umuhimu mkubwa kwa sababu sisi tauna uwezo wa kununua pikipiki “Alisema

Wednesday, November 22, 2023

HOTUBA YA MHE. DOTO BITEKO NAIBU WAZIRI MKUU MBELE YA MAKARDINALI NA MAASKOFU - JIMBO KUU TABORA

NA ALBERT GSENGO Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Serikali itaendelea kulinda uhuru wa wananchi wa kutoa mawazo, imani na uchaguzi katika dini na hivyo itahakikisha kuwa kunakuwa amani na utulivu ili uhuru huo wa kuabudu na kutoa mawazo uwepo. Dkt.Biteko amesema hayo tarehe 19 Novemba, 2023 wakati alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Sherehe za kumpongeza Mhasham Askofu Mkuu Mstaafu Paul Ruzoka na kumpokea rasmi Askofu Mkuu Mpya wa Tabora, Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa. Sherehe zilizofanyika katika Jimbo Kuu Kanisa Katoliki Tabora.

MKUTANO WA MWAKA WADAU WA VIHATARISHI WAFANYIKA MWANZA

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya usimamizi wa vihatarishi Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta binafsi na umma jijini Mwanza kwa lengo la kutoa elimu na kuwajengea uwezo watendaji wa sekta mbalimbali nchini.

DKT. BITEKO AIAGIZA TPDC KUANDAA MPANGO WA MUDA MREFU WA UPATIKANAJI GESI NCHINI


📌Aitaka pia kukagua ushuru wa huduma unaotolewa kwa Halmashauri

Dodoma

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameagiza Bodi na Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuja na mpango wa muda mrefu utakaoonesha jinsi nchi itakavyoweza kuongeza kiasi cha gesi asilia ili muda wote kuwe na hazina ya kutosha ya nishati hiyo inayotumika kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kuzalisha umeme, viwandani, majumbani na katika magari.


Dkt. Biteko ameyasema hayo tarehe 21 Novemba, 2023 wakati wa kikao chake na Bodi na Menejimenti ya TPDC ambacho kililenga kufahamiana, kubadilishana mawazo juu ya utendaji kazi na Mhe. Dkt. Doto Biteko kuelekeza matarajio ambayo nchi inayahitaji kutoka TPDC.


“TPDC tujiulize, Je uwezo wetu wa kuzalisha Gesi Asilia unaweza kujibu mahitaji yetu  ya Gesi ? tujiulize hili na tuchukue hatua. Tutambue kuwa mahitaji ya Gesi Asilia ni makubwa kwa sasa kwani dunia inahama kutoka matumizi ya mafuta na kwenda kwenye Gesi Asilia hivyo lazima tujipange, na pia tukumbuke tumesaini makubaliano ya kusafirisha nishati hii kwenda Uganda, Zambia na Kenya hivyo lazima tuwe na Gesi ya kutosha.” Amesisitiza Dkt. Biteko.


Dkt. Biteko pia amewataka TPDC kutokuwa na urasimu katika uchukuaji wa maamuzi mbalimbali ikiwemo kwenye shughuli za utafiti wa Mafuta na Gesi Asilia ili kutorudisha nyuma sekta hiyo nchini.


Kuhusu maelekezo aliyoyatoa wakati wa ziara yake, katika Kisiwa cha Songosongo mkoani Lindi na Kijiji cha Madimba na Msimbati mkoani Mtwara, Dkt. Biteko amesisitiza kuwa, maisha ya wananchi katika maeneo hayo ambayo kuna visima na mitambo ya Gesi Asilia lazima yabadilike na wapewe huduma bora ikiwemo maji, umeme, afya na usafiri.


“Nashukuru mmeanza kufanyia kazi maagizo niliyoyatoa kwa haraka, ikiwemo ya kuweka taa za barabarani Kijiji cha Msimbati, kupeleka umeme wa uhakika Madimba na Msimbati unaotoka kwenye mitambo ya Gesi Asilia, kupeleka kivuko kisiwa cha Songosongo na malipo ya mafao kwa wastaafu wa Knight Support ambao walikuwa wakilinda mitambo na visima vya Gesi Asilia Songosongo ambao hawakulipwa muda mrefu, watu hawa wanahitaji huduma bora.”


