Saturday, June 27, 2015
MAMIA WAJITOKEZA VIWANJA VYA LEADERS CLUB JIJINI DAR ES SALAAM KUMUAGA MHARIRI EDSON KAMUKARA
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Mhariri wa Kampuni ya Mwanahalisi, Edson Kamukara wakati ulipowasili viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam leo asubuhi, kwa ajili ya kuagwa. Kamukara alifariki dunia juzi na mazishi yake yanatarajia kufanyika nyumbani kwao Muleba mkoani Kagera. |
Mmoja wa waandishi wa habari akiwa amepoteza fahamu wakati wa kuaga mwili huo. |
Wanahabari na waombolezaji wengine wakiwa wamejipanga foleni wakati wa utoaji wa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Edson Kamukara. |
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwanahalisi, Said Kubenea (katikati), akisaidiwa baada ya kuishiwa nguvu wakati akitoa heshima za mwisho kwa marehemu. |
Wanahabari ni huzuni na vilio. |
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akisalimiana na Mbunge wa Bukoba mjini, Balozi Khamis Kagasheki wakati wa kuuaga mwili wa Edoson Kamukara. |
Wanafamilia ya marehemu wakiwa kwenye shughuli hiyo. |
Sehemu ya umati wa watu katika shughuli hiyo. |
Mwakilishi wa wanafunzi waliosoma na marehemu Shule ya Sekondari ya Majengo, Joachim Mushi akizungumza kabla ya kutoa rambirambi yao ya sh.500,000. |
Viongozi wa serikali na vyama vya siasa wakiwa kwenye shughuli hiyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda. |
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza katika uagaji wa mwili wa marehemu ambapo alipigania waajiri wa vyombo vya habari kutoa mikataba ya ajira kwa wanahabari. |
Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Regnald Mengi akimfariji Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwanahalisi, Said Kubenea alikuwa akifanyakazi marehemu Edson Kamukara. |
Ni vilio tu kwa wanahabari. |
Shughuli ya uagaji ikiendelea. |
Dada ya marehemu Edson Kamukara akitoa heshima za mwisho. |
93.7 JEMBE FM *PAMOJA SANA*
![]() |
*PAMOJA SANA* |
![]() |
Sikiliza 93.7 JEMBE FM MWANZA Popote pale ulimwenguni,. Nenda kwenye play store yako ya simu ya mkononi, download kitufe cha Jembe Fm. Sasa unaweza kushare nasi!! |
CHADEMA MOSHI VIJIJINI WARUDISHA FOMU ZA KUWANIA UBUNGE NA UDIWANI
![]() |
Mushi akipongezwa na makada wengine wa Chadema waliofika kumsindikiza ofisnini hapo. |
![]() |
Mwenyekiti wa Chadema jimbo la Moshi vijijini,Godlisen Maramia akipokea fomu toka kwa Tally Kisesa ya kuwania Ubunge wa viti maalumu katika jimbola Moshi vijijini. |
![]() |
Mtia nia wa nafasi ya Udiwani katika kata ya Kindi,kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Michael Kirawira akirejesha fomu ya kuwania nafasi hiyo katika ofisi ya Chadema kata ya Kindi. |
![]() |
Mgombea wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi vijijini,Deogratius Mushi,akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuasili katika kata hiyo. |
![]() |
Deo Mushi ambaye pia ni mwenezi wa Chadema wilaya ya Moshi vijijini ,akizungumza na baadhi ya wananchi katika kata ya Kibosho Magharibi . |
![]() |
Mwenyekiti wa Chadema katika kata ya Kibosho Magharibi Kikas Mmasi akizungumza katika kikao hicho mara baada ya kupokea fomu ya Deo Mushi. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. |
WANAHABARI WAPEWA SEMINA KUHUSU MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA
Kaimu Mkurugenzi Magonjwa Yasiyoambukiza wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Auson Rwehimbiza (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kwenye semina ya siku moja kuhusu magonjwa yasiyoambukiza. Kulia ni Meneja Mradi Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (TANCDA |
Kaimu Mkurugenzi Magonjwa Yasiyoambukiza wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Auson Rwehimbiza (kulia), akimuelekeza jambo Ofisa Habari wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Catheline Sungura wakati wa semina hiyo. |
Ofisa Habari wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Catheline Sungura (kushoto), akielekeza jambo kwenye semina hiyo. |
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye semina hiyo. |
Semina ikiendelea. |
Na Dotto Mwaibale
MAISHA ya watu katika nchi zinazoendelea, yapo hatarini kutokana na asilimia 50 ya magonjwa yasiyoambukiza kusababisha vifo.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati wa semina ya magonjwa yasiyoambukiza iliyondaliwa mahususi kwaajili ya wanahabari yenye lengo la kukamilisha mkakati pamoja na mpango kazi 2015/2020, Kaimu Mkurugenzi Magonjwa yasiyoambukiza, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Auson Rwehimbiza aliyataja magonjwa yasiyoambukiza ni moyo na mishipa ya damu, kisukari, kansa na magonjwa sugu ya mfumo wa hewa.
