ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 10, 2012

SITA ANG'ARISHA KAMPENI YA JACK FISH MWANZA

"Nichagulieni jembe hili linalofiti viganja vyangu" Waziri wa ushirikiano wa Afrika mashariki Mh. Samweli Sita akimnadi kwa wananchi bw. Jack Masamaki kwa wananchi wa Kirumba Mwanza kwaajili ya kinyang'anyiro cha kiti cha udiwani kata hiyo.

"Bado tunakabiliwa na changamoto kwenye miundo mbinu ya barabara, maji na umeme, muda wa kuzungumza umepitwa na wakati sasa ni wakati wa utekelezaji" Mpiganaji Jack 'Masamaki' kupitia tiketi ya CCM, alimwaga sera kwa wananchi wa kata yake kisha akapata nafasi ya kuomba kura za udiwani kwa uchaguzi utakaofanyika tarehe 1/04/2012.

Sehemu ya umati uliofurika kwenye uwanja wa Magomeni Kirumba katika mkutano wa hadhara wa kwanza wa kumnadi mgombea wa kiti cha udiwani kata ya Kirumba Mwanza, uchaguzi huu unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani ya kata hiyo marehemu Novatus Manoko.

"Mexico wamemudu sana ujenzi wa barabara sehemu za milima uko mkakati kuwawezesha madiwani wa Mwanza kufanya ziara wakaone ni jinsi gani wataboresha barabara sehemu za milima, wajifunze njia nyepesi za ujenzi wa barabara katika maeneo yote yanayopitika kwa tabu hivyo ndugu yangu Magufuli ajiandae kwani tunakwenda kushikamana" alisema Mh Samweli Sita

'Kubaliko' kwa vijana.

Kwa mugongo jeh!

Mh. Sita akishuka jukwaani na Jack Masamaki kuanza maandamano mara baada ya mkutano kumalizika.

Mh Sita -" Mie kifaa' Umeona mambo yangu jukwaani....???" Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza- Umetisha mheshimiwa...!!!

Kutoka kushoto meneja wa uwanja wa CCM Kirumba John Tegete, Mgombea udiwani Jack Masamaki na Mh. Sita.

Safari ikaanza kupita mitaani ambapo kituo cha mwisho ilikuwa ni ofisi za CCM kata ya Kirumba.

Akinamama walifunga vibwebwe kuhakikisha wanamuunga mkono mwana wao wa nyumbani kufanikisha adhma yake iliyo na nia njema kwa wakazi wa kata ya Kirumba.

Viatu isiwe tabu

Ngoma inogile.......

Salaaamu kwa wadau wa ukweli mitaa ya Kirumba Polisi.........

Msafara ulikatisha sokoni kwa mbwembwe ukitoa salamu kwa wapiga kura...

CHADEMA YAMWEKEA SIOYI SUMARI PINGAMIZI

PINGAMIZI
CHADEMA imemwekea pingamizi mgombea wa ccm,Sioyi,kwa madai kuwa sio raia wa Tanzania.CHADEMA imenasa barua ya siri yenye Kumb no.AR/C/32/VOL1/85, ya Feb 29/2/2012, kutoka kwa Afisa mfawidhi wa uhamiaji mkoa wa Arusha, kwenda kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha, ikifafanua uraia wa Sioyi, na katika ufafanuzi huo Ofisi ya uhamiaji inakiri kuwa kwa yeyote aliyezaliwa nje ya nchi, ukomo wa uraia wake ni pale anapofikisha miaka 18, na baada ya hapo anapaswa kuukana uraia wa nchi alipozaliwa, na Sioi Sumari alizaliwa Kenya,na hakuwahi kuomba uraia wa Tanzania.

From Mdau...

Friday, March 9, 2012

LIGI TAIFA NGAZI YA MKOA WA MWANZA YAANZA

Misungwi Stars.

Nange Fc.

Jukwaa kuu uwanja wa Mwanakanenge wilayani Misungwi.

Sehemu ya Mashabiki mchezoni.