Amesema Dkt. Biteko

Katika Hatua nyingine, Dkt. Biteko ameiagiza TPDC kupita kwenye Halmashauri zote nchini zinazopokea ushuru wa huduma kutokana na shughuli za Mafuta na Gesi Asilia kufanyika kwenye Halmashauri hizo ili TDPC ijihakikishie kwamba, fedha hizo zinaenda pia kwenye vijiji/maeneo ambayo shughuli za uzalishaji wa Gesi Asilia zinafanyika.


Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mussa Makame alimweleza Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati kuwa, TPDC inaandaa Mpango Mkakati wa Shirika (Corporate Strategic Plan) ambao utaweka mikakati ya Shirika kwa kipindi cha miaka 10 na zaidi ili kuwezesha upatikanaji wa Gesi Asilia ya kutosha kwa matumizi ya ndani na kuwekeza zaidi katika mnyororo wa thamani wa Mafuta na Gesi ili kukuza matumizi ya Gesi Asilia na hivyo kuchochea biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki.


Aidha, alieleza mipango ya utekelezaji wa mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda kuja Tanzania, Mradi wa Gesi ya Kusindika (LNG) ambapo majadiliano yamekamilika na mikataba ipo kwenye hatua za kuidhinishwa, utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia katika Kisiwa cha Songosongo Magharibi unaotarajiwa kuanza Septemba 2025 na utafutaji mafuta kitalu cha Eyasi Wembere ambapo tafiti zinaendelea. 

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC, Balozi Ombeni Sefue amemshukuru Naibu Waziri Mkuu kwa maelekezo yake ambayo yamewapa hamasa ya kufanya kazi na wameahidi kwamba wataenda mbali kiutendaji na watatoa ushirikiano kwa Naibu Waziri Mkuu ili kusukuma mbali zaidi Sekta ya Mafuta na Gesi Asilia nchini.

JEH TUCHANGIE HARUSI AU TUSICHANGIE?

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Askofu Robert Bundala wa kanisa la TGC ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Mkoa wa Mwanza anajibu.

Tuesday, November 21, 2023

AGIZO LA WAZIRI PROF.MKUMBO LIFANYIWE KAZI IPASAVYO NA MAMLAKA ZINAZOHUSIKA

 

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb,)wakati alipozindua kitabu cha mwongozo wa uwekezaji Mkoani Tanga wenye kauli mbiu Wekeza Tanga kwa Uwekezaji Endelevu.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula akizungumza wakati wa kongamano hilo

MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhamani akizungumza wakati wa Kongamano hilo

Na Oscar Assenga,TANGA

NI Ukweli usiopingika kwamba kumekuwa na urasimu usio wa lazima katika mchakato wa uwekezaji ambao wakati mwengine unatajwa kwamba ndio chanzo cha kuwakatisha tamaa wenye nia ya kufanya hivyo.

Jambo hilo limekuwa likipelekea kukwamisha watu wenye nia ya dhati ya kuwekeza na hilo kubwa linatokana na urasimu ambao unadaiwa kufanywa na mamlaka zinazohusika kwenye mchakato huo.

Kwa kuliona hilo kwamba jambo hilo ni changamoto kubwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb,) analitoa kauli wakati alipozindua kitabu cha mwongozo wa uwekezaji Mkoani Tanga wenye kauli mbiu Wekeza Tanga kwa Uwekezaji Endelevu.

Prof.Mkumbo anakemea vikali urasimu unaofanywa na Mamlaka zinazohusika na Uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi na kusababisha Serikali kukosa mapato yake ya msingi

Katika Taarifa hiyo Prof.Mkumbo anawaagiza viongozi wa Serikali ngazi za mikoa kuhakikisha wanaondoa changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wa kutoka ndani na nje yaa nchi ambao wakiwekeza wanalipa kodi na kukuza uchumi.

Katika hatua nyengine anazitaka mamlaka zote zinazohusika kwenye mchakato wa uwekezaji ziondoe urasimu usio wa lazima kiasi cha kuwakatisha tamaa wawekezaji.

