ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 5, 2013

MATUKIO YA MISS TUSKER LIGHT KAHAMA.

Chief Judge Kijukuu cha Bibi.

Vazi la Chubwiiii...!!! (majini...)
Huyu ndiye Tusker Light Miss Kahama 2013
African thing.

Simple.
Kiubunifu zaidi.
Mwanamke kangaaaa...
Dizaini za ufumkweni.
Burudani zaidi.
Mambo ya talent.
Maridadi.
Hapo vipi..
Vazi mtoko wa usiku.
Dance la utambulisho.
Vazi la ufukweni..
Tuko pamoja mazee.. 
Kwa picha zaidi tembelea http://bundalawilliam.blogspot.com/

BOTSWANA WILL SUPPORT "IBF SPORTS TOURISM PROGRAM" SAYS THE ENVIRONMENT & TOURISM MINISTER HON. T. KHAMA

INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICAMIDDLE EAST, ARABIAN & PERSIAN GULF SATURDAY 06, 2013 - Botswana’s Minister for Environment and Tourism Hon. Tshekedi Khama (seeing in the attached photo with the IBF/Africa President Onesmo Ngowi) pledged his government’s support to the success of "IBF Sports Tourism Program" for African countries.
Hon. Tshekedi Khama assured the IBF/Africa President, Onesmo Ngowi of his government's support towards the development of "Sports Tourism" to Africa as one of sustainable by-products of tourism sector.

The IBF/Africa President paid a courtesy visit to the Minister for Environment and TourismHon. Tsekedi Khama in the minister’s office as part of his marketing drive for the “IBF International Jr. Featherweight Title” which Botswana’s pro-boxer Lesley Sekotswe will meet a boxer from Britain to be announced soon.
  
This epic event will be televised live by Super Sports 9 and streamlined by VoxAfrica by to over 100 million homes in Europe, Asia, Africa and the USA.

The event will present great opportunity to Botswana to showcase its tourism attractions tomillions of inbound tourists. Such a befitting event will also attract direct investmentswhich Botswana needs for its economic diversification from its mineral based economy.

Over the decades, tourism has experienced continued growth and deepeningdiversification to become one of the fastest growing economic sectors in the world. Today, the business volume of tourism equals or even surpasses that of oil exports, food products or automobiles. 

Tourism has become one of the major players in international commerce, and represents at the same time one of the main income sources for many developing countries. This growth goes hand in hand with an increasing diversification and competition among destinations.


"Sports Tourism" globally provides a forum where stakeholders leans how to properly utilize it to effect profound positive change for destination positioning.


Through the much needed awareness and interactions provided over by the "Sports Tourism", stakeholders  are able to learn new trends in the industry, provide much needed information on their respective destinations and also the various tourism by-products in place which are effective promotional tools within the various destinations.


According to the UNWTO, tourism sector generates over US$ 4.5 trillion per annual and out of this figure "Sports Tourism" generated over US$ 100 billion.


BOTSWANA has made gigantic strides to pro-boxing as a result of the President of IBF/AFRICA Onesmo Ngowi's historic visit, in April 1-6 2013 this year. The visit excited a lot of boxing stakeholders in this countryAlso, the visit has also helped to encourage the number of experienced amateur boxers to join professional boxing ranks hence the October 5tournament.


Upon arrival in Botswana in October 02, the IBF/Africa President met several high ranking government officials as well as corporate leaders to encourage them to support the "IBF Sports Tourism" initiative to Africa of which Botswana is one of the six pilot countries. Other countries are Namibia, Tanzania, Ghana, UAE, South Africa and Tunisia respectively.

Botswana is endowed with great wealth in terms of mineral resources (diamond, gold and uranium) and exports of meat to Europe, Asia and USA. It has great amateur boxing foundation as most of her boxers perform well in various international meets hence the great potential fueling pro-boxing.
  
