ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, January 30, 2020

HAYAWI HAYAWI HATIMAYE MRADI WA MAJI MAGU WAKAMILIKA


Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa ujumla kama wilaya kwa sasa tumevuka asilimia 80 lakini kwa Magu mjini ni zaidi ya asilimia 100 kwasababu huu mradi ni mkubwa na umegharimu takribani bilioni 16 na unauwezo wa kuzalisha maji lita milioni 7 ambazo kiujumla zina uwezo wa kukidhi mahitaji ya watu zaidi ya laki moja na wakazi wa Magu mjini ni takribani 55,000" Ni kauli ya mkuu wa wilaya ya Magu Philemon Sengati wakati akitoa taarifa kwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Mwanza wakati wa ziara ya ukaguzi miradi ya maendeleo mkoani hapa. Kabla ya ujenzi wa chanzo kipya cha maji, awali chanzo cha Maji kilichokuwepo kilichojengwa mnamo mwaka 1974 pindi idadi ya watu wakiwa 6000 tu, kilikuwa hakiwezi kutosheleza wananchi wote kwani idadi ya watu tayari imeongezeka.



Wednesday, January 29, 2020

UJIO WA MV ILEMELA SASA WAMPA USINGIZI MBUNGE ANGELINA MABULA.


Ni dhahiri kuwa changamoto ya usafiri kwa wananchi wa eneo kati ya Kayenze na kisiwa cha Bezi wilayani Ilemela mkoani Mwanza sasa inakwenda kuwa historia mara baada ya kuanza majaribio ya usafiri na usafirishaji jumanne ya tarehe 28 Januari 2020.

Akizungumza mbele ya mamia ya wananchi Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt. Angeline Mabula amekiri kuwa "Kweli ukitaka maendeleo wahitaji kuwa na ndoto kubwa" kwani wakati wa ahadi za uchaguzi 2015 moyo ulimsukuma kutamka ndoto yake hiyo kwa wakazi jimboni mwake lakini ilimnyima usingizi akiwaza na kuwazua nini kitatokea iwapo ahadi hiyo isinge kamilika.

Mabula amemwaga sifa nyingi kwa Rais wa Serikali ya awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akidai kuwa ndiye aliyempa kiburi na kujiamini kupitia historia ya utendaji wake.

SERA YA USHIRIKA MSINGI WA MABADILIKO CHANYA YA SEKTA YA USHIRIKA



 Mkurugenzi mstaafu wa Rabo Foundation Netherlands Bw. Pierre Van Hedel akielezea namna Vyama vya Ushirika vinavyofanya kazi katika nchi ya Netherlands kwa lengo la kujifunza na kuongeza ujuzi katika maboresho ya Sera ya Ushirika ya Tanzania


 Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika wa Kifedha Bw. Josephat Kisamalala akieleza jambo wakati wa Warsha ya maboresho ya Sera ya Maendeleo ya Ushirika

 Mkurugenzi wa Mipango Ufuatiliaji na Tathmini wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Bw. Buji Bampebuye akifafanua jambo katika kikao cha Warsha ya kujadili maboresho ya Sera ya Ushirika (2002) kilichokuwa kikifanyika Mkoani Morogoro hivi karibuni
Mjumbe wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania (SCCULT) Bi. Anna Lupiano akieleza matarajio ya Vyama katika maboresho ya Sera ya Maendeleo ya Ushirika
 Mshauri wa Kibiashara wa Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali AGRITERRA Bw. Raymond Lyimo akitoa mada kwa wajumbe wa Warsha ya maboresho ya Sera ya Maendeleo ya Ushirika
 Mshauri wa Kibiashara wa Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali AGRITERRA Bw. Mikidadi Waziri akitoa mada wakati wa Warsha ya maboresho ya Sera ya Ushirika



Mkurugenzi wa Mipango Ufuatiliaji na Tathmini wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) Bw. Buji Bampembuye amesema wadau wote wa Ushirika wakitekeleza majukumu yao ya Kiushirika kupitia dira na mwelekeo wa Sera ya Ushirika, ni dhahiri kwamba Sekta ya Ushirika itakuwa na mabadiliko chanya na yenye tija kwa wananchi. 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Warsha ya kujadili maboresho ya Sera ya Ushirika (2002) iliyoanza Jumanne 28 Januari, 2020 hadi 29 Januari 2020, Mkoani Morogoro. 

