ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 7, 2012

MANENO YA MWISHO YA KANUMBA ALIYONENA KWA MAMA YAKE MZAZI JANA KABLA YA MAUTI.

Mama Kanumba anayeitwa Flora Mtegoa
Wakati Taifa la Tanzania likiwa katika majonzi mara baada ya kupoteza moja kati ya vijana wake walio peperusha vyema ndani na nje ya mipaka pendera yake kupitia tasnia ya Filamu STEVEN KANUMBA, yafuatayo ni mahojiano kati ya mdau wa blog ya G. Sengo mkoani Kagera mwandishi wa habari anayeitwa Nicolaus Ngaiza, aliyoyafanya na Mama Kanumba (Flora Mtegoa).
Mama yake Steven Kanumba (kushoto) akilia kwa uchungu huku akifarijiwa na moja ya nduguze.
Katika mahojiano yaliyofanyika leo majira ya saa nane mchana katika uwanja wa ndege Bukoba katika harakati za safari kuelekea jijini Dar es salaam ILIKUWA HIVI:-
Nicolaus Ngaiza:- Mama unamwelezeaje Steven Kanumba katika kipindi cha uhai wake?
MAMA:- Kanumba mtoto wangu mtiifu, rafiki yangu, mpendwa wangu, mtotowangu wa karibu na jana niliongea naye kwenye simu na alfajiri naambiwa kafa.

Nicolaus Ngaiza:- Pengine alizaliwa sehemu gani mwaka gani?
MAMA:- Kanumba alizaliwa tarehe 8/1/1984 mkoani Shinyanga, katika hospitali ya Government Shy.

Nicolaus Ngaiza:- Baba yake yuko hai?
MAMA:- Baba yake yuko hai yuko Shinyanga anaitwa Charles Kanumba

Nicolaus Ngaiza:- Katika kipindi hiki kigumu unawambiaje watu wa Bukoba?
MAMA:- Naomba waniombee kwani hali yangu siyo nzuri kwani niko katika kipindi hiki kigumu.

Nicolaus Ngaiza:- Labda mama kijijini kwenu ni wapi?
MAMA:- Mimi natoka Wilayani Muleba, kata ya Izigo, kijiji cha Itojo.

Nicolaus Ngaiza:- Steven Kanumba sisi tunamjua kwa jina hilo jeh! hakuwa na jina la kinyumbani?
MAMA:- Hakuwa na jina lolote la kinyumbani zaidi ya hilo Kanumba la Kisukuma yeye ni msukuma.

Nicolaus Ngaiza:- Tungependa kujuwa neno la mwisho mlio weza kuzungumza pamoja.
MAMA:- Aliniambia mama natuma nauli uje tuagane naondoka naenda Marekani, akiwa mwenye furaha, tunataniana...

Nicolaus Ngaiza:- Labda aliwahi kukwambia ndoto zake katika maisha kwamba analenga kufanya nini?
MAMA:- Yeye ndoto zake ni kuendeleza sanaa yake na ninashukuru alikuwa amefika mbali kisanaa.

Nicolaus Ngaiza:- Labda kifamilia alikuwa ameoa au alikuwa na mtoto?
MAMA:- Hajawahi kuoa na hakuwa na mtoto...
SIKILIZA Clouds fm USIKU HUU SAUTI YA MAMA HUYU ITASIKIKA.
RIP ... STEVEN KANUMBA 'THE GREAT'

KANUMBA THE GREAT IS DEAD


Taarifa nilizozipata sasa hivi kutoka kwa mwigizaji Dino, ni kwamba kweli mwigizaji STEVEN KANUMBA amefariki dunia na inaaminika chanzo cha kifo chake ni baada ya kuanguka na kuanza kutoa mapovu hapohapo nyumbani kwake, alikua akiishi na mdogo wake anaitwa Fetty aliekua chumba kingine ambae amethibitisha kweli kwamba alimkuta kaka yake akiwa ameanguka.

