ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 1, 2014

KAGERA SUGAR 1 vs 0 YANGA: PAUL NGWAI APELEKA KILIO JANGWANI! NADIR HAROUB ‘CANAVARO ALIMWA KADI NYEKUNDU

Kagera Sugar na Yanga wakisalimiana kabla ya mtanange kuanza katika dimba la Kaitaba mkoani Kagera.
Na. Faustine Ruta/G. Sengo 
BUKOBA.
KLABU ya soka Dar es salaam Young Afrika imekubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wenyeji wao Kagera Sugar kwenye mchezo uliopigwa ndani ya Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba.

Kipindi cha kwanza Timu zote mbili zilimaliza bila ya kufungana, Kipindi cha pili Kagera Sugar walitumia faida ya kucheza nyumbani na kufanikiwa kupata bao lililofungwa kiufundi na paul Ngwai na kuibuka na ushindi huo wa bao 1-0 na kuwaacha Yanga wakibaki na pointi zao 10 ambazo wamevuna katika michezo 6.


Katika mchezo huo Mwamuzi alitoa kadi nyekundu kwa Nahodha wa Yanga Nadir Haroub Cannavaro baada ya kumpiga Kiwiko mchezaji wa Kagera Sugar.

Kipindi cha kwanza kilimalizika 0-0, lakini kipindi cha Pili Kagera walifanya shambulizi kali na kuifunga Yanga bao 1-0 bao lililofungwa na Paul Ngwai na kuweza kutangulia kwa bao hilo 1-0 mpaka mwisho wa dakika 90. ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA TAARIFA.
Kikosi cha Kagera Sugar kilichoanza dhidi ya timu ya  Yanga kutoka Jijini dar es Salaam. Picha na Faustine Ruta wa bukobasports.com
Kikosi cha Yanga.
Picha ya pamoja Timu kepteni na Waamuzi wa Mtanange 
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania 'Taifa Stars'Martinus Ignatus 'Mart Nooij nae alikuwepo uwanjani kaitaba kujionea kipute hicho.
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho kwenye Patashika na mchezaji wa Kagera Sugar.
Mshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho akimtoka mchezaji wa kagera Sugar.
Andrey Coutinho akiwekwa chini ya Ulinzi na wachezaji wawili wa Kagera huku akionekana kuwazidi ujanja wenzake wa kagera.
Jaja juu kwa juu akigombea mpira wa kichwa.
Mchezaji wa kagera walipoteza muda mwingi kwa kujiangusha angusha wakivunga wameumia.
Nadir Haroub "Cannavaro" akisindikizwa nje ya Uwanja baada ya kuondolewa kwa kuoneshwa kadi nyekundu.
Nadir Haroub "Cannavaro" akisindikizwa nje ya Uwanja baada ya kuondolewa kwa kuoneshwa kadi nyekundu.
Tegete aliingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho na hapa alikuwa akichuana na Benjami Asukile wa Kagera Sugar.
Kocha msaidizi wa Kagera Sugar, Murage Kabange ndiye alikuwa kazini leo baada ya Kocha wao Jackson Mayanja kuwa nje kwenye Adhabu aliyopewa kwenye mechi iliyopita dhidi ya Coastal Union.
Mchezaji wa Kagera chini tena dah..!!!
KOCHA Mkuu wa Yanga Marcio Maximo akimnyooshea kidole Mwamuzi wa kati baada ya mpira kumalizika Kaitaba Jioni hii Baada ya kuchapwa bao 1-0.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Leonardo Neiva na Marcio Maximo wote hawakuridhishwa na maamuzi ya refarii wa mchezo huo na hapa walikuwa wakilalama kwa wasimamizi wa mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar ambao ulimalizika kwa Yanga kufungwa bao 1-0.

