ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 1, 2013

WAZIRI MKUU KESHO KUFUNGUA SHEREHE ZA BULABO 2013 MAANDALIZI YAKAMILIKA ASILIMIA 99.9

Tamasha la Bulabo huusisha ushindani wa ngoma za asili za watu wa kabila la wasukuma, na katika ushindani  waganga na wachawi huusishwa ili kupata ushindi, na hii ndiyo kamati ya ufundi, unaambiwa kwamba jamaa hawa wamejipaka dawa ambazo hawapaswi kuoga wiki nzima ya tamasha la Bulabo yaani mpaka litakapomalizika na wana masharti hawatakiwi kuzungumza na mtu mwingine zaidi ya watu wao tu!! (kwao ni tabasamu na minuno)

Mara baada ya kuwasili leo kwenyehimaya ya hii ya makumbusho ya Bujora walipaka dawa zao na kuelekea moja kwa moja uwanja wa tukio na kufanya mambo yao ya kamati wakizindika dawa zao pande zote za uwanja kisha wakarejea hapa eneo la matayarisho na kuwa kama sehemu ya watizamaji huku wakiwa kimyaaaa. 


Chekshia Kideo....upate uhondo wa pasha pasha za maandalizi kuelekea Bulabo.

Kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo ili wasili Kisesa na kudhuru maeneo yote kwaajili ya kuhakiki na kufanya ukaguzi mahususi kwaajili ya ugeni wa Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda ambaye ndiye atakuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi tarehe 2 juni 2013.

Mteni wa watu wa kabila la Wachaga ajulikanaye kwa jina la Mtemi Mariale (wa pili kutoka kulia) ambaye ni mwenyekiti wa watemi wote nchini naye ni mualikwa kwenye tamasha hili la tamaduni za watu wa kabila la wasukuma.

Katika viwanja hivi nakutana na Shangazi yangu ambaye naye ni Mtemi wa koo za eneo la Shinyanga.

Watoto ni sehemu ya tamasha la Bulabo hivyo walijumuika hapa mapema, unaowaona pichani ni viongozi wa watoto wao wakijinoa zaidi katika kukariri yanayopaswa kuzungumzwa shereheni kwani wataandamana wakirusha maua na kupaza sauti zao kwa kauli moja kwenye paredi. 

Ngoma ya Wigashe ikijinoa.

Hapa palikuwa patamu.

Mwnyekiti wa Kampuni ya bia ya Serengeti Paul Bomani akiwapungia mikono wadau wa ngoma za jadi mara baada ya kuwasili kituo cha Bujora.


Diwani wa kata ya Kisesa Mh. Clement akimkaribisha Mwenyekiti wa Kampuni ya bia ya Serengeti Paul Bomani ambaye pia ni mlezi wa jumba la makumbusho la Bujora ili kupata kuzungumza na watemi waliokusanyika hapa ukumbini.

Mwenyekiti wa Kampuni ya bia ya Serengeti Paul Bomani ambaye pia ni mlezi wa jumba la makumbusho lya watu wa kabila la Wasukuma yaani  Bujora akizungumza na watemi waliohudhuria kikao cha maandalizi jioni ya leo.

Mwaka huu 2013 Bulabo imechukuwa sura mpya, kwani idadi ya watu wengi inatajwa kuahidi kuhudhuria wakiwemo viongozi na makampuni mbalimbali, vikumndi mbalimbali vya ngoma asili vimejiandikisha kushiriki mashindano kikubwa zaidi ni ugeni wa Mh. waziri Mkuu.  

Pichani Mwenyekiti akisalimiana nakijana wake' mara baada ya kikao cha maandalizi kukamilika usiku wa leo hapa Bujora Kisesa mkoani Mwanza,  Watemi kutoka Moshi, Tabora na sehemu mbalimbali hapa nchini wamehudhuria kupata ujuzi na kujenga umoja. 

MWANZA NG'ARING'ARI...WIKI YA USAFI YAZINDULIWA RASMI

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo (wa 5 kutoka kushoto) akiongoza shughuli za usafi ndani ya jiji la Mwanza ikiwa ni sehemu ya Uzinduzi wa wiki hiyo ambayo itaadhimishwa kila mwanzo wa kila mwezi ndani ya jiji hilo ikiwashirikisha wananchi wote kwa kila kaya na kila mtaa.
HALMASHAURI ya JIji la Mwanza imewataka vijana na wananchi kuanzisha vikundi na kuvisajili kwenye halmashauri hiyo ili kufanyakazi ya kudhibiti wachafuzi wa mazingira.


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa Injinia Ndikilo amesema kuwa kupitia mpango huo utasaidia Jiji la Mwanza kuendelea kuwa safi na kuendelea kuvutia wawekezaji wa ndani na nje sanjari na kukabiliana na changamoto mbalimbali ili kulinda hadhi ya kitaifa na kimataifa.

“Tuendelee na utunzaji mazingira na usafi pia ili kuhakikisha Jiji hili linakuwa na muonekano na uhalisia kwa kuwavutia wawekezaji lakini pia tumeelezwa kuwa kupitia mpango unaoendelea wa Jiji ni kuhakikisha wafanyabiashara wadogo (MACHINGA) wanapangwa vizuri katika maeneo ya Mjini kati badala ya kuzagaa holela wakifanya biashara hadi maeneo hatarishi”alisema


Uzinduzi huo umefanyika leo katika eneo la Stendi ya zamani ya Tanganyika iliyopo Kata ya Pamba ambpo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa mwanza Injinia Evarist Ndikilo aliyeambatana na Meya wa Jiji hilo Stanislau Mabula (CCM), Naibu Meya John Minja (CCM), viongozi mbalimbali, wadau na Madiwani wa Kata zote za Jimbo la Nyamagana.


Wadau wa jiji dada na jiji la Mwanza kutoka nchini Sweden jiji la TAMPERE wakitoa utambulisho na pongezi kwa Jiji la Mwanza kwa hatua hii ya kuanzisha wiki ya usafi.


Rais wa chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT) Dovakimwene John Mcheshi akizungumza na wananchi waliohudhulria kusanyiko hilo la mazingira kuonyesha kuwa nao wako pamoja na uongozi wa mkoa kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama.


Afisa habari wa jiji la Mwanza Joseph Mlinzi akiteta jambo na meneja wa SBC.


Injinia Ndikilo amewapongeza wananchi wake kwa kuwa mshindi kwa mara nyingine ya Tuzo ya Usafi na Mazingira ambapo jiji la Mwanza limeshinda kwa mara ya nane mfululizo ambapo amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na madiwani,mkurugenzi na wadau mbalimbali wa usafi ili kuhakikisha Jiji hilo ikiwa ni pamoja na kulinda ushindi .


Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo, pamoja na Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula wakiiongoza meza ya viongozi kwenda kushiriki zoezi la usafi. 
“Wamiliki wa daladala,mabasi na wenye maduka kuhakikisha wanaweka vifaa vya kutunzia usafi na kwa kutumia sheria ndogo za usafi na mazingira ya mwaka 2010 Jiji limejipanga kutumia SHARREFF kutekeleza mpango huu hivyo ni fursa kwa vijana kuunda vikundi na kuvisajili ili kuwashughulikia baadhi yawatu wachache walio na tabia ya uchafuzi wa mazingira” alisisitiza mkuu wa Mkoa.
Kwa upande wake Meya wa Jiji la Mwanza Mabula alisema kwamba Jiji hilo limeandaa mpango wa kuwapanga wamachinga katika maeneo yaliyoruhusiwa kufanya biashara na kuwaondoa wale ambao wako katika maeneo hatarishi ikiwemo kandokando ya barabara kuu na zile za mitaa.Meya Mabula alisema kwamba baada ya ziara ya madiwani na watendaji katika Nchi ya Rwanda na tafiti mbalimbali Jiji hilo limeamua kuanzisha mpango huo ili kujizatiti zaidi huku pia likiwa limefanikiwa kupata magari mawili kutoka nchini Ujeruman ya kuzoa taka na kufagia barabara huku pia likipatiwa vifaa kupitia mpango wa mradi wa TSCP nchini.

Ametoa wito kwa wananchi kushiriki kila jumamosi ya kila juma la kwanza la mwezi katika shughuli ya usafi kwenye mitaa na kata zote za Jiji hilo kuanzia saa 1:30 hadi saa 4:00 asubuhi na kuhakikisha wanaochafua mazingira wanakamatwa na kutozwa faini kutokana uchafuzi ili kukomesha vitendo vyote vinavyeneza uchafu.
Friday, May 31, 2013

KWA MARA YA KWANZA MISS MWANZA KUPATA HESHIMA YA BURUDANI TOKA KWA MH. SUGU

Sindano la kumtafuta mrembo wa mkoa wa Mwanza, linatarajiwa kufanyika June 14 katika viwanja vya Yatch Club jijini Mwanza.

Warembo 18 kutoka wilaya mbalimbali za mkoa wa Mwanza wamejitokeza kushiriki shindano hilo la aina yake huku.... Burudani inayosubiriwa kwa hamu kubwa ni Mh. Mbunge Joseph Mbilinyi maarufu kama sugu atakapo panda jukwaani kukumbushia enzi hizo...akishindikizwa na mkali mwingine wa Chege Chigunda kutoka TMK.

Warembo wote wanatarajiwa kuanza kabi rasmi Jumanne hii katika moja ya hoteli maarufu jijini humo.

Itakumbukwa mkoa wa Mwanza tayari ulishatoa Mrembo wa Tanzania, ambaye ni Nasreem Karim 2009 na Miriam Gerald 2010. Pamoja na mchakato wa shindano la urembo kuendelea kwa hivi sasa nchini, macho na masikio yapo mkoani Mwanza, ambako kumekua kukileta changamoto na upinzani mkali wa warembo kila Mwaka. 

PEPSI KUDHAMINI MEYA CUP MIAKA MITATU MFULULIZO

Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (kulia) akizungumza na vyombo vya habari juu ya udhamini wa mashindano ya Meya Cup 2013, katikati ni Meneja wa kampuni ya SBC  watengenezaji wa vinywaji vya Pepsi Nico Coetzer, na kushoto ni meneja mauzo Sharif Taki, wakati kutangaza rasmi udhamini wa Pepsi katika Meya Cup. 


Meneja wa kampuni ya SBC  watengenezaji wa vinywaji vya Pepsi Nico Coetzer akifafanua udhamini wa kampuni yake kwa mashindano ya Meya Cup 2013.


Meneja mauzo wa kampuni wa SBC Sharif Taki, akielezea jinsi zawadi zilivyonuia kubadilisha maisha ya wajasiliamali kupitia Meya Cup.


Sehemu ya waandishi wa habari walio hudhuria hafla hiyo ya Udhamini wa Pepsi kwa michuano ya Meya Cup.


Sehemu ya waandishi wa habari walio hudhuria hafla hiyo ya Udhamini wa Pepsi kwa michuano ya Meya Cup.
Zawadi ni kama ifuatavyo:-
A. Mshindi wa kwanza-
-   Bajaji yenye thamani ya SH. 4,000,000/=
-   Fedha taslimu                  SH  1,000,000/=
-   Kikombe cha Ushindi 
-   Medali kwa wachezaji wote

B. Mshindi wa pili
-   Fedha taslimu                  SH 1,500,000/=
-   Kikombe
-   Medali za wachezaji wote

C. Mshindi wa tatu
-   Fedha taslimu                  SH. 500,000/=
-   Kikombe
-   Medali kwa wachezaji wote

D. Mfungaji Bora -  Kikombe

E. Timu yenye Nidhamu- 
Aidha Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula ametoa Shukurani kwa Mkurugenzi wa jiji la Mwanza na timu yake ya wataalamu wakishirikiana na My Way Entertainment katika kufanikisha kuratibu maandalizi ya mashindano ya Meya's Cup 2013.

Mwisho ametoa wito kwa wananchi na wanamichezo wote katika jiji la mwanza kushiriki pasipo kuchoka, wajue kwamba kuna fursa kubwa ya kushinda na hatimaye kujipatia zawadi kemkem na manufaa mengine kama yalivyoainishwa.

Thursday, May 30, 2013

MWILI WA NGWEA ULIANZA KUPATA UBARIDI KABLA YA KUFIKISHWA HOSPITALI, BUSHOKE NAYE ATHIBITISHA KUFARIKI KWA ALBERT MANGWEA

Moja kati ya marafiki wa karibu wa msanii albert Mangwea aliyekuwa karibu naye nyakati za mwisho za maisha yake aliyejitambulisha kwa jina la Goddy amezungumza na Amlifaya ya Clouds fm jioni ya leo ikiwa ni Live kutoka nchini Afrika ya kusini akihojiwa naye mtangazaji Milard Ayo na kusema kuwa mwili wa marehemu Mangwea kabla hajafikishwa hospitali ulikuwa tayari umepata ubaridi. 

Hivi ni nini sababu ya kifo cha Ngwea? ZAIDI SIKILIZA HAPA CHINI:

  BUSHOKE NAYE ATHIBITISHA KUFARIKI KWA ALBERT MANGWEA AWASHUKIA WATANZANIA WANAOZUSHA TAARIFA ZA VIPIMO VYA DAKTARI BILA KUFATA TAARIFA RASMI. 
Msanii wa muziki wa bongo flavour Bushoke ni mmoja kati ya watanzania walioko nchini Afrika ya kusini akifanya kazi ya sanaa kule, kwa upande wake amewalaumu watu wanaozusha taarifa za vipimo vya daktari kupitia mitandao wakimchafua marehemu kwa taarifa zisizofaa akiwataka kuwa waungwana na kusubiri taarifa rasmi.