Polisi wameondoka nyumbani kwa Kanumba muda mfupi uliopita baada ya kuwachukua waliokua wanaishi na Kanumba akiwemo mdogo wake Fetty ili kwenda kusaidia maelezo ya kilichotokea.

Bado watu wanazidi kuongezeka nyumbani kwa Kanumba ambapo tayari idadi kubwa ya wasanii wenzake wamefuka pamoja na watu mbalimbali, millardayo.com itaendelea kukufahamisha kinachoendelea kadri taarifa zitakavyozidi kupatikana.

Ila kumekua na taarifa nyingine ambazo hazijadhibitishwa kwamba Kanumba alianguka na kuumia kichwani baada ya mpenzi wake kumsukuma na kuanguka wakati wanagombana.

Hapo chini ni baadhi ya kauli nilizokutana nazo kwenye facebook wakati huu na chini yake ni maneno ya mwisho STEVEN KANUMBA kuyaandika kwenye kurasa zake za facebook na twitter.
CHANZO http://millardayo.com/

Friday, April 6, 2012

ALLIANCE WAIBUKA VINARA WA SOKA SHULE ZA MWANZA

Michuano ya soka yenye lengo la kukuza vipaji vichanga iliyoshirikisha shule za msingi 10 na sekondari 10 kwa jiji la Mwanza iliyoanza tangu machi 15 2012 imemalizika leo kwa mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu na fainali ya kumsaka bingwa.

Timu za waandaaji wa michuano hiyo Alliance Sports Academy zimetoka kidedea kwa kuzitwaa nafasi zote za ubingwa kwa Shule ya Msingi na Sekondari michezo ikifanyika kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mchezo wa kwanza ulikuwa wa kutafuta mshindi wa tatu baina ya Igoma Secondary iliyopepetana na Mahina Sec mchezo uliolazimu kuingia katika hatua ya matuta mara baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.

Kwenye mikwaju ya penati Igoma Sec imeitwaa nafasi ya tatu kwa kuifunga Mahina Secondary bao 4-2.

Mchezo wa pili ulikuwa ni fainali ambapo Alliance Sec iliichabanga Mtoni Secondary bao 1-0 na kutawazwa mabingwa, bao hilo la ushindi likifungwa na mshambuliaji Selemani Shadrack katika dakika za mwanzo tu za mchezo.

UZINDUZI WA TAMTHILIA YA 69 RECORDS SEASON II WAFANA NDANI YA NYUMBANI LOUNGE JIJINI DAR

Wasi Wasi Mwambulambo wa Clouds TV akiitambulisha sehemu ya crew iliyoifanikisha kwa kiasi kikubwa tamthilia ya 69 records season II,ambapo kwa maelezo ni kwamba tamthilia hiyo itakuwa ikirushwa Clouds TV pamoja na kwenye DSTV.

Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya H-Baba akitumbuiza kwenye hafla hiyo.

Msanii mwingine anayetikisa anga ya muziki wa Bongofleva,Ommy Dimpozz akiimba mbele ya wageni waalikwa (hawapo pichani) usiku huu.

Mmoja wa wasanii mahiri wa Filamu hapa nchini,ambaye binafsi namkubali sana,Jacob Steven a.k.a JB akitoa maneno machache ya kuisifia kazi nzima ya iliyofanywa ndani ya tamthilia ya 69 Recods season II.

Msanii Queen Doreen ambaye ni miongoni walioigiza kwenye tamthilia ya 69 Recods, wakijitambuliza, nyuma yake ni wasanii waliogiza kwenye tamthilia hiyo

Mambo ya shampeini'

Baba Jonii' along side....

Flash 2 ze place.

Kidoti'

Interview..'

Air DadazZ'
Picha zote na Michuzijr Blog

JUMATATU YA PASAKA USIKOSE CCM KIRUMBA

NJOO UPOKEE MIBARAKA YA BWANA KWENYE TAMASHA LA MUZIKI WA INJILI CCM KIRUMBA MWANZA.
SIKU JUMATATU YA PASAKA.
KIINGILIO WAKUBWA 2000/=
KIINGILIO WATOTO 1000/=
KARIBU SANA.