Under its pet project of "IBF Sports Tourism", the IBF/AFRICA has projected Botswana as the strong foundation for future boxing tournaments given its strong amateur boxing foundation, vibrant economy and good governance.

"These are the three pillars and ingredients of boxing development so we can see positive signs ahead” echoed the IBF/AFRICA PresidentOnesmo Ngowi who was a professional boxer on how he sees Botswana's direction in pro-boxing.

Ngowi illustrated that Botswana’s "economy and good governance" are key towards sustainable boxing development. "You need to build up a strong foundation for "Sports Tourism" and many developing countries fail to succeed due to their poor economies and governance. When you have GDP Per Capita Income in the region of  US$ 3000 then you can afford to pay $ 200 - $ 500 to see boxing events". he emphasized.

Also, the IBF/AFRICA's President alluded that lack of "TV and Corporate Sponsorship" may be another contributing factor for poor showing of Africa in the boxing industry. "Our TV Networks want promoters to pay them when showing their boxing tournaments instead of them TV paying for the boxing broadcasting" continued Ngowi.

The Botswana's October 5, 2013 tournament is coming at a time when the world’s diamond merchants De Beers are moving its international auction headquarter from London to Gaborone Botswana. The move herald Botswana’s robust economic development and the country’s keen interests to diversify its economy hence  development of tourism sector.


Given these rather positive trends, Sports Tourism as one of by-products of tourism is coming at the right moment.

Friday, October 4, 2013

GHASIA BAADA YA MAUAJI MOMBASA

Taarifa kutoka mjini Mombasa pwani ya Kenya zinasema kuwa vijana wameteketeza kanisa katika ghasia ambzo zimezuka kufuatia kuuwa kwa muhuburi wa kiisilamu. Inaarifiwa mtu mmoja ameuawa keenye ghasia hizo.
Sheikh Ibrahim Omar aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa na washirika wake watatu.
Polisi wamesema kuwa muhubiri huyo alikuwa amehubiri katika msikiti uliohusishwa na wanamgambo wa kiisilamu wa Al Shabaab.
Haijulikani aliyetekeleza mauaji hayo ya usiku wa kuamkia leo huku kukiendelea kuwa na hali ya wasiwasi miongini mwa waisilamu na maafisa wa usalama mjini humo.
Sheikh Ibrahim Rogo alikuwa muhubiri katika msikiti alipokuwa akihubiri marehemu Sheikh Aboud Rogo ambaye pia aliuawa kwa kupigwa risasi. Aliuawa na watu wengine watatu walipokuwa wanarejea nyumbani Alhamisi usiku baada ya kuhubiri.
Jeshi la zimamoto likifanya juhudi kuuzima moto huo uliozushwa kwenye kanisa hilo.
Sheikh Rogo alishutumiwa kutoa mafunzo yenye itikadi kali yaliyowashawishi vijana kujiunga na makundi ya kigaidi kama Al Shabaab.
Mauaji haya ni sawa na ya marehemu Aboud Rogo Mohammed mwaka jana na ambayo yalisababisha ghasia mjini humo.
Yanakuja wiki mbili tu baada ya shambulizi la kigaidi lililofanywa dhidi ya jumba la maduka la Westgate ambapo watu 67 waliuawa
Kundi la kigaidi la al-Shabab lilikiri kufanya mashambulizi hayo ya kigaidi.
Aboud Rogo alidaiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la al-Shabab na baadhi ya waisilamu walioshutumu polisi waliomuua walisema kuwa yalikuwa madai tu wala.
Ibrahim Rogo alionekana kama mrithi wa marehemu Aboud Rogo, alipohutubu katika msikiti huo.
CHANZO: BBC Swahili.