Anaeleza kuwa kongamano hilo linaashiria dhamira ya dhati ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kukuza uchumi nchini hivyo uzinduzi huu ni hatua muhimu katika safari ya kujenga taifa linalovutia wawekezaji kutoka pande zote duniani kuja kushirikiana na Mikoa yote nchini.

Prof. Mkumbo anasema kuwa mfumo imara wa mazingira wezeshi ya uwekezaji ndio uti wa mgongo wa Taifa lolote linalojinasibu katika kufufua na kuimarisha uwekezaji wenye ustawi.

“Katika kutengeneza fursa za ajira, kuimarisha miundombinu na kuinua ubora wa maisha kwa wananchi wake lakini pia Mamlaka za Serikali za Mitaa zitenge maeneo mahususi na kuyahodhi kwa ajili ya uwekezaji “Anasema

Anasema pia wahakikisha wanayaweka miundombinu yote muhimu na kuandaa mkakati wa mawasiliano ili kuongeza kasi ya kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo na mipango yote ya uwekezaji izingatie dhamira ya Serikali ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira.

Awali akizungumza katika Kongamano hilo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Waziri Kindamba anasema kuwa lengo la uzinduzi wa muongozo wa uwekezaji ni kufungua fursa za kilimo, uchumi wa bahari, viwanda, utalii, usafiri, afya, elimu, huduma za fedha, uendelezwaji wa miji na uboreshaji wa maeneo ya michezo.

Kindamba ameongeza kuwa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (East African Crude Oil Pipeline) wenye thamani ya dola za kimarekani 3.5 bilioni ni ishara tosha ya dhamira ya Serikali yetu katika kuhakikisha nchi yetu inafanya uwekezaji mkubwa na wenye tija kwa Taifa na wananchi wa kizazi cha sasa na cha baadae.

Anasema kuwa uwekezaji uliofanywa katika kuboresha Bandari ya Tanga uligharimu kiasi cha shilingi za kitanzania bilioni 429.1 ambapo kazi zilizofanyika zilikuwa ni kupanua gati na kuongeza kina na hivyo kuongeza uwezo na ufanisi wa Bandari hiyo.

Aliongeza ili kuhakikisha kwamba inaweza kukidhi ongezeko la shughuli inayoendelea ya ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki na shughuli nyingine za kibiashara, kiusafirishaji na kiuwekezaji. Bomba la mafuta linaloanzia Hoima nchini Uganda hadi chongoleani Tanga

Kongamano hilo limehudhuriwa na Waheshimiwa Mabalozi kutoka Rwanda, Burundi, Uganda na wengine kushiriki kwa njia ya mtandao, Naibu waziri Wizara ya Maliasiri na Utalii Mhe. Danstan Kitandula (Mb), Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge, Mheshimiwa Nurdin Babu, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na wakuu wa Wilaya, wabunge, makatibu tawala na wakurugenzi wa halmashauri.

Ndio maana tunasema kwamba kauli ya Prof.Mkumbo ifanyiwe kazi ipasavyo na mamlaka husika ili iweze kuleta tija kwa wawekezaji ambao wanakuja kuwekeza hapa nchini na wale wazawa na isipuuzwe.

DKT MAHERA ATOA AGIZO KWA VYUO VYA AFYA NCHINI

 

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi anayeshughulikia Afya Dkt Wilson Mahera akizungumza wakati akifungua mkutano wa madaktari wa kinywa na meno leo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Kinywa na Meno kutoka Wizara ya Dkt Baraka Nzobo wa pili kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo akizungumza wakati wa mkutano huo
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Kinywa na Meno kutoka Wizara ya Dkt Baraka Nzobo akizungumza wakati wa mkutano huo
Sehemu ya Washiriki wa kikao hicho 
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia matukio mbalimnbali
Sehemu ya Madaktari wa Kinywa na Meno kutoka maeneo mbalimbali nchini wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi Dkt Wilson Mahera ambaye hayupo pichani wakati alipofungua mkutano wa madaktari wa Kinywa na Meno.
Wakiwa kwenye picha ya pamoja 


Na Oscar Assenga, TANGA

NAIBU Katibu Mkuu Tamisemi Afya Dkt Wilson Mahera ameviagiza Vyuo vya Afya ambavyo havina kozi ya Shahada ya Udaktari wa Kinywa na Meno kuianzisha ili kusaidia kuongeza upatikanaji wa watalaamu wengi zaidi hapa nchini.

