ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 28, 2022

WALICHOKISEMA MAKOCHA WA YANGA NA SIMBA KUELEKEA NUSU FAINALI FA | HOFU NI KUBWA.

Kuelekea mechi ya nusu fainali za Kombe la Shirikisho Azam, makocha wa Yanga na Simba wamefunguka na kuelezea walivyojipanga kuelekea kwenye mchezo huo utakao fanyika jumamosi ya tarehe 28 may 2022 uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Thursday, May 26, 2022

TUME YA USHINDANI NCHINI (TFCC) NA TUME YA USHINDANI HALALI WA BIASHARA ZANZIBAR (ZFCC) ZAUNGANA KUDHIBITI BIDHAA FEKI

TUME ya Ushindani Nchini (FCC) na Tume ya Ushindani halali wa biashara Zanzibar (ZFCC), zimekubaliana kuendelea kushirikiana katika kudhibiti bidhaa bandia na kulinda ushindani katika soko ikiwa ni pamoja na kumlinda Mtumiaji (Mlaji).

Taasisi hizo zimepongeza jitihada zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan na Rais Hussein Ali Mwinyi za kuboresha mazingira ya biashara yanayo wavutia wawekezaji kwa lengo la kukuza uchumi.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa FCC,  Bw. William Erio wakati akihitimisha mafunzo na ziara ya siku tatu ya Mkurugenzi Mkuu  wa ZFCC, aliyoifanya katika ofisi ya Tume hiyo iliyopo Dar es Salaam akiwa na baadhi ya maofisa wa Tume hiyo.

Mkurugenzi Erio alisema japo suala la biashara sio jambo la Muungano, lakini muingiliano wa biashara biana ya Tanzania bara na Visiwani ni mkubwa hivyo wataendelea kushirikiana kwa lengo la kubadilishana uzoefu kwa mujibu wa Sheria na Taratibu zilizopo. 

"Muingiliano ni mkubwa sana kwakuwa wapo wafanyabiashara na wawekezaji ambao wamewekeza pande zote mbili, hivyo tutadumisha ushirikiano huu ili kutimiza malengo ya Tume hizo na adhma ya viongozi waliotuteua ili kuimarisha uchumi wa Nchi," Alisema.

Aidha, alimpongeza Rais Samia kwa jitihada zake za kuimarisha uchumi na uwekezaji kwa kutembelea mataifa mbalimbali kama vile Marekani, Dubai, Ufaransa na nchi nyinginezo, hivyo wataendelea kumuunga mkono kwa kulinda ushindani na kudhibiti bidhaa bandia zisiingie wala kuzalishwa nchini.

Alisema katika mawasiliano yao wamejipanga kuimarisha mikakati ili wafanyabiashara wa Tanzania wanufaike na Soko huru la Afrika na Afrika Mashariki.

 Kwa upande wa Mkurugenzi wa ZFCC, Bw. Mohammed Sijiamini Mohammed alisema Zanzibar wamejizatiti kudhibiti bidhaa bandia ili kukuza uchumi na kutekeleza adhma ya Serikali.

"Sasa kuna Sheria ya maendeleo ya  viwanda imeanzishwa ambayo hai hapo awali haikuwepo, hizi ni jitihada za makusudi zinazo fanywa na Rais Hussein Ali Mwinyi katika kukuza uchumi," Alisama. 

Aidha, alibainisha kuwa, wataendelea kushirikiana na kubadilishana uzoefu ili kuleta ufanisi katika utendaji wao na kutimiza adhma ya Serikali za pande zote mbili.

"TAASISI ZA FEDHA HIVI SASA ZINATUFUATA KUTUPA MIKOPO" - VIJANA MACHINGA MWANZA WAFUNGUKA.

 Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza leo wamempongeza Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi mbalimbali katika kuwaletea maendeleo Watanzania.

