ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 26, 2022

TUME YA USHINDANI NCHINI (TFCC) NA TUME YA USHINDANI HALALI WA BIASHARA ZANZIBAR (ZFCC) ZAUNGANA KUDHIBITI BIDHAA FEKI

TUME ya Ushindani Nchini (FCC) na Tume ya Ushindani halali wa biashara Zanzibar (ZFCC), zimekubaliana kuendelea kushirikiana katika kudhibiti bidhaa bandia na kulinda ushindani katika soko ikiwa ni pamoja na kumlinda Mtumiaji (Mlaji).

Taasisi hizo zimepongeza jitihada zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan na Rais Hussein Ali Mwinyi za kuboresha mazingira ya biashara yanayo wavutia wawekezaji kwa lengo la kukuza uchumi.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa FCC,  Bw. William Erio wakati akihitimisha mafunzo na ziara ya siku tatu ya Mkurugenzi Mkuu  wa ZFCC, aliyoifanya katika ofisi ya Tume hiyo iliyopo Dar es Salaam akiwa na baadhi ya maofisa wa Tume hiyo.

Mkurugenzi Erio alisema japo suala la biashara sio jambo la Muungano, lakini muingiliano wa biashara biana ya Tanzania bara na Visiwani ni mkubwa hivyo wataendelea kushirikiana kwa lengo la kubadilishana uzoefu kwa mujibu wa Sheria na Taratibu zilizopo. 

"Muingiliano ni mkubwa sana kwakuwa wapo wafanyabiashara na wawekezaji ambao wamewekeza pande zote mbili, hivyo tutadumisha ushirikiano huu ili kutimiza malengo ya Tume hizo na adhma ya viongozi waliotuteua ili kuimarisha uchumi wa Nchi," Alisema.

Aidha, alimpongeza Rais Samia kwa jitihada zake za kuimarisha uchumi na uwekezaji kwa kutembelea mataifa mbalimbali kama vile Marekani, Dubai, Ufaransa na nchi nyinginezo, hivyo wataendelea kumuunga mkono kwa kulinda ushindani na kudhibiti bidhaa bandia zisiingie wala kuzalishwa nchini.

Alisema katika mawasiliano yao wamejipanga kuimarisha mikakati ili wafanyabiashara wa Tanzania wanufaike na Soko huru la Afrika na Afrika Mashariki.

 Kwa upande wa Mkurugenzi wa ZFCC, Bw. Mohammed Sijiamini Mohammed alisema Zanzibar wamejizatiti kudhibiti bidhaa bandia ili kukuza uchumi na kutekeleza adhma ya Serikali.

"Sasa kuna Sheria ya maendeleo ya  viwanda imeanzishwa ambayo hai hapo awali haikuwepo, hizi ni jitihada za makusudi zinazo fanywa na Rais Hussein Ali Mwinyi katika kukuza uchumi," Alisama. 

Aidha, alibainisha kuwa, wataendelea kushirikiana na kubadilishana uzoefu ili kuleta ufanisi katika utendaji wao na kutimiza adhma ya Serikali za pande zote mbili.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.