“Ushirika ni moja ya nyenzo muhimu inayoweza kutumika nchini katika kuondoa umaskini na kuondokana na uchumi tegemezi. Hivyo, kwa kuimarisha Sera ya Ushirika tunajiwekea misingi imara ya kuendeleza Ushirika nchini,” alisema Bw. Bampebuye 

Bw. Bambebuye amesema Tanzania tunaweza kujifunza mambo mengi mazuri kutoka kwenye nchi zilizofanikiwa katika Sekta ya Ushirika pia tunaweza kutumia tafiti zetu zilizowahi kufanyika na kuingiza yatakayoongeza chachu ya ukuaji wa Sekta ya Ushirika na kupata Sera itakayokuwa ikijibu Changamoto za wakulima na Wanaushirika kwa ujumla. 

Mshauri wa Kibiashara wa Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Ushirika nchini liitwalo AGRITERRA Bw. Mikidadi Waziri akitoa mada katika Warsha hiyo ameeleza kuwa Shirika hilo kama mdau wa Ushirika limekuwa likifanya kazi katika kuongeza msukumo wa Maendeleo katika Sekta ya Ushirika kupitia mafunzo kwa Vyama vya Ushirika ya Utawala Bora, Usimamizi wa Fedha na uhamasishaji. 

Bw. Mikidadi alisema kuwa baadhi ya Changamoto zilizopo katika Sekta ya Ushirika ni pamoja na ushiriki mdogo wa vijana na wanawake hususan katika ngazi za uongozi za Vyama vya Ushirika. Hivyo, akashauri haya ni mambo ya msingi ya kuzingatiwa katika maboresho ya Sera ili kuhakikisha kuwa Sekta inakuwa endelevu na inatoa fursa za kiuchumi kwa makundi yote ya jamii zetu. 

Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania (SCCULT) Bi. Anna Lupiano amesema uboreshaji wa Sera ya Ushirika unatoa matazamio ya kupata utendaji na utekelezaji wa majukumu utakaoenda kujibu changamoto mbalimbali za Sekta ya Ushirika. 

Bi. Lupiano ametoa wito kwa Viongozi na Watendaji wa Vyama vya Ushirika kufuata na kutekeleza matakwa ya Sera mpya itakapokuwa tayari katika hatua za utekelezaji ili kuboresha na kuhakikisha uendelevu wa Vyama vya Ushirika. 

Tuesday, January 28, 2020

KITUO CHA KUKUZA BIASHARA ZA WAJASILIAMALI CHAZINDULIWA JIJINI MWANZA.


Tanzania kuelekea nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025 ni suala ambalo mgombea urais kupitia tiketi ya CCM katika uchaguzi mkuu uliofanyika 2015, Dk John Magufuli alikuwa akilihubiri kila alipokuwa akisimama katika mikutano ya hadhara.

Alieleza kwamba serikali atakayoiunda akipewa ridhaa hiyo amekusudia iwe ambayo itabadili maisha ya watanzania hususani wale wenye kipato cha chini, katika mwendelezo wa juhudi za kufanikisha adhma hiyo Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amezindua kituo cha kuendeleza ukuaji wa biashara za wajasiriamali kupitia shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) chini ya mradi wa SIDO TLED HUB, 

Mongella amefanya uzinduzi huo Januari 24, 2020 katika viunga vya ofisi za SIDO Nyakato jijini Mwanza na kubainisha kwamba serikali mkoani Mwanza iko tayari kutoa ardhi kwa ajili ya shughuli za viwanda vidogo.


