Saturday, June 8, 2024
Thursday, June 6, 2024
BAADA YA SAMAKI NA MIFUGO KUFA NEMC KANDA YA ZIWA YASITISHA SHUGHULI ZA MGODI KUPISHA UCHUNGUZI
NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
Baada ya malalamiko kutoka kwa baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Imalamate kilichopo Wilayani Busega Mkoa wa Simiyu, kuitaka Serikali kuufunga mgodi wa Dhahabu wa SHIYUAN Tanzania Co. LTD uliopo kwenye kijiji chao kutokana na madhara ambayo wamenza kupata kwa baadhi ya mifugo kufa vikiwemo viumbe vingine kama ndege na samaki huku chanzo kikidaiwa kuwa ni maji yaliyo na sumu yanayotiririshwa na mgodi hadi kwenye bwawa lao la maji. Siku tatu baadaye yaani leo Juni 06/2024 Baraza La Taifa La Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Kanda ya Ziwa Victoria, limesitisha shughuli za mgodi huo kwa lengo la kupisha uchunguzi. Jerome Kayombo ni Meneja wa NEMC Kanda ya Ziwa #nemc #samiasuluhuhassan #mwanza #simiyuWednesday, June 5, 2024
MHASIBU JIJI LA MWANZA AFARIKI AJALINI AKIENDA KWENYE MAZISHI
Mhasibu wa Idara ya Mapato ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Amon Joseph (41) amefariki dunia katika ajali ya gari akienda kwenye maziko ya baba mzazi wa mhasibu mwenzake, yaliyotarajiwa kufanyika leo wilayani Kwimba mkoani hapa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kifo cha mhasibu huyo akitaja chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva.
“Ni kweli imetokea ajali hiyo Saa 5:45, maeneo ya Kijiji cha Malembe Kata ya Igongwa Tarafa ya Ngudu Wilaya ya Kwimba kwenye barabara ya vumbi ya Mwabuki kuelekea Jojiro, gari aina ya Toyota Progress lililokuwa likitokea Mwabuki kwenda Ngudu ilimeacha njia na kutumbukia darajani na kusababisha kifo cha dereva (Amon),” amesema Kamanda Mutafungwa.
Awali, Ofisa Mawasiliano wa Halmshauri ya Jiji la Mwanza, Martine Sawema amesema Amon amefariki akiwa safarini kwenda kuhudhuria maziko ya baba mzazi wa mhasibu mwenzake Ngudu wilayani Kwimba.
“Nimeumizwa sana na kifo cha Amon, kiukweli baada ya kufika eneo lile nilichokiona nadhani hata kukosekana na alama za barabara zinazotoa tahadhari kwa madereva kuwa kuna daraja eneo lile kumechangia ajali hii kutokea. Niwaombe Tarura waweke alama katika barabara ile.”
“Pale inaonekana kama alishika breki kama hatua 50 hivi, lakini gari likapinduka hadi kwenye daraja ambalo limejaa maji na hakukuwa na winchi ya kulinyanyua, kwa hiyo amekufa akiwa ndani ya gari. Tumeshautoa mwili na kwenda kuuhifadhi Hospitali ya Bugando,” amesema Sawema.
Akimzungumzia Amon, Kocha wa mpira wa kikapu mkoani Mwanza, Rajabu Kabonga amesema alikuwa mchezaji mwenye upendo ambaye alitamani kuona watoto wakichipukia na kufikia mafanikio katika mpira wa kikapu.
“Alikuwa anacheza Basketball hapo Mirongo, pia alikuwa mwalimu na mchezaji mwenzangu, bado alikuwa na miaka kama mitatu ya kucheza basketball, alikuwa anasifika kuwa na upendo. Ndiyo kocha wa timu ya mpira wa Kikapu ya Profile mkoani Mwanza, tutamkumbuka,” amesema Kabonga.
JE, UNAFAHAMU TATIZO LA MGUU KIFUNDO AU NYAYO ZILIZOPINDA?
NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
Mguu kifundo ni aina ya ulemavu ambao mtoto anazaliwa nao baada ya kupatikana na hitilafu katika mifupa ya kwenye nyayo. Chanzo cha tatizo hilo hakijakuwa bayana ila wahusika hulazimika kutembea kwa kutumia sehemu ya nje ya unyayo, hali inayoleta matatizo na shaka katika ufanisi. MDH inashirikiana na Serikali kwa ufadhili wa Miracle Feet katika utoaji wa huduma za Mguu kifundo na matibabu yake na hii ndiyo kazi inayofanyika Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza, ambapo Kipindi cha DRIVE MIX kutoka radio Jembe Fm kinazungumza na Dr. Mussa Hamisi kujua undani wa changamoto hiyo.Tuesday, June 4, 2024
ANAANDIKA MWANAMICHEZO MAXIMILLIAN
Wakati Jonas Mkude anasaini katika klabu ya Young Africans wapo watu waliongea mengi sana ikiwemo kuuliza maswali, Eti atacheza nafasi ya nani? mara Ohh amezeeka!! mara Mkude ameshamaliza soka lake hivyo hana tena motivation!!
Hii picha nadhani ina majibu mengi sana,
Picha ina maelezo ya kutosha sana kuhusu Atacheza nafasi ya nani?…. Hapo unaona ametoka kumaliza mechi akiwa na Dr. Aucho na walicheza wote.
.
