ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 28, 2013

PICHA ZA MKUTANO WA UTOAJI TUZO ZA UTUNZAJI MAZINGIRA ZIWA VICTORIA UONAO ENDELEA USIKU HUU JB BELMONT MWANZA

Waziri wa Maingira Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Terezya Luoga akihutubia wadau wa mazingira na wamiliki wa viwanda eneo la Ziwa Victoria katika hafla ya utoaji tuzo kwa viwanda vilivyoimarika katika utunzaji wa mazingira Ziwa Victoria, shughuli imefanyika JB Belmont Hotel Mwanza. 

Tangu Julai 2010, kituo cha uzalishaji Bora na Hifadhi ya Mazingira Tanzania (CPCT) kikishirikiana na vituo mwenza vya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki kimekuwa kikihamasisha utekelezaji wa mbinu na teknolojia zenye kuleta ufanisi katika matumizi ya rasilimali na kupunguza uchafuzi wa mazingira katika viwanda na shughuli za kibiashara ndani ya bonde la Ziwa Victoria chini ya mwavuli wa Mradi wa Usimamizi wa Mazingira ya Ziwa Victoria - Awamu ya pili (LVEMP-II).

LVEMP-II ni mradi unaotekelezwa na nchi tano zinazozunguka bonde la Ziwa Victoria, hususan Burundi, kenya, Rwanda, Uganda na Tanzania, tangu September 2009 hadi Juni 2014.
Eneo la kusanyiko la wadau wa mazingira na wamiliki wa viwanda eneo la Ziwa Victoria katika hafla ya utoaji tuzo kwa viwanda vilivyoimarika katika utunzaji wa mazingira Ziwa Victoria, shughuli imefanyika JB Belmont Hotel Mwanza. 

Madhumuni makuu ya mradi kijenzi (Project sub-component) wa uzalishaji bora na upunguzaji uchafuzi wa mazingira (cleaner production) chini ya LVEMP-II ni kupunguza msongo wa mazingira ndani na pembezoni mwa Ziwa kwa kuzuia na kudhibiti vyanzo vya uchafuzi kutoka viwandani na kwenye shughuli za kibiashara kwa kutumia mbinu n ateknolojia mbalimbali za uzalishaji bora.
Hadi sasa viwanda na shughuliza kibiashara zipatazo 63 ndani ya Bonde upande wa Tanzania zimepata mafunzo kuhusu ufanisi wa matumizi ya rasilimali na upunguzaji wa uchafuzi yaliyoendeshwa na kituo cha Uzalishaji Bora na Hifadhi ya Mazingira (CPCT) na 20 miongoni mwao zimefanya tathimini ya uzalishaji bora (Resource Efficient & Cleaner Production Assessments)  kwenye maeneo yao na kutambua fursa mbalimbali za kuboresha shughuli zao.
Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akitambulishwa kusanyikoni.

Wadau kwenye hafla.
Kampuni kumi kutoka Bukoba, Musoma na Mwanza zimeshiriki kakita kinyang'anyiro cha tuzo za RECP, 2013. Kampuni zote zinazawadiwa usiku huu vyeti na washindi watazawadiwa vikombe na /au vyeti maalum watakavyo tunukiwa na Waziri wa Nchi, ofisi ya Makamu wa Rais (Mazinrira) Mhe. Dr. Terezya Luoga Hovisa (Mb),kulingana na kiwango cha utekelezaji wa fursa za uboreshaji zilizokuwa zimeainishwa ili kushughulikia changamoto za ufanisi wa matumizi ya nishati,maji, malighafi na kuzuia ama kupunguza taka kwenye vyanzo.
Kuna aina tano za tuzo ambazo ni:- (i) tuzo ya kupunguza taka ngumu (Solidi waste reduction),
(ii) Tuzo ya kupunguza maji taka (Waste water reduction)
(iii) Tuzo ya ufanisi wa matumizi ya maji (Water use management),
(iv) Tuzo ya ufanisi katika matumizi ya nishati (kupunguza hewa ukaa)
(v) Tuzo ya mshindi wa Jumla (Overall Cooperate Award).

