ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 9, 2018

TID AFUNGUKA JUU YA WAUWAJI.


TID amekataa Kabisa kuitwa mkongwe kwenye Game ya mziki Bongo akidai kuwa wanafanya hivyo ili kuwashusha wao na kuwapandisha wasanii wao wasiojua.!

IFIKAPO JULY MOSI 2018 SERIKALI KUPIGA STOP MATUMIZI YA KARATASI KWA BAADHI YA TAASISI ZAKE.

 Ng'wananyamate Mgengeli  Mtaalam Mshauri  kutoka mradi wa PS3, akichangia mada wakati wa mafunzo ya maofisa Manunuzi kuhusu mfumo wa Epicor 10.2 yaliyofanyika katika ukumbi wa Victoria Palace jijini Mwanza 
(Picha na Atley Kuni- OR TAMISEMI)
 Baadhi ya Maafisa Manunuzi wakimsikiliza kwa makini, mwezeshaji Stanslaus Msenga hayupo pichani wakati wa mafunzo jijini Mwanza 
(Picha na Atley Kuni OR TAMISEMI)
Stanslaus Msenga, Mhasibu Mwezeshaji akitoa somo kwa Maafisa Ugavi wa Halmashauri za Mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera, Geita, Tabora na Simiyu wakati wa Semina ya mfumo wa Epicor 10.2 jijini Mwanza 
(Picha na Atley Kuni- OR TAMISEMI) 

“LPO” za Makaratasi sasa Basi
Na. Atley Kuni- OR TAMISEMI
Wataalam wakufunzi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa wamesema mikataba ya manunuzi (Local Purchasing Order LPO), itafikia ukomo mara baada ya kuanza kutumika kwa mfumo wa uhasibu na uaandaji hesabu za serikali (Epicor 10.2) ifikapo 01 Julai, 2018.

Akizungumza wakati wa mahojiano maalum Mhasibu mwezeshaji Melkizedeck Kimaro kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, wakati wa mafunzo ya maOfisa manunuzi yanayo washirikisha maOfisa kutoka Halmashauri za mikoa ya Mwanza, Simiyu, Tabora, Mara, Geita na Kagera alisema serikali katika kurahisisha utendaji kazi na kuondokana na matumizi ya karatasi kuanzia Mwezi Julai, 2018 taratibu zote za manunuzi zitakuwa zikifanyika kwa kutumia mfumo.

“Lengo la Serikali ni kuondokana na LPO za Makaratasi ndio maana unaona hivi sasa maOfisa manunuzi wanapatiwa mafunzo, kabla ya hapa mpango wa manunuzi ulitumia karatasi nyingi ambazo kwa kiasi fulani zilikuwa hazina umadhubuti katika uhifadhi wake lakini pia kukosewa kosewa kwa makaratasi na kuwafanya kutumia makaratasi mengi” anasema Kimaro.

Kimaro amesema kuwa katika mfumo wa Epicor 10.2 itasaidia pia suala la udhibiti wa vifungu, ambapo kila kifungu kilicho bajetiwa kwa mwaka husika ndicho kitakacho kutumika kufanya manunuzi kwa njia ya kieletroniki na kwamba itamlazimu Ofisa manunuzi kujiridhisha juu ya uwepo wa fedha katika fungu husika kabla yakuanza kwa mchakato wa manunuzi.

“Katika utaratibu wa sasa Ofisa Manunuzi anaweza kufanya mchakato wa manunuzi bila hata kuangalia kama kwenye kifungu husika kinafedha na anapofikia mwisho anapotaka kufanya malipo anajikuta hana fedha katika kifungu, lakini tutakapo anza kutumia Epicor 10.2 suala hilo linakwenda kuondoshwa” alisisitiza Kimaro.

Wataalam hao wanasema katika utaratibu wa sasa, kutamwezesha Ofisa manunuzi, mbali ya kufanya manunuzi vilevile itamwezesha kuupokea mzigo (Receipt entry) aliouagiza kupitia mfumo huo ambao umebuniwa na kusanifiwa na wataalam wa ndani.

Naye Emelda Malima Mkufunzi Mwezeshaji kutoka OR TAMISEMI, yeye anasema kwamba kupitia mfumo wa Epicor 10.2 utawezesha upatikanaji wa taarifa za robo mwaka, nusu mwaka na hata mwaka mzima kwa urahisi na wepesi.

“Kupitia mfumo huu kila jambo linalofanyika, litakuwa linanakiliwa katika mfumo na pindi Ofisa manunuzi anapohitaji taarifa sio lazima kuanza kukusanya makaratasi na kuanza kuyaunganisha ili apate taarifa badala yake kupitia mfumo ataweza kupakua taarifa husika kulingana na mahitaji yake” alifafanua Emelda.

Mfumo huo pia unaelezwa kuwa ni ‘Web Base system’ inayotoa fursa kwa wataalam watumiaji kuweza kufanya kazi zao mahali popote pale walipo tofauti na sasa ambapo katika Epicor 9.5 na zingine zilizotangulia hazikuwa na uwezo huo.

