GSENGOtV
Jeshi la Polisi mkoa wa
Mwanza limewatia mbaroni Wananchi thelathini na watano, kwa tuhuma ya
kuliteketeza kwa moto gari la abiria aina ya Isuzu Journey, baada ya gari hilo
kumgonga mtoto na kusababisha kifo chake katika eneo la kata ya Bugogwa
wilayani Ilemela.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa polisi Ahmed Msangi amemtaja mwanafunzi aliyefariki papo hapo kuwa ni Naomi Opio mwenye umri wa miaka 12 mwanafuzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Kisundi, huku mdogo wake aitwaye Baton Opio mwenye umri wa miaka 9 anayesoma darasa la tatu katika shule hiyo akijeruhiwa kichwani na kuvunjika mkono wa kulia na amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou toure kwa matibabu zaidi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.