Naye Brother Rick ni mmoja kati ya watanzania ambao wamebahatika leo hii kuonana na msanii aliyekuwa amezirai M2tha P na kuishuhudia hali yake, anasema kuwa kwa sasa inaendelea vizuri ametolewa toka katika chumba cha ICU na kuhamishiwa kitanda kingine chumba cha wagonjwa kawaida ZAIDI SIKILIZA HAPA CHINI:
Mwili wa marehemu Albert Mangwea unatarajiwa kuwasili nchini Juni mosi (1 juni 2013) saa 8 adhuhuri na itafanyika mipango kuwawezesha mashabiki, ndugu, jamaa na marafiki kuuaga siku ya jumapili ya tarehe 2 juni 2013 viwanja vya Leaders Club kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 6 mchana.

Majira ya saa 6 mchana siku hiyo ya jumapili msafara utaelekea mkoani Morogoro kwaajili ya mazishi yaliyopangwa kufanyika jumatatu ya tarehe 3 mwezi juni 2013 katika eneo la makaburi litakalopangwa.

Tutaendelea kukupa taarifa zaidi endelea kuwa nasi.

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI MHE. EZEKIAH WENJE KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014 ILIYOLETA KIZAAZAA BUNGENI LEO

Ezekiel Wenje.

1.0 UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, katika hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika bajeti ya wizara hii mwaka 2012/13, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA ilibaini mapungufu mengi ya kiutendaji na kiuwajibikaji katika wizara hii, na hivyo kuitaka Serikali kufanya mambo yafuatayo ili kuboresha utendaji na ufanisi:

1. Kuziwezesha balozi zetu nje kwa kuzitengea fedha za kutosha  ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi
2. Kutoa idadi ya majengo ya balozi zetu nje (nyumba za mabalozi, nyumba za maafisa wa balozi na ofisi za balozi) kwa mchanganuo wa idadi ya nyumba katika nchi na kama nyumba hizo zina hati miliki au la.

3. Kutoa taarifa ya namna kila ubalozi ulivyotekeleza sera ya Diplomasia ya uchumi kwa kuzingatia kwamba balozi nyingi ziko hoi kifedha kiasi cha kwamba waambata wa kiuchumi wanakosa fedha za kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa ajili ya upelelezi wa masuala ya kiuchumi.

4. Kulikarabati jengo la ubalozi wa Tanzania huko Msumbiji lililokuwa limechakaa kwa kutofanyiwa ukarabati tangu 1975 ingawa jengo hilo tulipewa bure na Serikali ya Msumbiji chini ya FRELIMO.

5. Kujenga kitega uchumi katika kiwanja  cha Tanzania kilichopo Dubai na kukiendeleza kiwanja namba 19 tulichopewa bure na Serikali ya Uingereza kilichopo Uingereza (Central London) ambavyo vimekuwa maficho ya wezi kwa kutoendelezwa kwa muda mrefu na kusababisha Serikali za nchi hizo kutaka kutaifisha viwanja hivyo.

6. Kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma za balozi zetu nchini China, na Uingereza kutoa hati za kusafiria kwa mataifa mengine hasa ya Afrika Magharibi ili kubaini ukweli na kuliondolea taifa aibu kutokana na tuhuma hizi.

7. Kukarabati jengo la ubalozi wetu nchini China ambalo lilikuwa na nyufa na kuvuja nyakati za mvua, na kununua samani  na vifaa vya ofisi kama mashine za nukushi na za kurudufu ambazo zilikuwa hazipo,

8. Kununua magari mapya ya ofisi ya ubalozi wetu nchini China kwa kuwa  magari matatu yaliyokuwepoyalikuwa yameshapitiliza muda wa miaka 10 ambao kwa mujibu wa sheria za China hayapaswi kutumika tena,

9. Kupeleka mwambata wa kiuchumi (economic attaché)  nchini China ili kufuatilia fursa mbalimbali za kiuchumi katika kutekeleza diplomasia ya uchumi kutokana na mahusiano makubwa ya kibiashara  kati ya nchi yetu  na China

10. Kuwawekea zuio wahusika wa kashfa ya rada kuwa viongozi wa shughuli za kiserekali ili walau kuonesha uwajibikaji wa kimaadili (moral accountability) baada ya kushindwa kuwawajibisha kisheria, ili kuondoa dhana iliyojengeka miongoni mwa jamii kwamba dola imetekwa na mafisadi.

11. Kuchunguza na kuwachukulia hatua watanzania (wafanyabiashara na wanasiasa) waliotorosha kiasi kikubwa cha fedha za nchi yetu (zaidi ya shilingi bilioni 315) na kuzificha katika mabenki ya uswisi

12. Kutoa mchanganuo wa jinsi fedha za rushwa ya rada (chenji ya rada) zilivyotumika

13. Kueleza bayana faida za kiuchumi tunazopata kama taifa kwa kushirikiana na jumuiya mbalimbali za kimataifa ili kuthibitisha kwamba mashirikiano hayo hayatumiki kupora rasilimali za nchi yetu kwa hila ya “uwekezaji”

Mheshimiwa Spika, kabla sijajielekeza kwenye mambo mahsusi kwa kipindi hiki cha bajeti ya 2013/2014, napenda kuchukua nafasi hii kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA, kuitaka Serikali kutoa majibu mbele ya Bunge hili tukufu, kwamba imetekeleza kwa kiwango gani masuala yaliyoorodheshwa hapo juu, tuliyoitaka iyatekeleze (moja baada ya jingine) kwa mwaka wa fedha unaomalizika wa 2012/2013?


1.1 Upotevu wa Fedha za Safari za Rais, Shilingi bilioni 3.5

Mheshimiwa Spika, katika hotuba yangu ya mwaka 2012/2013 nilihoji kuhusu serikali Kuchunguza na kuchukua hatua kwa waliohusika na upotevu wa shilingi bilioni 3.5 kwa ajili ya safari “hewa” za Rais nje ya nchi, ili waweze kubainika na kuchukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria zetu.

Mheshimiwa Spika, fedha hizi ni nyingi sana na hasa  ikikukumbukwa kuwa mwaka jana 2012 wapo mawaziri ambao walichukuliwa hatua na Bunge hili kutokana na upotevu ama madhaifu yaliyofanyika kwenye wizara zao, wapo ambao walihukumiwa kutokana na kupotea kwa Twiga kwenye wizara zao, wapo waliohukumiwa kutokana na udhaifu katika kusimamia wizara zao na taasisi zilizoko chini yao. 

Kambi rasmi ya upinzani, inahoji iweje leo waziri aliyeshindwa kusimamia wizara yake na kusababisha upotevu wa fedha hizi mpaka leo bado yupo, wakati wapo mawaziri wengine walioshughulikiwa kutokana na udhaifu walioonyesha kwenye kusimamia wizara zao, au ndio kusema kuwa Serikali hii ya CCM inafanya upendeleo na kuonea baadhi ya mawaziri na kuwaacha wengine? “This clearly indicates the “double standard” nature of this Government in the performance of its functions”

1.2. Kuanzishwa kwa Ubalozi Mdogo Guangzhou -China

Mheshimiwa Spika, mwaka jana Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilipendekeza kuwa serikali ianzishe ubalozi mdogo katika Jiji la Guangzhou kwa ajili ya kurahisisha biashara kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na wale wa China. Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, inatambua kuwa serikali imelifanyia kazi wazo hili na imeamua kuanzisha ubalozi mdogo katika mji huo ,ila tunataka kujua ni lini ubalozi huu utazinduliwa rasmi, kupata watendaji na vitendea kazi ili uweze kuanza kufanya kazi .