Friday, October 31, 2014

SKYLIGHT BAND INAKUKARIBISHA USIKU WA LEO THAI VILLAGE

DSC_0089
Sam Mapenzi;……Kuna Watu Hatari, Wenye Mapenzi Zenye Siri Kali,…Letu Nalo Lina Jua Kali, Penzi Letu Serikali,….Wajua Nakupenda, Malaika…..Aneth Kushaba;…..I'm Going Koo Koo Koo, So Koo Koo Coz I, I, Love You, (Aiyayaaaaa)….I'm Going Koo Koo Koo, So Koo Koo Coz I, I Love You,….(Aiyayaaaaa)...Hizi zote utazipata Skylight Band si kwingine bonge la colabo.
DSC_0159
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar huku akisindikizwa na waimbaji wenzake kutoka kushoto ni Digna Mbepera, Joniko Flower a.k.a Baba lao, Sony Masamba pamoja na Sam Mapenzi.
DSC_0007
Aneth Kushaba sambamba na Digna Mbepera wakiwapa raha mashabiki wao (hawapo pichani) kwenye show zao za kila Ijumaa ndani ya ukumbi wa maraha wa Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0012
Kifaa kipya cha Skylight Band Bela Kombo akitoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo ndani ya ukumbi wa Thai Village Ijumaa iliyopita.
DSC_0024
Kutoka kushoto Bela Kombo, Hashim Donode na Digna Mbepera wakiporomosha burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani ya uwanja wao wa nyumbani Thai Village.
DSC_0057
Binti mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni Digna Mbepera kwenye hisia kali za muziki wa Live kwa mashabiki wa Skylight Band ndani ya ukumbi wa Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0026
Burudani ikiendelea.
DSC_0105
Anaitwa Sony Masamba akifanya yake jukwaani huku Sam Mapenzi na Joniko Flower wakipiga back vocal.
DSC_0126
Aaaah ni full raha wake kwa waume wakionekana kukunwa na uimbaji wa Sam Mapenzi mzee wa Naija Flava, unakosaje uhondo ndugu....Njoo tujumuike leo pamoja ndani ya Thai Village.
DSC_0137
Mpiga drum wa Skylight Band Baraka akifanya yake kuhakikisha mashabiki wanapata ladha nzuri ya ala hizo za muziki huku pale pembeni Amos Kinanda naye akisababisha.
DSC_0141
Na hivi basi ndivyo wanavyochizika mashabiki wa Skylight Band kwa shangwe za aina yake mwenye kigelegele haya...mwenye mluzi haya....ni furaha si kingine.
DSC_0163
Mkongwe wa muziki Joniko Flower akiwasebenesha mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar huku waimbaji wenzake wakimpa sapoti.
DSC_0115
Nyomi la mashabiki wa ukweli wa Skylight Band likiwa limefurika Ijumaa iliyopita ndani ya Thai Village.
DSC_0045
We are twin sisters......!
DSC_0117
Blogger King Kif (kushoto) akiwa na wadau wa Skylight Band ndani ya ukumbi wa Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0096
Meneja Maneno na King Kif wakimezea mate kuku choma ndani ya kiota cha Thai Village Masaki.

KITUO CHA HABARI CHA UMOJA WA MATAIFA WASHIRIKI ALHAMISI YA BURUDANI NA KIKUNDI CHA MTANDAO WA VIJANA TEMEKE


 Afisa habari wa Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi Stella Vuzo akitoa mada kuu iliyokuwa inahusu malengo ya maendelea ya milenia na kuangalia imefikia wapi kwenye malengo hayo pamoja na kuwaelimisha kuhusu maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015(Post 2015 Sustainable Development) iliyotolewa kwa Mtandao wa vijana wa Temeke.

Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa jana iliandaa Alhamisi ya Burudani kwa ajili ya kujifunza kazi mbalimbali za Umoja wa Mataifa. Kwa kila Alhamis ya mwisho wa mwezi Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa huandaa burudani kwa makundi mbalimbali na kujifunza kazi mbalimbali za Umoja wa Mataifa. Alhamisi ya mwezi wa kumi kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa kilitembelea Mtandao wa Vijana wa temeke na kujadili mambo makuu ya malengo ya Milenia pamoja na kuangalia ni jinsi gani vijana wanashiriki katika shughuri za kimaendeleo katika jamii zao
 Mkutubi - Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa, Bi Harriet Macha akisisitiza jambo kwenye mada kuu iliyokuwa inahusu malengo ya maendelea ya milenia na kuangalia imefikia wapi kwenye malengo hayo pamoja na kuwaelimisha kuhusu maendeleo endelevubaada ya mwaka 2015(Post 2015 Sustainable Development)
 Mwenyekiti wa Kituo cha Vijana wa Makangalawe, Bwana  Ismael Mnikite akizungumza jambo kuhusu mada husika na kuangalia ni njia  gani zinaweza kuwapelekea vijana kushiriki kwenye shughuli nzima za maendeleo
Mwenyekiti wa Kituo cha Vijana wa Makangalawe, Bwana  Ismael Mnikite akigawa vipeperushi vya Umoja wa mataifa pamoja na fomu kwa vijana hao wa Temeke.
Mada ikiendelea
Katibu wa Mtandao wa Vijana Temeke, Bwana Yusuph Kutengwa akichangia mada
 Omari A. Mketo akichangia
 Ishengoma ambaye ni mlemavu wa macho akieleza faida alizozipata baada ya kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa kutoa mafunzo hayo kwa mtandao wa vijana wa Temeke.

Baadhi ya vijana wa mtandao wa vijana wa Temeke wakisoma kwa umakini malengo ya milenia wakati kituo cha habari cha umoja wa mataifa walipokuwa wanatoa mada kwa vijana hao
Picha ya pamoja

Thursday, October 30, 2014

ASKARI POLISI AMKATA VIDOLE VINNE MFANYAKAZI WAKE KWA PANGA AKIMTUHUMU KWA KUMWIBIA DEKI YA VIDEO.

Steven Magessa (18) akizungumza nasi kusimulia kisa na mkasa.

ASKARI POLISI ASHIKIRIWA KWA KUMKATA MFANYAKAZI WAKE VIDOLE VINNE KWA PANGA KWA MADAI YA KUMWIBIA DEKI YA VIDEO NYUMBANI KWAKE. 

JESHI la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia askari wake WP Fatuma wa Kituo cha Polisi Igogo wilayani Nyamagana kwa kosa la kumjeruhi mtumishi wake wa ndani kwa mkumkata vidole vyake vinne vya mkono wa kulia kwa panga, akimtuhumu kumwibia Deki ya Video nyumbani kwake. 

Tukio hilo la kujeruhiwa kijana Steven Magessa (18), lilitokea Oktoba 20 mwaka huu katika kijiji cha  Magange Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara nyumbani kwao kijana huyo aliyekuwa amekimbilia huko baada ya kudaiwa kumwibia mwajili wake nyumbani eneo la Igogo.

Akizungumza na G.SENGO BLOG kijana huyo alieleza kuwa kufanya kazi kwa askari huyo kulikuja mara baada ya askari huyo kumfuata kijijini na kumuomba ridhaa ya wazazi wa kijana huyo kuambatana naye jijini Mwanza ili kumsaidia kazi za nyumbani ambapo walikubaliana malipo ya kiasi cha Sh 50,000/= kila mwezi jambo ambalo askari huyo alilikiuka na kushindwa kulitekeleza kwa muda wa miezi sita bila kumlipa mshahara.

“Nilipoona hajanilipa mshahara wangu kwa muda wa miezi sita huku kila ni kimwambia ananijia juu na kunitukana matusi basi nilimuomba ruhusa ya kwenda kijijini Oktoba 15 mwaka huu kumuona mama yangu mzazi aliyekuwa anaumwa ili kupata nafasi ya kurudi nyumbani” alisema.

Ni kidole gumba tu kilicho nusurika kukatwa nacho ilikuwa ni kama bahatikusalia kwani kilikwanyuliwa huku vingine vinne vikifyekwa na panga mkono wa kulia wa Steven Magessa.
Steven alieleza kuwa wakati akiwa kijijini askari huyo (Mwajili wake) alikuwa akimpigia simu kumtaka arudi Mwanza kuendelea na kazi na kudai kuwa atamlipa malimbikizo ya mshahara wake kiasi cha Sh 300,000/= zilizokuwa kama deni, Steven alikubali ombi hilo kwa kuomba atumiwe nauli na pesa kidogo ya kumwachia mama yake, jambo ambalo askari huyo alikaa kimya bila majibu.

