NA ALBERT G. SENGO/MUGUMU/SERENGETI/MARA
Mkurugenzi wa operesheni Bayport Financial Services Mr. Nderingo Materu amesema kuwa huu ni mwendelezo wa kampeni ya Bayport kupanda miti 1,000,000 Tanzania nzima, kampeni ikiwa imebebwa na lengo mahususi la kuihamasisha jamii kutunza mazingira, kukabiliana na changamoto za tabia nchi sanjari na kuunga mkono juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan.Saturday, December 2, 2023
Friday, December 1, 2023
VIDEO: TRA PWANI YAWAKOMBOA WAKINAMAMA WAJAWAZITO YATOA VIFAA ZAHANATI YA MISUGUSUGU
VICTOR MASANGU/PWANI
Wananchi wa kata ya Misusugu wilayani Kibaha, mkoani Pwani, hususan wajawazito wanatarajiwa kuondokana na changamoto ya kutembea umbel i mrefu wa zaidi ya kilometa 12 kwenda kutafuta huduma ya Afya ya mama na mtoto baada ya mradi wa ujenzi wa jengo la huduma hiyo kuanza utekelezaji wake kwa nguvu za wananchi. Hayo yamebaishwa na Afisa Maendeleo ya jamii wa kata hiyo, wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi kwa ajili ya mradi wa jengo jipya la mama na mtoto linalojengwa kwa lengo la kuweza kuwasaidia wakinamama wakati wa kujifungua.TRA PWANI YATISHA YAMWAGA VIFAA VYA UJENZI JENGO LA MAMA NA MTOTO MISUGUSUGU
NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
MAAMBUKIZI YA VVU YAPUNGUA KAGERA
KARAGWE
Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na VVU Katika Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera yameshuka kutoka asilimia 2.3 mwaka 2022 mpaka kufikia asilimia 1.3 kwa waliojitokeza kupima January -November mwaka huu
Akisoma risala mbele ya Mgeni Rasmi ,Afisa mtendaji wa Kata ya Bugene Happyness Kanyoro ,katika maadhimisho ya kumbukizi ya siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Bugene amesema hali ya maambukizi mapya katika wilaya yanapungua ukilinganisha na miaka iliopita
Akitaja takwimu za miaka iliopita amesema zinapungua kutokana na mwitikio wa watu kujitokeza kupima afya zao na kufuata ushauri wa taalama na kusema kuwa kwa mwaka 2020 hali ya maambukizi ilikuwa asilimia 5,mwaka 2021 3.2,mwaka 2022 asilimia2.3,
Wakitoa ushuhuda baadhi ya watu ambao wamepata maambuzi ya virusi vya Ukimwi kwa zaidi ya mika 20 ,wamewaondoa hofu baadhi ya watu wanaogopa kupima na waliogundulika na kuwahimiza kupima jambo litalowasaidia kujitambua na kujikubali
Naye Mgeni Rasmi,Mwk wa kamati ya Kudhibiti Ukimwi Wilaya ya Karagwe Dauson Byamanyirwoi ambae pia ni Diwani wa kata ya Rugera kupitia maadhimisho hayo amemuagiza Mganga Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Idara ya maendeleo ya Jamii kushirikina kwa kutoa elimu na kuhakikisha wanatoa huduma ya tohara vijijini ili kusaidia kupungua maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi na VVU.
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani yameambatana na kauli mbiu isemayo Jamii iongoze kutokomeza Ukimwi.
Thursday, November 30, 2023
SELINA KOKA AMUENZI BIBI TITI KWA KUTOA SAPOTI YA DOTI 80 ZA VITENGE KWA UWT KIBAHA MJI
VICTOR MASANGU,KIBAHA
MCHUNGAJI MBAGA AWASHAURI WATANZANIA KUWA NA UTARATIBU WA KUCHEKI AFYA ZAO KILA WAKATI
Na Oscar Assenga,TANGA
WATANZANIA wameshauriwa kuwa na utaratibu wa kucheki afya zao mara kwa mara kutokana na kwamba afya ndio kitu muhimu katika maisha ya kila siku.
Ushauri huo ulitolewa na Mchungaji wa Kanisa la Waadvestista Wasabato Mtaa wa Makorora Jijini Tanga Mchungaji Elinihaki Mbaga wakati akihitimisha majuma mawili ya semina ya Neno la Mungu iliyokwenda sambamba na utoaji wa huduma za kijamii.