Dkt Mahera aliyasema hayo leo Jijini Tanga wakati akifungua Mkutano wa Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania Kitaifa unaofanyika mkoani hapa ambapo alisema kwamba atafikisha ujumbe huo kwa wakuu wa vyuo hivyo hapa nchini.

Alisema kwamba kufanya hivyo kutawezesha kusaidia upatikanaji wataalamu wengi ambao watasaidia katika utoaji huduma kwa wananchi ambao wanakumbana na changamoto mbalimbali za afya ya kinywa na meno hapa nchini.

“Kupitia mkutano huu niagize vyuo vya Afya nchini ambavyo havina kozi ya Shahada ya Udaktari wa Kinywa na Meno kuanzisha ili kusaidia kuongeza upatikanaji wa watalaamu hao hapa nchini”Alisema Dkt Mahera.

Katika mwaka 2022 kitaifa kulikuwa na wagonjwa wa kinywa 747,858 waliooza meno 522,777 sawa na asilimia 68.9 ya wagonjwa wote wa kinywa na meno na waliokuwa na matatizo ya fizi ni 78,755.

Alisem kwa takwimu hizo tatizo la kuoza kwa meno bado ni kubwa hapa nchini bado na wana kazi kubwa ya kufanya wagonjwa 156,576 sawa na asilimia 30 walioza meno yalizibwa na wagonjwa 265,249 sawa 49.6 na asilimia walioza meno yaliny’olewa.

“Tatizo la meno yakikubana mtu ukiamka asubuhi yanang’olewa niwatake wataalamu mjikite zaidi kutibu na sio kuyang’oa kwa maana Serikali imewekeza miundombinu yote wezeshi kuhakikisha wananchi wanapatiwa tiba ya meno na sio kungoa jino”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba kuna maeneo ya huduma za kinywa na meno hazipatikani lakini bado wananchi wanatembelea umbali mrefu kufuata huduma hya afya ya kinywa na meno hii sio sawa.

Aidha aliagiza na kuwaelekeza waganga wakuu wa mikoa na Halmashauri kuhakikisha vituo vya afya vya kimkakati na visivyo vya kimkakati kuhakikisha vinaaza kutoa huduma ya matibabu ya kinywa na meno ili kuepusha wananchi kutembelea umbali mrefu.

Hata hivyo aliwataka pia kuhakikisha wanakuwa na vifaa stahiki ikiwemo viti vya kutolea huduma na vifaa vya kisasa zikiwemo mashine za kifanyia uchunguzi wa afya ya kinywa na meno kulingana na miongozo inayotolewa na Wizara ya Afya.

Awali akizungumza wakati akitoa salamu katika mkutano huo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo alisema kwamba mkoa huo upo salama aliwataka wajumbe kuhakikisha wanakuwa makini vitu ambavyo vitawasilishwa kwenye mkutano huo.

Naye kwa Upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Kinywa na Meno kutoka Wizara ya Dkt Baraka Nzobo alisema kikao hicho cha Kinywa na meno kwa madaktari kitasaidia kuleta mapinduzi makubwa kwenye sekta hiyo.

Alisema tokea wameanza vikao hivyo kila mwaka wameweza kufanya huku akielezea sekta ya kinywa na meno imebebwa sana na ofisi ya Rais Tamisemi kwa sababu Hospitali za wilaya,vituo vya afya,Hospitali Rufaa Kanda na Taifa ni chache.

Alisema kwamba wizara ya afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tamisemi wamekuwa wakiratibu vikao hivyo na kuna baadhi yao hawatilii mkazo vikao vya maamuzi kwa sababau leo upo nikuombe kuna watu wanaandikiwa barua hawafikia .