Akizungumzia mafunzo hayo yanayo endelea jijini mwanza, Meneja mradi katika mradi wa PS3 mkoani humo Bw. Pelestian Masai, alisema matokeo ya maboresho ya mfumo yalitokana na mahitaji ya watumiaji kupitia changamoto zilizo kuwepo hapo awali.

“Maboresho ya mifumo ni suala endelevu, kikubwa hapa ni suala la mahitaji (requirements)  kutoka kwa watumiaji, walicho kifanya wasanifu mfumo (Programmers) ni kuangalia changamoto za kimfumo  zilizo kuwa zikitolewa na watumiaji wa mfumo wa Epicor iliyo tangulia (Epicor 9.5) na kuzifanyia kazi kwa kutafuta suluhisho la changamoto hizo, na matokeo yake ndio maboresho yanayo onekana katika Epicor 10.2 kwa hiyo Epicor 10.2 ni zao la watumiaji wenyewe” amenukuliwa Masai.

Masai anasema chini ya Mradi wa PS3 ambao lengo lake mahsusi ni kushirikiana na kuzisaidia halmashauri na serikali kwa ujumla katika kuongeza (kuboresha) urahisi na ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi hasa walio pembezoni, kumekuwa na dhamira ya dhati katika kuboresha mifumo mbalimbali ya kiutendaji ikiwemo Epicor na mifumo mingine iliyo katika halmashauri zetu, ili kuongeza tija na uwajibikaji kwa wananchi wa Tanzania.

“Nadhani wote tunafahamu dhamira ya serikali ya awamu ya tano katika kufanya mageuzi makubwa hususan katika utoaji wa huduma na uwajibikaji kwa wananchi, hatuwezi kuifikia dhamira hiyo ya dhati kama hatuna mifumo imara na madhubuti kama huu wa Epicor 10.2 na mingine mingi, ndio maana Shirika la USAID kupitia Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) wamendelea kutoa ufadhili na ushirikiano wa kina katika kuimarisha mifumo mbalimbali ya utoaji huduma kwa wanachi iliyo katika halmashauri nchini.

Jumla ya maofisa manunuzi 44 kutoka Halmashauri za Mikoa ya Kagera, Geita, Tabora, Mara, Simiyu na wenyeji Mwanza wameshiriki mafunzo hayo ya mfumo wa Epicor 10.2, yanayoendeshwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa Kushirikiana na Serikali ya Marekani kupitia mradi wa kuimarisha mifumo ya Sekta ya umma PS3 kwa muda wa siku 2. 

SAUTI:- TAKUKURU NJOMBE WAANZA KUCHACHAMAA NA MIRADI ILIYOKATALIWA NA MWENGE


GSENGOtV
NJOMBE 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Njombe Imeanza Kufanya Uchunguzi Wa Awali Katika Miradi Saba Ambayo Kiongozi wa Mbio Za Mwenge Alikataa Kuzindua Kwa Madai Ya Kwamba Imekosa Ubora Ikilinganishwa na Thamani Ya Fedha Iliyotumika.

TAARIFA NA AMIRI KILAGALILA 

JEZI YA NIGERIA YAPEWA NAMBA MOJA KWA MVUTO LINAPOKUJA SUALA LA MITUPIO.


Mashabiki mbalimbali wa soka duniani, wamezichagua jezi za Nigeria kuwa namba moja kwa timu zinazoshiriki Kombe la Dunia.

Mashabiki hao kupitia mitandao mbalimbali ukiwemo ule wa Gazeti la Marca la Hispania, wametoa namba moja kwa jezi ya Nigeria kwamba inavutia sana.

Jezi inayofuatia kwa kuvutia ni lie ya Ufaransa ambayo mashabiki wameipa namba mvili na namba tatu imekwenda kwa Croatia.

Ujerumani imeshika nafasi ya nne, tano imekwenda kwa Iceland na ’namba sita ni Mexico.

Hivi karibuni, jezi za Nigeria zilizotengenezwa na Nike, zilinunuliwa kama njugu na kuzua gumzo kubwa.

Friday, June 8, 2018

MWENYEKITI IRINGA KUNYANG’ANYA KADI WANAO VUNJA KANUNI, SHERIA NA KATIBA YA CHAMA




 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Albert Chalamila ametoa onyo kali kwa wana CCM wanaokiuka kanuni na katiba ya chama cha mapinduzi kwa kuanza kampeni za chini kuwania ubunge na udiwani katika majimbo matatu ya wilaya ya Mufindi akisema wanakwenda kinyume na kanuni za uongozi na maadili.
Baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) wa wilaya ya Mufindi wakimusikiliza kwa umakini mkubwa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Albert Chalamila wakati wa ziara yake ya kwanza ya kikazi 
Baadhi ya wanahabari wa mkoa wa Iringa wakiwa kazini kupata habari kutoka kwa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Albert Chalamila
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Albert Chalamila akipokelewa na green gard wa wilaya ya Mufindi na kupewa heshima anayostahili
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Albert Chalamila akivishwa skafu nagreen gard wa wilaya ya Mufindi 

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Albert Chalamila ametoa onyo kali kwa wana CCM wanaokiuka kanuni na katiba ya chama cha mapinduzi kwa kuanza kampeni za chini kuwania ubunge na udiwani katika majimbo matatu ya wilaya ya Mufindi akisema wanakwenda kinyume na kanuni za uongozi na maadili.

Akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM ya wilaya hiyo mjini Mafinga,Chalamila alisema kuwa amesikia kuwa kuna wanachama wameanza kupita pita kuanza kufanya kampeni za chini chini na kusababisha wapunge wa majimbo hayo kutofanya kazi zao kwa ufanisi. 

Chalamila aliyataja Majimbo ambayo wananchama hao hao wameanza kupita ni jimbo Mafinga Mji linaloongozwa na Mbunge Cosato Chumi, jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamudu Mgimwa na Mufindi Kusini Meldrad Kigolla.

Alisema kuwa anafanyakazi kwa ukaribu na vyombo ya usalama wa taifa ili kupata taarifa ambazo ni sahihi na kuwabaini baadhi ya wana CCM walioanza kujitengenezea mazingira kwa ajili ya kupata uteuzi katika uchaguzi mkuu ujao kinyume na kanuni hizo za chama.
  
Chalamila aliwataka viongozi waliochaguliwa na wananchi kufanya kazi kwa kujituma na kukitendea haki chama cha mapinduzi (CCM) ili kiendelee kuaminiwa na wananchi 

Aidha Chalamila alisema katika mazingira ya kusikitisha alisema wana CCM wengine wanaoshiriki kuhatarisha amani ndani ya chama hicho ni wale waliopewa dhamana ya kuwa wajumbe wa vikao vikubwa vya chama na katika onyo lake kwao aliwatahadharisha dhidi ya hatua zinazoweza kuchukuliwa kwao.

“Waacheni wabunge na madiwani waliopo wafanye kazi, wamalize miaka yao mitano kwa uhuru. Mliwachagua wenyewe, wapeni nafasi na kama mnataka kuamua vinginevyo subirini hadi pazia la uchaguzi litakapofunguliwa lakini sio sasa,” alisema Chalamila.

Mwenyekiti  huyo aliwataka wajumbe  hao,kuhakikisha wanaweka mikakati  ya ushindi katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa kuhakikisha wanazirudisha ndani ya ccm  kata  2 zilizochukuliwa na Chadema katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 wilayani humo.

Chalamila alizungumzia visasi na mioyo ya kinyongo miongoni mwa wana CCM wakati na baada ya chaguzi za chama na jumuiya zake, na za serikali akisema; mambo hayo yamekuwa yakisabisha mpasuko wa muda mrefu ndani ya chama hivyo ni lazima yaachwe.

“Visasi na vinyongo vimevuka mipaka. Wapo pia wana CCM ambao kila kukicha kazi yao ni kuwazushia na kuwachafua wenzao kwamba ni wafuasi wa vyama vingine vya siasa kikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kwamba wana mienendo mibaya ndani ya chama mambo ambayo si ya kweli. Wana CCM tupendane na tutendeane mema,”alisema Chalamila.

Aliwataka wenye taarifa za wanachama wenye mienendo mibaya na inayotishia uhai wa chama waziwasilishe kwa kuzingatia taratibu, kanuni na katiba ya chama ili ziweze kufanyiwa kazi.

Mwenyekiti Chalamila alimalizia kwa kusema kuwa watawanyang’anya kadi wanachama wote ambao watakuwa wanaendelea kuvunja kanuni,sheria na katiba ya chama cha mapinduzi

“Kwakweli nitakuwa mkali sana na nitasimamia vilivyo kwa wale ambao watakuwa wanavunja kanuni,sheria na katiba ya chama cha mapinduzi kwa kuwa madaraka hayo ninayo kwa mujibu wa kanuni na sheria za chama chetu” alisema Chalamila

Baada ya kukutana na halmashauri kuu ya CCM ya wilaya ya Mufindi, Chalamila anatarajiwa pia kukutana na na wajumbe wa vikao hivyo wa wilaya ya Kilolo, Iringa Vijijini na Manispaa ya Iringa katika ziara yake anayofanya akiwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Viti 15 Bara), Theresia Mtewele

SAUTI:- WAKULIMA NJOMBE WALIA NA SOKO LA MAHINDI

NA AMIRI KILAGALILA NJOMBE/WANGING'OMBE
GSENGOtV

Wakulima wa zao la mahindi wilayani wanging'ombe mkoani Njombe wameiomba serikali kuwasaidia kuboresha  na kutafuta soko la zao hilo kutokana na hali ya mavuno iliyopatikana kwa kiasi kikubwa na kuwalazimu kuuza debe moja  kwa sh.3,500/= kutoka 15,000/= ya mwaka juzi na mwaka jana huku wengi wao kuhifadhi katika maghala kwa mda mrefu ili kusubiri soko la zao hilo.