Wanaosema kazeeka … Picha inawajibu kuwa muwa unakolea utamu unapokaa sana…. Tazama Penalty ya kikongwe aliyopiga😂😂 Yani Humu tuuu….
Monday, June 3, 2024
HUYU HAPA DAKTARI WA TIBA ASILI ANAYETIBU MIFUPA BILA KUGUSA
NA ALBERT G. SENGO/ MWANZA
Dr Mossi, ni Bingwa wa Tiba asili, Ajali za moto, Vidonda vya tumbo, Utumbo kuoza, Ganzi mwilini, Uzazi kwa kina dada , Chango la kuchoma na Kuhariibu mimba, Uvimbe tumboni na Walio vimba matumbo , Kusafisha Figo ghalama ni nafuu sana kwa atakae hitaji huduma ya kuonana na daktari. Dr. Mossi atakufuata popote ulipo kwa huduma maalum, pia kwa wale wanaosumbuliwa na Bawasili au Mang'ondi daktari anatibu ndani ya wiki moja tu, Matatizo ya ngozi au Mapele yanayo toa maji maji tiba ipo ambapo ngozi yako itarudi vizuri kama awali. Kwa maelezo na ushauli tembelea TikTok ya Dr. Mossi, au Whatsapp 0764219747 na utahudumiwa popote pale ulipo. Nawatakia afya njema na Mungu awabariki.BRELA YAWATAKA WAFANYABIASHARA KUJISAJILI ILI KUCHANGAMKIA FURSA KIBIASHARA
Na Oscar Assenga,TANGA
WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELA) umewataka wafanyabiashara kuchangamkia fursa ya kujisajili na wakala huo kutokana na kwamba kama haujasajiliwa hauwezi kuomba tenda rasmi ambazo zinatangazwa na Taasisi mbalimbali za Serikali na Idara zake.
Hayo yalisemwa leo na Afisa Sheria za Wakala huo Lupakisyo Mwambiga wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya 11 ya Biashara na Utalii yanayofanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Usagara Jijini Tanga.
Lupakisyo alisema kwamba ni vema wafanyabiashara na wajasiriamali kuona umuhimu wa kurasimisha biashara zao kwa kusajili brela na kupata leseni inayostahili ili waweze kuchangamkia fursa za kibiashara
“Wengi wanachanganya leseni kati ya daraja A na B ambazo zinatolewa na halmashauri na Manipsaa kuna biashara zenye sura ya kitaifa na kimataifa unatakiwa kupata leseni kutoka brela hivyo nawahimiza wafanyabishara waje kupata elimu kwa kueleza biashara wanazofanya “Alisema
“Kwa lengo la kushauriwa ni leseni gani anapaswa kuomba kutoka brela na wale wafanyabiashara wenye viwanda vidogo vidogo tunatoa leseni za viwanda watu wengi hawajua unapoanzisha viwanda lazima uwe na leseni kutoka Brela”Alisema
Alisema kwamba kuna leseni ya uanzishwaji wa kiwanda na leseni biashara kwa wajasirimali wenye viwanda vidogo na wafanyabiashara wenye viwanda vikubwa huku akiwataka kutembelea banda lao ili waone ni vitu gani wanaweza kufanya kupata leseni.
Hata hivyo alisema kwamba wapo kushiriki kwenye maonyesho ya biashara na utalii kutokana na kwamba ni moja ya taasisi za kusimamia usajili wa biashara pamoja na leseni na wamekuja kutoa elimu na huduma za papo kwa papo ikiwemo usajili wa kampuni ,majina ya biashara.
Alisema pia wanatumia maonyesho hayo kutoa leseni kundi A na utoaji wa leseni za viwanda na usajili wa alama za biashara kwa wateja wao huku akiwataka wananchi wa mkoa wa Tanga kuendelea kujitokeza kufika kwenye banda lao ili wawez kupata ushauri jinsi gani wanaweza kusajili kampuni ,jina la biashara au alama ya bisharaa na waliokuwa tayari wanasajiliwa kupitia mtandao kwa kuwasaidia kwa sababu wapo kwenye maonyesho na wamekuwa wakitoa elimu kwa wafanyabiashara umuhimu wa kusajili au kurasimisha biashara maana wengi mpaka wakipata changamoto Fulani ndio wanakilimbia brela.
“Wengi mpaka wanapopata changamoto ndio wanakimbili brela labda amepata tenda unatakiwa kupeleka cheti kutoka brela ndio wanahangaika kusajili au benki wakitaka taarifa kuhusu brela ndio wanakwenda kusajili”Alisema
NHIF YATUMIA MAONYESHO YA 11 YA BIASHARA NA UTALII KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUHUSU VIFURUSHI VYAO
Na Oscar Assenga, TANGA
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Tanzania (NHIF) Mkoani umeshirikia maonyesho ya 11 ya Biashara na Utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara ili kutoa elimu kuhusu huduma wanazotoa ikiwemo vifurushi wanavyovitoa.
Banda la Mfuko huo limekuwa lililopo kwenye maonyesho hayo limekuwa ni kivutio kwa wananchi ambao wamefika kupima afya zao na kupata ushauri namna ya kuepukana na magonjwa yasiyoyakuambikizana.
Pia wananchi hao wamekwenda kwa ajili ya kuona namna ya kujiunga na vifurushi mbalimbali vinavyotolewa na mfuko huo ili kuweza kunufaika na matibabu bure pindi wanapougua.