WENGINE TENA WAULA DROO YA SUMSUNG

Meneja masoko wa Kampuni ya Samsung nchini, Sylivester Manyara (kushoto),Msimamizi mwandamizi wa Bahati na sibu ya Taifa, Emmanuel Mdaki na Mratibu wa Programu za Samsung, Lawrence Andrew wakichezesha droo ya mwezi kwa wateja wa bidhaa za Kampuni hiyo Mwenge Dar es Salaam jana.
Meneja masoko wa Kampuni ya Samsung nchini, Sylivester Manyara (kushoto),Msimamizi mwandamizi wa Bahati na sibu ya Taifa, Emmanuel Mdaki na Mratibu wa Programu za Samsung, Lawrence Andrew wakimpigia mteja aliyeshinda kwenye droo ya mwezi kwa wateja wa bidhaa za Kampuni hiyo Mwenge Dar es Salaam jana.
Meneja masoko wa Kampuni ya Samsung nchini, Sylivester Manyara(wa tatu kushoto) akiwaonyesha baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam namana  ya droo inavyochezesha na washindi wanavyopatikana wakati wa kuchezesha droo ya mwezi iliyochezeshwa Mwenge Dar es Salaam jana.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Toleo La leo;

SAMSUNG YALETA UHAKIKA NA MFUMO WA “E-WARRANTY”.
 “Mfumo wa E-Warranty yawasaidia wateja wa Samsung kishinda zawadi mabalimali”

Alhamisi, October 3  2013;

Dar es Salaam: Kwa mara nyingine tena Kampuni ya Samsung Tanzania imechezesha droo ya mfumo wake wa “E-Warranty”, washindi walitangazwa katika hafla iliyoandaliwa katika Stendi Kuu ya Mwenge, jijini Dar es Salaam. Mfumo huu wa “E-Warranty ni mbinu inayotumiwa na Kampuni ya Samsung kama jinsi ya kukumbana na bidhaa feki zinazopatikana kwenye soko la Tanzania.

Mfumo huo wa e-warranty unawasaidia wateja kujua kama simu ya Samsung ni halali au ni feki. Wateja wanapaswa kusajali simu zao pale wanapozinunua na hivyo kupata dhamana ya miezi 24.
Meneja Mkuu wa Samsung Tanzania, Bwana Kishor Kumar akizungumuza na waandishi wa habari alisema “Mfumo wa E-Warranty imeonyesha kwamba ni mbinu bora zaidi dhidi ya kukumbana na bidhaa feki kwani wateja wengi wanasajili simu zao. Tunawahimiza wateja wetu  waendele kutuunga mkono kwa kununu bidhaa bora na kuzisajili na hivyo kupata nafasi ya kujishindia bidhaa kabambe za Samsung katika droo zetu”.

Washindi wanaweza kushinda zawadi 1 kati ya hizi 10: Televisheni 1 aina ya LED ya inchi 32, laptop 1, Kamera 3, home theatre 3 na simu 2 aina ya Galaxy Grand.

Bwana Kumar aliendelea kusema “ Licha na kujua kama simu mteja anayotaka kununua ni bora au feki, mfumo wa e-warranty unawasiadia wateja kujua kama simu hiyo inadhama ya miezi 24, kama simu hiyo inatafutwa au imeibiwa na kama simu hiyo ni mpya au imeshatumika”.

Kujua kama simu ni halali, mteja anatakiwa kufuta maelekezo yafuatayo: Tuma ujumbe na neno ‘Check’ ikifuatiwa na alama ya nyota (*) kisha namba ya IMEI, ikifuatiwa na alama ya reli (#) na kutuma kwa namba ‘15685’. Ujumbe unatumwa moja kwa moja kuelezea hadhi ya simu hiyo ya Samsung.

“Mfumo huu wa e-warranty ulianzishwa haswa kukabiliana na changamoto moto inayoikumba soko la simu za mkononi huku Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, ambapo kuna simu nyingi ni za bandia, za wizi, zilizotumika na simu ambazo hazina dhamana”, alisema Bwana, Kumar.