“Siku ya Oktoba 20 mwaka huu majira ya saa 4:00 asubuhi alifika kijijini akiwa na askari watatu kwenye gari la Polisi (Difenda) wa Kituo cha Mugumu na kudai kuwa nipo chini ya ulinzi kisha kunifunga pingu, akidai kuwa nilimwibia Deki ya Video na kutoroka nyumbani kwake, walinipandisha kwenye Difenda kunipeleka kituoni “ alisema.

Kijana huyo alieleza kuwa baada ya kufikishwa kituoni Mugumu askari huyo na wenzake walianza kumuhoji huku wakimpa maneno ya vitisho, kijana huyo alipokataa kuwa hakuiba wala kutoroka, Sajenti Fatuma aliamuru kijana huyo kuvulishwa shati alilovaa na kisha akafungwa usoni na kuombwa anyooshe mkono mezani ili apewe 'Sapraizi'.
Ni kidole gumba tu kilicho nusurika kukatwa huku vingine vinne vikifyekwa na panga mkono wa kulia wa Steven Magessa.

"Sekunde chache nilihisi kitu kikali kimenipitia kwenye vidole vyangu vinne vya mkono wa kulia na kufuatiwa na maumivu makali, niliusogeza mkono wangu mdomoni kuupoza kwa kuupuliza ndipo nilipo gundua kuwa nimekatwa kabisa vidole vyangu vinne vya mkono wangu wa kulia ikibakia  dole gumba tu" kijana Steven alisimulia kwa uchungu.
“Niliangua kilio kutokana na maumizu na sijui vidole vyangu hadi sasa sijui vikowapi, askari wenzake baada ya kuona nimetokwa na damu nyingi walimshauri anipeleke hospitali ya Wilaya ya Mugumu ili nipatiwe matibabu kabla ya kuondoka kuja Mwanza,”alisisitiza.

Steven alisema baada ya kupatiwa matibabu, tulienda kupanda basi ili kuja Mwanza kwa madai kuwa amenifungulia kesi ya wizi wa Deki ya Video na tuliopfika alinipeleka kituo cha Polisi Kati Nyamagana na kuniweka Mahabusu akinituhumu wizi, lakini nilipochukuliwa maelezo nilikana tuhuma za wizi na kueleza ukweli wangu ili kupata msaada.

Huku taarifa zingine kutoka ndani ya jeshi zilizopatikana zilidai kuwa askari huyo alikusudia kufanya ukatili huo kutokana na udanganyifu ambao alifanya kwa uongozi wake akiomba kupatiwa silaha (SMG) kwa ajili ya kuitumia kwenye kazi za nje lakini lengo ikiwa ni kwenda na silaha hiyo kwa ajili ya kumkamata na kumtishia kijana huyo, jambo ambalo uongozi ulimgomea.

JESHI LA POLISI LINASEMAJE
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza (RPC), Valentino Mlowola, jana ofisini kwake amethibitisha kuwepo kwa taarifa za tukio hilo na kueleza kuwa tayari Jeshi hilo limechukuwa hatua madhubuti hatua ya awali ikiwa ni kumshikilia askari huyo kwa kufanya ukatili huo kwa kuvunja sheria na kujichukulia sheria mkononi kumjeruhi kijana huyo.

Mlowola alisema pamoja na kijana huyo awali kufunguliwa jarada la kutuhumiwa kufanya kosa la wizi (Jinai) na kudaiwa kutorokea kijijini kwao, bado askari huyo alitakiwa kufuata mfumo wa kiutawala na kisheria uliopo kushughulikia suala hilo badala ya kuamua kujichukulia maamuzi ya kumwadhibu mtuhumiwa kabla ya uthibitisho wa mashitaka yaliyokuwa yamefungulia.

“Nilipopokea taarifa hizi kwa mashangao na masikitiko makubwa na zimenisitua sana, si kitendo cha kiungwana hata kidogo kwa mtu ambaye anatakiwa kufuata taratibu za mfumo wa utawala na sheria katika utekelezaji wa kushughulikia kero na matatizo ya jamii, alitakiwa kutumia busara kwani tayari aliishamfungulia jarada la kumtuhumu kumwibia ikizingatiwa naye ni mzazi wa watoto watano ni lazima anaujua uchungu,”alisema. 
  