Boniface Zephania ni Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Nyamagana ndiye aliyeongoza jumuiko hilo ambalo pia lilihudhuriwa na vijana wafanyabiashara wadogo maarufu kama 'Wamachinga' mkoa wa Mwanza ambapo kwa upande wao wamepongeza hatua ya Serikali kuwaondoa mitaani na sasa wako kwenye maeneo rasmi, kiasi ambacho kimezivutia taasisi mbalimbali za fedha kwaajili ya kuwapatia mikopo, kisa tu wana anuani rasmi.

Wednesday, May 25, 2022

SIMBA AU YANGA, NI NANI TUTAMKOSA FAINALI?

 Jiji la Mwanza kwa sasa halilali kwani kila uchwao linapokea ugeni toka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi hasa ukizingatia jiji hilo ndiyo lango la nchi za maziwa makuu.

Ni bahati iliyoje kwa jiji la Mwanza kuwekeza vyema katika masuala ya hoteli hivyo wageni hawajaonekana kutaabika kwa kukosa mahala pa kufikia. Shuhudia tambo za leo mbele ya wandishi wa habari...... (cheki video) Kiingilio cha chini katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baina ya watani, Simba na Yanga ni Sh. 10,000 Jumamosi Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Taarifa ya TFF imesema viingilio vingine ni Sh, 30,000 VIP A na Sh, 20,000 VIP B na mchezo utaanza Saa 9:30 Alasiri.

MAJESHI YA TANZANIA YAKABIDHIWA BENDERA TAYARI KWA SAFARI KUELEKEA UGANDA

 JESHI la Wananchi Tanzania na Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Jumanne ya Tarehe 24 Mei 2022 limekabidhiwa Bendera ya Taifa tayari kuianza safari kuelekea nchini Uganda, kushiriki mazoezi ya pamoja ya Majeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Meja Jenerali wa Jeshi la Wananchi Tanzania Athony Suguti ndiye aliyelikabidhi bendera kwa jeshi hilo katika viwanja vya Kikosi Cha Usafirishaji Nyegezi jijini Mwanza. Tanzania imetuma askari wake 299 kushiriki kwenye mazoezi ya kijeshi ya pamoja ya Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Uganda. Na kwa mujibu wa Mkuu wa kikundi cha Tanzania kinachokwenda kushiriki zoezi hilo la Ushirikiano Imara nchini Uganda Brigedia General Charles James Ndiege amesema mazoezi hayo yanayoshirikisha Zaidi ya askari na raia elfu moja kutoka Tanzania, Burundi, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, DRC Kongo na wenyeji Uganda ni pamoja na operesheni za kuunga mkono amani, usimamizi wa maafa, vita dhidi ya ugaidi na uharamia. Mazoezi hayo yalianza kwa mara ya kwanza mwaka 2004 kwa lengo la kuimarisha uwezo wa majeshi ya nchi wanachama katika kulinda amani ili kuzuia matukio chungu katika eneo hilo kama tukio la mauaji ya kimbari ya Rwanda mwaka 1994.

TUNDA MAN USO KWA USO NA HARMONIZE NI BALAA.

 

Tuesday, May 24, 2022

Takukuru Pwani yaja na mtego wa kuwanasa matapeli wa ardhi

 


Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani Christopher Myava Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

NA VICTOR MASANGU,PWANI


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Pwani imekemea vikali na kuwaonya baadhi ya makundi ya watu wanaojihusisha na  kufanya utapeli wa kuuza ardhi kiholela na kusababisha kuibuka kwa migogoro.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake  Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani  Christopher Myava alipokuwa akitoa taarifa ya utendaji kazi ya  robo ya tatu  ya kuanzia mwezi januari mwaka huu. 


Kamanda huyo alisema kuwa kuna baadhi ya  watu wanatuhumiwa kuuza eneo kwa mtu zaidi ya mmoja jambo ambalo limekuwa chanzo cha kutoishq kwa migogoro ya ardhi katika mkoa huo.