Bwana Kumar alimaliza kwa kusema ‘ili kuboresha huduma zetu za mfumo wa e-warranty, wateja watakaonunua simu aina ya Galaxy S 4 (iliyozinduliwa mwezi huu jijini Dar es Salaam), watapata huduma mpya inayoitwa ADH. ADH (Accidental Damage from Handling), ni huduma inayoilinda simu hiyo ya S 4 kutoka uharibifu kutokana na matumizi ya kawaida’.

Ilikujiunga na huduma ya ADH, wateja wanatakiwa kujisajili na mfumo wa e-warranty na usajili untakiwa kufanywa ndani ya siku 30 tangu kununuliwa kwa simu. Athari ya kutokujiunga na mfumo wa e-warranty kwa muda unaotakikana ni kwamba simu hiyo ya S4 haitaweza kutengenezwa kwa bure pale ambapo itaharibika.

Baada ya Draw washindi waliobahatika ni;

1.       Mshindi wa Kwanza:
                                Jina Kamili:
                                Anatokea:
2.       Mshindi wa Pili:
                                Jina Kamili:
                                Anatokea:                          
3.       Mshindi wa Tatu:
                                Jina Kamili:
                                Anatokea:          
4.       Mshindi wa Nne:
                                Jina Kamili:
                                Anatokea:          
5.       Mshindi wa Tano:
                                Jina Kamili:
                                Anatokea:          
6.       Mshindi wa Sita:
                                Jina Kamili:
                                Anatokea:
7.       Mshindi wa Saba:
                                Jina Kamili:
                                Anatokea:          
8.       Mshindi wa Nane:
                                Jina Kamili:
                                Anatokea:          
9.       Mshindi wa Tisa:
                                Jina Kamili:
                                Anatokea:          
10.   Mshindi wa Kumi:
                                Jina Kamili:
                                Anatokea:                          
Kwa maelezo zaidi wasiliana na;
Sylvester Manyara, Meneja wa Mauzo na Usambazaji,
Mobile; +255 683 984 215,

Kuhusu Samsung;

Samsung inafahamika Dunia nzima kwa teknolojia ya kisasa, inatengeneza bidhaa bora kabisa kwa kuzingatia mazingira halisi ya Afrika. Samsung ina idara tatu ambazo ni Samsung Mobile inayohusika na simu za mkononi za Samsung za aina zote. Samsung Electronics inayohusika na vifaa vya Samsung majumbani kama Viyoyozi, majokofu, mashine za kufulia etc. Na mwisho kabisa Samsung IT inayohusika na laptop, mashine za nukushi (photocopy), na kamera. Kwa maelezo zaidi tembelea www.samsung.com

KUANZIA SASA MBAVU ZAKO ZIKO HATARINI KUPITIA TBC 2.

Babatan family comedy, show hii kuruka TBC 2 kuanzia leo na kila Ijumaa saa 3 usiku na marudio Jumapili saa nane mchana... USKOSE MJOMBA....

Thursday, October 3, 2013

MKUU WA MKOA WA MWANZA KUSHIRIKI ROCK CITY MARATHON

Afisa Michezo Jiji la Mwanza Mohamed Bitegeko ambaye alisimama kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akimpokelea fomu Mkuu wa Mkoa ushiriki wa mbio za Rock City Marathon.
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza kushiriki Rock City Marathon 2013
Na Albert G. Sengo Mwanza.

MARA baada ya Kamati ya maandalizi ya mbio za Rock City Marathon 2013 hii leo kutangaza usajili rasmi kwa washiriki, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo ametangaza kushiriki mbio hizo kutokana na umaarufu wake maeneo mengi Kanda ya Ziwa.

Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika tarehe 27 Oktoba ,2013 katika uwanja wa CCM Kirumba na tayari watu wengi wameanza kuchukua fomu ili kushiriki.
Afisa Michezo Jiji la Mwanza Mohamed Bitegeko ambaye alisimama kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akipokea jezi atakayo vaa Mkuu wa Mkoa siku ya ushindani mbio za Rock City Marathon.
 Ndikilo alitangaza ushiriki wake hii leo katika hafla fupi ya uzinduzi wa Rock City Marathon 2013 kanda ya ziwa yenye lengo la kuhamasisha wananchi wengi kujitokeza mwaka huu.