 Mkurugenzi Mkuu SIDO, alisema Profesa Sylvester Mpanduji akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Meneja SIDO Mkoa Mwanza, Bakari Songwe akitoa salamu zake kwenye uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Mariam Munanka akitoa salamu zake kwenye uzinduzi huo.
 Rais wa chama cha wafanyabiashara, viwanda na kilimo TCCIA, Paul Koyi akizungumza kwenye ufunguzi huo.
Mkurugenzi Mkazi Shirika la VSO, Dawn Hoyle akitoa salamu zake kwenye mkutano huo.
Mwakilishi Ubalozi wa Canada nchini Tanzania, Christopher Duguid akitoa salamu zake kwenye uzinduzi huo.
Mwakilishi shirika la Africa CUSO International, David Forest akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mwakilishi Mkazi Shirika la Africa CUSO International, Romanus Mtunge akitoa salamu zake kwenye uzinduzi huo.
 Wadau mbalimbali wakifuatilia uzinduzi huo.
 Wadau mbalimbali wakiwemo kutoka Kituo cha Biashara, Viwanda na Kilimo nchini (TCCIA) walikuwa sehemu ya waliojumuika kwenye hafla hiyo.
 Wadau kwa umakini na tafakari wakifuatilia hafla hiyo.

 Wadau kwa umakini na tafakari wakifuatilia hafla hiyo.
 Mkurugenzi wa kampuni ya Mwanza Quality Wines inayotengeneza mvinyo wa matunda (Power Banana), Leopord Lema (kulia) akitoa ufafanuzi kuhusiana na bidhaa hiyo baada ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto) kutembelea mabanda ya wajasiriamali mbalimbali waliohudhuria halfa hiyo.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto) akifurahia jambo baada ya kutembelea banda la kampuni inayotengeneza mvinyo kwa kutumia ndizi jijini hapa ijulikanayo kama  Mwanza Quality Wines.

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto) akiwa banda la wajasiliamali akinamama.

"Wote ni mashahidi kwamba kuna baadhi ya wajasiliamali kupitia mikopo wameuziwa nyumba zao, viwanja vyao hata mali zao walizokuwa nazo, wamesaidiwa kuanzisha mpango wa biashara unaouzika benki na kukopesheka lakini hawakusaidiwa mpango unaolingana na wazo la mwenye biahsra na muelekeo wa mfanyabiashara. Kituo hiki kitahakikisha wajasiliamali wanapata mikopo inayofanana na wao, kuwaelekeza maeneo yanayotakiwa sanjari na masoko yanavyohitaji"  alisema Mwakilishi Mkazi Shirika la Africa CUSO International, Romanus Mtunge akitoa salamu zake kwenye uzinduzi huo.

Monday, January 27, 2020

HIVI NDIVYO WADAU WA MADINI NCHINI TANZANIA WANAVYOPAMBANA KUIKUZA SEKTA HIYO.



Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki ametanabaisha fursa za kibiashara zilizopo ndani ya sekta ya madini katika soko la nchini China, na kuwahimiza watanzania kuzichangamkia kwani uwakilishi wake upo tayari kuwahuwisha wafanyabiashara hao kwa kila hatua.


Balozi Kairuki amezibainisha fursa hizo mwishoni mwa wiki (Januari 24, 2020) jijini Mwanza wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa madini Tanzania uliolenga kujadili fursa za uwekezaji, teknolojia, mitaji na masoko ya madini huku akiwasihi wafanyabiashara wa madini Tanzania kujiandaa na safari ya kutembelea China mwezi ujao ili kusaka fursa mbalimbali katika sekta ya madini.

KATIKA PICHA:-

HAYA ndiyo yaliyojiri katika kikao cha wadau wa madini kilichofanyika jijini Mwanza Januari 24, 2020.











AJABU:- NDEGE YA IRAN YAANGUKA BARABARANI BAADA YA RUBANI KUKOSA MWELEKEO .


Ndege ya abiria ya Iran ilijipata katika barabara ya umma baada ya kuteleza katika barabara ya uwanja wa ndege ilipokuwa ikitua.
Abiria wawili kati ya 136 waliokuwa wakiabiri ndege hiyo walipata majeraha ya miguu kufuatia kisa hicho katika mji wa Mahshahr, kulingana na maafisa wa afya.
Ndege hiyo ya kampuni ya Caspian iliondoka mjini Tehran . Matairi yake hayakujitokeza kabisa wakati ilipotarajiwa kutua.
Picha za abiria waliokuwa wakitoka katika ndege hiyo zilichapishwa katika mitandao ya kijamii.
Runinga ya serikali ilinukuu maafisa wa usafiri wa angani wakisema kwamba rubani aliishusha ndege hiyo kuchelewa hivyobasi akakosa barabara ya ndege.
Ripota mmoja ambaye alikuwa ndani ya ndege hiyo alisema kwamba matairi ya nyuma ya ndege hiyo yaliharibika na kwamba ndege hiyo iliteleza bila matairi yake.

