ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, April 19, 2018

YANGA YATINGA HATUA YA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA.


Klabu ya soka ya Yanga imefanikiwa kuingia hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kupata ushindi wa jumla wa mabao 2-1, licha ya kufungwa katika mchezo wa leo jioni na wapinzani wao Welayta Dicha.

Yanga imefungwa bao 1-0 kwenye mchezo uliomalizika jioni ya jumatano tarehe 17 April 2018 huko Ethiopia lakini imesonga mbele kutokana na ushindi wa mabao 2-0 iliopata nyumbani kwenye mchezo wa kwanza jijini Dar es salaam.

Hii sio mara ya kwanza kwa Yanga kutinga hatua ya makundi ambapo msimu wa 2015/16 iliingia katika hatua hiyo lakini ilimaliza katika nafasi ya mwisho na kushindwa kuendelea na michuano.

Yanga leo imecheza bila ya kocha wake mkuu George Lwandamina ambaye ameondoka klabuni hapo wiki iliyopita na kurejea kwenye timu yake ya zamani ya Zesco United ya Zambia.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.