2.0 DIPLOMASIA YA UCHUMI

Mheshimiwa Spika, moja ya matarajio ya ushirikiano wa kimataifa ni kuweza kutafuta, na kunufaika na fursa mbalimbali za kiuchumi zinazoweza kupatikana katika mashirikiano hayo ili kama Taifa, tuweze kujikwamua kiuchumi na kujitegemea.

Mheshimiwa Spika, kinyume na matarajio hayo mazuri, sasa nchi yetu imegeuzwa kuwa kitega uchumi cha nchi zilizoendelea kwa kisingizio cha “ushirikiano wa kimataifa” chini ya mwavuli wa “uwekezaji”. Matokeo ya ushirikiano huu wa kinyonyaji (exploitative relationship) ni kwamba kiwango cha umasikini katika nchi yetu kimeongezeka na hivyo kuifanya nchi yetu kuwa tegemezi zaidi kuliko ilivyokuwa hapo kabla.

Mheshimiwa Spika, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikerwa na unyonyaji na unyanyasaji uliokuwa ukifanywa na wakoloni, hali iliyompelekea kusema maneno yafuatayo:

“Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha, tumepuuzwa kiasi cha kutosha. Unyonge wetu ndiyo uliotufanya tuonewe, tunyonywe na kupuuzwa. Sasa tunataka kufanya mapinduzi”

Mheshimiwa Spika, baada uhuru, Mwalimu akaanzisha siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Ujamaa ulilenga kujenga umoja wa kitaifa  na umoja wa bara la Afrika dhidi ya unyonyaji wa kibeberu, wakati kujitegemea  kulimaanisha kujenga uchumi endelevu ili kulijengea taifa heshima na nguvu ya maamuzi mbele ya mataifa mengine, na kuliepusha taifa na fedheha ya kuombaomba.

Mheshimiwa Spika,  Kambi Rasmi ya Upinzani imesikitishwa sana na kitendo cha Serikali kulidanganya taifa, kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010 kwamba: “Katika kipindi cha miaka mitano 2010 -2015, Serikali ya Chama cha Mapinduzi itatekeleza Sera ya Diplomasia ya Uchumi” wakati Ibara ya 98 (i) ya Ilani hiyohiyo ya CCM inasema kwamba Serikali ya CCM itaendelea kushinikiza nchi tajiri kutekeleza ahadi yao ya kutenga asilimia 0.7 ya pato la taifa la nchi zao kwa ajili ya misaada kwa nchi masikini”.

Mheshimiwa Spika, ikumbukwe kwamba ahadi hii ya asilimia 0.7 ya pato la taifa la nchi tajiri ambayo Serikali ya CCM inakodolea macho ni fedha za walipa kodi wa nchi hizo kama ambavyo wananchi wetu wanavyolipa kodi. Aidha ni aibu kwa Serikali hii ya CCM kuchukua ahadi za wahisani na kuziweka kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM kama ahadi kwa wananchi ili kubembelezea kura.

Mheshimiwa Spika, kutokana na uvivu wa kufikiri na kubuni mbinu za kuikwamua nchi hii na umasikini, Serikali hii ya CCM sasa hivi imeachana kabisa na sera ya kujitegemea, ambayo Mwalimu kupitia Azimio la Arusha alisema kwamba “ … Hakika ni ujinga na upumbavu zaidi kwetu sisi, kufikiri kwamba tutaondokana na umasikini wetu kwa misaada ya fedha kutoka nje kuliko rasilimali zetu wenyewe”

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kulieleza bunge hili, kama inatekeleza Diplomasia ya Uchumi kwa kutegemea ahadi ya misaada ya fedha kutoka kwa wahisani na kama hilo ndio suluhisho la matatizo yanayokumba uchumi wetu kama taifa kwamba tutaweza kuendelea kwa kutegemea hisani na fadhila za wafadhili huku tukishindwa kuzitumia rasilimali zetu kwa ajili ya kujikomboa kiuchumi.

Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani imejiridhisha kwamba kauli mbiu ya ‘Diplomasia ya  Uchumi’ imeendelea kubakia kama ilivyo kauli mbiu ya ‘Kilimo Kwanza’ ambayo imebakia kutamkwa na viongozi bila kuwa na mkakati wa utekelezaji wala vigezo vya kupima kiwango cha utekelezaji wake.

3.0.  VYAMA VYA SIASA NA MISAADA KUTOKA NJE YA NCHI.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa ‘United Nations University’(UNU-WIDER) ya mwezi Aprili 2012 iliyoandaliwa na Aili Mari Tripp ilionyesha kuwa misaada ya wahisani kutoka nje katika mabadiliko ya kisiasa Tanzania ‘Donor Assistance and Political Reform in Tanzania’, inaonyesha kuwa Tanzania imepokea misaada kutoka nje yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 26.85 toka mwaka 1990-2010.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa ripoti hiyo ni kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza kusini mwa jangwa la Sahara kwa kupokea misaada mingi kutoka nje ya nchi na hasa kutoka mataifa ya Ulaya na taasisi za nchi za Uingereza, Marekani, Ujerumani, Uholanzi, Norway, Canada, Sweden, na taasisi kama Benki ya Dunia, IMF ,UNDP ,UNICEF na mengineyo. 

Pamoja na misaada yote hiyo, bado tumeendelea kuwa nchi maskini sana duniani pamoja na kuwa na rasilimali lukuki ambazo tumepewa na Mungu ila tunashindwa kuzitumia kwa manufaa ya watanzania na badala yake tumeendelea kudanganywa na vimisaada vidogo vidogo na kubadilishana na rasilimali zetu kama madini, misitu ,wanyama nk kwa ajili ya misaada hiyo.

Mheshimiwa Spika, pamoja na misaada hiyo kwa serikali hii ya CCM bado vyama vya siasa vimekuwa na mahusiano na baadhi ya vyama vingine vya siasa katika mataifa ya magharibi na vimekuwa vikipokea misaada ya aina mbalimbali kama fedha , nyenzo na mengineyo kadiri ya makubaliano na mirengo ya kiitikadi ya vyama husika.Pamoja na ukweli huo bado vipo vyama vya siasa vinavyopotosha umma kuhusiana na misaada vinayopokea kutoka nje ya nchi na vyama hivi vimekuwa mstari wa mbele kueneza propaganda za uongo kuwa vyenyewe havipokei misaada kutoka nchi za magharibi.