Ndikilo ambaye aliwakilishwa na, Afisa Michezo Jiji la Mwanza Mohamed Bitegeko, mbali na kuipongeza kampuni ya Capital Plus International ambayo ni mwaandaji wa mbio hizo, alitoa wito kwa viongozi wa chama cha Riadha Mkoani Mwanza, waratibu na wasimamizi wa michezo wilayani na Mkoa wa Mwanza kuongeza nguvu katika kuhamasisha ushiriki wa watu ili mkoa huo uweze kuvumbua na kuinua vipaji vipya katika riadha.

“Ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), African Barrick Gold, Precision Air, Airtel, Bank M, Parastal Pensions Fund (PPF), Nyanza Bottlers, New Mwanza Hotel, Sahara Communication na Umoja Swithch ambao wamejitokeza kuunga mkono jitihada hizi ambazo zitasaidia kuinua mchezo wa riadha nchini pamoja na kutangaza nchi yetu,” alisema.
Wadau mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo kuelekea Rock City Marathon.
Aliagiza viongozi wa michezo na utamaduni wa Mwanza kuitumia fursa inayoletwa na mbio hizo ili kutangaza mkoa wa Mwanza, na Tanzania kwa jumla kimataifa.

“Tumeshuhudia wanariadha mbali mbali vijana wa nchi kama Kenya wakiibuka washindi katika mbio zilizofanyika mjini Berlin, Ujerumani hivi karibuni na kujinyakulia fedha nyingi pamoja na zawadi mbali mbali. Hii iwe chachu kwetu kama mkoa na Taifa kwa ujumla kutilia mkazo mchezo huu kwani licha ya kuwa ni ajira kwa vijana lakini pia zinatumika kama kitambulisho kikubwa cha taifa letu kimataifa endapo wanariadha wetu wataweza kufanya vizuri,” alisema Ndikilo. 

Picha ya pamoja ya wadauna wadhamini wa Rock City Marathon 2013.
 Nae Mwenyekiti wa Chama cha Riadha mkoa wa Mwanza Silas Nkungu alisema mbiyo za Rock City Marathon imeleta hamasa kubwa katika mkoa wa Mwanza hasa kwa kuitangaza kimichezo na kuongeza kuwa kwa mwaka huu, Mwanza imeshika nafasi ya nne kitaifa katika michezo.
Mratibu wa mbio hizo Mathew Kasonta .
 Mratibu wa mbio hizo Bw Mathew Kasonta alisema tofauti na mwaka jana, kwa mwaka huu washiriki wataweza kujisajili kupitia Airtel Money na kuongeza kuwa fomu zitapatikana kwenye maduka yote ya Airtel.

“Kwa wale watakao tumia Airtel Money kujisajili, unapaswa kutuma pesa kwa jina la fumbo (MARATHON) ambapo utapokea ujumbe utakaouonyesha pale utakapokwenda kuchukua fomu za usajili katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam, Dodoma, Zanzibar, Mbeya, Arusha na Mwanza,” alisema.
Mwenyekiti wa Chama cha Riadha mkoa wa Mwanza Silas Nkungu akizungumza na waandishi wa habari.
Kasonta aliongeza kuwa washiriki wenye vigezo pia wataweza kusajili kwa kupata fomu zipatikanazo katika uwanja wa Nyamagana mkoani Mwanza, na katika ofisi za kampuni ya Capital Plus International zilizopo ghorofa ya tatu, upande wa kulia katika jengo la ATC, Mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam.

Alibainisha kuwa fomu za usajili zitapatikana katika viwango vya bei vifuatavyo; shilingi 5,000 kwa mbio za km 21 (kwa watu wote), shilingi 3,000 kwa mbio za km 5 (mbio kwa makampuni na taasisi).

