HIVI KARIBUNI WAANDISHI WA HABARI JIJINI MWANZA TULIPATA FURSA KUHUDHURIA WORKSHOP YA UKUSANYAJI WA TAARIFA ZA UTENDAJI NA UWAJIBIKAJI AMBAYO ILIFANYIKA CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII WILAYANI SENGEREMA WAANDAAJI WAKIWA MWANZA POLICY INITIATIVE(MPI). WADAU WA HABARI SENGEREMA PAMOJA NA NGO MBALIMBALI NAO WALISHIRIKI.
TULITEMBELEA OFISI ZA HALMASHAURI YA WILAYA YA SENGEREMA KUKICHAMBUA KIPENGELE CHA 'UTAWALA BORA NA UTENDAJI' JIBU BAADA YA MAKUSANYO LIKAWA:- KUNA UGUMU KWA MADIWANI KUSIMAMIA KIKAMILIFU UTENDAJI HASA KUZUIA UBADHILIFU KWASABABU HAWAPATI MUDA WA KUTOSHA KUSOMA BAJETI NZIMA NA KUIELEWA KABLA YA KUPITISHWA.
MRADI WA BARABARA YA SENGEREMA MOJA KATI YA MIRADI YA KUJIVUNIA KWA WAKAZI WAKE.
MTAALAM KUTOKA TANROAD AKIPATA VIPIMO VYAKE.
PAMOJA NA UJENZI HUO KUWA NA MANUFAA KWA MAENDELEO YA NCHI UPANUZI HUO WA BARABARA UMEWAATHIRI WAMILIKI WA MAJENGO PEMBENI MWA BARABARA KWANI MAJENGO MENGI YAMEBOMOLEWA KUPISHA UJENZI KAMA INAVYOONEKANA PICHANI MOJA KATI YA KIOTA TEGEMEO KWA BURUDANI KILICHOPIGWA CHINI.
MWISHO WA WORKSHOP YETU AMBAYO ILILENGA KATIKA KUJIFUNZA UFUATILIAJI WA TAARIFA ZA MIPANGO, MAPATO NA MATUMIZI(BAJETI) NA KUZIFANYIA KAZI, KWA UPANDE WA WILAYA YA SENGEREMA ILIGUNDULIKA KUWA MIRADI INAYOTEKELEZWA NA TASAF KWA USIMAMIZI WA WANANCHI INAONEKANA KUWA NA UBORA ZAIDI KULIKO MIRADI KAMA HIYO INAYOTEKELEZWA NA HALMASHAURI CHINI YA USIMAMIZI WA WATAALAM WAKE WENYE TAALUMA YA UHANDISI.
HII INAONYESHA KUWA BAADHI YA WATUMISHI WA HALMASHAURI SI WAADILIFU KTK MATUMIZI YA FEDHA ZA UMMA.
MFANO.SHULE YA MSINGI ISABAGENI,SHULE YA MSINGI MNADANI
SHULE HIZI ZIMEJENGWA CHINI YA UFADHILI WA TASAF NA UBORA WAKE UNAONEKANA DHAHIRI TOFAUTI NA UJENZI WA SOKO KUU LA SENGEREMA LILILOJENGWA CHINI YA KIWANGO HATA IKAAMULIWA KUBOMOLEWA NA KAZI KUPEWA MKANDARASI MWINGINE.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.