“Nikuombe ikikupendeza uwachukulie hatua kwani maendeleo hayawezi kupatikana kama watu wana puuzia vikao vya msingi vya kisekta ambavyo vinaleta mabadiliko katika kutoa huduma bora ya kinywa na meno ofisi hii iliandikia Halmashauri 36 kuleta wataalamu ngazi ya Halmashauri lakini mpaka leo wamefika 17 tunaomba ofisi yao ituulizie kwa wakurugenzi hao 18 kwanini hawajafika mahali hapa wamekaidi”Alisema .

Sunday, November 19, 2023

DKT MAHERA WATAKAOBAINIKA WAMEFANYA UZEMBE HANDENI TUTAWACHUKULIA HATUA

 

Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt Wilson Mahera  akizungumza na waandishi wa habari  mara baada ya kutembelea na kukagua Hospitali ya wilaya ya Muheza
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt Wilson Mahera  akitembelea maeneo mbalimbali katika Hospitali ya wilaya ya Muheza kushoto ni Mganga Mkuu  wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo 
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt Wilson Mahera  akikagua hali ya upatikanaji wa dawa wakati alipotembelea Hospitali ya wilaya ya Muheza
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt Wilson Mahera  akikagua hali ya upatikanaji wa dawa katika Hospitali ya wilaya ya Muheza

Na Oscar Assenga Muheza

Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt Wilson Mahera amefanya ziara ya kutembelea na kukagua hospitali ya wilaya ya Muheza huku kieleza kwamba kwa wale watakaobainika walifanya uzembe wilayani Handeni watachukuliwa hatua kali ikiwemo kuwanyang’anya leseni.

Dkt Mahera aliyasema hayo mara baada ya ziara hiyo ambapo alisema kwamba Serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya afya ili wananchi wapate huduma bora hivyo wao hawatakubali kuona watumishi wanakiuka maadili.

Alisema hivyo lazima watumishi wabadilike waache kufanya kazi kwa mazoea na vitendo hivyo visijirudie kwani kufanya hivyo kunapelekea kuzorotesha huduma hivyo niwasihi muendelee kutoa huduma nzuri na kufanya kazi kwa waledi katika kuwahudumia wananchi.

Dkt Mahera alisema yupo mkoani Tanga kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa madaktari wa meno hivyo akaona apite katika Hospitali hiyo kuangalia huduma za afya kutokana na kwamba Serikali ya imewekeza fedha nyingi kuwekeza kwenye sekta ya afya ikiwemo miundombinu.

“Kwa kweli niwapongeze mnaosimamia mradi huu wa Hospitali ya wilaya ya Muheza changamoto niliyoiona hapa ni maji Hospitali ya wilaya kama hii inapata maji kutoka Tang tumekagua maabara maji hakuna bahati nzurti mmechimba kisima na halmashauri imenunua pamp niagize mkamilisha haraka miuondombinu ya maji iweze kuingia kwenye maabara”Alisema Dkt Mahera

“Lakini pia watumishi fanyeni kazi kwa waledi na kujituma na kuendelea kuhakikisha watoto njiti pale wanapojitokeza waendele kuboresha huduma hizo kwenye maeneo yenu kama nchi tumepata mafanikio makubwa sana kuzuia vifo vinavyotokana na mama na mtoto.

Hata hivyo alisema kwamba katika bajeti ya mwaka kesho wataangalia namna ya kupata fedha kwa ajili ya kukamilisha mradi huo ambao ni muhimu kwa ajili ya utoaji huduma

“Mh Rais Dkt Samia Suluhu amekuja na mpango wa M-Mama ili mama anapohitaji huduma ya Rufaa anaipata na niwaambie kwamba kwa wale kwa wale ambao watabainika wanafanya kazi kwa mazoea na kukiuka maadili hatutawavumilia tutaendelea kuwachukulia hatua kali “Alisema

Hata hivyo alisema kwamba miaka 5 iliyopita walikuwa na Hospitali za wilaya 77 sasa zipo 177 za Serikali hivyo hilo ni jambo la kujivunia sana na huduma zinazotolewa kwenye hospitali hizo ni za msingi unakutana na huduma mbalimbali muhimu.