"Hii gari ilikuwa inatiokea Bugarika inashuka kuelekea mjini, kwa spidi aliyokuwa nayo dereva kwa kweli ilikuwa hairidhishi kwani gari liliyumba kabla ya kufika eneo la Bar ya Bugando Hill, imagine sisi tulikuwa pembeni ya barabara lakini kwa hofu tukalipisha tukakaa pembeni kabisaa. Lilipofika karibu na Shule ya msingi Bugando dereva wa gari kona ikawa kama imemshinda akakwepa akaenda kugonga nguzo ya umeme akawa anahangaika kurudi barabarani eneo ambako kuna kama kivuko kwa wanafunzi ikamshinda na kupitia watoto wawili waliokuwa wakisubiri kuvuka barabara kisha akagota kwenye mawe yaliyopangwa pembezoni" alisema Joseph Nyanda Karumbeti almaarufu kwa jina Baba Teresa, shuhuda wa ajali hiyo.
TUNAOMBA RADHI KWA PICHA ZIFUATAZO
Baadhi ya abiria waliopata majeraha kwenye daladala iliyosababisha ajali wamepelekwa hospitali ya Bugando kupatiwa matibabu.
Mwenyezi Mungu zilaze pema peponi roho za marehemu.
Amen.
Tupe maoni yako
inasikitisha sana kwa madereva wetu kukosa umakini nani alaumiwe ni jeshi la polisi kutowajibika ipaswavyo wao wamegeuza magari hayo mabovu kuwa mtaji kuyaacha yafanye kazi.
ReplyDeleteMagari ya Bugarika yote vimeo tunategemea nini sasa?
ReplyDeleteNimeiona kupitia star tv jana usiku nimeogopa kweli hata kutumia usafiri wangu leo kazini nimmeamuakupanda tax.
ReplyDeleteKuhusu suala la dereva abanwe mwajiri wake atapatikana tu.
ReplyDeleteEwe Mola tunusuru waja wako zilaze pema roho za marehemu.
Sasa ao waliweka mawe huku ambulance yenye mgonjwa ikipaswa kupita kuwahisha mgonjwa ni akili au matope busara ni kuzuia magari ya huduma za hawaida na si magari yenye wagonjwa hata ivo nimeumia sana kwa tukio la ajali pole kwa familia zilizopoteza watoto wao ongera jisengo kwa habari.
ReplyDelete