KATIKA kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya elimu hapa nchini Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete kwa kushirikiana na shirika lisilokuwa la kiserikali la KULEA Child Care Villages wametoa msaada wa vitabu 3468 vya kujifunzia masomo ya sayansi na hisabati katika shule za msingi na sekondari vyenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni 70.
.
Akikabidhi msaada huo wa vitabu kwa Mwalimu mkuu shule ya sekondari Mdaula , Melkisedek Komba ambaye aliyepokea vitabu hivyo kwa niaba ya wakuu wa shule nyingine Ridhiwani amesema kwamba vitabu hivyo vitaweza kuleta mabadiiko makubwa katika Nyanja ya elimu hususan katika masomo ya sayansi na ufaulu utaweza kuongezeka.
MSIKILIZE MHE. RIDHIWANI KIKWETE
Aidha Ridhiwani amesema vitabu hivyo vitagawanywa katika tarafa tano zilizopo kwenye halmashauri ya Mji wa Chalinze ambapo tarafa ya Chalinze imepatiwa vitabu 998 na tarafa nne za Msoga, Miono, Msata na Kwaruhombo zitapata vitabu 610 kwa kila tarafa na kuwataka wanafunzi na walimu kuwahimiza wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao mashuleni.
MSIKILIZE MBUNGE
Kwa upande wake Mkuu wa shule ya sekondari Mdaula Melkisedek Komba amesema msaada huo wa vitabu utaweza kuleta mabadiliko chanya kwa kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi hasa katika masomo ya sayansi kwani hapo awali walikuwa wanakabiliwa na uhaba wa vitabu vya kufundishia.
MSIKILIZE MWALIMU MKUU
Mariam Bofi ni mmoja wa wanafunzi wanaosoma katika shule ya sekondari Mdaula kidato cha tatu akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake ametoa shukrani kwa Mbunge pamoja na Shirika hilo na kusema kuwa vitabu hivyo vitaweza kuwasaidia zaidi kujisomea katika masomo ya sayansi kwani hapo awali walikuwa na changamoto ya uhaba wa vitabu.
MSIKILIZE MWANAFUNZI
SHULE za msingi na sekondari katika Jimbo la Chalinze kwa sasa bado zinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vitabu vya kufundishia masomo ya sayansi hivyo kutolewa kwa msaada huo utakuwa ni mkombozi mkubwa wa kuleta mabadiliko na kuongeza kiwango cha ufaulu zaidi kwa wanafunzi katika masomo hayo ya sayansi.