Ligi ya Taifa ngazi ya mkoa wa Mwanza imeanza leo katika uwanja wa Mwanakanenge wilayani misungwi kwa mchezo kati ya Misungwi Stars na Nange Fc matokeo Misungwi stars wametoka kifua mbele kwa ushindi wa 4-1.

Iliwachukuwa dakika mbili tu timu ya Misungwi Stars kujipatia bao la kwanza kupitia mshambuliaji wake Godwin Mganga, dakika ya 10 goli la pili, la tatu dakika 35 kupitia Kulwa Mahamoud na Selemani kisendi alishindilia msumari wa mwisho dakika ya 89. Goli la kufutia machozi kwa Nange Fc lilipatikana dakika ya 13 kipindi cha kwanza.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho mchezo kati ya Nyamagana United watakaoshuka dimbani dhidi ya Chanel Afrika.

Nako kituo cha Geita uwanja wa Katolo mchezo utachezwa kati ya West Boyz na Polisi Geita.

Ligi ya kusaka nane bora ngazi ya mkoa inashirikisha timu 19 zilizojigawa katika makundi manne.

MBUNGE CHADEMA ASHINDA KESI YA UCHAGUZI MZ.

Wakili T. Lisu (kulia) ndiye aliyesimamia kidete kesi hiyo iliyompa ushindi mteja wake mbunge Highness Kiwia.
Mahakama kuu ya kanda ya Mwanza imemwachilia huru mbunge wa Ilemela Highness Kiwia kutokana na kesi ya madai namba 12 ya mwaka 2010, iliyo funguliwa na walalamikaji watatu ambao ni Lupilya, Nsubuga pamoja na Madenge, ambapo waliiomba mahakama Kuu Kanda ya Mwanza itengue ushindi wa Mbunge wa huyo kupitia CHADEMA, kwa madai kwamba mbunge huyo hakushinda kihalali kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Jaji Mjema alihitimisha kusoma hukumu hiyo kwa kusema kwamba: "Kwa kuzingatia ushahidi uliotolewa na walalamikaji pamoja na upande na maelezo ya wa wadaiwa, mahakama hii inatupilia mbali mashtaka haya, na walalamikaji wanapaswa kulipa gharama zote za kesi hii".

"Kwa kweli huu ni ushindi wa kihistoria kwa nchi hii ya Tanzania. Lakini naamini kesi ni gharama na nitawafungulia kesi hawa watu ili walipe gharama zote nilizotumia. Nitakaa na mwanasheria wangu Tundu Lisu tuone gharama kiasi gani tumetumia", alisema Mbunge Kiwia huku akishangiliwa na mamia ya wafuasi wake.

Jaji Gadi Mjema akitoa hukumu hiyo leo amesema ushahidi uliotolewa na wakazi hao hautoshelezi na hivyo mahakama imemuachia huru mbunge huyo dhidi ya kesi iliyokuwa ikimkabili.

UWF YAMTWAA MAMA MJASIRIAMALI ANAYEFUATA NYAYO ZA MWANAMAKUKA 2012

Pichani shoto ni Meneja matukio na Udhamini wa benki ya NBC,Rachel Remona akimkabidhi Mwanamke Mjasiliamali aliyeibuka na tuzo ya Mwanakuka,Bi.Tatu Mwenda mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni sita. Pichani kati kulia ni Mwenyekiti wa UWF (waandaji wa tuzo hiyo ya Mwanamakuka),Bi.Mwate Madinda sambamba na Mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, Dina Marios wakishuhudia tukio hilo adhimu kabisa, katika kuadhimisha siku ya Mwanamke Duniani, iliyofanyika leo,Hafla hiyo imefanyika usiku huu ndani ya hotel ya Serena, jijini Dar na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.

Pichani kushoto ni Meneja matukio na Udhamini wa benki ya NBC, Rachel Remona akimkabidhi mshindi wa pili wa tuzo ya Mwanamakuka, Bi. Mwanne Msekalile mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni mbili. Pichani kati kulia ni Mwenyekiti wa UWF (waandaji wa tuzo hiyo ya Mwanamakuka), Bi. Mwate Madinda sambamba na Mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, Dina Marios wakishuhudia tukio hilo adhimu kabisa, katika kuadhimisha siku ya Mwanamke Duniani, iliyofanyika leo, Hafla hiyo imefanyika usiku huu ndani ya hotel ya Serena, jijini Dar na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.