RAIS WA MALAWI AFARIKI DUNIA

Rais wa Malawi Bingu wa Mutharika amefariki dunia kwa mshuto wa moyo akiwa Johannesbuerg nchini Afrika Kusini alipopelekwa kwa matibabu.

Akiwa ameandamana na mkewe na jamaa zake wa karibu, rais huyo alisafirishwa hadi Afrika kusini katika hali ya usiri mkubwa huku akiwa hana fahamu.

Hali iliyozua hofu na utata mkubwa nchini Malawi kwani kwa muda mrefu kumekuwa na shinikizo za kumtaka Mutharika ang’atuke.

Awali afisa mmoja mkuu wa serikali ya Malawi alinukuliwa akisema kuwa Rais Mutharika mwenye umri wa miaka 78 aliangua akiwa katika makaazi yake rasmi na kupelekwa hospitalini ambako aliwekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Kuhusu nani ataongoza taifa hilo fuatia kifo cha rais huyo, kulingana na katiba ya Malawi, Makamu wake Bi Joyce Banda atalazimika kushikilia hatamu za uongozi kwa kipindi kilichosalia .

Hata hivyo Bi banda na rais Mutharika walikuwa hawasikilizani kwani walikosana mwaka wa 2009 na Makamu huyo wa Rais akalazimika kuhamia upinzani.

RIP MUTHARIKA.

Thursday, April 5, 2012

KUNDI LA WATU 1000 WAVAMIA MGODI GEITA

MGODI wa dhahabu wa Geita (GGM) leo umechafuka baada ya kundi la wachimbaji wadogo zaidi ya 1000, kuvamia mgodini humo kwa lengo la kuchukua mawe ya dhahabu, na kuteketeza gari moja kwa moto huku watu watano wakijeruhiwa.

Inasemekana watu hao waliovamia ni wachimbaji wadogowadogo ambao wamekuwa wakihangaika kutokana na maeneo waliyoaidiwa na waziri Ngereja kutengwa kwa ajili yao kukosekana, hivyo kila wanapokabiliwa na hali ngumu wamekuwa wakivamia mgodini kuchukua mawe ili nao wakajitafutie mali.

HABARI KUTOKA NDANI.

Hali imekuwa tete sana katika mji wa Geita na hata hapa mgodini, FFU wamemwagwa kwa wingi sana kutoka Mwanza na sasa wenzetu walioko Geita mjini wanasema hali kidogo inaanza kurudi katika hali yake ya kawaida. Magari yote madogo yanayotumiwa na supervisors wanaokaa mjini yamezuiwa kwenda mjini, hivyo watumiaji wake nao wametakiwa na uongozi wa mgodi kutumia mabasi, ambayo nayo yanasafiri kwenda mjini kutoka mgodini kwa escort ya polisi (FFU). Wafanyakazi hapa mgodini wameshikwa na wasiwasi mkubwa, na wengi wamekuwa wakifikiri kuwa huenda wakafanyiwa fujo pindi wafikapo mjini na nguo za kazini zenye reflectors.

Ni hali ambayo haijawahi kutokea nafikiri toka mgodi huu umeanza, jambo linaloashiria kuwa kuna tatizo mahali flani ambalo linahitaji kufanyiwa kazi haraka iwezekanavyo na mamlaka zinazohusika. Mambo haya yanayotokea hapa yamekuwa yakitokea kwenye migodi mingine, hususani mgodi wa North Mara, na kila mtu anakumbuka ni kwa jinsi gani mgogoro ule ulivyochukua sura mbalimbali zisizopendeza zilizopelekea vyombo vya usalama na wanasiasa kulaumiana. Natumaini vyombo vya habari vitaendelea kutujuza mengi leo usiku na hata kesho kwenye magazeti yetu maana natumaini waandishi wa habari watakuwa wamewasiliana na mamlaka husika na hivyo kujua mengi kuhusiana na mgogoro huu.