Mheshimiwa Spika, CCM wao ‘wanajiita’ kuwa wapo mrengo wa kijamaa/kikomunisti na wamekuwa wakipokea misaada mingi sana ya fedha na nyenzo kutoka Umoja wa Vyama vya Kikomunisti Ulimwenguni ‘Socialist International’ kutoka katika nchi kama za Ujerumani kupitia SDP ,Uingereza kupitia chama cha Labour,China kupitia chama cha Kikomunist ,Marekani kupitia chama cha Democrats. Pamoja na misaada ya kifedha na kiufundi ambayo CCM imekuwa ikipata kutoka nje wamekuwa hawatangazi hadharani hata mara moja kuhusiana na kiasi ambacho wamekuwa wakipokea na hivyo kila kitu kwao imekuwa ni siri kuu ya viongozi wao.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa chama cha CUF, kutokana na itikadi zake za mrengo wa Kiliberali ambazo miongoni mwa misingi yake mikuu ni pamoja na “kupigania haki za ndoa ya jinsia moja, usagaji na ushoga”. Hii ni kwa mujibu wa tangazo lao kwenye mtandao wao wa umoja wa maliberali ulimwenguni, likiungwa mkono na Waziri wa Haki na Usawa wa Uingereza, Lynn Featherstone kutoka chama cha Liberal Democrats wakati chama hicho([url]www.liberal-international.org[/url])  kilipokuwa kinapitisha azimio la kuruhusu ndoa za jinsia moja kama haki ya mtu mmoja mmoja, wanashirikiana na vyama kama vile LPC ya Canada, Det Radikale Venstre cha Norway, FDP cha Ujerumani, Israel Liberal Group cha Israel,PDS cha Senegal na Liberal Democrats cha Uingereza.

Kutokana na umoja huo, CUF wamekuwa wakipata msaada wa kifedha na nyenzo nyingine mbalimbali kutoka kwa vyama hivyo vya mrengo wa Kiliberali na msaada wa mwisho ni hivi majuzi mwezi Machi 2013 waliposaini makubaliano na chama cha Kiliberali kutoka Norway.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa CHADEMA, wapo kwenye Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia Ulimwenguni (International Democratic Union - IDU). Huu ni umoja wa vyama ambavyo vipo kwenye mrengo wa kati na ambavyo msingi wake mkuu  ni pamoja na kuwa na familia, kama taasisi muhimu katika jamii, ikimaanisha kwamba: “tunapinga vitendo vyote vya ushoga na usagaji”. Tunatetea demokrasia, haki za binadamu na kupambana na ufisadi katika serikali. Vyama wanachama wa umoja huu ni pamoja na Conservative Party cha UK, CPP cha Norway, Republican cha Marekani na vingine vinavyofuata   mrengo huo.

Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya upinzani Bungeni, inavitaka vyama vyote ambavyo vimekuwa na mahusiano na vyama vya nje viweke wazi mikataba yao na malengo ya mahusiano hayo ikiwa ni pamoja na misaada ambayo vimekuwa vikipokea kutoka kwenye nchi hizo .

4.0 MPANGO WA KUJITATHIMINI KIUTAWALA BORA (APRM)

Mheshimiwa Spika, itakumbukwa kuwa mnamo mwezi Januari, 2013 ulifanyika mkutano wa 20 wa wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa ,Ethiopia na ni katika mkutano huo Mhe. Rais Kikwete aliwasilisha taarifa ya nchi yetu kuhusu kujitathimini katika utawala bora kwenye mpango wa nchi zinazojitathimini katika utawala bora (APRM).

Mheshimiwa Spika, baada ya taarifa hiyo (randama uk.15) nchi yetu ilitakiwa kutafutia ufumbuzi changamoto zifuatazo;

i. Migogoro baina ya wakulima na wafugaji
ii. Imani za kishirikiana (uchawi)
iii. Kuhakikisha kuwa manufaa ya kukua kwa uchumi yanawafikia wananchi
iv. Kutoa elimu kwa umma kuhusu mipango na sera za serikali
Mheshimiwa Spika, changamoto hizi ambazo nyingine zinatia aibu taifa letu mbele ya mataifa mengine kama vile sisi kuonekana ni wachawi na hivyo kutakiwa kuchukua hatua dhidi ya uchawi !ni fedheha na aibu kubwa kwa taifa letu .

Aidha , Kambi rasmi ya upinzani Bungeni inataka kujua serikali na wizara imechukua hatua gani mpaka sasa katika kukabiliana na changamoto hizi na hasa tatizo la wakulima na wafugaji na kuhakikisha kuwa manufaa ya kukua kwa uchumi wetu yanawanufaisha wananchi na sio kuwanufaisha baadhi ya viongozi na mafisadi wachache.

5.0 MLIPUKO WA BOMU ARUSHA NA BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA.

Mheshimiwa Spika, mwaka huu tarehe 05 Mei,   Kanisa Katoliki Parokia ya Olasiti  huko Arusha lililipuliwa  kwa bomu.  Tukio hili lilitokea wakati akiwepo balozi wa Vatican Nchini na ambaye ndio alikuwa mgeni wa heshima kwenye tukio la kuzindua Parokia hiyo.

Mheshimiwa Spika, mara baada ya tukio hilo, Balozi wa Vatican nchini aliwasilisha taarifa hiyo kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuonyesha kuwa Tanzania sio nchi salama sana kutembelewa na wageni na kama wakitembelea basi wanapaswa kuchukua tahadhari kubwa kwa kipindi chote watakapokuwa hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, inataka kujua nini kauli ya serikali kuhusiana na tukio hili na hasa kuhusiana na taarifa za hali ya usalama wa nchi yetu na wageni zilizowasilishwa kwenye Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa .

6.0 SAFARI ZA VIONGOZI NJE NA MISAFARA MIKUBWA

Mheshimiwa Spika, tangu mwaka 2011/2012 Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni imekuwa ikihoji suala la misafara ya Viongozi wa kitaifa kuwa mikubwa kutokana na kuambatana na watu wengi ambao wengine wanakuwa hawana hata majukumu ya msingi ya kufanya wakati wa ziara hizo huku wakiliongezea taifa gharama kubwa ya kuwasafirisha na na kulipia malazi yao na starehe zao.

Aidha , tumekuwa tukipendekeza na kushauri kuwa sasa ni wakati muafaka kwa Rais wa nchi kuamua kutuma wasaidizi wake kwenye baadhi ya ziara za nje kama wanavyofanya viongozi wengine wa nchi jirani kama Rais Kagame wa Rwanda na hata Mwai Kibaki,  Rais mstaafu wa Kenya alivyokuwa anafanya akiwa Rais, kwani kwa kufanya hivyo atapunguza msururu wa maafisa na viongozi mbalimbali wa kuambatana naye. Tunashauri tena kuwa rais awe anatuma wasaidizi wake kwenye ziara za kawaida na yeye awe na jukumu la kushiriki kwenye ziara rasmi za kiserikali ‘State Visits’ na mikutano maalum ya Kimataifa kama UN na AU.

Hivyo basi Kambi rasmi ya Upinzani inashauri mambo yafuatayo yafanyike ili kupunguza gharama hizi kubwa za kuwasafirisha viongozi na misafara isiyokuwa na tija kama ifuatavyo;

i. Serikali itengeneze kanuni za kuthibiti idadi ya maafisa na watu ambao watakuwa wakiambatana na Rais kwenye ziara za nje (idadi ya wajumbe kwenye misafara iwe wazi na ijulikane)

ii. Pawepo na kanuni za kuainisha kuwa ni nani watapaswa kupanda ndege daraja la kwanza na wale wenye haki ya kulala kwenye hoteli za daraja la kwanza wajulikane.