Meneja matukio na Udhamini wa benki ya NBC, Rachel Remona akimkabidhi mshindi wa tatu wa tuzo ya Mwanamakuka, Dada Sikudhani Daudi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano.

Mshindi wa tuzo ya mwanamke mjasiriamali ya Mwanamakuka, Bi. Tatu Mwenda akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa UWF huku akiwapungia mkono wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani) waliofika kwenye hafla hiyo iliyofana kwa kiasi kikubwa.

BIG UP WADAU.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUSITISHWA MGOMO WA MADAKTARI


Kwa: Wahariri wote;
TV,
RADIO,
MAGAZETI,
BLOGU,
Leo, tarehe 8, Machi 2012, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, mbele ya Jaji R.M. Rweyemamu, baada ya kusikiliza Ombi No. 24 la 2012 lililowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Mwombaji) dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari (Walalamikiwa), imetoa uamuzi ufuatao:

i) Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari pamoja na Wanachama wao, kusitisha Mgomo waliouanzisha rasmi tarehe 7 Machi 2012 nchi nzima na kurejea kazini mara moja kwa kuendelea na kazi zao kama kawaida, mara tu Amri hii itakapowafikia. Aidha, waombaji watatakiwa kutoa Kiapo cha kuthibitisha kwamba wamewasilisha Amri hiyo kwa Walalamikiwa na kuwasilisha Kiapo hicho Mahakama Kuu – Divisheni ya Kazi kesho tarehe 9,Mach 2012.

ii) Mara baada ya Amri hii kuwasilishwa kwa Walalamikiwa (Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari) watatakiwa kuwatangazia Wanachama wao kupitia Vyombo vya Habari kusitishwa kwa Mgomo huo Nchi nzima kama walivyowatangazia wakati wa kuitisha Mgomo huo;

iii) Mahakama inaamuru pande zote mbili (Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania pamoja na Jumuiya ya Madaktari) kutumia fursa za Kisheria zilizopo katika kutatua Mgogoro wa Kikazi uliopo kati yao kwa haraka.
(mwisho)
Imetolewa na:

Ofisi ya Waziri Mkuu,
S.L.P. 3021
DAR ES SALAAM.
Alhamisi Machi 8, 2012

WAUGUZI 25,000 WALIOGOMA WAFUTWA KAZI KENYA

WAKATI wauguzi nchini Tanzania wakiwa kwenye mgomo usio na kikomo serikali ya Kenya imewafukuza kazi wauguzi 25000 waliogoma kwa kushindwa kurudi kazini.

Msemaji wa serikali Alfred Mutua ametoa wito kwa ‘ watu wenye taaluma ya afya wote’ ambao hawana ajira au waliostaafu kufika hosiptali za umma kwa ajili ya kuajiriwa siku ya Ijumaa.

Wafanyakazi wa umma ambo wengi ni manesi waligoma tangu wiki iliyopita wakitaka kupandishiwa mishahara, marupupurupu na kuboreshewa mazingira ya kazi. Kwa wastani mfanyakazi wa sekta ya afya anapata kiasi cha shilingi 25,000 zaKenya($300, £190) kwa mwezi kwenye mshahara wake na posho.

Bw Mutua alisema wafanyakazi wa afya ‘hawaufuata maadili’ kwa kutorejea kwenye majukumuyao. Majina ya wafanyakazi hao yameondolewa katika orodha ya wafanyakazi wanaolipwa mshahara na si ‘waajiriwa wa serikali tena’

Thursday, March 8, 2012

BREAKING NEWS: DALADALA YAUWA WANAFUNZI WAWILI ENEO LA BUGANDO MWANZA

Leo majira ya saa nne asubuhi katika barabara ya kuelekea Hospitali ya Bugando imetokea ajali mbaya ya basi dogo la abiria (daladala) iliyokosa uelekeo na kusababisha vifo vya watoto wawili.Askari wa jeshi la polisi wakiondoa vizui vya mawe njiani barabara ya keuelekea Huspitali ya Bugando jijini Mwanza.