KILICHOFUATA ARUSHA MARA BAADA YA GODBLESS LEMA KUVULIWA UBUNGE

Maandamano ya wafuasi na wanachama wa CHADEMA wakimsindikiza "Aliyekuwa mbunge wao" wa Arusha mjini ndugu Godbless Jonathan Lema kuelekea viwanja vya Ngarenaro majira ya saa nane na dakika 15 ambapo hatimaye alihutubia wananchi. Mahakama imetengua ubunge wa Lema kutokana na kesi iliyofunguliwa na wanachama watatu wa CCM.

Godbless Jonathan Lema amekubali uamuzi wa mahakama na amesema haina haja ya kukata rufaa isipokuwa ATASHINDA TENA kiti hicho katika uchaguzi mdogo utakaoandaliwa na tume ya Taifa ya uchaguzi.
PICHA/HABARI NA SUBI

BREAKING NEWS LEMA APOTEZA UBUNGE ARUSHA

Habari kutoka mjini Arusha zikipenyezwa na 'Breaking News' ya Clouds fm zinasema kwamba aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kupitia CHADEMA, amepoteza kiti hicho kupitia kesi iliyokuwa inamkabili.Godbless Lema akiwa na mkewe kwenye moja ya mashauri ya kesi hiyo.

Maamuzi hayo yamekuja kupitia kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa muda sasa ikihusiana na uchaguzi wa mwaka 2010 ambapo katika kusikiliza kesi hiyo upande wa Lema uliwakilisha mashahidi wanne.

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kupitia jaji Gabriel Rwakibarwa wa Sumbawanga imemvua Ubunge bwana Godbless Lema kwa madai kwamba kulikuwa na chembechembe za udhalilishaji wa matusi, kidini, kijinsia na kikabila, hivyo wananchi wa jimbo hilo wanalazimika kufanya uchaguzi tena. Ikumbukwe kuwa katika uchaguzi wa 2010 Godbless lema aliibuka kwa ushindi wa kura 56,569 wakati mpinzani wake Dr.Batilda Buriani alipata kura 37,460.

Hata hivyo, Lema hakuondolewa haki ya kugombea ubunge huo tena na kwa taarifa za watu wa karibu, Lema hatakata rufaa mahakamani juu ya hukumu ya kesi hiyo, bali atakata rufaa kupitia kura ya wananchi wa Arusha Mjini, hivyo tutarajie uchaguzi mpya hivi karibuni.

Tanzania, nchi ya uchaguzi kila uchao...mmmmmmh!

Wednesday, April 4, 2012

MWANDISHI ALIYEPATA AJALI MWANZA ATOKA HOSPITALI

Mwandishi wa habari Hussein Mtanda aliyepata ajali hivi karibuni nakupoteza jicho lake la kushoto hatimaye leo karuhusiwa kutoka hospitalini ambako alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza, na yafuatayo ni maneno yake:-
"Jamani nashukuru kwa moyo wa pamoja mlio nionyesha kuanzia nilipo ugua mpaka sasa, kwakweli Mungu awabariki, ninavyozungumza niko nyumbani kwa mapumziko.
AKSANTENI SANA"

JUMBA LA TAMTHILI SOMALIA LALIPULIWA KATIKA MAADHIMISHO YA MWAKA MMOJA WA TELEVISHENI YA TAIFA YA SOMALIA.

Kumetokea mlipuko katika Jumba la Tamthilia lililofunguliwa upya katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.

Mlipuko huo umefanyika wakati wa hafla ya kuamdhimisha mwaka mmoja tangu televisheni ya taifa kuanza kuyapeperusha matangazo yake.


Takriban watu saba wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa, wakiwemo wabunge. Waziri Mkuu Abdiweli Mohamed Ali alikuwepo kwenye hafla hiyo lakini haijabainika ikiwa alijeruhiwa.