Mchungaji Mbaga alisema kwa sababu Serikali inahitaji watu waliona na afya nzuri na Kanisa pia nalo linahitaji watu wenye afya nzuri huku akisisitiza umuhimu wa kufanya hivyo kwa ustawi wa jamii
“Katika hilo nitoe wito kwa jamii ya watanzania kuwa na uratibu wa kucheki afya zao mara kwa mara kwani hii itawasaidia kujua wanaumwa na nani na namna ya kupata tiba mapema kabla tatizo halijawa kubwa “Alisema
Huduma za Kijamii za Kitabibu zilizotolewa ni upimaji vipimo kwa magonjwa yasiyokwa ya kuambukiza ikiwemo sukari na Presha, Madaktari 5 ambao wamekuwa wakifanya huduma za kitabibu ikiwemo kutoa kipimo kwa magonjwa yasiyoambukiza.
“Tunamshukuru Mungu katika Huduma hii watu wengi wamejitokeza zoezi la upimaji wa macho watu 87 wamehudumiwa na 78 wamepewa miwani, na mwitikio umekuwa mzuri watu watu 167 wamepewa huduma mbalimbali”Alisema
Awali akizungumza Mwinjiliti Elifuraha Jonas alisema kwamba mkutano huo umekuwa wa kipekee na nzuri kutokana na huduma za kupima macho na wanatamani wakati mwengine wananchi waenda kucheki afya zao huku akieleza suala la macho limekuwa ni changamoto kwa jamii na huduma ni bure ambapo kanisa limechangia matibabu hayo ili watu watibiwe.
Hata hivyo Mwinjiliti huyo alisema wamekuwa wakibarikiwa na huduma za kiafya kutoka kwa madaktari maana wagonjwa wengi walitibiwa na walikuwa na huduma ya familia na mashauri kwenye ndoa na vijana wakihamiza wachape kazi maana Taifa linahitaji watu wachapa kazi na hata kanisa linahitaji wachape kazi.
Wednesday, November 29, 2023
POLISI TANGA YAWAKAMATA WATUHUMIWA 107 , WAMO WA MAUAJI, WIZI WA MIFUGO NA UNYANG’AJI WA KUTUMIA SILAHA
Na Oscar Assenga, TANGA
JESHI la Polisi Mkoani Tanga limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 107 kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya Mauaji,Wizi ya Mifugo,Unyang’anyi wa kutumia silaha ,kuingia nchini bila kibali pamoja na kupatikana dawa za kulevya aina mbalimbali.
Hayo yalisemwa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Almachius Mchunguzi wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Jijini Tanga kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Octoba hadi Novemba 27, 2023.
Kamanda Mchunguzi alisema kwamba kati ya watuhumiwa hao 21 wamekamatwa na Bhangi kilogramu 43, Mirungi Kilogramu 124,
Heroin Gramu 242 huku wanne (4) wakikamatwa kwa kosa la kusafirisha wahamiaji haramu na watuhumiwa saba (7) raia wa Ethiopia kuingia nchini bila kibali.
Aliwataja wengine ni mtuhumiwa 01 kupatikana na kosa la unyang’anyi kwa kutumia silaha aina ya Panga na watuhumiwa wengine 74 wamekamatwa huku upelekezo ukiwa bado unaendelea.
Aidha Kamanda Mchunguzi alisema pia katika kuimarisha doria za nchi kavu na baharini Novemba 21 mwaka huu huko maeneo ya Kisiwa cha Jambe wilaya ya Tanga walifanikiwa kukamata boti aina ya Fibre yenye rangi nyeupe na bluu isiyokuwa na usajili ikiwa na injini ya Yamaha HP 15.
Alisema vitu nyengine vilivyokuwepo kwenye boti hiyo ni Chupa za Hewa ya Oxygen 02,(Diving Cylinder),mipira ya kupumulia 02 (regulator),Tega ya kuokotea Samaki,Kiberiti 01 na Samaki aina mbalimbali Kilogramu 30 waliovuliwa kwa kutumia baruti ambao walithibitishwa na Afisa Uvuvi kuwa hawafai kwa matumizi ya Binadamu.
Aliongeza kwamba watuhumiwa wamekimbia na kutelekeza boti hiyo baada ya kugundua wanafuatiliwa na Polisi wa Kikosi cha Wanamaji Tanga huku Upelelezi unaendelea kwa kuwatafuta watuhumiwa wa tukio hilo.
Hata hivyo Kamanda Mchunguzi alitaja tukio lingine kuwa ni Novemba 18 mwaka huu Jeshi hilo lilifanikiwa kumkamata Hamisi Kombo (46) mkazi wa Kwediboma wilaya ya Kilindi akiwa na wenzake nane .
Alisema wenzake wote hao ni waganga wa kienyeji ambao wanajihusisha na rasmi chonganishi wakiwa katika kijiji cha Kivindani Kata ya Tongoni Tarafa ya Pongwe wilaya ya Tanga ambapo wananchi wa eneo hilo waliwaita waganga hao kwa ajili ya kufanya ukaguzi katika nyumba za kijiji hicho ambazo zinasadikiwa kuwa na uchawi.