Mchoro wa ajali.
"Hii gari ilikuwa inatiokea Bugarika inashuka kuelekea mjini, kwa spidi aliyokuwa nayo dereva kwa kweli ilikuwa hairidhishi kwani gari liliyumba kabla ya kufika eneo la Bar ya Bugando Hill, imagine sisi tulikuwa pembeni ya barabara lakini kwa hofu tukalipisha tukakaa pembeni kabisaa. Lilipofika karibu na Shule ya msingi Bugando dereva wa gari kona ikawa kama imemshinda akakwepa akaenda kugonga nguzo ya umeme akawa anahangaika kurudi barabarani eneo ambako kuna kama kivuko kwa wanafunzi ikamshinda na kupitia watoto wawili waliokuwa wakisubiri kuvuka barabara kisha akagota kwenye mawe yaliyopangwa pembezoni" alisema Joseph Nyanda Karumbeti almaarufu kwa jina Baba Teresa, shuhuda wa ajali hiyo.

Mtoto Elizabeth Kamsoka mwanafunzi wa darasa la 7 shule ya Msingi Sahara alifariki dunia papo hapo katika eneo la ajali mara baada ya kupasuka kichwa mazingira yanayotisha, nae Baraka Revocatus mwanafunzi wa darasa la 4 shule ya msingi Bugando amefariki dunia akiwa Hospitali ya Rufaa Bugando wakati juhudi za madaktari kuokoa maisha yake zilipogonga mwamba.

Licha ya gari hili kuwa na mgonjwa aliyekuwa amezidiwa wananchi hawakutoa nafasi lipate pita.

Askari usalama barabarani akihusika na mchoro wa ajali hiyo iliyosababishwa na daladala ambapo dereva wake mara baada ya ajali alikimbia kusikojulikana.

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA ZIFUATAZO
Haya ni mabaki ya vipande vya fuvu la mtoto Elizabeth, blogu hii inaomba radhi kwa picha hii.

Ilikuwa ni hali ya kutisha blogu hii inaomba radhi kwa picha hii ya masalia ya ubongo wa marehemu eneo la ajali.

Kwa muda wa takribani saa nzima barabara hiyo haikupitika kwani mara baada ya ajali hiyo kutokea kundi la watu wanaoishi maeneo hayo walijitokeza na kufunga barabara kwa kuweka mawe makubwa hali iliyosababisa ugumu wa huduma za usariri kwa magari ya wagonjwa na abiria wanao toka au kuelekea Hospitali ya Bugando kupata huduma.

Nguzo iliyogongwa.
Baadhi ya abiria waliopata majeraha kwenye daladala iliyosababisha ajali wamepelekwa hospitali ya Bugando kupatiwa matibabu.

Mwenyezi Mungu zilaze pema peponi roho za marehemu.
Amen.

Wednesday, March 7, 2012

YATAKAYOJIRI KESHO JIJINI MWANZA

MH. VICKY KAMATA KUTOA BURUDANI TAMASHA LA KUONGEZA MAARIFA KUFANYIKA, MARCH 8, SIKU WANAWAKE DUNIANI KATIKA UKUMBI WA GOLD CREST JIJINI MWANZA!!
Tamasha la kuongeza maarifa, linatarajiwa kufanyika machi 8 mwaka huu, ikiwa ni siku ya wanawake duniani.

Tamasha limeandaliwa na akina dada kutoka kundi la Bedefesera hapa jijini Mwanza na litafanyika kwenye hoteli iliyo na hadhi ya kimataifa ya Gold crest.
Unajua utapata maarifa gani siku hiyo? Karibu uungane, kwa kununua kadi yako ya Tsh 30,000/= itakayokuwezesha pia kupata chakula cha jioni na vinywaji laini. Piga simu namba 0683962902 kwa manunuzi ya kadi yako.

Bedefesera inaundwa na watangazaji mahiri hapa nchini, akiwemo Rahab fred, Beatrice Rabach, Felister Kulwijira, Deborah Mpagama, Erica Elias na Seda Ilija.