Alisema magonjwa hayo yanazidi kuongezeka nchini hasa kwa jamii ya watu waishio mjini na kuongeza kuwa watu wazima wenye umri wa miaka 80 kuwa na magonjwa hayo kwa asilimia 1 hadi 3 na msukumo wa juu wa damu kwa asilimia 5 hadi 10.
"Tathmini ya mwaka 2012 iliyohusisha watu wazima katika wilaya 50, inaonesha viwango vya ugonjwa wa kisukari viliongezeka kwa asilimia 9, huku asilimia 27 kwa msukumo wa juu wa damu," alisema Dk. Rwehimbiza.
Alisema ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa utandawazi, ukuaji wa miji, kutofanya mazoezi ya mwili, ulaji usiofaa, utumiaji wa tumbaku pamoja na unywaji wa pombe kupita kiasi.
Aidha, alisema Tanzania ilianza kujihususha na magonjwa yasiyokuambukiza kuanzia mwaka 2009 hadi 2015, kwa kuandaa mpango mkakati na mpango kazi ambao ulihusisha utekelezaji wa mpango wa taifa wa kisukari kwa kushirikiana na chama cha wagonjwa wa kisukari nchini.
"Hadi sasa utekelezaji wa mpango wa taifa wa kuanzisha kliniki za magonjwa yasiyoambukiza umefikia asilimia 75 katika hospitali za mikoana wilaya na vituo vya afya,". Nakuongeza kuwa asilimia 75 ya elimu zinazotolewa na watoa huduma wa afya katika hospitali za mikoa, wilaya na vituo vya Afya.
Anaongeza kuwa, shirika la afya duniani WHO, liliandaa mpango mkakati ambao ulidhamiria kupunguza viwango vya sasa vya vifo vitokanavyo na magonjwa hayo kwa asilimia 25 ifikapo mwaka 2025 na kupendekeza mapendekezo ya hiari lengo ikiwa kufanikiwa kwa mkakati huo.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba -0712-727062)
CHAMA CHA WAFANYAKAZI MADEREVA TANZANIA (TADWU), CHAMKABIDHI MLEZI WAO MKUU WA WILAYA YA KINONDONI PAUL MAKONDA RASIMU YA MKATABA WA MABORESHO YA MASLAHI YAO.
Saturday, June 27, 2015
No comments
Mlezi wa chama cha wafanyakazi madereva Tanzania (TADWU), Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akizungumza na madereva kabla ya kukabidhiwa rasimu ya maboresho ya maslahi ya madereva hao na cheti cha utambulisho wa chama hicho Dar es Salaam jana. Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), Abdallah Lubara na Mwenyekiti wa zamani wa Umoja wa Madereva Tanzania, Clement Masanja.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), Abdallah Lubara (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, rasimu ya mkataba wa maslahi ya madereva waliyokuwa wakiidai serikali kwa muda mrefu Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa zamani wa Umoja wa Madereva Tanzania, Clement Masanja (kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda cheti cha utambulisho wa chama chao kipya kitakachoitwa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU) baada kuundwa rasmi ambacho kitazindulia Julai Mosi mwaka huu.