Myava alisema Taasisi hiyo iko kazini kupambana na watu hao wanaodaiwa kushiriki kufanya utapeli ili wasiwaingize wawekezaji wenye lengo la kupata maeneo katika mkoa huo na kuzirotesha uwekezaji


Alisema kati ya malalamiko yaliyopokelewa katika kipindi hicho 17 yanahusiana na migogoro ya ardhi ambayo inadaiwa kuchangiwa na watu wanaodaiwa kuwa matapeli.


Alisema malalamiko 98 yalipokelewa katika kipindi cha miezi mitatu kati ya hayo 51yalihusu rushwa ambayo yalianzishiwa majalada ya uchunguzi huku malalamiko ya 47 yakielezwa kuwa hayakuhusu rushwa.


Mkuu huyo wa Takukuru pia amewatahadharisha wagombea wa nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kijiepusha kujihusisha na vitendo vya rushwa.


"Nawaambia Takukuru hatujalala tuko kazini tutazuia vitendo vyote vyenye viashiria vya rushwa, na kwa matapeli wa ardhi tunaendelea kuchunguza malalamiko yaliyoletwa kukomesha tabia hii isituchafulie mkoa wetu" alisema .


Katika kipindi cha miezi mitatu TAKUKURU imeeleza kuwa imefuatilia miradi 182 katika sekta ya afya, Elimu, ujenzi na maji yenye thamani ya sh. Bilioni  8.4.
Kadhalika aliongeza kuwa lengo lao kubwa ni kuendelea kupambana usiku na mchana ili kuweza kuthibiti wimbi la vitendo rushwa na kuwataka wananchi kuwafichua wale wote ambao wanahujumu miradi ya maendeleo.

    


MAJALIWA AWASIMAMISHA KAZI VIGOGO SITA ARUSHA.

vigogo pic

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Arusha. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi sita wa Halmashuri ya Jiji la Arusha, akiwapo Mkurugenzi wa Jiji hilo, Dk John Pima ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma zinazowakabili.

Waziri Mkuu amewasimamisha vigogo hao leo Jumanne Mei 24, 2022 baada ya kubaini ubadhirifu unaofanyika katika Halmashauri ya Jiji la Arusha ikiwamo kupangisha shule ya msingi binfsi ya mchepuo wa kiingereza ya Sojemu iliyopo Kata ya Muriet.

Wengini waliosimamishwa kazi ni Mariamu Mshana ambaye ni mweka hazina wa Jiji hilo, Alex Daniel , Innocent  Maduhu na Nuru Kinana kutoka ofisi ya mchumi pamoja na Joel ambao yupo katika Halmashauri ya Longido kwa sasa.

Majaliwa ameagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuanza kazi ya ukaguzi tuhuma hizo kwani ni kinyume na sheria na itakapobainika hatua za kisheria zichuliwe haraka ili kukomesha tabia hiyo.

"Kwa hiyo basi kwa mujibu wa sheria John Pima, mweka hazina Mariamu Shabani, Inocent maduhu, Alex Daniel wote ni wachumi wakae pembeni kupisha uchunguzi," amesema

Majaliwa amesema kuwa kuna baadhi ya vifaa vya ujenzi wa miradi ya Serikali ilijenga miradi yake ikiwamo mabanda ya ng’ombe na nyumba ya mkurugenzi wa Jiji hilo.

Majaliwa amesema halmashauri hiyo kupitia mkurugenzi huyo imekuwa ikighushi nyaraka pamoja na tabia ya kuhamisha wafanyakazi mara kwa mara ikiwa kama njia ya kufanya maovu.

"Ikiwa madudu hayo ikiwemo mtumishi wa Jiji la Arusha ambaye ni mchumi kuingiziwa Sh65 milioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mitaa na kata kitendo ambacho si kweli ikiwa kila kata huwa na akaunti," amesema Majaliwa