Alisema kuwa fomu kwa mbio za kilometa 3 (kwa wazee kuanzia miaka 55 na watu wenye ulemavu wa ngozi) na mbio za kilometa 2 kwa watoto (wenye umri wa miaka 7 mpaka 10) zitapatikana bure.

KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI CHAENDESHA UKAGUZI WA MAGARI KWA WAFANYAKAZI WA AIRTEL

CPL Jumaa mwalimu wa kituo cha polisi Oyesterbay akikagua gari la mmoja wa wafanyakazi wa Airtel  Bi Susan Kajubili wakati  polisi kikosi cha usalama barabarani kilipoendesha zoezi la ukaguzi wa magari kwa wafanyakazi Airtel katika kutimiza lengo la wiki ya Nenda kwa usalama barabarani,. zoezi hilo liliyofanyika katika makao makuu ya Airtel morroco

Pic 2

CPL Jumaa mwalimu wa kituo cha polisi Oyesterbay akikagua tairi la gari la mmoja wa wafanyakazi wa Airtel  James Majwala wakati   polisi kikosi cha usalama barabarani kilipoendesha zoezi la ukaguzi wa magari kwa wafanyakazi Airtel  katika makao makuu ya Airtel morroco

Pic 3

Mfanyakazi wa Airtel bwana Jacob Malisa akibandika stika ya usalama barabarani mara baada ya gari lake kukaguliwa na kuthibitisha kufaa kutembea barabarani.  Zoezi la ukaguzi wa magari lilifanyika jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel na kuwashirikisha wafanyakazi wa Airtel

Pic 4
CPL Jumaa mwalimu wa kituo cha polisi Oyesterbay akikagua uhalali stika ya leseni ya barabarani katika moja ya gari la wafanyakazi wa Airtel bwana Francis Ndikumwami wakati  polisi kikosi cha usalama barabarani kilipoendesha zoezi la ukaguzi wa magari kwa wafanyakazi Airtel  katika makao makuu ya Airtel morroco

PIc 5
Inspector Serengeti Action wa kituo cha polisi Oyesterbay akiingia katika moja ya gari la mfanyakazi wa Airtel bi Aminata Nakieta tayari kwa ukaguzi

PENTHIAS SCRABBLE TAKING SHAPE AS HE PREPARES FOR THE OCTOBER 26 RUMBLE IN LUSAKA, ZAMBIA

PENTHIAS CHISENGA
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA) – THURSDAY 03 OCTOBER, 2013, DAR ES SALAAM, TANZANIA – Zambian flyweight Champion Penthias Chisenga has set his "PATH" and as he prepare for his impending rumble against the Tanzanian slugger  Issa Omari. In a move that may see him becomes the first ever "IBF Continental Africa Flyweight Champion" from Zambia,  Penthias is training almost 10 hours a day and as he builds up his fighting arsenals while his eyes are glued on the continental diadem!
 
Zambians from all walks of life are enthusiastic about this rumble which is coming at a time when the country under the strongman Michael Sata is rebuilding up its economy. To the Zambians, nothing would be so important than the victory and the prospects has elicited lots of excitements in various quarters.
 
Pethias is a young man who want to emulate his countrymen and heroes the like of Musankabalas thenCommonwealth Boxing Champions. Albert Musankabala was the Flyweight Commonwealth Champion in the 80s and Zambians vividly remembers his fireworks in the ring. They expect Penthias to rekindle the memories of the 80s and to the young man, this is the tallest order.
As the rumble gears up to homestretch, betting houses are busy selling tickets in different parts of this great copper producing nation. "It is Zambia this time:" or so they keep on saying in reference to their national soccer teamChipolopolo defeat on the hands of Tanzania national soccer team the "Taifa Stars" recently!
  
