Wafanyabiashara wa vyombo vya usafiri majini kupitia ulinzi shirikishi kwakushirikiana na jeshi la polisi Mwanza hivi majuzi katika eneo la Mwanza South wamefanikiwa kukamata watu wanaojihusisha na biashara haramu ya wizi wa mafuta kwa meli zinazopaki mara baada ya kutoka safari.
Chini ya ulinzi: Kulia ni mfanyakazi wa meli hiyo
Mchezo huo mchafu ulistukiwa na mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza bwana Kitana, ambaye pia ana miliki vyombo vya usafirishaji na uvuvi ziwani Victoria, mara baada ya kuona mazingira yasiyoeleweka alito taarifa kwa wamiliki wa meli ya Mv. Allez ambao kwa haraka walipanga mchakato wa mtego na siku iliyofuata walifanikiwa kushuhudia wizi huo mwanzo mwisho live bila chenga jinsi unavyochezwa.
Mpira wa kufyunzea mafuta hupita njia hii hadi chini kwenye injini.
Watuhumiwa hao katika mahojiano wamesema kuwa wamekuwa wakijihusisha na mchezo huo kwa kipindi kirefu wakishirikiana na wafanyakazi wa meli hiyo nao hufanya zoezi hilo nyakati za usiku pindi meli zinapotoka safari, kwa kufyonza mafuta yaliyosalia mara baada ya meli kutoka safarini na hili hufanyika kabla meli haijaandikiwa mafuta kwa safari inayofuata.
Mpira wa kufyonzea ukiwa kwenye chanzo (matanki ya mafuta) melini.
Wezi hao wakiwa na boti yao maarufu yenye jina la upako ‘ASANTE MUNGU’ waliokutwa wakifyonza mafuta hayo kiulaini, huku jumla ya madumu 140 yakinaswa mengine yakiwa tayari yameshibishwa mafuta huku mengine yakiwa kwenye foleni.
Watuhumiwa wakiwa sambamba na mtuhumiwa namba moja mfanyakazi wa meli hiyo (wa tatu kutoka kushoto)
Wizi wa mafuta umekuwa kero kubwa nao ukilalamikiwa sana na wamiliki wa vyombo mbalimbali vya usafirishaji ziwani Victoria hasa wamiliki wa TRC, Kampuni ya Marine Services.