ZANTEL YASITISHA MAUZO YA LAINI ZA SIMU KWA MAWAKALA

Zantel inapenda kuwataarifu wateja wake, wadau na jamii kwa ujumla kuwa imesimamisha mauzo ya laini zake za simu kwa mawakala wake wakuu kuanzia sasa.

Maamuzi haya magumu yamechukuliwa kutokana na tuhuma za kuwepo kwa matumizi kuanzia wa Zantel.

Zantel imedhamiria kuzingatia na kusimamia sheria zote na kanuni zote pamoja na kufuata viwango vya juu vya maadili na kampuni haitavumilia vitendo vyovyote vya udanganyifu kupitia mtandao wake. Tunashirikiana na Mamlaka za serikali kushughulikia tuhuma za makosa haya na tutachukua hatua zote ili kuepusha hatari zaidi katika suala hili.

Zantel inawahakikishia wateja wake kuwa hakuna madhara kwenye huduma zinazotolewa kwao na wateja wanaweza kuendelea kutumia huduma na kununua laini za simu katika maduka ya Zantel na mawakala wake usajili wa laini za Zantel.

Imetolewa na uongozi wa Zanzibar Telecommunications PLC.

SERIKALI YASEMA BARUA WALIOANDIKIWA KKKT NI BATILI.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema barua iliyoandikwa na wizara hiyo na kulitaka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) kuufuta waraka wa Pasaka ni batili.

Dk Nchemba ameyasema hayo Leo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari amesema taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii ni batili na siyo maelekezo ya serikali au wizara.

“Tunawaomba viongozi wa dini waendelee na kazi zao, nasema jamii iwe macho na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya jamii na wasifanyie kazi taarifa hizo,” amesema.

Pia Dk Nchemba amesema amefuatilia barua hizo na kuona zina mkanganyiko wa anuani.

“Viongozi wa dini wasiwe na taharuki na taarifa hizo, hazina baraka za Serikali. Wasisite kuwasiliana na Serikali kujua uhalali wake.” Amesema.

Pia Dk Nchemba amesema waraka wa viongozi wa dini uliotolewa miezi iliyopita ni jambo lililopita na hivyo akawataka viongozi wa dini waendelee na kazi zao.

Dk Nchemba amewataka viongozi wa dini kuendelea na kazi zao. “Nchi yetu ni moja na tunaishi kwa taratibu tulizojiwekea na tuna madhehebu mengi.” Amesema na kuongeza: “Wengine wameliona jambo hilo kama ajenda. Wananchi wawe makini, wasiwafuate watu hao wanaotaka kuwagawa.”

AIRTEL KUENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZAKE KWENDA NA TEKNOLIJIA

 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Airtel Tanzania akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Tanzania Sanjay Rughani wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Airtel kwa wateja na washirika wake jijini Dar es Salaam jana. Kati kati ni Mkurugenzi wa Biashara Airtel Tanzania Rohit Tandon.

 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Airtel Tanzania akimkaribisha moja ya wageni waalikwa wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Airtel kwa wateja na washirika wake jijini Dar es Salaam jana. Kati kati ni Mkurugenzi wa Biashara Airtel Tanzania Rohit Tandon
 Mkurugenzi Mtendaji Airtel Tanzania Sunil Colaso akiongea na wafanya kazi wa kampuni hiyo, wateja na wageni waalikwa wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Airtel kwa wateja na washirika wake jijini Dar es Salaam jana
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Tanzania Sanjay Rughani akiongea na moja ya wageni waalikwa wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Airtel kwa wateja na washirika wake jijini Dar es Salaam jana. Kati kati ni Mkurugenzi Mtendaji Airtel Tanzania Sunil Colaso.
 Mkurugenzi wa Biashara kwa wateja maalum Boniface Bwambo akiongea na wafanya kazi wa kampuni hiyo, wateja na wageni waalikwa wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Airtel kwa wateja na washirika wake jijini Dar es Salaam jana