6.1. Idara ya Protocol na Mabilioni ya Fedha za Safari za Nje.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2011/2012 fungu 221100 ‘travel out of country’zilitumika shilingi 36,121,942,870.00 kwa ajili ya safari za nje ya nchi kwa viongozi wakuu. Katika mwaka wa fedha uliopita wa 2012/2013 kifungu 1010 ambacho ni kwa ajili ya protocol walitengewa shilingi 8,372,581,824 na fedha ambazo zilikuwa zimepokelewa na wizara mpaka mwezi Februari 2013 zilikuwa jumla ya shilingi 26,081,860,727.16! (randama uk.4)jedwali la 2 na zilitumika kwa ajili ya kugharamia safari za viongozi nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2012/2013 Bunge lilikuwa limetenga na kuidhinisha kiasi cha shilingi 8,372,581,824 kwa ajili ya kifungu hiki cha Protocol ‘travel out of Country’kwa mujibu wa kitabu cha matumizi ya kawaida juzuu ya pili (volume II). Jambo  la kushangaza ni kwamba, wizara iliieleza kamati na Bunge hili kuwa walishatumia zaidi ya bilioni 26.081 kutokana na fedha walizokuwa wamejitengea wenyewe wizara ambazo hazikuidhinishwa na Bunge kiasi cha bilioni 29.404

Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA, inataka maelezo ya kina kuhusiana na mamlaka ya wizara hii kwenda kutenga na kutumia fedha nyingi kuliko zilizokuwa zimeidhinishwa na Bunge hili na zilikuwa fedha kwa ajili ya safari za kwenda nje ya nchi, ni nani aliipa wizara mamlaka hiyo na kiburi hicho kiasi cha kupuuza maamuzi ya Bunge hili tukufu.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka huu wa fedha 2013/2014 kitengo hiki cha Protocol kimetengewa jumla ya shilingi 15,155,377,400.00 kwa ajili ya matumizi mengineyo ,ambazo katika mchanganuo wake kwenye kifungu 1010 kifungu kidogo cha 221100 ‘travel out of Country’ zimetengwa shilingi 9,381,328,850.00 kwa ajili ya kugharamia safari za kikazi za viongozi wa Kitaifa nje ya nchi.

Aidha, katika kifungu kidogo cha 220700 ‘rental expenses’ zimeombwa jumla ya shilingi 2,925,445,000.00 kwa ajili ya kukodisha ndege ,magari na kumbi za mikutano kwa ajili ya viongozi wa kitaifa.

Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, haikubaliani na kamwe haitakubaliana na ufujaji huu wa fedha za walipakodi maskini wa Tanzania . Tunamtaka waziri atoe maelezo ya kina kwa watanzania ni kwanini nchi maskini kama yetu tutumie fedha nyingi kiasi hicho kwa ajili ya safari za viongozi nje ya nchi? Aidha , hatukubaliani na kitendo cha kutenga fedha kwa ajili ya kukodi ndege  wakati  Rais ana ndege yake ambayo ilinunuliwa na mabilioni ya fedha za watanzania. 

Ikumbukwe kwamba ndege hii ya Rais ilinunuliwa kwa mbwembwe nyingi kiasi kwamba Waziri wa Fedha wa wakati huo Ndugu Bazili Mramba alisema watanzania wafunge mkanda, hata kama watakula majani, lazima ndege ya Rais inunuliwe. Watanzania hawa wamekula majani sasa kiasi cha kutosha, bado tena Serikali inaendelea kuwanyonya ili ipate pesa za kukodisha ndege wakati Rais ana ndege? Hivi Serikali sasa inataka watanzania wale mawe ndio ijue kwamba watu wamefunga mkanda kiasi cha kutosha?

6.2 Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje

Mheshimiwa Spika, mwaka 2012 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama, ilifanya ziara kwenye balozi takribani zote na iliona matatizo yanayozikumba balozi zetu huko na ilikuwa matumaini yetu kuwa baada, ya ziara ile ya kamati ingehakikisha kuwa fedha zinaongezwa kwenye wizara hii na hasa kwenye fungu la maendeleo ili tuweze kuboresha mazingira ya balozi zetu. Kinyume na matumaini hayo, ni kwamba hakuna jitihada zilizofanyika kuongoeza bajeti ya wizara hasa katika fedha za maeendeleo.

Mheshimimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inaitaka kamati ya Bunge ya Ulinzi na usalama, kuishinikiza Serikali ili kuhakikisha kuwa katika mwaka huu wa fedha wizara hii inaongezewa fedha kwa ajili ya kuboresha mazingira ya balozi zetu , na hiyo ndio njia pekee ya kuonyesha kuwa kamati haikuenda kufanya utalii bali ilienda kuona matatizo ya balozi zetu na kuchukua hatua.

7.0 UFISADI KATIKA UNUNUZI WA JENGO LA OFISI NA MAKAZI KATIKA UBALOZI WA TANZANIA JIJINI PARIS – UFARANSA.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka huu wa fedha kwa mujibu wa randama ya wizara ni kuwa mwaka huu wa fedha kiasi cha shilingi bilioni 28 (28,000,000,000.00) zimepangwa kwa ajili ya matumizi ya maendeleo na kati ya hizo kiasi cha shilingi bilioni 24 na milioni 188 (24,188,000,000.00) ni kwa ajili ya ununuzi wa jengo la ofisi na makazi ya balozi jijini Paris ,Ufaransa (randama uk 25) na kiasi cha shilingi bilioni 3 na milioni 812 (3,812,000,000.00) ni kwa ajili ya gharama za ukarabati wa majengo ya ofisi na makazi yaliyopo Ubalozi wa Tanzania Maputo,Msumbiji. 

Mheshimiwa Spika, ukisoma randama ya wizara (uk.120) katika kasma 6391 ,kifungu kidogo 411100 kiasi cha fedha kilichoombwa ni shilingi bilioni 23 na milioni 900 (23,900,000,000) kwa ajili ya ununuzi wa jengo la ofisi na makazi ya Balozi jijini Paris, Ufaransa na shilingi bilioni 3 namilioni 700 (3,700,000,000.00) kinaombwa kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya ofisi na makazi yaliyopo ubalozi wa Tanzania Maputo,Msumbiji.

Hata hivyo, katika mwaka huu wa fedha 2013/2014 kwenye kasma 6391 katika fungu la Maendeleo (randama uk.120) wizara inaomba kutengewa kiasi cha shilingi milioni 400 (400,000,000.00) (kifungu 221100 ) fedha ambazo hazipo kwenye kitabu cha matumizi ya kawaida juzuu ya pili (volume II) kwa ajili ya posho ya kujikimu na gharama za usafiri kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Wizara, miradi yenyewe ni miwili mmoja wa kununua nyumba Ufaransa na kukarabati jengo Msumbiji.