Kamanda huyo alisema uchawi huo ambao wanajiji hao walilalamika kuwa wakitendewa vitendo vya kudhalilishwa kwa kuvuliwa nguo na kuachwa wakiwa watupu kimazingara wakati wakiwa wamelala usiku,ambao watuhumiwa hao wote wapo nje kwa dhamana wakati upelelezi wa shauri hilo ukiendelea.
Katika hatua nyengine Kamanda Mchunguzi alisema katika kipindi mwezi mmoja Jumla ya watuhumiwa 41 wamefikishwa mahakamani,kesi 11 zinaendelea mahakamani na kesi 27 zimetolewa hukumu mbalimbali ambapo watuhumiwa watatu ambao ni Justis Kunael(40),Saidi Adam (32) na Maliki Amiri (38) wote wakazi wa Handeni wamehukumiwa kifungo cha Maisha kwa kosa la kubaka.
Kwenye tukio la Mauaji,Kamanda Mchunguzi alisema watuhumiwa Rashid Mwalimu “Chidi Kiwangwa”(32),Siwajui Kigaa “Sahonelo” (27) na Zuberi Hassani (34) wote wakazi wa Kijiji cha Kwandugwa wilayani Handeni walihukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la mauaji ya mtoto wa Kike mwenye umri wa miaka (9).
Tuesday, November 28, 2023
MVUA ZA EL NINO WAKAZI WA MABATINI MWANZA WANAISHI ROHO MKONONI
NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
MWENYEKITI WA MTAA WA NYERERE B KATA YA MABATINI ELIUS MGONDA AMEELEZA WASIWASI WAKE JUU YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA KUATHIRI MAAKAZI YA WANANCHI WALIOPO PEMBEZONI MWA MTO MIRONGO. AMEELEZA HAYO WAKATI AKIZUNGUMZA NA JEMBE HABARI AMESEMA WANAENDELEA KUTOA ELIMU YA TAHADHALI KWANI NYUMBA PIA ZILIZOPO MAENEO YA MLIMANI ZIMEJENGWA KWA UDONGO ZIPO HATARINI KUTOKANA NA MVUA HIZO. #samiasuluhuhassan #mwanza #tanzaniaMonday, November 27, 2023
VIDEO - TUME YA MIPANGO SHIRIKISHENI WANANCHI UANDAAJI DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2050 - DKT. BITEKO
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameagiza Tume ya Mipango nchini kuweka uratibu wa ushiriki wa makundi mbalimbali ya wananchi na Wadau wengine katika kutoa maoni kwenye mchakato unaoendelea wa uandaaji Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2050.
TUME YA MIPANGO SHIRIKISHENI WANANCHI UANDAAJI DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2050 - DKT. BITEKO
📌 Ataka miradi inayofadhiliwa na Wadau wa Maendeleo pia ifuatiliwe na kufanyiwa tathmini
📌Awaasa Maafisa Mipango kutembea kifua mbele, wao ni wadau muhimu Serikalini
📌Aagiza watoe elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutoa maoni kwa ajili ya maendeleo ya nchi
Arusha
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameagiza Tume ya Mipango nchini kuweka uratibu wa ushiriki wa makundi mbalimbali ya wananchi na Wadau wengine katika kutoa maoni kwenye mchakato unaoendelea wa uandaaji Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2050.
Amesema hayo wakati akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, katika hafla ya ufunguzi wa Kongamano la kwanza la Wanamipango 2023 iliyofanyika tarehe 27 Novemba 2023 jijini Arusha.
"Tume ya Mipango hakikisheni Wananchi wote wanashiriki kikamilifu kutoa maoni yao kuhusu Tanzania wanayoitaka katika miaka 25 ijayo, maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050
yameanza na kutokana na umuhimu wa Dira kwa Taifa letu, wanamipango na wadau wote ni muhimu kila mmoja kwa nafasi yake ashiriki kikamilifu katika hatua zote za maandalizi kama atakavyohitajika." Amesisitiza Dkt. Biteko
Suala jingine alilosisitiza ni kwa Maafisa Mipango kubadilika na kufanya ufuatiliaji na tathmini ya Miradi na Programu zote zinazotekelezwa katika maeneo yao ikiwemo zinazofadhiliwa na Wadau wa Maendeleo badala ya ile inayogharamiwa na Serikali Kuu au Halmashauri pekee.
Vilevile, Dkt. Biteko ameelekeza Wakurugenzi wa Mipango kuzingatia utamaduni wa kuwa na mawazo ya pamoja katika kupanga mipango ya Serikali na nchi kwa ujumla ili kuleta mipango imara itakayosaidia Taifa kufikia uchumi wa juu.