Airtel yatangaza huduma mpya mbili, yatamba kuendelea kuboresha huduma zake kwendana na teknolojia
Kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania imehaidi kuendelea kutoa huduma bora na za kisasa kwa wateja wake. Hii ni kutatua kero na changamoto ambazo zimekuwa zikiikumba sekta ya mawasiliano hapa nchini.
Akiongea jijini Dar es Salaam jana jioni baada ya futari iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa wateja na washirika wake, Mkurugenzi wa Biashara kwa wateja maalum Airtel Tanzania Boniface Bwambo alisema kampuni hiyo itaendelea kutoa huduma bora na za kisasa ili kukidhi matakwa ya wateja wake pamoja na kuongeza pato kutoka na huduma zake kwenye kipindi hiki ambacho ushindani umekuwa mkubwa kwenye sekta ya mawasiliano.
Bwambo alisema baadhi ya bidhaa mpya zinazotolewa na kampuni hiyo ili kwenda na wakati ni fixed portfolio ambayo huwapa wateja nafasi ya kufurahia huduma ya mtandao ya kasi ya Fiber Solutions, Line Solutions na Co-Location Solutions. Huduma hizi ni suluhisho kwa biashara za mtandaoni, inapatikana kwa gharama nafuu katika vifurushi zinazotolewa na Airtel.
Bwambo alisema hayo wakati wa futari iliyoandaliwa na Airtel Tanzania kwa wateja na washirika wake jijini Dar es Salaam. ‘Mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kipindi muhimu sana kwa waumini wa dini ya Kislam duniani kote. Kwa kutambua umuhimu huo, sisi Airtel tumeona ni Faraja kukutana hapa siku ya leo na kufuturu kwa pamoja. Hii ni moja ya njia nzuri pia kukutana na wateja na kuonyesha tunawajali. Vile vile, kwa kukutana pamoja hapa inatoa fursa ya kuzungumza na kuonyesha baadhi ya bidhaa zetu kwa wateja wetu, aliongeza  Bwambo.
‘Ni furaha sana kuwa nasi zote hapa. Ni furaha zaidi kuweza kutambua kuwa sisi Airtel tunatoa huduma zaidi ya mawasiliano. Kwa kuongea tu ni kwamba wengi wanajua huduma yetu ya Airtel Money ni kutuma na kupokea fedha na kununua au kulipia bidhaa. Lakini vile vile imeenda zaidi kwa kuweza kukusanya mauzo au mapato kwa wateja na kupeleka moja kwa moja kwenye akaunti yake ya benki. Kwa sasa mfanya biashara hana haja ya kutoka kukusanya mauzo ua mapato kwa sisi kupitia Airtel Money tufanya kazi hio na ndio sababu tunasema Airtel Money ni salama na njia nafuu ya kuweka na kutunza fedha. Alisema Bwambo .
Kwenye tukio la futari hiyo alikuwepo pia Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Tanzania Sanjay Rughani. Alipongeza kampuni ya Airtel kwa kutambua umuhimu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na pia kwa kutoa huduma bora na nafuu kwa wateja wake.
 ‘Airtel inafanya vizuri kwa kuboresha huduma zake kila siku ili kwenda na wakati kitu ambacho ni muhimu kwa wateja na washirika wake kama sisi. Kuja kwangu hapa leo kumeweza kunipa na kutambua huduma na bidhaa mpya kutoka Airtel ambazo nilikuwa sina taarifa nazo hapa awali. Hii ni jambo la kupongezwa sana, alisema Rughani.
On her side the Administration and Project Manager of the National Industrial and Commercial (NIC) Bank, MsBadriaLema, said out of enjoying sharing iftar with the Airtel staffs and other people, she gets a chance to know other services offered by the company especially Airtel Money profit distribution.
Kwa upande, Meneja Utawala na miradi wa benki ya NIC Tanzania Badrial Lema alisema ni furaha kubwa kuungana na wafanya kazi wa Airtel Tanzania kushiriki futari ya leo. ‘Nimefurahi sana kukutana na wafanyakazi wa Airtel na wageni wengine waalikwa. Ni tukio la iana yake kwani nimeweza kupata marafiki wapya na kuongeza ufahamu juu ya huduma zinazotolewa na Kampuni ya Airtel Tanzania.

Thursday, June 7, 2018

RIDHIWANI ASEMA 'KIFO CHA SAM WA UKWELI MAUMIVU YAKE NI KAMA MSIBA WA NYUMBANI'

GSENGOtV
Kwenye ukurasa wake wa kijamii Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete ameonesha kuguswa na kifo cha Msanii wa Bongo fleva Sam wa Ukweli, na  kushindwa kujizuia na kuandiaka maneno yafuatayo
“Innallillah Wainnaillah Rajuun, Nadhani sihitaji kusema mengi ila kumshukuru Mungu Mwenyezi kwa mapenzi yake kwetu Binadamu na hasa kwako rafiki yangu Sam “Mwana Wa Ukae, Mzukulu wa Mwali Bonele Wa Kiwangwa”.Tangulia Rafiki Yangu, Pumzika kwa Amani Sam Wa Ukweli.”
Kazi na Ngoma ya Jembe Fm imezungumza na mbunge huyo kujua
1. Habari za msiba alizipata kwa njia gani na akiwa wapi?
2. Alimfahamu vipi marehemu?
3. Jeh marehemu Sam wa Ukweli alikuwa na mchango wowote katika shughuli za maendeleo na siasa za Ridhiwani kwenye jimbo lake?



BREAKING NEWS: WANANCHI 35 WATIWA MBARONI KWA KUCHOMA MOTO GARI LA ABIRA.