Presentational white space

Msemaji wa shirika la udhibiti wa safari za angani Reza Jafarzadeh aliambia chombo cha habari cha Isna news kwamba ndege hiyo iliteleza kutoka katika barabara yake siku ya Jumatatu alfajiri .
Aliongezea kwamba uchunguzi unaendelea.

MAREKANI YAMUOMBOLEZA BINGWA WA MPIRA WA KIKAPU KOBE BRYANT.


Nyota wa mpira wa kikapu nchini Marekani Kobe Bryant na binti yake Gianna ni miongoni mwa watu tisa waliofariki katika ajali ya helikopta iliyotokea mji wa Calabasas, California.
Bryant amefariki akiwa na miaka 41, alikuwa anasafiri na ndege binafsi aina ya helikopta ambayo ilianguka na kuwaka moto.
Mkuu wa polisi wa Los Angeles anasema kuwa hakuna yeyote aliyenusurika katika ajali hiyo.
Ripoti za awali zilisema kuwa kulikuwa na watu watano ndani ya ndege.
Bryant, ambaye ni bingwa wa Ligi ya Kikapu NBA mara tano alikuwa anatambuliwa duniani katika historia ya kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi wa kikapu.

Mashabiki wamekusanyika katika eneo lililotokea ajali
Salamu za rambirambi kutoka kwa watu maarufu na wachezaji wenzake nyota huyo zimekuwa zikimiminika kuonyesha mshtuko wa kifo cha nyota huyo wa mpira wa vikapu.
Viwanja vyote vya mpira wa vikapu nchini Marekani vilitenga muda wa kuwa kimya kwa heshima ya mchezaji huyo.
Bryant atakumbukwa katika tuzo za Grammy ambazo zilikuwa zikitolewa katika uwanja wa LA Lakers, eneo ambalo alikuwa akichezea kipindi chote.
"Tumechanganyikiwa na tuna uzuni sana kwa sasa," alisema mtangazaji wa Grammys Alicia Keys.
"Kwa sababu mapema leo katika mji wa Los Angeles, Marekani na duniani kwa ujumla tumepoteza shujaa.

Kobe Bryant alikuwa bingwa wa NBA mara tano na mshindi wa Oscar
Tumesikitishwa sana kwa kumpoteza Kobe Bryant, ndio maana leo tumesimama katika nyumba aliyoijenga."
NBA ilitoa tamko linalosema kuwa ,imesikitishwa sana na ajali iliyosababisha kifo cha Kobe Bryant na binti yake, Gianna" mwenye umri wa miaka 13.
"Kwa misimu 20 , Kobe alituonyesha kile ambacho kinawezekana kwa mtu ambaye ana kipaji na nia ya ushindi," alisema.

Ajali ilitokeaje?

Afisa wa polisi Alex Villanueva alisema kuwa helkopta inaonyesha uwa na watu tisa wakati inaanguka, na kuondoa idadi ya watu watano ambao walitajwa hapo awali na maofisa.
Katika taarifa iliyotolewa na mji wa Calabasas zilisema kuwa wamepokea taarifa hiyo kwa maskitiko makubwa sana.
"Ndege hiyo ilianguka nje kidogo ya mji wa Las Virgenes majira ya asubuhi wa saa za Marekani . Hakuna aliyenusurika, aliongeza.
Gavin Masak, alikuwa anaishi karibu na eneo tukio hilo lilipotokea, alikiambia kituo cha CBS News kuwa helkopta ilianguka.
"Haukuwa kama mlipuko lakini tulisikia kama bomu limelipuka kwa sauti kubwa. Lakini ilisikika kama sauti ya ndege au helkopta, ilisikika sauti kubwa sana, niliingaia ndani na kwenda kumtaarifu baba yangu na kumwambia kilichotokea. Hivyo nilivyotoka nikaona moshi mweusi ukitokea mlimani, ulikuwa mweusi au kama kijivu", alisema.