Lengo kuula Tuzo hizi (RECP Awards) ni kujenga kichocheo na mfumo wa kuwatambua wanaofanya vyema katika shughuli za viwanda na biashara kwa kuzingatia ufanisi wa rasilimali na kupunguza uchafuzi wa mazingira kama namna ya kuongeza tija katika uzalishaji, kupunguza uzalishaji wa taka, kuboresha usalama na afya kazini na kuongeza ushindani.

MRADI WA TIBU HOMA WAZINDULIWA LEO JIJINI MWANZA

Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akimjulia hali mmoja kati ya watoto walio hudhuria uzinduzi wa Maadhimisho ya Tibu Homa yaliyofanyika katika eneo la Kata ya Igoma jijini Mwanza hii leo.

Udadisi wa zoezi la upimaji afya kwawananchi.

Meya akiwa ameambatana na viongozi wengine wakitoka kwenye banda la kutolea Tiba ya Homa eneo la kata ya Igoma. 

Diwani wa viti maalum kata ya Igoma kupitia Chadema Upendo Robert akizungumza na wananchi kusisitiza umuhimu wa kupima afya  mara kwa mara.

Hotuba ya Mstahiki Meya kwa wananchi ilikuwa darasa tosha kwa waliohudhuria.

Show ya muziki wa kizazi kipya ya asili ya kabila la Sukuma wew... ni Nowma..!!

Kikundi cha waigizaji kikitoa elimu kwa wananchi juu ya mradi huo wa Tibu Homa.

Diwani wa kata ya Igoma Mhe. Chagulani alisisitiza jukumu la wazazi kusimamia suala la afya kwa jamii zao.

Burudani zaidi hapa ilikuwa zamu ya Makhirikhiri wa Ziwa Victoria.

Ngoma ya moja ya makabila ya kusini toka mkoa wa Ruvuma.

Eneo la tukio, Igoma mahala kulikokuwa kukifanyika maadhimisho hayo yenye mrengo wa kuimarisha afya za wananchi.

GAPCO TANZANIA LTD YAENDEREA NA PROMOSHENI YA GAPCO RELSTAR OIL

Wasanii wa  JCB Dominion wakitoa burudani wakati wa promosheni ya Gapco Relstar Oil inanayotengenezwa na Kampuni ya Gapco T LTD Eneo laMwananyamala  Dar es salaam kutoka kushoto ni Omar Salimu Halima Masoud na Jafari Halawi 

Mwakilishi wa Kampuni ya Gapco T LTD Bw.Stevin Mwakamele Akimkabidhi mmoja wa wateja Selemani Yusufu dumu la lita tano wakati wa promosheni ya Gapco Relstar inayoendelea katika jiji la Dar es salaam jana eneo la Mwananyamala

Mwakilishi wa Kampuni ya Gapco ,Lightnes Samwel kulia akimkabidhi Mwendesha pikipiki Mrema Johnson Oil ya Gapco Relsta wakati wa promosheni inayoendelea jijini Dar es salaam Picha na www.burudan.blogspot.com

MBASPO WATAWAZWA MABINGWA AIRTEL RISING STAR MBEYA

Mshambuliaji wa  Msimamo Youth Educator’s,Saimon Kizito (kulia) akipiga mpira huku beki wa Buguruni Youth Center,Mzee Bazil akijaribu kumzuiya katika mashindano ya vijana  U-17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa Ilala,kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam juzi.

Mshambuliaji wa  Msimamo Youth Educator’s,Adeus Kizito akijaribu kumpiga chenga  beki wa Buguruni Youth Center,Husein Hamza  katika mashindano ya vijana  U- 17  ya Airtel Rising Stars mkoa wa Ilala,kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam juzi.

Kiungo wa timu ya Buguruni Youth Center,Razak  Abdalah (wapili kulia) akiwania mpira na beki wa Msimamo Youth  Educator’s, Adam Zogombwa (kulia)  katika mashindano ya vijana  U- 17  ya Airtel Rising Stars mkoa wa Ilala, kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam, jezi namba tatu ni Mzee Bazil akijiandaa kutoa msaada kwa mwenzake.

