Thursday, January 21, 2010
MWANZA
Thursday, January 21, 2010
MWANZA
Wednesday, January 20, 2010
BANGO
HUKU JESHI LA POLISI LIKIENDELEA NA MSAKO KUBAINI MAJAMBAZI WANAOTUHUMIWA KUVAMIA KISIWA CHA IZINGA NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU 14 NA WENGINE 17 KUJERUHIWA IMEBAINIKA KUWA WATUHUMIWA WAWILI KATI YA WANAOHUSISHWA NA MAUAJI HAYO NI MAOFISA WA JESHI LA POLISI WAILAYANI UKEREWE.
TAARIFA ZA CHINI CHINI TOKA KWA MAJERUHI WALIOLAZWA KTK HOSPITALI YA WILAYA AMBAO WALIPIGWA MKWARA NA OFISA MMOJA WA POLISI KUTOTOA MAELEZO YA INSHU NZIMA ILIVYOKWENDA, WANASEMA WALIWEZA KUBAINI MAOFISA HAO WA JESHI LA POLISI KWA SURA, MAJINA NA HATA MAZUNGUMZO YAO AMBAPO WANADAI HATA MOJA KATI YA SILAHA ZILIZOTUMIKA ILIKUWA MALI YA JESHI LA POLISI NCHINI.
SILAHA HIYO NDIYO ILIYOSABABISHA KUUWA IDADI HIYO KUBWA YA WANANCHI KWA KILE KINACHOELEZWA KUWA NI HARAKATI ZA POLISI HAO KUJIOKOA WASITAMBULIKE BAADA YA KUZIDIWA NGUVU NA WANANCHI.
MKURUGENZI WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI DCI ROBERT MANUMBA BAADA YA KUFANYA UKAGUZI AMESEMA WANAENDELEA KUKUSANYA USHAHIDI NA KUYAFANYIA KAZI MALALAMIKO JUU YA ASKARI WAKE NA LEO HII AFISA HUYO AMEAHIDI KUTOA TAARIFA KAMILI.