Akizungumza na Blog hii, Mwenyekiti wa kikundi hicho Rahab Fred, amesema Tamasha litatoa mafunzo ya Ujasiriamali, Malezi ya Familia, Afya na jinsi ya kuweza kupata mikopo kwa masharti nafuu.

Burudani kabambe inatarajiwa kutolewa na mbunge wa viti maalum kutoka Geita Mh. Vick Kamata, pamoja na wasanii wengine maarufu kibao

Kazi kwenu wadau kuhudhuria tamasha hilo, hakika Blog hii, inawatakia mafanikio mema katika mwanzo mzuri wa kuongeza maarifa kwa wanajamii...Bigup Bedefesera!!!!!

SAYANSI NA TEKNOLOJIA YA KESHO ?

MAAJABU YA ULIMWENGU!
*Fahamu mikasa na vituko mbalimbali wanavyofanya baadhi ya wenye nyumba na wapangaji wa hapa Tanzania kwenye nyumba za kupanga, kwa kusoma hadithi yenye vituko vilivyotokea kwenye baadhi ya nyumba: HASIRA ZA MPANGAJI(HM).

*Fahamu pia jitihada mbalimbali wanazofanya wanasayansi wa nchi za magharibi katika kutafiti viumbe hai nje ya dunia (extraterrestrial life). NASA (National Aeronautics and Space Administration) yenye makao makuu yake Marekani, kwa kupitia projekti yao ya SETI, wanatafiti uwezekano wa kuwa na viumbe wenye akili na utashi kama binadamu wa hapa duniani. Viumbe vinavyosadikiwa kuishi kwenye sayari zilizo nje ya mfumo wa jua, kama vile sayari za Kepler-22b, GJ 1214b na Gliese 581d. (Mwanga {300,000km/s} huchukua miaka 20, kusafiri toka duniani hadi sayari ya Gliese 581d).

Utafiti huo hautaleta uhalisia kama utafanyika huku watafiti wakiwa duniani tu. Hivyo, wamejenga maabara yao huko nje ya dunia(International Space Station au ISS). Ipo kwenye kiwanja kinachoelea hewani!.

Wazo la kujenga maabara hiyo ya aina yake liliibuliwa mwaka 1869, baada ya mwandishi wa ki Amerika(Edward Everett Hale) wa hadithi ya kisayansi iitwayo “Brick Moon”, kuchapisha hadithi hiyo. Malighafi ya kwanza ya kujengea ISS ilipelekwa kwenye kiwanja hicho novemba 1998.Roketi ya Kirusi ilifanya kazi hiyo.Malighafi nyingi zaidi ziliongezwa kwa miaka miwili iliyofuata. Mpaka kufikia mwaka 2000, tayari jengo hilo lilifaa kwa watu kuishi ndani yake. Hivyo kikosi cha kwanza cha wana utafiti kilitua (docking) kwenye jengo hilo mwezi octoba, 2000.

Mwezi Julai mwaka jana (2011), NASA walikwenda ISS kwa kutumia usafiri maalumu,ATLANTIS. Mwishoni mwa mwaka jana, Warusi nao wakajitosa huko kwa kutumia SOYUZ.Na hivyo, kuhitimisha ukarabati wa nyumba hiyo inayoizunguka dunia kila baada ya dakika 90. ISS ina mabafu mawili na sehemu ya michezo(GYM). Jengo hilo la kiunajimu, ni kubwa kama nyumba ya vyumba vitano.

Ni changamoto gani wanakutana nazo?. Kwa nini jengo hilo linaelea?. Wanazigunduaje sayari mpya?. Kwa nini wanahatarisha maisha yao na kuteketeza mabilioni ya fedha ili kuwekeza kwenye utafiti huo?.Wataalamu mbali mbali duniani,wanasemaje juu ya utafiti huo?. Usiachwe nyuma, kimbia pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa kusoma riwaya ya HASIRA ZA MPANGAJI, uhabarike, uburudike na kujiongezea maarifa ya mtindo huo.

