MKUU wa mkoa wa Mwanza John Mongella anatazamiwa kuwa mgeni rasmi wa uzinduzi wa Chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi, uzinduzi huo utakaofanyika mnamo tarehe 23 mwezi April 2018 katika Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana unategemewa kuhusisha zaidi la wasichana 31,291 walio na umri kati ya miaka 9 hadi 14.
Katika semina kwa waandishi wa habari wa jijini Mwanza kwaajili ya kukuza uelewa wa ugonjwa huo wa saratani ya shingo ya kizazi mafunzo mafupi yametolewa ikiwa ni pamoja na taarifa ya uzinduzi.
Waandishi hao pia walipata fursa ya maswali na majibu.
Saratani ya shingo ya kizazi ni saratani ambayo hutokea kwenye shingo ya kizazi cha mwanamke - ambayo ni kiingilio kutoka uke hadi katika mfuko wa uzazi.
Ni moja kati ya zaidi ya aina 100 ya virusi vya human papilloma (HPV), ambavyo 13 vinasababisha saratani.
Pia aina fulani ya HPV vinaambukizwa kwa njia ya ngono.
Baadhi ya sababu za kupata ugonjwa huo ni kushiriki ngono ukiwa na umri mdogo, ukifanya ngono na washiriki wengi , kuvuta sigara na kuwa na virusi vya Ukimwi.
Dalili ni
- kupata hedhi kwa mzunguko usio wa kawaida au kutoka damu baada ya kujamiana
- maumivu ya mgongo, mguu na fupanyonga
- uchovu, kupungua kwa uzito na kutokuwa na hamu ya kula
- maumivu kwenye uke au kutoa harufu mbaya
- kuvimba kwa mguu mmoja
Uchunguzi wa virusi hivyo unastahili kufanyika ili kuvigundua mapema. Chanjo za HPV ni hatua nyingine ya kuziuzi.
Matibabu kwa wagonjwa walio na virusi hivyo yanategemea na viwango vya virusi hivyo mwilini, hata hivyo yanaweza hitaji kutibiwa kwa njia ya upasuaji na kutoa sehemu au mfuko wa uzazi mzima au kutumia miyonzi.
Chanzo: Shirika la Afya duniani
Mambo kumi unayoweza kufanya kupunguza hatari ya kuugua saratani:
- Usivute sigara wala kutumia tumbaku ya aina yoyote
- Hakikisha nyumbani kwako hamna moshi
- Kula chakula chenye afya
- Kunyonyesha kunapunguza hatari kwa mama kuugua saratani
- Hakikisha watoto wako wanapata chanjo dhidi ya hepatatis B na HPV
- Epuka kuchomwa sana na miale ya jua, au tumia mafuta yanayo kukinga dhidi ya miale hiyo.
- Punguza uchafuzi wa hewa ndani na nje ya nyumba
- Jishughulishe kuupa mwili mazoezi
- Punguza unywaji wa pombe
- Jitahidi kufanyiwa ukaguzi wa mapema kutambua uwepo wa saratani.