Penthias Scrabble could be Issa's nightmare and the young Tanzanian is equipping himself for this major task knowing that he would be fighting at the hostile crowd. Nobody would come to his aid in that ring save for his talents and stamina. Oh! yes, he has to win this one for himself and his country too!

The "IBF Continental African Flyweight Title" is taking place in Lusaka, the capital city of this copper producing nation of Zambia OCTOBER 26, 2013. Exodus Stables Boxing Promotion owned and managed by AnthonyMwamba Chiwila will be in charge for this rumble. On the bill that day, will see Francis Zulu and Joseph Chingangu fight for the Africa's greatest Apple, the "IBF Continental Africa Heavyweight Title".
  
Zambia used to be one of the boxing powerhouses in Africa when great boxers like Lottie Mwale and Chisanda Mutti shook the boxing fraternity. The task of promoting Zambian image is now left to Pethias Chisenga and this could well be the hard one as he meet the man of his equal qualities in Issa Omari from the neighboring country ofTanzania.
 
"Penthia's Scrabble" could be Issa's Nightmare" check out this space for more news as we wait for this impending great action packed tournament which may take Zambia back to the days when it dominated boxing fraternity inSouthern Africa.
 
 
Congratulations Zambia. Africa is Proud of YOU!

Wednesday, October 2, 2013

TANZANIA NA AFGHANISTAN HAZIWATUNZI VYEMA WAZEE

Wazee wakiwa wameketi ufukweni.
Sweden ndio nchi nzuri zaidi duniani kuishi maisha ya uzeeni wakati Afghanistan ndio kubaya zaidi kwa wazee kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Umoja wa Mataifa.
Utafiti huo unaotizama hali ya watu wazee na mazingira wanamoishi, ulifanywa katika mataifa 91. Norway na Ujerumani, zilikuwa katika nafasi za juu huku Ingereza ikiwa katika nafasi ya 13.

Utafiti huo unaonya kuwa nchi nyingi duniani, hazina mifumo mizuri ya kutunza wazee.
Ifikapo mwaka 2050, wazee watakuwa wengi kuliko vijana walio chini ya miaka 15, wengi wakiwa ktika nchi zinazostawi.
Nchi zenye mifumo mizuri ya kuwatunza wazee:
  • Sweden, Norway na Ujerumani zilikuwa juu kwenye orodha.
  • Uingereza ilikuwa ya 13 nyuma ya Ireland
  • Nchi zengine ambazo ziko katika fasi za kwanza kumi ni Uholanzi, Canada, Switzerland, New Zealand, Marekani, Iceland na Japan
  • Afghanistan, Tanzania na Pakistan ni za mwisho kwenye orodha hiyo.
Utafiti huo ulikusanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la kukadiria idadi ya watu, UNPF na shirika la kimataifa la kutetea maslahi ya wazee HelpAge.
Watafiti wanasema walitumia vigezo 13 ikiwemo mapato, ajira, huduma za afya, Elimu, na mazingira....katika kile wanachosema ni utafiti wa kwanza wa aina yake duniani.
Aidha , watafiti wanasema kuwa nchi nyingi kote duniani zinakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na idadi kubwa na inayoendelea kukuwa ya wazee 72katika mataifa hayo.
"kutokana na ongezeko la mahitaji ya nchi mbali mbali duniani, nchi hizi nazo zinaendelea kukabiliwa na matatizo ya kukidhi mahitaji ya wazee,'' alisema Silvia Stefanoni, kaimu afisaa mkuu mtendaji wa shirika la HelpAge International.
Sweden ilikuwa ya kwanza katika nchi bora zaidi kwa kukidhi mahijati ya wazee, Afghanistan ilikuwa ya mwisho. Mataifa ya ulaya ndio yalifanya vyema katika kuwatunza wazee.
Sio kwa kuwa nchi hizo ni tajiri ndiposa zinawatunza wazee vyema kwa sababu hata nchi ambazo uchumi wao sio mzuri, bado huwatunza vyema wazee, ikiwemo Sri Lanka, Bolivia na Mauritius.
Urusi ilikuwa nambari, (78), India (73) na Uturuki (70) wakati Brazil ilishikilia nambari (31) huku China ikiwa nambari (35)
CHANZO: BBC SWAHILI.