Kiungo wa  Msimamo Youth Educator’s,Rajabu Mohamed (katikati) akiwania mpira na wachezaji wa Buguruni Youth Center,Karim Matola  (kushoto) na Razak  Abdalah  katika mashindano ya vijana  U- 17  ya Airtel Rising Stars mkoa wa Ilala,kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam,jezi namba tatu ni Mzee Bazil akijiandaa kutoa msaada kwa mwenzake.

Mbaspo watawazwa mabingwa ARS Mbeya

Kama ilivyotarajiwa, timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Mbaspo jana ilitawazwa kuwa mabingwa wa Airtel Rising Stars mkoa wa Mbeya baada ya kukusanya pointi nne sawa na mahasimu wao Mbosa lakini wakiwa na magoli mengi ya kufunga. Timu ya Mbeya Secondari haikupata hata pointi moja katika mtanange huo wa kusaka vipaji

Mbaspo walianza mbio zao za kutwaa ubingwa kwa kutoshana nguvu ya 3-3 dhidi ya Mbosa siku ya Jumatatu Juni 24 kabla ya kufanya mauaji makubwa ya 6-0 dhidi ya timu dhaifu ya Mbeya Sekondari siku ya Jumanne. Michezo yote imefanyika kwenye uwanja wa Magereza jijini Mbeya. 

Mbosa walifikisha point nne juzi Jumatano walipoitandika Mbeya Sekondari 3-0 hivyo kumaliza wakiwa na point nne na magoli sita wakati wapinzani wao Mbaspo wakifikisha jumla ya magoli tisa ya kufunga. Katika mechi ya juzi, magoli ya Mbosa yalitiwa kwenye kamba na Michael Mwashilanga, Riziki Juma na Julius Landa.

Wakati huo huo, chama cha mpira wa miguu mkoa wa Mbeya kimetangaza kikosi cha wachezaji 18 kuuwakilisha mkoa huo kwenye michuano ya Taifa ya Airtel Rising Stars inayoanza kutimua vumbi kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 2.

Wachezaji hao ni Ismail Yesaya, Emmanuel Alex, Gift Sanga, Jackson Mwaibambe, Boaz Mwangole, Costa Sanga, Seif Zubery, Stanley Angelo, Enock Sikaonga, Kaunda Malata, Joel Kasimila, Hamprey Nyeo, Elia Salengo, Peter Noah, Emmaneul Mtimbi, Michael Bosco, Richard Kalinga na Zamoyoni Mwashambwa. 

Katika mkoa wa Morogoro, mji kasoro bahari, timu ya Moro Kids imetoka sare ya bila kufungana na Techfort katika mchezo wa kushambuliana kwa zamu uliopigwa kwenye uwanja wa shule ya sekondari ya Morogoro juzi Jumatano na kushuhudiwa na mashabiki wengi wa mji huo.

Airtel Rising Stars vile vile imeanza kutimua vumbi katika jiji la Mwanza ambapo timu ya Marsh Athletical imedhihirisha umwambe wake katika soka baada ya kuifunga Nyamagana United 2-0 kwenye uwanja mkongwe wa Nyamagana.

Timu za mikoa zimepangwa kuanza kuwasili jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki tayari kwa ajili ya kindumbwe ndumbwe cha Airtel Rising Stars ngazi ya taifa katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. Wachezaji 16 watachaguliwa wakati wa mashindano hayo ili kuunda timu itakayoiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars. Nchi mwenyeji wa michuano hiyo itatangazwa baadaye mwezi ujao.

Thursday, June 27, 2013

MAZISHI YA DADA YAKE MWANAKANDANDA WA ZAMANI CLEMENT KAHABUKA MAREHEMU VICTORIA KAHABUKA YAFANYIKA LEO MWANZA

Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (wa pili kutoka kulia) akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Victoria Kahabuka aliyefariki hivi majuzi na kuzikwa leo eneo la makaburi ya Nyakato jijini Mwanza.  

Dada zake marehemu Victoria Kahabuka wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mpendwa wao.

Clement Kahabuka akiongoza wadogo zake kuweka shada kwenye kaburi la dada yao.

Victoria kahabuka amezikwa leo eneo la makaburi ya Nyakato jijini Mwanza.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.