GSENGOtV


Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza limewatia mbaroni Wananchi thelathini na watano, kwa tuhuma ya kuliteketeza kwa moto gari la abiria aina ya Isuzu Journey, baada ya gari hilo kumgonga mtoto na kusababisha kifo chake katika eneo la kata ya Bugogwa wilayani Ilemela.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa polisi Ahmed Msangi amemtaja mwanafunzi aliyefariki papo hapo kuwa ni Naomi Opio mwenye umri wa miaka 12 mwanafuzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Kisundi, huku mdogo wake aitwaye Baton Opio mwenye umri wa miaka 9 anayesoma darasa la tatu katika shule hiyo akijeruhiwa kichwani na kuvunjika mkono wa kulia na amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou toure kwa matibabu zaidi.

WATU WATATU KWENDA URUSI KWENYE KOMBE LA DUNIA 2018 KUPITIA PROMOSHENI YA BIA YA KILIMANJARO LAGER

Meneja wa Mawasiliano ya wateja wa TBL, David Tarimo akitoa ufafanuzi wa promosheni ya Kilimanjaro kwa waandishi wa habari,kulia ni Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha,Hamidu Semvua na Raj Chandarana aliyeko kwenye mafunzo chini ya mpango wa Global Management Trainee katika kampuni ya TBL.
Meneja wa Mawasiliano ya wateja wa TBL, David Tarimo na Raj Chandarana kutoka TBL wakijadiliana jambo.
Zoezi la droo ya kupata washindi ikifanyika kupitia teknolojia za kisasa.
Meneja wa Mawasiliano ya wateja wa TBL, David Tarimo akiongea kwa simu na mmoja wa washindi wa droo kupitia promosheni ya bia ya Kilimanjaro.

Na Mwandishi Wetu.

Wakazi wawili wa jijini Dar es Salaam na mmoja wa mkoa wa Geita wameibuka wamejishindia tiketi na kugharamiwa safari ya kwenda, Urusi, kuona michuano ya Kombe la Dunia, mubashara kupitia promosheni inayoendelea ya bia rasmi ya Tanzania, katika msimu huu wa Kombe la Dunia ya Kilimanjaro Lager.

Droo ya kuwapata washindi hao imefanyika jijini Dar e Salaam, chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Taifa na kushuhudiwa na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari. Washindi katika droo hiyo wametajwa kuwa ni Charles John (Geita), Kaijage Kironde (Dar es Salaam) na Leodgard Isaac (Dar es Salaam).

Washindi hao walipokea habari hizo kwa furaha baada ya kupigiwa na Meneja wa Mawasiliano ya wateja wa TBL, David Tarimo,ambapo walieleza kuwa wanaisubiri safari yao kwa shauku kubwa na kuwataka wateja kuendelea kuchangamkia promosheni hiyo ambayo ilizinduliwa mapema mwezi uliopita.

Promosheni hiyo inaenda sambamba na kujishindia muda wa maongezi 2,500/= kila wanaponunua bia ya Kilimanjaro na kushiriki mara (sita) 6 kutuma number iliyopo chini ya kizibo kwenda 15451 fedha taslimu kiasi cha shilingi 1,000,000/- Kila wiki kwa wiki kumi.

Meneja wa Mawasiliano ya Wateja wa TBL, David Tarimo, alisema,  washindi wapatao 10 watawezeshwa kugharamiwa kuona mashindano ya kombe la Dunia na washindi wengi wataweza kujishindia fedha taslimu, na muda wa maongezi. “Lengo kubwa la promosheni hii ni kuwazawadia wateja wetu ili waburudike katika msimu huu wa shamrashamra za kombe la dunia la FIFA 2018”, alisisitiza.

Ili kujishindia zawadi mteja anapaswa kutuma namba zilizopo  kwenye chupa za bia ya Kilimanjaro kwenda namba 15451 ili kujipatia fedha taslimu na muda wa maongezi, zawadi ya tiketi ni kwa wale wataoshiriki kujibu maswali yatakayoendeshwa kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya www.Kililager.com  na kujipatia pointi za ushindi.

Promosheni hii itadumu kwa muda wa miezi miwili na nusu na itaendeshwa nchi nzima na matangazo yake yanaendelea kutangazwa rasmi  kupitia  televisheni, radio na mitandao ya kijamii.

WAVUVI 109 WAKAMATWA KENYA.


Jeshi la majini nchini Kenya limewakamata wavuvi 109 raia wa Tanzania kwa kosa la kufanya shughuli za uvuvi kwenye mipaka ya Kenya katika bahari ya Hindi kinyume na sheria.

Wavuvi hao walikamatwa katika kijiji cha Shimoni kilichopo kusini mwa Kenya karibu na mpaka wa Tanzania na kufikishwa katika mahakama ya Kwale June 3. Aidha wavuvi hao walishindwa kujiwekea dhamana ya zaidi ya shilingi laki nne za kitanzania kwa kila mmoja.

Kwa upande mwingine Mbunge wa Lunga Lunga, Khatibu Mwashetani amewateteta wavuvi hao na kuomba makamu wa rais  wa Kenya Ruto kuingilia sakata hilo ili kuzuia mgogoro wa kidiplomasia unaoweza kutokea.