Mshambuliaji wa kike wa kujitoa mhanga ameripotiwa kufanya shambulio hilo.

Kundi la Al Shabaab limekuwa likitumia mashambulio ya mhanga kama mbinu mpya ya harakati zake tangu kutimuliwa mjini Mogadishu mwaka jana.

TANZIA

TANGAZO LA MSIBA:

Ndugu wana M.I.S kwa masikitiko makubwa tumepokea taarifa za msiba wa kifo cha mama mzazi wa mwenzetu (mchungaji John MWAISAKA) Jou-Ntwa John uliotokea April 3,2012. MSIBA upo nyumbani "kota za reli" Pasiansi jijini Mwanza.

Ibada ya mazishi itafanyika kesho Alhamis april 5,2012 SAA SITA MCHANA kanisa katoliki Pansiansi na baadaye makaburi ya LUMALA.

Mungu awatie nguvu familia ktk kipindi hiki kigumu. Twakuomba ewe Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya MAMA MWAISAKA mahala pema peponi.
AMINA

Tuesday, April 3, 2012

VITUKO PICHANI: CUF NA BANGO LA MAITI YA MGOMBEA WA CCM TANGA

Wakuu.
Leo katika pitapita yangu maeneo ya kata ya Msambweni hapa jijini Tanga,nimekutana na kituko cha kusikitisha lakini kilichobeba ujumbe mzito kwa chama tawala. Ujumbe huo unasikitisha sana sana sana...kwa sababu umebeba picha ya umauti, Mimi kama mwanachama wa chadema, nimeshangazwa na namna wanachama wa CUF walio amua kutumia jeneza bandia na kikaragosi cha maiti kuonyesha hisia zao za kufurahia ushindi wa kata hiyo walioupata kwenye uchaguzi uliofanyika jana.

Haya ndio nimeya shuhudia kwenye upita njia wangu eneo la kata yaMsambweni ambayo ni mojawapo ya ngome za CUF kwa hapa jijini Tanga.

Kikaragosi cha maiti.

Bango pembeni mwa jeneza likiwa limebeba ujumbe mzito, nalo naona limebeba aina ya mchoko wa siasa za ushirika baina ya CUF na CCM.

Kwa mtazamo wangu , Cuf Hata kama wamekuwa na furaha ya namna gani ya kutetea kata yao hawakupaswa kusherehekea kwa kuweka picha ya mgombea wa ccm alieshindwa kwenye uchaguzi kwenye mfano wa jeneza bandia tena huku wakiweka sania ambalo kila anae pita njia anatupia pesa kama rambirambi.
Naomba kuwasilisha
From: "Mohamedi Mtoi"
Tanga, Tanzania

Monday, April 2, 2012

CHEZEA TWANGA WEYE....!!!!

Ziara ya Twanga Pepeta kanda ya ziwa imedhihirisha kuwa bendi hiyo bado ni mahiri linapokuja suala la kuwa na mashabiki wengi. Kwa mujibu ya wakuu wa kumbi mbalimbali za burudani ambao hutumiwa na www.gsengo.blogspot.com kwa shughuli mbalimbali za burudani kila mmoja amekiri kupata faida kupitia ziara ya Bendi hiyo. Ukianzia Villa Park Mwanza ambapo kamera yetu ilikuwa pale, Musoma mkoani Mara na hata katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kwa show iliyofanyika jana Club Dimpoz.
Dogo Rama akisalimia watu wake wa nyumbani.

Mmoja kati ya mashabiki aliyejitambulisha kwa jina moja tu Selemani, amesema kuwa hata fitina gani ziwaandame hawa jamaa watabaki kuwa juu kwani kama Uongozi wanao, jina wanalo, mashabiki wanao vizazi hadi vizazi kuanzia watu wazima, wazee, wanaume kwa wanawake vijana hadi watoto.