*Waandalie watoto mazingira mazuri ya kuipenda sayansi na teknolojia kwa kuwazawadia riwaya ya kisayansi: HASIRA ZA MPANGAJI.
*Kwa wapenzi wa kutalii,usikubali kutalii ndani ya dunia tu, ungana na mwandishi wa HASIRA ZA MPANGAJI usafiri kwenda nje ya dunia, uitalii jiografia, sayansi na maisha ya watu wa huko.
Kwa kanda ya ziwa, HASIRA ZA MPANGAJI inapatikana kwa Tshs 3500/= tu kwa wauza magazeti na vitabu walio maeneo yafuatayo;
<>MWANZA MJINI(PPF PLAZA,MAKOROBOI,SOKONI,TANESC O,KAMANGA FERRY,0764331568,0755734574)-Pia inapatikana kwenye VICTORIA BOOKSHOP. (BURUDIKA!: BAADA YA MIAKA 1200 TOKA SASA, TEKNOLOJIA YAWEZA KUFIKIA WAPI?,JIBU=HM)

<>KAKOLA (0764361519), KAHAMA (0753574124), MUSOMA- KAMISA(0755004410), BUKOBA (0713918505, 0754552485), BUNDA(0655282034), TARIME(0765649612), SHINYANGA (0755873500),GEITA(0759419303) , SENGEREMA(0753982040, 0769359373).
NA HIVI KARIBUNI, ITATUA DAR ES SALAAM.

Tujadiliane kupitia riwaya za kisayansi na kiteknolojia!.

Tuesday, March 6, 2012

TUZO ZA DIAGEO ZA WAANDISHI WA HABARI ZA BIASHARA AFRIKA 2012-ZAZINDULIWA RASMI.

Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Bi. Teddy Mapunda akifafanua kwa msisitizo namna ya kushiriki, kwenye uzinduzi wa tuzo za Diageo za Waandishi wa habari za Biasharara Afrika ((Diageo Africa Business Reporting Awards 2012). (Picha kwa hisani ya Michuzijr Blog)

----
*TUZO HIZI ZINAENZI UANDISHI WA HABARI ZA BIASHARA AFRIKA.

*Usajili wa tuzo sasa uko wazi kufanyika kwenye tovuti.

Kampuni ya Biaya Serengeti (SBL), ambayo ni kampuni tanzu ya Diageo, inayoongoza duniani katika biashara ya vinywaji vyenye kileo, leo wamezindua rasmi tuzo za habari za kibiashara kwa mwaka huu 2012.

Tuzo hizi zilianzishwa na Diageo mwaka 2004, kwa ajili ya kuwatambua waandishi wa habari na wahariri ambao wameweza kutoa taarifa zilizojitosheleza na za hali ya juu katika mazingira ya biashara Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Bi. Teddy Mapunda alisema“ Kampuni ya Diageo inaamini kwamba taarifa nzuri na zina mchango mkubwa wa kuinua mtazamo wa maendeleo na uchumi wa Afrika na changamoto zake.”

Habari hizo kwa kiasi kikubwa zinahamasisha nia ya kufanya biashara na zinaangaza mazingira mazuri na ya uhakika juu ya utajiri wa bara hili,”alisema Bi Mapunda.

Bw. Nick Blazquez, Raiswa Diageo Afrika, naye alitoa vielelezo kuhusu tuzo hizi na alikuwa na haya ya kusema: “Ni dhahiri kabisa sasa kwamba hamasa ya biashara Afrika imepanuka na dunia nzima sasa imeridhika na kiwango cha ukuaji wa uchumi barani Afrika.

Kama kampuni inayoendesha shughuli za kibiashara Afrika, tunaelewa umuhimu wa kuongezeka kwa taaluma ya uandishi wa habari za kiabishara na jinsi inavyounda mazingira mazuri na kuvutia kwa uwekezaji wa muda mrefu,” aliongeza.

“Nikiangalia miaka ya nyuma n amaendeleo ya tuzohizi, nimetambua uamsho wa hali ya juu na viwango vilivyomo katika uandishi wa habari za kibiashara na kuongezeka kwa juhudi za vyo mbo ya habari ndani na njeya Afrika ili kuhamasisha biashara na ujasiria mali barani humu.