Na mbunge huyo aliongeza kwa kusema kuwa wavuvi hao ni kama ndugu zao kwa sababu wanashirikiana katika mambo mengi.

ZIMAMOTO NCHINI YAPATA TUZO YA UTENDAJI BORA


 Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia, Wazee na Watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA), Mohamed Shabani (wapili kulia) akimkabidhi Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye tuzo ya cheti cha heshima, kwa mchango wao katika kupambana na majanga ya moto na uokoaji. Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, akionesha zawadi ya fulana ya mabalozi wa Taasisi ya Salama Salimini aliyokabidhiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia, Wazee na Watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA), Mohamed Shabani (kushoto), kama alama ya kutambua mchango wao katika kupambana na majanga ya moto na uokoaji, (kulia) ni balozi wa Salama Salimini Mwinyi Mangara. Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, akifafanua jambo kwa Waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kukabidhiwa tuzo ya cheti cha heshima kutoka kwa Idara ya Jinsia, Wazee na Watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA), kwa mchango wao katika kupambana na majanga ya moto na uokoaji. Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (wa tatu kulia) akiwa na Viongozi Waandamizi wa Jeshi pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia, Wazee na Watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA), Mohamed Shabani (wapili kushoto), (kulia) Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo Billy Mwakatage, (kushoto) Kamishna wa Usalama Dhidi ya moto Jesuald Ikonko na (wapili kulia) ni balozi wa Salama Salimini Mwinyi Mangara. Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)



ZIMAMOTO NCHINI YAPATA TUZO YA UTENDAJI BORA
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limepokea tuzo ya cheti cha heshima kwa kutambua mchango wao katika kupambana na majanga ya moto na uokoaji hapa nchini kutoka katika Taasisi ya Wazalendo na Maendeleo. Tuzo hiyo imepokelewa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo Dar es salaam.

Akizungumza Kamishna Jenerali baada ya kupokea tuzo ya cheti hicho. Alisema, anawashukuru Taasisi hiyo kwa kulipa Jeshi hilo tuzo hiyo kwa kazi nyingi ambazo taasisi hiyo imezifanya kwa kushirikia na Jeshi hilo ikiwepo kampeni ya kuitangaza namba ya simu ya dharura 114.

Kamishna Jenerali Andengenye, amezitaka Taasisi nyingine kushirikiana na Jeshi hilo katika kuzifufua Fire Hydrant zilizo haribika na zilizofukiwa ili kuongeza idadi ya vifaa hivyo ambayo ni msaada mkubwa wakati wa majanga ya moto. ‘‘Jamii ishirikiane na Jeshi letu katika kuvilinda visima hivyo (Fire Hydrant) vilivyopo mitaani kwani ni msaada mkubwa pale majanga ya moto yanapotokea’’.

Ni vema sasa mamlaka zinazoshughulikia miundombinu ya maji safi kwenye miji na majiji ikazingatia wanapotengeneza miundo mbinu hiyo, wakumbuke kuweka na mifumo ya maji ya zimamoto Fire Hydrant, pamoja na kuhakikisha wamiliki wanaojenga majengo makubwa na madogo wanaweka mifumo hiyo ya maji.

Tuna changamoto kubwa kwa upande wa visima hivyo, kwa hiyo kamapeni yetu ya kufufua na kuongeza visima hivyo vitasaidia kuleta tija katika utendaji kazi katika fani yetu. Tunashirikiana na Mamlaka za Maji kuhakikisha miundo mbinu hiyo inarudi na kutoa ushauri pale miradi mipya ya maji inapo jengwa.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania Bw. Muhammad Shaban alisema wamechukua uamuzi huo wa kutoa Tuzo hiyo kutokana na kuona mchango mkubwa wa Jeshi hilo walioutoa katika jamii. Pia amesema wataendea kutoa ushirikiano na Jeshi hilo katika utoaji elimu kwa umma. “Tupo tayari kushirikiana na Jeshi hili kuwaonesha sehemu zote ambazo fire hydrant zilizopo Mkoa wa Dar es salaam.”

“Kampeni ya kufufua fire hydrant imetugusa sana na kuona hatua hiyo ni msaada mkubwa kwa jamii kwani zitasaidia magari ya zimamoto na uokoaji kupata maji eneo la karibu majanga ya moto yanapotokea.”

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA - JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

REFA MKENYA ALIYETEULIWA NA FIFA KUSIMAMIA KOMBE LA DUNIA 'ANASWA NAKAMERA AKIPOKEA RUSHWA'


Takriban maafisa 100 wa kandanda katika eneo la Afrika Magharibi na Kenya walipatikana katika kamera wakipokea fedha katika operesheni kali.

Ni miongoni mwa upelelezi wa miaka miwili uliofanywa na mwandishi wa Ghana mwenye utata Anas Aremeyaw Anas. Kipindi cha BBC Africa Eye kimepata kanda za video za kipekee katika makala yao ya mwisho.