Naibu katibu mkuu wa chama hicho, Rashid Said (kulia) akizungumzia yaliyomo kwenye rasimu hiyo na maboresho ya maslahi yao.
DC Makonda akisalimiana na madereva baada ya kumaliza kwa mkutano huo.
Madereva wakiwa wamesimama wakisubiri kusalimiana na mlezi wao DC Paul Makonda.
Ni usikivu kwa mlezi wao wakati akihutubia.
Mkutano ukiendelea.
Hapa ni furaha tupu kwa madereva hao.
Madereva wakiwa kwenye mkutano huo.
Madereva wakishangilia hutuba ya mlezi wao Paul Makonda.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea
Na Dotto Mwaibale
CHAMA cha Madereva nchini nchini kimemkabidhi mlezi wao Mkuu wa Wlaya ya Kinondoni Paul Makonda rasimu ya mkataba uliobeba maboresha ya maslahi waliokuwa wanaidai kutoka kwa wamiliki pamoja na Serikali.
Katika hatua nyingine madereva hao Julai Mosi mwaka huu wanatarajiwa kuzindua chama chao ambacho kitaitwa Chama cha Madereva Wafanyakazi Tanzania (TADWU).
Hatua ya kutengeneza rasmu hiyo hiyo imekuja baada ya kikao walichokaa Juni 21 mwaka huu ambapo lengo lilikuwa ni kuwashinikiza waajiri kuwapa mikataba ya kudumu wakiwa kazini ikiwa ni pamoja na likizo za uzazi.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu katibu mkuu wa chama hicho, Rashid Said alisema rasimu ya mkataba huo imebeba maboresho ya maslahi yao waliyokuwa wanadai.
Alisema madai hayo ni pamoja na bima ya maisha , mazishi yenye staha, muda wa kazi kisheria, matibabu, na nauli ya kwenda kazini.
"Leo tuna chama cha wafanyakazi madereva Tanzania , pia tumepewa mkataba hivyo nawatangazia madereva wote kuwa tumepata chombo cha kuzungumzia tofauti na ilivyokuwa awali.
Kwa sasa imebaki kujadili na serikali kuhusu kuboreshwa kwa mishahara hivyo napenda kuwatangazia madereva kuwa tumepata mikataba tuliyohitaji miaka mingi,"alisema.
Katibu huyo aliongeza kuwa chama hicho hakitasita kumchulia hatua za kisheria mmiliki atakayekiuka sheria hizo na kuongeza hakitasitakumpeleka kwenye vyombo vya sheria kama walivyokuwa wanawafanyia mwanzoni.
Akikabidhiwa mkataba huo kwa chama hicho, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda alisema mahali walipofikia madereva hao kwa sasa ni jambo la kuleta maendele makubwa.
Alisema watanzania wanatakiwa kutambua kuwa madai hayo si kwa ajili ya madereva peke yao bali ni kwa ajili ya taifa zima na kwamba kutatuliwa kwa changamoto hiyo kutapunguza ajali zinazoendelea kutokea nchini.
Makonda alisema asilimia kubwa ya madereva wamekuwa wakipata ajali kutokana na kuchoka hivyo wanaposinzia usahau kuwa wanaendesha vyombo vya moto hivyo kusababisha ajali.
Katika hatua nyingine Makonda alisema kuwa asilimia 80 ya waandishi wa habari hawana mikataba ya kudumu na kwamba ni changamoto hivyo aliwataka kwenda kuonana nae ili kupata ushauri wa namna ya kuwawezesha kuhakikisha wanapewa mikataba ya ajira na waajiri wao. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Subscribe to:
Posts (Atom)