Shahidi mwingine alisema kuwa alisikia injini ikiwa inashida hata kabla ndege haijafika chini.
Polisi wa LA wameonyesha picha za tukio la ajali hiyo zikionyesha gari la zima moto na moshi ukivuka kutoka milimani.

Presentational white space

Bodi ya taifa ya usafiri imeitambua ndege iliyoanguka kuwa ni Sikorsky S-76B na imesema kuwa itatuma kikosi chake kuchunguza chanzo cha ajali hiyo.

Bryant alikuwa nani?

Bryant alicheza mpira wa kikapu kwa 20-katika viwanja vya Los Angeles Lakers. Aliacha kucheza mpira huo Aprili 2016.
Mafanikio yake ni pamoja na kuwa mchezaji bingwa wa NBA kwa mwaka 2008, mara mbili aliibuka kuwa bora zaidi ya wengine.
Vilevile alikuwa mfungaji bora wa NBA pamoja na bingwa mara mbili wa mashindano ya Olympiki.
Aliwahi kupata pointi 81 dhidi ya wachezaji wa Toronto Raptors mwaka 2006, katika historia ya michezo ya NBA.
Bryant alishinda tuzo za Oscar kama mchezaji wa filamu fupi mwaka 2018 filamu hilo ilikuwa 'Dear Basketball', filamu ya dakika tano iliyoangazia barua moja ya
Aliwahi kupata pointi 81 dhidi ya wachezaji wa Toronto Raptors mwaka 2006, katika historia ya michezo ya NBA.
Bryant alishinda tuzo za Oscar kama mchezaji wa filamu fupi mwaka 2018 filamu hilo ilikuwa 'Dear Basketball', filamu ya dakika tano iliyoangazia barua moja ya michezo aliyoandika mwaka 2015.
Bryant na mke wake, Vanessa, walikuwa na watoto wengine wakike watatu ambao ni Natalia, Bianca na Capri.

Presentational white space

Bryant alishutumiwa kwa kesi ya unyanyasaji wa kingono mwaka 2003, na binti mwenye umri wa miaka 19-aliyekuwa akifanya kazi katika mgahawa wa Coloradot. Alikanusha madai hayo, na kusema kuwa walikuwa na mahusiano ya kimapenzi ya kukubaliana.
Kesi hiyo ilifutwa baada ya mtu aliyemshtaki kukataa kutoa ushahidi mahakamani.
Ingawa baadae aliomba radhi kwa kitendo kile na kusema sababu ilikuwa msichana aliyekuwa naye hakuwa na mtazamo sawa na wake wakati walipokuwa kwenye mahusiano yao.

Watu wanasemaje kuhusu kifo cha nyota huyo?

Salamu nyingi za rambirambi zimemiminika katika mitandao ya kijamii kufatiwa taarifa ya ajali hiyo.
Shaquille O'Neal,ambaye alicheza na Bryant huko Lakers kati ya mwaka 1996 na 2004,alisema kuwa hana neno la kusema kwa sababu ya maumivu ambayo anayo.
"Ninakupenda na utakumbukwa," aliandika katika mtandao wa Instagram wakiwa katika picha ya pamoja na jezi zao za Lakers.
Deron Williams, alikuwa mshindi wa medali ya dhahabu ya Olympiki akiwa na Bryant, aliishiwa maneno. alimuelezeaBryant kuwa mchezaji bingwa aliyewahi kucheza naye.
Mchezaji wa mpira wa vikapu wa zamani Tony Parker alisema kusikitishwa kwa kifo hicho.
"Hii ni habari ya kuhuzunisha sana", alisema rais wa Marekani Donald Trump.
Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama alimuelezea Bryant kuwa bingwa na aliyeonesha umahiri katika kipaji chake.
Usain Bolt ambaye ana medali nane za dhahabu za olimpiki alisema kuwa haamini taarifa hizi.
Mwanamuziki Kanye West aliandika katika mtandao wa twitter kuwa Bryant aliishi maisha ambayo yaliwavutia wengi.
Mariah Carey naye alisema alivyoshtushwa na taarifa hizi.