USIKU WA KUAMKIA SIKU YA UCHAGUZI WABUNGE WA CHADEMA WACHARANGWA MAPANGA MWANZA

Wabunge wawili wa Chadema wamejeruhiwa vibaya kwa mapanga na mashoka jijini Mwanza katika tukio lililotokea saa nane usiku katika eneo la Ibanda Kabuhoro baada ya kuvamiwa na watu ambao bado haijajulikana walikuwa na dhamira gani katika usiku wa kuamkia uchaguzi wa diwani Kata ya Kirumba. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow alisema jana kwamba mbali na wabunge hao, Samson Highness Kiwia wa Ilemela (kushoto) na Salvatory Machemuli wa Ukerewe (kulia) PICHANI, wengine walioshambuliwa ni pamoja na Ahmed Waziri ambaye inasemekana kuwa ni kada wa UVCCM aliyekatwa kiganja chake cha mkono wa kulia.

Wengine ni Haji Mkweda (21), ambaye alijeruhiwa mguu wa kulia, Judhith Madaraka (26), aliyechomwa kisu kwenye titi lake la kushoto na mkono wa kushoto, Ivory Mchimba (26), aliyejeruhiwa kichwani na mdomoni. Majeruhi wote ukiondoa wabunge hao na Waziri, wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Sekou Toure.

Awali, wabunge hao walilazwa katika Hospitali ya Rafaa Bugando lakini baadaye walisafirishwa kwa ndege kupelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam. Kwa upande wake, Waziri amelazwa Bugando.

Kamanda Barlow alisema katika vurugu hizo magari matatu likiwemo la Kiwia yaliharibiwa.

Majeraha aliyopata kichwani mh.Highness
Polisi ilipata mapema taarifa za tukio hilo lakini ilichelewa kufika kutokana na eneo hilo kuwa lenye mawe na milima hivyo kufika wakati tayari wabunge wameshajeruhiwa vibaya na mali hizo kuharibiwa.
Majeraha mgongoni mwa mh. Highness.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Mabina amekana wafuasi wake kuhusika na uvamizi huo dhidi ya wabunge hao, akidai kwamba pengine wabunge hao walikutana na wahuni au majangili wakawavamia na kuwashambulia kwani mazingira ya usiku namna hiyo huwezi kuamini kwamba CCM wamefanya shambulio hilo nakuwataka wabunge hao wahojiwe zaidi walikwenda kufanya nini maeneo hayo nyakati hizo.

TWANGA PEPETA WALIPO TIKISA ROCK CITY

Mkurugenzi wa Aset Entertainment Asha Baraka akimtambulisha mgeni rasmi wa uzinduzi wa Twanga Mwanza, Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja uliofanyika Villa Park.

Mtoto wa nyumbani Dogo Rama aliyejiunga na Twanga akitokea Mwanza Carnival Band akituzwa na Dulla.

Wakali majembe ukweli Twanga Pepeta, Luiza Mbutu na Amigoras.

Mwana wa nyumbani Haji Ramadhani alitumia fursa yake kikamilifu kutoa shukurani zake kwa watu wake wa nyumbani kumpigia kura hata akaibuka kinara BSS.

Ze utamuuuu.

Dadazz wa Twanga na 'visigino'..

BrazazZz.

Dansi la Twanga.

Kutoka kushoto ni Dj Maliz, Mkali wa bongo Fleva Dudu Baya na G.Sengo, burdanini.

Mauno mauno...

Handsome boy.

Dj Maliz, Dj John, Dudu Baya na G. Sengo.

mwimbaji wa Twanga Pepeta Dogo Rama akishirikiana kwenye kiitikio na watangazaji wa Star Tv Muhksin Mambo (C) na Ben 'Star' jamaa walienda nae sambamba kinomanoma.

Rapa wa Twanga na flash ya www.gsengo.blogspot.com

Mazingira ya Jiografia na stage la Twanga Pepeta at Villa Park Mwanza usiku wa Ijumaa mwishoni mwa wiki.