Kamanda Mlowola alieleza kufatia ukatili huo kufanywa na askari wake ameunda timu ya kikosi cha askari kwenda hadi kijijini Magange wilayani Serengeti mkoani Mara ili kufanya uchunguzi wa tukio hili ikiwa ni pamoja na kufanya mahojiano na familia, wananchi wa kijiji hicho kisha Hospitali ya Wilaya ya Serengeti alipopatiwa matibabu ya awali.

“Ili tupate ukweli wa jambo hili tumeunda timu hiyo, kwani kijana Steven tumemhoji ametueleza jinsi askari Fatuma alichomfanyia na kudai hakumwibia, lakini askri wetu pia amehojiwa awali amedai hakufanya kitendo hicho bali wananchi ndo walimfanyia ukatili huo hivyo ni mkanganyiko lakini ukweli utapatikana tu japo kuwa tukio hili halikufanyika Mwanza”alisisitiza.

Mlowola alisema kwamba tayari tunamshikiria askari huyu na kumfungulia jarada la uchunguzi kwa taratibu za kijeshi na ikibainika kutenda kosa hilo tutumfukuza kazi na kumfikisha katika vyombo vya sheria ili kuchukuliwa hatua zaidi kulingana na kosa alilofanya, lakini pia kijana Steven naye anashikiriwa kwa tuhuma alizonazo za wizi kufatia jarada lililopo.

“Hatuwezi kuendelea kucheka na kufumbia macho kitendo hiki ni jambo ambalo linamgusa kila mtu hata mimi ni mzazi ukiachana na utumishi wangu wa umma, ntahakikisha jambo hili nalishughulikia kwa umakini na kutoa taarifa kwa umma ili pia kueleza wananchi kuwa tukio hili limefanywa na mtumishi kama mtu si Taasisi ya Jeshi la Polisi na ahidi kutenda haki kwenye hili,”alisisitiza. 

Wito wangu kwa wananchi ni kuacha kujichukulia sheria mkononi na kuwaadhibu watuhumiwa mbalimbali kabla ya kuthibitika kwa makosa na tuhuma hizo, lakini wazingatie kufuata taratibu za kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria ili kushughulikia matatizo yao nawaomba waendelee kutoa ushirikiana na kufuata mfumo uliopo badala ya kujichukulia sheria mkononi.

BUNGE LA BURKINA FASO LACHOMWA MOTO

CHANZO: BBC SWAHILI.
Waandamanaji nchini Bukina Faso wameteketeza majengo ya Bunge mjini Ougadougou, kupinga hatua ya kuongeza muhula wa Rais Blaise Compaore ambaye ametawala nchi kwa miaka 27.
Runinga ya itaifa ililazimika kusitisha matangazo baada ya waandamanaji kuvamia shirika la utangazaji.
Waandamanaji kisha wameelekea Ikulu ya Rais na wanajeshi wamekua wakiwafyatulia risasi.
Vilevile baraza la jiji pamoja na makao makuu ya chama tawala yameteketezwa moto.
Umati mkubwa wa watu umeonekana ukielekea ikulu ya Rais huku uwanja wa ndege ukifungwa.
Rais Blaise Compaore ameomba utulivu ,katika ujume aliotumwa kwa Twitter.
Wabunge wamelazimika kuahirisha kura hiyo ya kubadilisha katiba kumkubalia Compaore kuwania tena Urais mwaka ujao.
Watu watano wameuawa katika maandamanao hayo ambayo yametajwa kuwa mabaya zaidi kukumba utawala wa Blaise Compaore.
Awali wanajeshi waliwafyatulia risasi waandamanaji waliovamia majengo ya bunge.
Compaore alitwaa madaraka kupitia mapinduzi mwaka wa 1987. Amekua akishinda uchaguzi lakini kura hio hukumbwa na utata.
Ufaransa na muungano wa Ulaya zimemuomba Rais Compaore kutobadilisha katiba ili kuwania tena.