MKUTANO WA 23 WA MWAKA WA WANACHAMA NA WADAU WA PPF WAANZA LEO JIJINI ARUSHA

Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,Waziri wa Fedha,Dkt William Mgimwa (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Nembo Mpya ya PPF iliyoambatana na Tovuti Mpya ya PPF.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa PPF,Dk. Aggrey Mlimuka na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,William Erio.
 Hivi ndivyo inavyoonekana Nembo Mpya ya PPF.
Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,Waziri wa Fedha,Dkt William Mgimwa akitoa hotuba yake wakati akifungua mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini Arusha kwa siku tatu mfululizo kuanzia leo Oktoba 2 mpaka Oktoba 5,2013.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF,Dk. Aggrey Mlimuka akitoa hotuba yake mapema leo asubuhi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,William Erio akizungumza leo kwenye Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa PPF,unaofanyika leo kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha.
Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,Lulu Mengele akifafanua jambo juu ya Muonekano wa Logo Mpya ya Mfuko huo iliyozinduliwa Rasmi leo kwenye Ukumbu wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Chama cha Wakuu wa Mashirika ya Hifadhi za Jamii nchini,Daudi Msangi akitoa shukrani kwa mgeni rasmi na kwa wadau wote kwa ujumla kwa kuitika kwao wito kwenye Mkutano huo.
Bw. Bonda Nkinga akitoa Ushuhuda wake wake mbele ya Wanachana na Wadau wa PPF waliohudhuria kwenye Mkutano wa 23 wa Mwaka,juu ya PPF ilivyoweza kuwasaidia watoto zake kusoma kupitia Fao la elimu.
Kijana Peter William Mulokozi ambaye ni Mwanafunzi wa Kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari ya Mzumbe akitoa ushuhuda wake mbele ya Wanachana na Wadau wa PPF waliohudhuria kwenye Mkutano wa 23 wa Mwaka,juu ya PPF ilivyoweza kumsaidia yeye kusoma,mara baada ya Baba yake kupoteza maisha ghafla.PPF ambao ni Mfuko pekee unaotoa fao la Elimu nchini endapo Mwanachama anakuwa amefariki akiwa kwenye ajira.PPF imeweza kumsaidia kijana huyu kusoma mpaka hapo alipofikia.
Kijana Pascalia Nsatto ambaye ni Mwanafunzi wa Kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Kimataifa ya Moshi akitoa ushuhuda wake mbele ya Wanachana na Wadau wa PPF waliohudhuria kwenye Mkutano wa 23 wa Mwaka,juu ya PPF ilivyoweza kumsaidia yeye kusoma,mara baada ya Wazazi wake wote wawili kupoteza maisha.
Ilikuwa ni huzuni tu wakati vijana hao wakitoa ushuhuda wao wa namna walivyoweza kusaidiwa kimasomo na Mfuko wa Pensheni wa PPF pindi walipoondokewa na wazazi wao.
Waheshimiwa Wabunge wakifatilia kwa umakini Hotuba ya Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,Waziri wa Fedha,Dkt William Mgimwa (hayupo pichani) alipokuwa akifungua.
 Viongozi kutoka Chama cha Wafanyakazi.
 Baadhi ya Wakurugenzi wa Idara mbali mbali ndani ya Mfuko wa Pensheni wa PPF wakifatilia mkutano huo.
 Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,Waziri wa Fedha,Dkt William Mgimwa akitoa Tuzo wa Washindi mbali mbali wa PPF wanaoongoza kwa kuwasilisha michango yao kwa wakati. 
 Mrisho Mpoto akitoa burudani. 
 Burudani ya Ngoma za asili. 
 Mkutanoni. 
Picha ya pamoja.