Mheshimiwa Spika, mkanganyiko huu wa kimahesabu unatia mashaka makubwa sana kuhusiana na dhamira ya serikali na wizara hii hasa fedha zinapotengwa bila kufuata utaratibu wa kibajeti na bila kuingizwa kwenye vitabu vya fedha na mafungu husika.

Kambi rasmi ya Upinzani, inajiuliza tunapitisha mafungu yapi? Kwani kwenye randama fedha zinatofautiana kwenye fungu moja la maendeleo baina ya (ukurasa 25 na 120) , vilevile kwenye kitabu cha matumizi ya kawaida hali ni tofauti kwenye fungu la travel out of the Country kwani sasa wizara imejiongezea shilingi milioni mia nne kwa ajili ya kufuatilia miradi miwili ambayo ni kununua jengo Paris na kukarabati Jengo la ubalozi - Maputo,Msumbiji.

Mheshimiwa Spika, utata wa fedha unaendelea kuonekana kwenye randama ya wizara katika kiambatanisho Na.1 ‘utekelezaji wa ushauri na mapendekezo ya kamati ya kudumu ya Bunge ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa’ katika ushauri/mapendekezo Na.5 kamati iliitaka ‘Wizara itoe mchanganuo wa matumizi ya fedha za bajeti ya maendeleo zilizopokelewa kutoka hazina katika mwaka wa fedha 2012/13’

Maelezo ya wizara yalikuwa kama ifuatavyo; nanukuu randama ya wizara “katika mwaka wa fedha 2012/2013 ,hadi kufikia mwezi Machi ,2013 wizara imepokea kutoka Hazina kiasi cha shilingi 13,261,281,600.00 ambapo kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi 9,660,000,000.00 zimetumika kwa ajili ya kulipia malipo ya awali ya ununuzi wa Jengo la Ofisi na Makazi ya Balozi Paris,Ufaransa;shilingi 995,930,000.00 zimetumika kwa ajili ya ukarabati wa jengo la serikali lililopo Maputo,Msumbiji ;shilingi 626,899,155.00 zimetumika kwa ajili ya ukomboaji wa vifaa vya ujenzi bandarini vilivyotumika katika ujenzi wa kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere na safari ya kikazi ya wataalam katika balozi za Maputo,Pretoria na Lusaka kwa ajili ya kazi ya upembuzi yakinifu wa miradi ya maendeleo iliyopo katika Balozi hizo; na shilingi 1,978,452,485.20 bado hazijatumika na zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya kulipia gharama za ukarabati wa jengo la Serikali lililopo Maputo’

Mheshimiwa Spika, baada ya kufuatilia na kufanya tathimini ya kina kuhusiana na majibu hayo ya wizara kuhusu fedha za maendeleo kwa ajili ya ukarabati wa Jengo la Maputo na kununua Jengo la Ofisi na Makazi ya Balozi Ufaransa na kukuta kuwa ni fedha nyingi sana kuliko uhalisia wenyewe , kwa mfano waziri anataka Bunge na taifa tuamini kuwa kufanya ukarabati wa jengo moja la ofisi Maputo Msumbiji tunahitaji kutumia kiasi cha shilingi 4,695,930,000.00 kwa kutumia fedha inayoombwa mwaka huu wa fedha na zile ambazo tayari zilishalipwa katika mwaka wa fedha wa 2012/2013. 

Aidha wakati wizara inawasilisha majibu yake kwenye kamati ya kudumu ya Bunge walisema kuwa (swali 12 uk.5) ‘kiasi cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya Serikali yaliyopo Maputo ni shilingi 3,812,000,000.00……kiasi hicho cha fedha kinatosheleza kukamilisha kazi ya ukarabati wa majengo hayo ya Serikali yaliyopo Maputo, Msumbiji’

Aidha, kununua jengo moja la ofisi na makazi katika Jiji la Paris Ufaransa tunahitaji kutumia kiasi cha shilingi bilioni 33 na milioni 560 33,560,000,000.00.

Mheshimiwa Spika, kwa majibu haya ya wizara ni kuwa tayari wizara imeshafanya malipo ya shilingi bilioni 9.66 kama malipo ya awali kwa ajili ya ununuzi wa jengo la ofisi na makazi huko Paris Ufaransa , na kuwa tayari tumeshafanya malipo ya awali kiasi cha shilingi milioni 995.930 kwa ajili ya ukarabati wa jengo la ubalozi huko Maputo,Msumbiji.

Mheshimiwa Spika, hakika kiasi hiki ni kikubwa kupitiliza na hata utafiti na tathimini ambayo ilifanywa na Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni ilionyesha kuwa kununua jengo la ofisi katika jiji la Paris kwenye mji wa bei ghali kama Co’te d’Azur (most expensive area in Paris) huwezi kutumia fedha nyingi kiasi hicho kwa ajili ya manunuzi ya jengo la ofisi na makazi.

Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni tunakumbuka sakata la ununuzi wa jengo la ubalozi lililomkumba balozi Prof.Mahalu huko Roma - Italia na yaliyofuatia mpaka kesi na fedha zetu tulizoambiwa kuwa zimepotea hazikuweza kurejeshwa baada ya Prof.Mahalu kushinda kesi hiyo mahakamani.

Hivyo basi, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inataka kupata majibu kuhusiana na mambo yafuatayo;

i. Ni eneo gani ambalo tumepata jengo la kununua kwa ajili ya ubalozi na makazi ya balozi huko Paris, Ufaransa, na ni nyumba ya aina gani .

ii. Je, Serikali inaweza kuonyesha mkataba wa manunuzi wa nyumba hizo (Paris) kwa Bunge na tutalipa kiasi gani kununua jengo hilo?

iii. Ni nani au wakala gani wa serikali aliyefanya tathimini ya hayo majengo na kuamua kuwa tulipe kiasi hicho cha fedha?
iv. Ni kampuni gani iliyohusika katika kufanya makubaliano ya mauziano ya nyumba hizo na tunawalipa kamisheni ya shilingi ngapi?

v. Nani, aliidhinisha kutumika kwa kiasi kikubwa hivyo kwa ajili ya kununua jengo la Ubalozi na makazi huko Paris, je Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, ilishirikishwa katika manunuzi haya?

vi. Ukarabati unaofanywa kwenye jengo la Maputo Msumbiji ni wa aina gani, au tunajenga upya nyumba hizo?
vii. Ni kampuni gani ya ujenzi inayofanya ukarabati wa jengo letu huko Msumbiji na mkataba wa ukarabati huo uko wapi, tungetaka uwekwe hadharani.

Aidha , kambi rasmi ya Upinzani Bungeni , inatoa hoja ya kumtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya uchunguzi maalum (Special Audit) kuhusiana na ununuzi wa majengo haya na ukarabati unaofanyika kwenye jengo letu huko Maputo, Msumbiji, na kuona kama thamani halisi ya fedha imezingatiwa , na kama sheria ya manunuzi ya umma imefuatwa kikamilifu.