Ninajivuniakwamba Diageo inatambua mafanikio haya na tunategemea kuona mchango wa hali ya juu kwa siku za usoni.”

Wakati tuzo hizi za waandishi wa habari za biashara Afrika kutoka Diageo zinakaribia kutimiza miaka kumi tangu kuanzishwa kwake, Diageo inaendelea kufikiria jinsi watakavyobadilisha uhalisia, matokeo na namna ya kuwafikia zaidi walengwa wa tuzo hizi.

Diageo inategemea kuboresha zaidi utoaji wa tuzo hizi kupitia mafanikio ya mwaka uliopita, kukaribisha usajili kutoka vyombo vyote vya habari na kutoka bara zima la Afrika na nje yaAfrika.

Mwaka huu, kundi la mfumo mpya wa utoaji wa habari limeondolewa na kuwa kundi linalojitegemea ili kuonyesha upana wa vyombo vinavyotumia mfumo huu wa utoaji habari.

Waandishi wa habari wanahamasishwa kutuma maombi yao. Habari ziwe zimetolewa kupitia mfumo wa vyombo vyote vya habari, ikiwa ni pamoja na gazetimtandazo (blogs) na habari zilizochapishwa kupitia tovuti mbalimbali pia wanaruhusiwa katika makundi yote, yaani 'categories'.

Sherehe yaTuzo hizi zitafanyika mjini London, Uingereza tarehe 28 mwezi Juni.Tarehe ya mwisho wa kupokelewa kwa maombi haya ni siku ya Ijumaa tarehe 23 mwezi Machi mwaka huu. Maombi yote yatumwe kupitia tovuti yetu: www.diageoafricabusinessreportingawards.com.

Hakuna kiingilio.

KAZI YA POLISI TABORA

Hassani akikanyagwa na askari wa jeshi la polisi Tabora.
From DEBORAH MPAGAMA,
Urambo Tabora.

Hivi karibuni nilikuwa katika wilaya ya urambo mkoani Tabora ambapo kijana mmoja aitwae Hassan Mgalu akiwa katika soko la wilaya hiyo aligongwa na baiskeli na aliye mgonga alikuwa askari aliyevaa nguo za kiraia baada ya Hassani kugongwa na askari huyo hali ilikuwa hivi:-

Hassani; kwanini umenigonga ?
Askari ; kwanini unataka nini?
Hassani; yani unanigonga na baiskeli na unasema nataka nini?

Hassani akampiga kibao askari huyo ambaye alikuwa amevaa nguo za kiraia, kufatia hali hiyo askari huyo aliondoka na kuwafata wenzie ambao walikuwa na nguo za kirai na walimkuta Hassani akicheza pull katika eneo la standi ya zamani wilayani humo, mmmmh, wamshushia kipigo cha hali ya juu na kumvuta kwa moja kushika mguu wa kulia na mwingine mguu wa kushoto kichwa kikijibuluza chini umbali wa mita 2000 mpaka karibu na ofisi ya ushirika ya urambo na benki ya NMB ambapo walimtupia katika bajaji hiyo ambayo unaiyona hapo katika picha mmoja akiwa amemkanyaga kichwa chake.

Kutokana na mateso makali aliyoyapata hassani alipoteza maisha , katika jalada lililofunguliwa kwenye kituo cha polisi urambo maelezo yaliandikwa amepigwa na wananchi wenye hasira jambo ambalo si kweli na lilileta utata kati ya wanafamila na wananchi wa eneo hilo ,ni meeandika haya ili upate picha.

Je askari anahaki ya kumpiga raia, manyanyaso haya ya raia kwa kutofahamu sheria mpaka lini, umegongwa na baiskeli, unapigwa na hata kutolewa uhai wako tutafika?