Suala jingine alilosisitiza Dkt. Biteko ni Wanamipango waliopewa jukumu la kusimamia miradi pamoja na ufuatiliaji na tathmini kuzingatia utaratibu wa kutoa taarifa za utekelezaji wa programu na miradi ya maendeleo inayotekelezwa.
Sanjari na hayo, Dkt. Biteko amesema kuwa, Shughuli za tathmini na ufuatiliaji ni muhimu nchini hivyo zinapaswa kupewa kipaumbele cha kutengewa rasilimali za kutosha.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo, amewataka Maafisa Mipango kuona thamani ya kada yao na wahakikishe kuwa wanakuwa wafuatiliaji wakubwa katika upangaji wa mipango kutoka ngazi ya chini hadi Taifa, kwa ajili ya manufaa ya nchi.
Vilevile, amewaagiza Wakurugenzi wa Sera na Mipango kuhakikisha kuwa wanaweka mipango inayotekelezeka kwa manufaaa ya nchi kiuchumi.
Kongamano hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Mipango na
Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela.
Sunday, November 26, 2023
WAKANDARASI WABABAISHAJI WASIPEWE KAZI-WAZIRI BASHUNGWA.
Na Oscar Assenga,TANGA
Waziri wa ujenzi Innocent Bashungwa amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kuhakikisha kuwa wakandarasi wasumbufu na wababaishaji hawapewi kazi za ujenzi wa barabara nchini kote.
Akizungumza alipokagua Barabara ya Handeni-Mafuleta 20km Bashungwa amesema ni aibu kuwa na mkandarasi msumbufu anaechelewesha kazi na bado kupewa miradi mingine hali inachelewesha maendeleo kwa wananchi.
Alimuagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini kuhakikisha Mkandarasi huyu HHEG hapewi mradi nyengine ya km 30 mpaka watakapojiridhisha na kasi yake ya ujenzi wa km 20 alizonazo sasa ifikapo Januari mwakani
Alisema haiwezekani mkandarasi anapewa kazi ya mradi wa km 30 na hakamilishi kwa wakati na bado wanafikiria kumpa eneo nyengine suala hilo haliwezi kukubalika hata kidogo
Aidha Waziri Bashungwa alimtaka Mtendaji Mkuu wa Tanroad kuhakikisha wanajipanga vizuri na kusimamia wataalam wake ili Barabara ziweze kukamilika kwa wakati
" Wana ujenzi wote tuwahudumie watanzania kwa kutanguliza uzalendo mbele," amesisitiza Waziri Bashungwa"
Waziri huyo amezungumzia umuhimu wa wakandarasi kuwa na uhusiano mzuri na wananchi katika ni maeneo wanayofanyia kazi kwani kufanya hivyo ni sehemu ya ulinzi kwenye miradi wanayoitekeleza.
Katika hatua nyengine Waziri Bashungwa amemuagiza Meneja wa TANROADS Mkoa wa Tanga Eng. Eliazari Rweikiza kuhakikisha HHEG anayejenga Barabara ya Handeni-Mafuleta anaboresha barabara inayotumika kati ya Handeni na Kilindi ili kupunguza kero ya usafiri kwa wananchi.
"Lakini Mtendaji Mkuu wa TANROADS hakikisheni katika vipaumbele vya barabara zitakazojengwa kwa lami iwe ni pamoja na barabara za Handeni-Mziha -Turiani( KM 108.2), Kiberashi-Songe (KM 33.5)na Songe-Gairo ili kuufungua vizuri mkoa wa Tanga hususan wilaya za Handeni na Kilindi"Alisema
Awali akizungumza katika ziara hiyo Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Mohammed Besta alimueleza Waziri huyo kwamba tayari TANROADS wameshawapanga mameneja wa miradi katika miradi yote 69 inayoendelea nchini ili kuhakikisha inatekelezwa kwa ubora unaotakiwa.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Handeni mjini Mh.Ruben Kwagirwa amempongeza Waziri wa ujenzi kwa miradi mbalimbali ya barabara inayoendelea mkoani Tanga na kusisitiza kwamba kufunguka kwa barabara ya Mkata -Kwamsisi (Km 36), Handeni Turiani (KM 108.2), Handeni- Kiberashi- Singida, (KM434), Kiberashi- Songe ( KM 33.5) na Songe -Gairo kutaufungua vizuri mkoa wa Tanga na kuuunganisha na makao makuu ya nchi Dodoma kwa njia fupi.
Waziri Bashungwa yupo katika ziara ya kukagua athari za mvua za vuli mkoani Tanga na kukagua miradi ya ujenzi wa barabara na madaraja inayoendelea mkoani Tanga.