Mheshimiwa Spika, Vile vile, tungetaka sehemu ya fedha hizi zitumike kwa ajili ya kukarabati jengo letu la zamani la ubalozi lililopo Washngton ambalo kwa sasa halitumiki baada ya kutekelezwa kwani likikarabatiwa litaweza kuliongezea taifa mapato kutokana na matumizi ya kibiashara ya jengo hilo.

8.0 MPANGO WA WIZARA WA KUTOA VISA KWENYE BALOZI TU

Mheshimiwa Spika, mpango wa Wizara kutoa visa kwenye balozi tu haukubaliki. Kwa Mujibu wa majibu ya wizara kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa ilionyesha kuwa ili wizara iweze kukusanya fedha za kutosha kwenye balozi zetu ni kwa kurudisha utaratibu wa utoaji wa viza kufanywa na Balozi zetu tofauti na utaratibu unaotumika hivi sasa ambapo wageni huweza kupatiwa viza pindi wanapowasili katika vituo vya kuingilia nchini (viza on arrival).

Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, haikubaliani na wazo hili la wizara kwani badala ya kuongeza wageni kuja nchini litapunguza sana hasa ikizingatiwa kuwa ni nchi chache sana ambako tuna ofisi za Balozi na pia kuna nchi nyingine kama Marekani ambapo, kama mgeni yupo Carlifonia na anataka kusafiri kuja Tanzania atalazimika kwanza kusafiri kwenda Washington ambako ndiko kwenye ubalozi atafute visa na ndipo aweze kuja nchini.  Utaratibu huu utaongeza gharama kubwa za usafiri kwa wageni na watalii na hivyo kulipotezea taifa mapato yataokanayo na utalii kwani wageni watapungua.

Aidha, tunaikumbusha wizara kuhusiana na Itifaki ya kuwa na“Single Tourist Destination Protocol” na uwepo wa hati ya kusafiria na visa moja ya utalii “Single Tourist Visas” kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, hivyo kama sisi tukifanya huo uamuzi basi wenzetu Kenya wataendelea kupata wageni wengi zaidi kutokana na visa ya pamoja na wageni wataingia Tanzania kutokana na visa za Kenya chini ya Itifaki hiyo.

8.1 Mkutano wa Mabalozi wa Mwaka 2013/2014

Mheshimiwa Spika, wizara inahitaji kiasi cha shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kufanikisha mkutano wa mabalozi kwa mwaka wa fedha 2013/2014 , na wizara iliwasilisha maombi ya fedha hizo Hazina kama sehemu ya kipaumbele lakini hazikuweza kupatikana .

Kambi rasmi ya upinzani Bungeni, inaitaka serikali kuiondoa aibu hii na kutenga hizo fedha kwa ajili ya kufanikisha mkutano huo na tunapendekeza kuwa katika fungu la protocol safari za nje ndipo fedha hizo zipunguzwe na kutumika kwa ajili ya mkutano wa mabalozi wetu ili waweze kupeana ushauri na uzoefu,ili kuboresha ufanisi wa majukumu yao.

8.2 Utaratibu wa Kupeleka Fedha kwenye Balozi

Mheshimiwa Spika, kutokana na utaratibu wa kupeleka fedha kwenye balozi zetu kuwa na mlolongo mrefu wa kwanza kutoka Hazina na kupelekwa Wizarani, ndipo wizara isambaze fedha hizo kwenye balozi zetu mbalimbali umesababisha fedha kuchelewa kufikishwa kwa wakati kwenye balozi zetu na hivyo kusababisha usumbufu mkubwa na ucheleweshaji wa kazi kwenye balozi zetu.

Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, inaitaka serikali kubadilisha utaratibu huu na hazina iwe inapeleka fedha hizo moja kwa moja kwenye balozi husika badala ya kuzipitisha wizarani kama ilivyofanya kwenye fedha za Halimashauri mbalimbali nchini ili kupunguza usumbufu huo.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo kwa niaba ya kambi rasmi ya Upinzani naomba kuwasilisha.

________________________________
Ezekiah Dibogo Wenje
MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI NA WAZIRI KIVULI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

ERICK SHIGONGO AUNGANA NA WADAU WENGINE KUSHIRIKI UZINDUZI WA FLORA SHOW MWANZA

Mjasiliamali ambaye pia ni mkurugenzi wa Global publishers Bw. Erick Shigongo akizungumza na wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa kipindi kipya cha televisheni kiitwacho Flora Show ambacho kitaanza kuruka hivi karibuni Star Tv. 

Meneja wa TBL Mwanza Mr. Mbwambo (katikati) akiwa na meneja wa matukio wa kampuni hiyo tawi la Mwanza Mr. Erick (kulia) wakiwakilisha jambo ndani ya uzinduzi huo.

Sasa ni zamu ya Airtel Mwanza.......

Mwanamama huyu kutoka Shinyanga amevunja rekodi kwa kuwa moja kati ya watu waliotunza kucha zao kwa miaka muda mrefu bila kuzikata. Guinness Book mko wapi?

 Si za bandia bali zimefugwa, na ni takribani miaka mitatu sasa hazijakatwa.

Kwa karibu zaidi...

Wadau mbalimbali katika meza zao wakifurahia jambo.


Flora akimtambulisha Jontwa moja kati ya wabunifu ambao wataonekana ndani ya moja ya vipindi vya Flora Show vitakavyoruka Star Tv.

Engo na flash kwa blog.
Ni kwa takribani miongo mingi sasa masuala ya urembo, mitindo na ubunifu yamekuwa yakienda sambamba mkono kwa mkono na televisheni.

Iwe ni zama za vipindi vya televisheni za Black and White au sasa zama za kidigitali.

Imekuwa ni ada mara kwa mara, baada ya misoto ya shughuli mbalimbali za mwanadamu, mwisho wa siku mamilioni kati yao huketi chini na kujiburudisha na vipindi vya mitindo na ubunifu vilivyoandaliwa kutoa elimu ya masuala ya urembo na utanashati.

Face book

StorizZ.

Paul Mabuga akitoa uzoefu wake katika masuala ya digitali na utoaji taarifa.

Kipindi cha Flora Show kimekuja katika zama hizi ili kwenda sambamba na mahitaji ya watu kwa kukidhi mahitaji ya Televisheni  ambazo kiukweli zimekuwa kichocheo namba moja katika kusaidia ukuaji wa sekta za mitindo na ubunifu.

'Sasa pale fanya hivi..." ni kama sehemu ya mazungumzo 

Flora wa Flora Show (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Global Publishers Erick Shigongo (katikati) pamoja na Mr. David (kulia) ambaye ni mme wa Flora. 
Africa beauty centre in year 2010 and 2013 in East and Central Africa realize most of woman and ladies in East Africa concentrate  on External look (beauty) leaving the internal and other beauties a side.

Flora Show will criticall feature External Beauty, Internal beauty latest trends in fashion, art, fine dining and home decoration.

The show will also focus on swahili beauty rituals in which only natural and indigenous herbal flowers and spices are used.