Monday, March 5, 2012

PICHA ZA AWALI ZA FIDELINE IRANGA ZAANZA KULIKI

Mara baada ya kimya kingi na na maswali mengi kutawala fikra na vinywa vya watu juu ya wapi alipojificha Super Model mwenye mvuto wa kipekee toka nchini Tanzania anayekwenda kwa jina la Fideline Iranga hatimaye picha zake za awali za 'modo' huyo zimeanza kuliki' kupitia mitandao ya marafiki zake tena akiwa katika muonekano mpya kabisa ambao umewashtua wengi akiwa 'kimodo' hata wakihoji kunani na wasipate majibu.

Picha hii na hiyo ya awali juu zimetoka hivi majuzi katika siku yake ya kuzaliwa kupitia Blogu ya U-turn
zikimuwishi na zikiwa na maneno 'Karudije kuwa mwembamba usupa model umerudi tutakomaje sasa kwenye runway.... chezea Fide'

Idadi ya watu waliokomenti juu ya picha hizo wameonekana wakijigawa katika pande mbili, kundi la kwanza likilaumu hatua aliyoichukuwa ya kujikondesha na kundila pili likisifia mpango huo.

Komenta mmoja kasema:- "Wabongo bwana yaani mtz akipungua hata kama alikuwa anafanya diet watauliza kaumwa nini? Kawaje? na wengine watampachika maradhi kuwa siyo diet, lakini akifanya mzungu/black mzungu kama Jernifer Hudson itawatoka wow na masifa kibao, kafanya diet kapendeza blah blah!"

Fide tha way back.....

Alitambulika sana kwa picha za vivazi nusu dizaini halikadhalika zenye mikao ya 'UTATA' swali ni jeh! SECOND SEASSON ya ujio wake Fide, atarejea na style zipi?

Si mara ya kwanza kwa watz kuhusika na projekti kama hizi za kupunguza mwili kwani hata mbunifu maarufu wa mavazi nchini Hassanali naye alipata kuhusika na sasa maisha yanasonga...

Any ways twakungoja sana siku utakapo jitokeza hadharani, Kila la kheri mdafada Fideline Iranga.

Sunday, March 4, 2012

MKISIKIA PWAAA.... MSISHANGAE!!!

Ni jengo la ghorofa moja linalopatikana katikati ya jiji la Mwanza, jengo ambalo halijamalizika miaka mingi sasa kiasi cha kuonekana kama kumomonyoka baadhi ya sehemu zake, eneo la chini shughuli za biashara muhimu zinaendelea kama kawaida....

Hebu tulisogelee bango la mkandarasi... duh limechoka halisomeki kwa ufasaha..niiii....ah wapi, ila CLIENT ni some body Mohamed Khan

Katika mjengo huu juu ambao kimsingi unamazingira hatarishi kuna familia zinaishi, baadhi ya sehemu za kuta zinavuja kwa mimea kuota juu ya kuta hizo hivyo kuozesha baadhi ya samani ambazo ni nguzo mhimili wa 'lihausi hili'.

Wadau husika pale Halmashauri MUPO au MUMERARA?....?

SIMBA WAIONDOSHA KIYOVU KOMBE LA SHIRIKISHO

Mchezo baina ya timu ya Simba dhidi ya Kiyovu ya nchini Rwanda uliomalizika jioni hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba imeshinda 2-1 na kujihakikishia kuendelea na mashindano ya Kombe la Shirikisho.

Simba Sc

Kiyovu

Wachambuzi wa soka toka Clouds Fm na Clouds Tv Ephraim Kibonde (L) na Shaffih Dauda (R) wakiliendeleza gurudumu.

Tamu tamu ya burudani dimbani.

Mshambuliaji Felix Sunzu ndiye aliye pachika mabao ya timu ya Simba katika Dakika ya 19 na 32 za kipindi cha kwanza cha mchezo baada ya kupata pasi safi kabisa kutoka kwa mchezaji Emmanuel Okwi nao Kiyovu walipata goli dk ya 76.

Hadi mwisho Simba 2 Kiyovu 1.
(Picha zote kwa hisani ya blogu ya JIACHIE)

ZAIDI BOFYA HAPA CHINI
http://www.michuzijr.blogspot.com/2012/03/simba-sc-wanaongoza-goli-2-dhidi-ya.html