Katika kisa kimoja naibu refa kutoka Kenya anayeelekea Urusi kuchezesha dimba la dunia kutoka Kenya alikubali dola 600 kutoka kwa mtu aliyejifanya kuwa afisa wa shirikisho la soka la Ghana.

Fifa inasema kuwa refa huyo kwa Jina Aden Range Marwa , ambaye ni mmojawapo wa marefa walioteuliwa na Fifa kushiriki katika kombe la dunia nchini Urusi , hataelekea tena Urusi baada ya kupatikana akipokea zawadi ya $600.

Marwa alipewa fedha hizo na mwandishi mpelelezi aliyejifanya kuwa afisa mkuu wa timu moja kuu ya Ghana. Hatahivyo refa huyo amekana kufanya makosa yoyote.

Mwanachama wa baraza la Fifa nchini Ghana Kwesi Nyantakyi , ambaye ndiye afisa wa pili kwa uwezo katika soka ya Afrika , pia alipatikana na operesheni hiyo kali.

Alionekana akipokea $65,000 kutoka kwa mwandishi mpelelezi aliyejifanya kuwa mwekezaji katika soka ya Ghana.

Nyantakyi amekataa kutoa tamko lolote. Kwa jumla zaidi ya marefa 100 na maafisa wakuu walipatikana katika kamera wakichukua fedha kinyume na sheria za Fifa na GFA .

Makala hiyo iliofanywa na mwandishi aliyezua utata Anas Aremayaw Anas imezua maswali makali kuhusu hatma ya mchezo wa kandanda wenye ushabiki mkubwa barani Afrika.

DK TULIA AZUIA WAZIRI MKUU KUJIBU SWALI WARAKA WA KKKT.


CHANZO/MWANANCHI
DODOMA. Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amemkingia kifua Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kujibu swali kuhusu Serikali kulipa siku 10 Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kufuta waraka wake wa Pasaka uliotolewa Machi 24, 2018, ambao mbali na masuala ya kiroho, ulitaja changamoto tatu za kijamii.
Swali kuhusu KKKT iliyoandikiwa barua ya kutakiwa kufuta waraka huo na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, limeulizwa leo Alhamisi Juni 7, 2018 katika kipindi cha Maswali ya papo hapo kwa Waziri Mkuu na mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia.
Katika swali lake, Mbatia ametaka kujua ukweli kuhusu barua hizo lakini baada ya kumaliza kuuliza swali hilo, Dk Tulia amesema haliwezi kujibiwa na kiongozi huyo wa shughuli za Serikali bungeni.
“Kuna barua wamepewa KKKT na TEC (Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ) wakitakiwa kufuta nyaraka zao za Kwaresima,” amesema Mbatia na kuitaka Serikali kueleza uamuzi huo una lengo gani.
Mara baada ya swali hilo, naibu spika huyo amesema, “mtakumbuka mheshimiwa Kubenea (Saed-mbunge wa Ubungo-Chadema) alimuuliza waziri Mkuu swali linalohusu dini na mheshimiwa Spika alizuia suali hilo lisijibiwe.”
Baada ya maelezo hayo, Dk Tulia alimuita mbunge mwingine kuuliza swali huku Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi akiketi na kuzungumza na na wabunge wengine wa vyama vya upinzani chini kwa chini.

KAMA ULIIKOSA PERFOMANCE YA DIAMOND PLATNUMZ KATIKA ONE AFRIKA MUSIC FESTIVAL BASI CHUNGULIA HAPA



Diamond Platnumz Performance at One Africa Music Fest, London 2018

TANZIA:- MSANII WA BONGO FLEVA SAM WA UKWELI HATUNAYE.

Enzi za uhai wake msanii Sam wa Ukweli.

GSENGOtV
Msanii wa Bongo Fleva, Sam wa Ukweli amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Palestina, Sinza jijini Dar baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Chanzo cha kifo chake kimelelezwa na Producer wake Steve kuwa “Sam alianza kuzidiwa toka J’mosi, tulipomuuliza anaumwa nini alisema ukimwi lakini sio ukimwi wa kawaida bali wa kulogwa”

Mwili wa marehemu umepelekwa katika hospitali ya Mwananyamala kuhifadhiwa.


Sam aliwahi Ku-Hit na ngoma zake kama vile Sina Raha, Milele, Kisiki, Ameolewa aliyowashirikisha wakali Z-Anto na Rich Mavoko na nyingine nyingi ambazo licha ya kukubalika majumbani kwa wakubwa na watoto pia alitumika sana katika majukwaa ya kampeni mbalimbali za kijamii, huduma za afya na vilevile majukwaa ya siasa hasa uchaguzi mkuu uliopita ulioiweka madarakani Serikali ya Rais John Pombe Magufuli, ambapo yeye alikisimamia barabara chama hicho kwenye kampeni zake kama picha mbalimbali zinavyoonekana hapa chini.